Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Funga (saumu)

Kutoka wikishia


Funga au Saumu ni ibada ya kujizuia na yanayobatilisha saumu (kila chenye kufunguza), kama vile kula, kunywa kuingiliana, na mambo mengine, hii ni kuanzia kuchomoza kwa alfajiri hadi kuzama kwa jua ambayo ni magharibi ya kisheria, kwa nia ya kutii amri ya Mwenyezi Mungu. Funga inahesabiwa kuwa ni miongoni mwa matawi ya dini ya Kiislamu, miongoni mwa ibada bora kabisa na ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Pia saumu ilikuwepo katika dini zilizotangulia kabla ya Uislamu. Funga kifiqhi imegawanyika katika makundi manne: ya wajibu, ya sunna, iliyo makruhu na iliyo haramu; ambapo funga ya mwezi wa Ramadhani inasimama kama funga ya wajibu.

Katika vyanzo vya kidini, kuna athari nyingi za kiroho na kimaadili zilizotajwa kwa ajili ya funga; ikiwemo kupata taqwa (uchamungu), kuwa ngao dhidi ya moto wa Jahannamu, kufutiwa madhambi, zaka ya mwili, na kujiweka mbali na Shetani. Pia inasemekana kuwa kufunga kuna athari chanya za kimwili na kisaikolojia, kama vile kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo, kuongeza kujiamini, na kuzuia magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Mfungaji anapaswa kujiepusha na mabo yote yanayobatilisha saumu (vifunguza saumu) ambayo nayo ni pamoja na: kula na kunywa, kuingiliana (kufanya tendo la ndoa), kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s), kufikisha vumbi zito kooni, kubakia na janaba, hedhi na nifasi, kujichua (punyeto), kuzamisha kichwa chote ndani ya maji na kutapika. Mtu ambaye funga ni wajibu kwake, akifanya kwa makusudi moja ya mambo yanayobatilisha funga, anapaswa kutekeleza khadha ya funga pamoja na kutoa kafara.

Nafasi na Athari za Funga

Funga ni amali ya kujizuia na mambo maalum kama vile kula na kunywa kuanzia alfajiri (kuchomoza kwa alfajiri) hadi magharibi ya kisheria kwa nia ya kujikurubisha Kwa Mwenyezi Mungu.[1] Hata hivyo, Ali Meshkini, fakihi wa Kishia, ameifafanua funga kuwa ni kuiandaa nafsi ili kujiepusha na mambo yanayobatilisha Saumu.[2] Kwa mtazamo wa Sayyid Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi, mfasiri wa Kishia, Uislamu hauoni kuwa kujizuia tu na kula na kunywa kunatosha katika funga, bali unaamrisha kwamba mfungaji anapaswa kujiweka mbali na kila jambo linalosababisha uchafu na kutenda dhambi, au linalomvutia kwenye matamanio na wasawasi wa nafsi.[3] Sayyid Muhammad Kadhim Tabataba'i Yazdi katika kitabu chake cha Al-Urwatu al-Wuthqa amezingatia ulazima wa kufunga katika mwezi wa Ramadhani kuwa ni miongoni mwa mambo ya dharura ya dini, na amesema kuwa yeyote anayepinga uwajibu wa kufunga mwezi wa Ramadhani anakuwa ni mritadi na ni wajibu kuuawa.[4]

Funga imehesabiwa kuwa ni miongoni mwa ibada zenye fadhila kubwa zaidi,[5] moja ya nguzo tano za Uislamu,[6] aina ya jihadi,[7] na kuiacha kumetajwa kuwa ni sababu ya kutoka katika imani.[8]

Dalili na Hekima ya Kuwajibishwa kwa Saumu

Allamah Tabataba'i na Nasir Makarim Shirazi, ambao ni miongoni mwa wafasiri wa Kishia, kwa kutumia msemo wa “لعلکم تتقون; Ili mpate kumcha Mungu” katika Aya ya Saumu, wanaona kuwa falsafa ya kufunga ni kufikia taqwa (uchamungu).[9] Katika Riwaya iliyomo katika kitabu cha Ilal al-Shara'i'i sababu ya kuwajibishwa kwa funga imetajwa kuwa ni kuwaonjesha matajiri wa jamii shida na njaa ili wapate kuwahurumia masikini.[10]

Katika Riwaya nyingine, imeelezwa kuwa pale Nabii Adam (a.s) alipokula tunda la mti uliokatazwa, athari zake zilibaki tumboni mwake kwa siku 30, na hivyo Mwenyezi Mungu akawajibisha siku 30 za funga kwa kizazi chake.[11] Katika Riwaya kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) kuhusu sababu ya kuwajibishwa kwa funga, kumeashiriwa jambo la kuikumbusha nafsi ugumu na dhiki ya Siku ya Kiyama.[12] Baadhi pia wanaona kuwa afya ya mwili ni miongoni mwa sababu nyingine za kuwajibishwa kwa funga, na wanategemea Hadithi ya Sumu Tasihhu "صوموا تصحوا" (Fungeni mpate afya) inayonasibishwa na Mtume.[13]

Athari za Kibinafsi na Kijamii za Kufunga

Katika Riwaya zilizopokewa kutoka kwa Maasumina (a.s), kumetajwa athari na matokeo mbalimbali ya kufunga, baadhi yakiwa ni:

  1. Ni njia ya mtihani na kuimarisha ikhlasi.[14]
  2. Ni zaka ya mwili.[15]
  3. Ni ngao dhidi ya moto wa Akhera.[16]
  4. Ni sababu ya kujibiwa dua,[17] hasa wakati wa kufuturu.[18]
  5. Afya njema ya mwili.[19]
  6. Kuimarisha kumbukumbu.[20]
  7. Kujiweka mbali na Shetani.[21]
  8. Thawabu maalum kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[22]
  9. Shauku ya Pepo kwa mtu aliyefunga.[23]

Kwa mujibu wa Abdallah Jawadi Amoli, katika kitabu chake cha Tafsir Tasnim, funga huimarisha roho ya nidhamu, kinai, na subira dhidi ya madhambi na matatizo ya kimaisha ndani ya mtu binafsi na jamii.[24] Kadhalika, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Tanzania, kiwango cha uhalifu wa kijamii hupungua katika mwezi wa Ramadhani.[25]

Pia kulingana na tafiti za kitabibu, kufunga kuna faida kwa afya ya mwili pamoja na akili.[26] Athari chanya kwenye mfumo wa kinga ya mwili, kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo, afya ya akili, kuongezeka kwa hali ya kujiamini, na kuzuia magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa athari za saumu zinazotajwa katika afya ya mwili na akili.[27]

Historia ya Funga

Kwa mujibu wa Aya ya 183 ya Suratu al-Baqarah, funga ilikuwepo katika dini zilizotangulia kabla ya Uislamu.[28] Katika Taurati[29] na Injili[30] kumeripotiwa taarifa za kufunga kwa umma zilizopita. Kwa mujibu wa Taurati, Nabii Musa (a.s) kabla ya kupokea Mbao (الواح), alifunga siku arobaini mchana na usiku.[31] Katika Qur'ani, inazungumziwa funga ya Nabii Zakariya (a.s)[32] na Bikira Mariam (s.a)[33][Maelezo 1] na katika Riwaya[34] pia imeelezewa kuwepo kwa saumu katika dini mbalimbali za kabla ya Uislamu. Kadhalika inasemekana kuwa, pia funga ilikuwepo miongoni mwa jamii nyingine za kale kama vile jamii ya Wamisri, Wagiriki, Warumi, na Wahindi wa kale.[35]

Kulingana na vyanzo vya Kiislamu, funga ya mwezi wa Ramadhani ilifaradhishwa mnamo tarehe 2 Shaabani[36] au 28 Shaabani mwaka wa pili Hijria, ambayo ni sawa na siku 13 baada ya tukio la kubadilishwa kwa Kibla.[37] Amri hii na baadhi ya hukumu zake zimeelezwa wazi kabisa ndani ya Qur'ani.[38] Mwanzoni mwa uanzilishi wa kuwekwa kwa sheria ya kufunga, wafungaji baada ya kufuturu waliruhusiwa kula chakula tu hadi kabla ya kulala, na ilikuwa ni haramu kuingiliana (kufanya tendo la ndoa) katika mwezi mzima wa Ramadhani, lakini hukumu mbili hizi zilikuja kufutwa (Kufutwa kwa hukumu/نسخ) baada ya muda fulani.[39]

Aina za Saumu

Funga kisharia imegawika katika makundi makuu manne:

Aina Hukumu na mifano
Funga ya Wajibu
Funga Haramu
  • Funga ya siku ya Eid al-Fitr na Eid al-Adha
  • Funga ya siku ya shaka (yawm al-shakk) kwa nia ya kuwa ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani
  • Funga ya mtu mwenye yakini au dhana kwamba funga inamletea madhara
  • Funga ya sunna ya mke bila idhini ya mume
  • Funga ya mfululizo (sawm al-wisal)
  • Funga ya nadhiri kwa ajili ya kufanikisha jambo la haramu. Mulla Mahdi Naraqi katika kuhesabu funga haramu, ameeleza kuwa funga ya nadhiri ya maasi ni kama mtu kuweka nadhiri kuwa akifanikiwa kutenda kosa fulani atafunga; nadhiri hii ni batili na funga yake ni haramu.[41]
  • Funga ya kunyamaza kimya (sawm al-samt): yaani kuweka nia ya kutozungumza wakati wa mchana au baadhi ya masaa akiwa amefunga.
  • Funga ya Siku za Tashriq (Ayyam al-Tashriq) (11, 12, na 13 Dhu al-Hijjah) kwa yule aliye katika eneo la Mina (Makka)
  • Funga ya sunna ya mtoto ikiwa inawasumbua na kuwaudhi wazazi.[42]
  • Funga ya mgonjwa ikiwa funga inamsababishia madhara.[43]
Funga Iliyo Makruhu [Maelezo 2]
  • Funga ya Siku ya Ashura
  • Funga ya siku ya Arafa kwa mtu anayehofia kudhoofika asiweze kusoma dua
  • Funga ya siku anayoshuku kuwa ni siku ya Arafa au Eid al-Adha
  • Funga ya sunna ya mgeni bila idhini ya mwenyeji
  • Funga ya kulipa (khadha) ikiwa bado muda upo wa kutosha bila idhini ya mwenyeji
  • Funga ya sunna ukiwa safarini
  • Funga ya sunna ya mtoto bila idhini ya baba[44]
Funga ya Mustahabu (Sunna)

Ahkamu (Hukumu) za Funga

Mambo Yanayobatilisha Funga

Kulingana na ahkamu za kifiqhi, kufanya baadhi ya mambo wakati wa kufunga ni marufuku:

  1. Kula na kunywa
  2. Kufanya tendo la ndoa
  3. Kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu, Mtume wa Mungu na Maimamu Maasumu (a.s)
  4. Kufikisha vumbi zito kooni
  5. Kubaki na janaba, hedhi na nifasi hadi adhana ya asubuhi
  6. Kujichua (kujitoa manii)
  7. Kupiga pampu ya maji sehemu ya nyuma (enema) kwa kutumia vimiminika
  8. Kuzamisha kichwa chote ndani ya maji[Maelezo 3]
  9. Kutapika
  10. Kuweka nia ya kukata funga au kutia nia ya kufanya moja ya mambo yanayobatilisha funga.[46]
Sherehe za Futari nchini India

Mambo Yaliyo Makruhu Katika Funga

Kulingana na kauli za mafakihi, kufanya baadhi ya mambo ukiwa umefunga ni makruhu; kama vile: kugusa, kubusu, na kucheza na mke, kujipaka wanja, kufanya jambo lolote linalosababisha udhaifu, kunusa maua, kulowesha nguo, kufanya jambo lolote linalosababisha mdomo kujaa damu, kama kung'oa jino, na kusukutua maji kinywani bila sababu ya msingi.[47]

Watu Wasiopaswa Kufunga

Funga ya mwezi wa Ramadhani ni wajibu kwa kila mukallafu, isipokuwa watu wafuatao:

  1. Mtu ambaye kwa sababu ya uzee hawezi kufunga, au kufunga ni kugumu sana kwake; hata hivyo, katika hali ya pili, anapaswa kutoa mudd moja ya chakula (kibaba) kwa masikini kwa kila siku.[48]
  2. Mgonjwa anayekumbwa na kiu kali na hawezi kuvumilia kiu, au anapata shida kubwa kuvumilia kiu; hata hivyo, katika hali ya pili, anapaswa kutoa mudd ya chakula kwa masikini kwa kila siku.[49]
  3. Mwanamke mjamzito au anayenyonyesha ambaye maziwa yake ni machache na kufunga kuna madhara kwa mtoto wake au kwake yeye mwenyewe; hata hivyo, anapaswa kutoa mudd ya chakula kwa masikini kwa kila siku, na aswali (alipe) khadha ya funga zake.[50]
  4. Mtu ambaye, haweazi kufunga kwa sababu ya udhaifu wa mwili, au kuna khofu ya funga hiyo kumdhuru; bila shaka, khadha ya funga hii ni wajibu kwake, na iwapo hatawezi kulipa khadha hiyo hadi Ramadhani inayofuata, hapo anapaswa kutoa mudd ya chakula kwa masikini kwa kila siku ayoacha kufunga.[51]
  5. Msafiri[Maelezo 4] anayekaa chini ya siku kumi safarini (sehemu aliyosafiria).[52] Hata hivyo, msafiri wa mara kwa mara (kathiru al-safar) na watu kama madereva ambao kazi yao ni kusafiri, wametolewa kwenye hukumu hii.[53]

Kufuturu (Iftar) au Kufungua Funga

Futari katika Haram ya Imamu Ridha (a.s)

Kuvunja au kufungua funga huitwa iftar (kufuturu).[54] Kwa mtazamo wa wafakihi wa Kishia, mfungaji hapaswi kufuturu hadi iingie magharibi ya kisheria (adhana ya Magharibi).[55] Kulingana na Riwaya, inashauriwa (mustahabu) kusoma dua na kusoma Surat al-Qadr wakati wa kufuturu,[56] na kufungua funga kwa maji, maziwa, na tende.[57] Kwa mujibu wa Riwaya, kumpa futari mfungaji kuna fadhila kubwa mbele ya Mungu.[58] Kulingana na kile kilichonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika Hotuba ya Shaabaniya, malipo ya kumpa futari muumini mmoja katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na thawabu za kumkomboa mtumwa, na ni jambo linalopelekea kusamehewa dhambi.[59]

Khadha na Kafara za Funga

  • Mtu ambaye ilikuwa wajibu kwake kufunga mwezi wa Ramadhani lakini hakufunga, anapaswa kuilipa (kuifanyia khadha).[60] Khadha ya funga si wajibu wa haraka (fauri), lakini inapaswa kufanywa kabla ya kuanza mwezi wa Ramadhani unaofuata.[61]
  • Mtu ambaye hakufunga katika mwezi wa Ramadhani kwa sababu ya ugonjwa na akashindwa kufunga hadi Ramadhani inayofuata, khadha si wajibu tena kwake, lakini anapaswa kutoa mudd moja ya chakula (gramu 750 za ngano) kwa masikini kwa kila siku.[62]
  • Mtu ambaye kwa makusudi na bila udhuru wa kisheria hakuifunga funga yake ya wajibu, mbali na khadha, kafara pia ni wajibu kwake;[63] kafara yake ni kuwalisha masikini sitini, au kufunga miezi miwili ambapo siku 31 kati ya hizo zinapaswa kufuatana mfululizo.[64]
  • Ikiwa mtu atachelewesha bila udhuru kutekeleza khadha ya funga hadi mwezi wa Ramadhani unaofuata, kafara ya kuchelewesha (ambayo ni kutoa mudd moja ya chakula kwa kila siku) inamuwajibikia.[65]
  • Ikiwa funga ya mwezi wa Ramadhani itabatilishwa kwa jambo la haramu kama vile kunywa pombe au kufanya zinaa, inawajibisha kafara jumuishi (kafaratu al-jam'i); yaani anapaswa kufunga siku sitini na kuwalisha masikini sitini kwa kila siku.[66] Hata hivyo, Sayyid Ali Husayni Sistani ameichukulia kafara jumuishi kama tahadhari inayopendekezwa (ihtiyati mustahab).[67]

Kuharamishwa Kula Hadharani Mwezi wa Ramadhani

Katika fiqhi ya Kiislamu, kujitokeza hadharani ukila (kufanya dharau ya kula hadharani) katika mwezi wa Ramadhani ni jambo haramu na linapelekea ta'aziri.[68]

Daraja za Funga

Kuna daraja (ngazi) mbalimbali za funga zilizotajwa: funga ya kawaida (صوم العام), funga maalum (صوم الخاص), na funga maalum zaidi (صوم خاص‌الخاص).[69]

  • Funga ya Kawaida: Ni kujizuia na kujiepusha na kula na kunywa, na kujiweka mbali na matamanio ya kimwili (kama tendo la ndoa), na kufuata kanuni za dhahiri za kufunga.[70]
  • Funga Maalum: Ni kudhibiti masikio, macho, ulimi, mikono, miguu na viungo vingine vyote vya mwili dhidi ya madhambi.[71]
  • Funga Maalum Zaidi: Hii inamaanisha mwanadamu ajiweke mbali na masuala na malengo yote ya kidunia, isipokuwa mambo yale ya dunia ambayo ni utangulizi (njia) wa dini.[72] Katika maneno ya Imamu Ali (a.s), pia kumeashiriwa kufunga kwa mwili (kujizuia kwa hiari na vyakula), kufunga kwa nafsi (kudhibiti hisia (milango ya fahamu) dhidi ya madhambi na kusafisha moyo na mambo mabaya), na kufunga kwa moyo.[73]

Katika احادیث, funga ya kweli inatambulishwa kama kuacha kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu hapendi,[74] na funga ambayo macho, masikio, nywele, na ngozi pia zimefunga,[75] aidha, imeelezwa kuwa funga ya moyo ni bora kuliko funga ya ulimi, na funga ya ulimi ni bora kuliko funga ya tumbo.[76]

Rejea

  1. ↑ Meshkini, Mustalahat al-Fiqh, uk. 363.
  2. ↑ Meshkini, Mustalahat al-Fiqh, uk. 363.
  3. ↑ Tabataba'i, Ta'alim-e Islam, uk. 272.
  4. ↑ Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, jz. 3, uk. 521.
  5. ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, jz. 16, uk. 181.
  6. ↑ Tazama: Kulayni, Al-Kafi, jz. 2, uk. 18-24 na jz. 4, uk. 62.
  7. ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, jz. 93, uk. 257, Hadithi 14.
  8. ↑ Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, jz. 2, uk. 118, Hadithi 1892.
  9. ↑ Tazama: Tabataba'i, Al-Mizan, jz. 2, uk. 8; Makarim Shirazi, Tafsir Nemuneh, jz. 1, uk. 623-624.
  10. ↑ Saduq, Ilal al-Shara'i, Al-Maktabat al-Haidariyya, jz. 2, uk. 378.
  11. ↑ Saduq, Ilal al-Shara'i, Al-Maktabat al-Haidariyya, jz. 2, uk. 378.
  12. ↑ Tazama: Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), jz. 2, uk. 116.
  13. ↑ Suri Laki, «فلسفه وجوب روزه», uk. 32-33.
  14. ↑ Nahj al-Balagha, Usahihishaji wa Subhi Salih, Hekima ya 252, uk. 512.
  15. ↑ Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, jz. 2, uk. 75, Hadithi 1774.
  16. ↑ Kulayni, Al-Kafi, jz. 4, uk. 62, Hadithi 1; Ibn Shu'ba, Tuhaf al-Uqul, uk. 258.
  17. ↑ Kulayni, Al-Kafi, jz. 2, uk. 510.
  18. ↑ Rawandi, Al-Da'wat, jz. 1, uk. 27.
  19. ↑ Payandeh, Nahj al-Fasaha, uk. 547, Hadithi 1854.
  20. ↑ Tabarsi, Makarim al-Akhlaq, uk. 51.
  21. ↑ Kulayni, Al-Kafi, jz. 4, uk. 62.
  22. ↑ Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, jz. 2, uk. 75, Hadithi 1773.
  23. ↑ Nuri, Mustadrak al-Wasa'il, jz. 7, uk. 400.
  24. ↑ Jawadi Amuli, Tafsir Tasnim, jz. 9, uk. 288.
  25. ↑ «NASAHA: Ramadhani ni fursa ya kuzitakasa nafsi zetu na kuacha maasi». Tovuti ya Taifa Leo.
  26. ↑ Ridha'i, «روزه‌داری و سلامت از نگاه پزشکی» Kituo cha Utoaji Habari cha Hawzah.
  27. ↑ Ridha'i, «روزه‌داری و سلامت از نگاه پزشکی» Kituo cha Utoaji Habari cha Hawzah.
  28. ↑ Tazama: Tabataba'i, Al-Mizan, jz. 2, uk. 7 na 8.
  29. ↑ Tazama: Kitabu سفر خروج (Sifre Khuruj), sura ya 34, Aya ya 28; Kitabu cha Pili cha Samweli, Sura ya 12, Aya ya 16; Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati, Sura ya 20, Aya ya 3.
  30. ↑ Injili ya Luka, sura ya 2, Aya ya 37; Sura ya 4, Aya ya 2; na Sura ya 5, Aya ya 34.
  31. ↑ Kitabu cha Sifr Tathniye (Kumbukumbu la Torati), Sura ya 9, Aya ya 9.
  32. ↑ Tazama: Tabataba'i, Al-Mizan, jz. 2, uk. 7.
  33. ↑ Surah Maryam, aya ya 26.
  34. ↑ Kwa mfano tazama: Majlisi, Bihar al-Anwar, jz. 13, uk. 427 na jz. 17, uk. 292.
  35. ↑ Tazama: Tabataba'i, Al-Mizan, jz. 2, uk. 7.
  36. ↑ Qumi, Waqayi' al-Ayyam, uk. 495.
  37. ↑ Ya'qubi, Tarikh Ya'qubi, Dar Sadir, jz. 2, uk. 42.
  38. ↑ Surat al-Baqarah, aya ya 183-185 na 187.
  39. ↑ Tabarsi, Jawami' al-Jami', Jami'at al-Mudarrisin, jz. 1, uk. 106; Hurr Amili, Wasa'il al-Shia, jz. 7, uk. 81.
  40. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, jz. 3, uk. 658.
  41. ↑ Naraqi, Tadhkirat al-Ahbab, uk. 104.
  42. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, jz. 3, uk. 661-663.
  43. ↑ Naraqi, Tadhkirat al-Ahbab, uk. 104.
  44. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, jz. 3, uk. 660-661.
  45. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, jz. 3, uk. 658-660.
  46. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), 1419 AH, jz. 3, uk. 541-577; Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 891.
  47. ↑ Muassasat Da'irat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhange Fiqh Farsi, 1385 SH, jz. 4, uk. 171 na 172.
  48. ↑ Imamu Khomeini, Taudhihu al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 955, suala la 1725.
  49. ↑ Imamu Khomeini, Taudhihu al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 956, suala la 1727.
  50. ↑ Imamu Khomeini, Taudhihu al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 957-958, masuala 1728 na 1729.
  51. ↑ Imamu Khomeini, Istifta'at, jz. 1, uk. 333, suala la 88; «نظر مراجع عظام تقلید پیرامون روزه‌داری با ضعف جسمانی», Shirika Rasmi la Habari la Hawzah.
  52. ↑ Imamu Khomeini, Taudhihu al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 951, masuala 1714 na 1723.
  53. ↑ Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 701.
  54. ↑ Muassasat Da'irat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhange Fiqh Farsi, 1385 SH, jz. 1, uk. 624.
  55. ↑ Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 880.
  56. ↑ Hurr Amili, Wasa'il al-Shia, 1409 AH, jz. 10, uk. 147-151.
  57. ↑ Hurr Amili, Wasa'il al-Shia, 1409 AH, jz. 10, uk. 156-161.
  58. ↑ Tazama: Kulayni, Al-Kafi, 1407 AH, jz. 4, uk. 68 na 69; Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 AH, jz. 2, uk. 134 na 135.
  59. ↑ Saduq, Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), 1378 AH, jz. 1, uk. 296.
  60. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), 1419 AH, jz. 3, uk. 635-637; Imamu Khomeini, Tahrir al-Wasila, Dar al-Ilm, jz. 1, uk. 298.
  61. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), 1419 AH, jz. 3, uk. 639; Imamu Khomeini, Tahrir al-Wasila, Dar al-Ilm, jz. 1, uk. 298.
  62. ↑ Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), 1419 AH, jz. 3, uk. 640 na 641; Imamu Khomeini, Tahrir al-Wasila, Dar al-Ilm, jz. 1, uk. 299.
  63. ↑ Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 926; Muassasat Da'irat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang-e Fiqh Mutabiq-e Maktab-e Ahl al-Bayt Alayhim al-Salam, 1385 SH, jz. 4, uk. 169.
  64. ↑ Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 928 na 929; Imamu Khomeini, Tahrir al-Wasila, Dar al-Ilm, jz. 1, uk. 289.
  65. ↑ Imamu Khomeini, Tahrir al-Wasila, Dar al-Ilm, jz. 1, uk. 298.
  66. ↑ Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il, 1426 AH, uk. 344.
  67. ↑ Sistani, Taudhih al-Masa'il, 1393 SH, uk. 298-299.
  68. ↑ Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa, 1420 AH, jz. 3, uk. 521.
  69. ↑ Ansariyan, Irfan Islami, 1386 SH, jz. 6, uk. 272.
  70. ↑ Ansariyan, Irfan Islami, 1386 SH, jz. 6, uk. 272.
  71. ↑ Ansariyan, Irfan Islami, 1386 SH, jz. 6, uk. 272.
  72. ↑ Ansariyan, Irfan Islami, 1386 SH, jz. 6, uk. 272.
  73. ↑ Tamimi Amidi, Ghurar al-Hikam wa Durar al-Kalim, 1410 AH, uk. 423.
  74. ↑ Ibn Abi al-Hadid, Sharh Nahj al-Balagha, 1404 AH, jz. 20, uk. 299, Hadithi 417.
  75. ↑ Kulayni, Al-Kafi, 1407 AH, jz. 4, uk. 87.
  76. ↑ Tamimi Amidi, Ghurar al-Hikam wa Durar al-Kalim, 1410 AH, uk. 423, Hadithi 80.

Tanbihi

  1. ↑ Kwa mujibu wa baadhi ya tafsiri, makusudio ya funga ya Zakariya na Maryam katika Qur'ani ni funga ya kunyamaza kimya. (Allamah Tabataba'i, Al-Mizan, Chapa ya Ismailiyan, jz. 2, uk. 7.)
  2. ↑ Makruhu hapa inamaanisha kupata thawabu chache. (Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), jz. 3, uk. 521).
  3. ↑ Baadhi ya maraaji'i kama Shubairi na Sistani hawaoni kuzamisha kichwa ndani ya maji kuwa kunabatilisha funga, bali wanaona kuwa ni haramu au makruhu. (Tazama: Tabataba'i Yazdi, Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha), 1419 AH, jz. 3, uk. 555; Imamu Khomeini, Taudhih al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 891.)
  4. ↑ Makusudio ya msafiri kisheria ni yule ambaye masafa ya safari yake ni angalau ni jumla ya farsakh nane (kilomita 41, kwenda na kurudi); (Imamu Khomeini, Taudhihu al-Masa'il (Muhashsha), 1424 AH, jz. 1, uk. 684, suala la 1272).

Vyanzo

  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf bin Mutahhar. Tadhkirat al-Fuqaha. Qum: Muassasat Al al-Bayt (a.s), Chapa ya Kwanza, ۱۴۱۴Q/1993M.
  • «NASAHA: Ramadhani ni fursa ya kuzitakasa nafsi zetu na kuacha maasi». Tovuti ya Taifa Leo, Tarehe ya Kuwekwa: 20 May 2019, Imetembelewa: 12 Septemba 2026.
  • Ansariyan, Husayn. Irfan Islami. Qum: Dar al-Irfan, ۱۳۸۶H/2007M.
  • Ayyashi, Muhammad bin Mas'ud. Tafsir Ayyashi. (Usahihishaji: Sayyid Hashim Rasuli Mahallati). Tehran: Al-Maktabat al-Ilmiyya, Chapa ya Kwanza, ۱۳۸۰Q/1959M.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hasan. Hidayat al-Ummah ila Ahkam al-A'immah. Taasisi ya Utafiti ya Astan Quds Radhawi, ۱۴۱۲Q/1991M.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hasan. Wasa'il al-Shia. Qum: Muassasat Al al-Bait (a.s), ۱۴۰۹Q/1988M.
  • Ibn Abi al-Hadid. Sharh Nahj al-Balagha. Utafiti: Muhammad Abu al-Fadhl Ibrahim. Qum: Maktabat Ayatullah al-Mar'ashi al-Najafi, Chapa ya Kwanza, ۱۴۰۴Q/1984M.
  • Ibn Shu'ba, Hasan bin Ali. Tuhaf al-Uqul. Qum: Muassasat al-Nashr al-Islami, ۱۳۶۳H/1984M.
  • Imamu Khomeini, Sayyid Ruhullah. Istifta'at. Qum: Daftar Nashr Islami, Bita.
  • Imamu Khomeini, Sayyid Ruhullah. Tahrir al-Wasila. Qum: Dar al-Ilm, Chapa ya Kwanza.
  • Imamu Khomeini, Sayyid Ruhullah. Taudhih al-Masa'il (Muhashsha). Utafiti na Usahihishaji: Sayyid Muhammad Husayn Bani Hashimi Khomeini. Qum: Daftar Intisharat Islami, Chapa ya Nane, ۱۴۲۴Q/2003M.
  • Imamu Sadiq (kimenasibishwa). Misbah al-Shari'a. Beirut: A'lami, Chapa ya Kwanza, ۱۴۰۰Q/1979M.
  • Jawadi Amuli, Abdullah. Tafsir Tasnim. Qum: Intisharat Israa, Chapa ya Tatu, ۱۳۸۹H/2010M.
  • Kulayni, Muhammad bin Ya'qub. Al-Kafi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyya, Chapa ya Nne, ۱۴۰۷Q/1986M.
  • Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, Chapa ya Pili, ۱۴۰۳Q/1983M.
  • Meshkini, Ali. Mustalahat al-Fiqh. Utafiti: Hamid Ahmadi Julfayi. Qum: Muassasa Ilmi wa Farhangi Dar al-Hadith, ۱۳۹۲H/2013M, ۱۴۳۴Q/2013M.
  • Muassasat Da'irat al-Ma'arif Fiqh Islami. Farhang-e Fiqh Mutabiq-e Maktab-e Ahl al-Bayt Alayhim al-Salam. Qum: Muassasa Da'irat al-Ma'arif Fiqh Islami, Chapa ya Pili, ۱۳۸۵H/2006M.
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hasan. Shara'i' al-Islam fi Masa'il al-Halal wa al-Haram. Qum: Ismailiyan, Chapa ya Pili, ۱۴۰۸Q/1987M.
  • Najafi, Muhammad Hasan. Jawahir al-Kalam fi Sharh Shara'i' al-Islam. Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, Chapa ya Saba, ۱۴۰۴Q/1984M.
  • Nuri, Mirza Husayn. Mustadrak al-Wasa'il. Qum: Muassasat Al al-Bayt (a.s), Chapa ya Kwanza, ۱۴۰۸Q/1987M.
  • Payandeh, Abu al-Qasim. Nahj al-Fasaha. Qum: Dar al-Ilm, ۱۳۸۷H/2008M.
  • Qumi, Ali bin Ibrahim. Tafsir Qumi. Usahihishaji: Tayyib Musawi Jaza'iri. Qum: Dar al-Kitab, Chapa ya Tatu, ۱۴۰۴Q/1984M.
  • Rawandi, Qutb al-Din. Al-Da'wat. Madrasat al-Imam al-Mahdi (a.t.f.s), ۱۳۶۶H/1987M.
  • Ridha'i, Ali. «روزه‌داری و سلامت از نگاه پزشکی» (Kufunga na Afya kwa Mtazamo wa Kitabibu). Kituo cha Utoaji Habari cha Hawzah. Imewekwa: Agosti 2004. Imetembelewa: 7 Septemba 2026.
  • Saduq, Muhammad bin Ali. Man La Yahdhuruhu al-Faqih. Utafiti: Ali Akbar Ghaffari. Qum: Daftar Intisharat Islami, Chapa ya Pili, ۱۴۱۳Q/1992M.
  • Saduq, Muhammad bin Ali. Uyun Akhbar al-Ridha (a.s). Utafiti: Mahdi Lajwardi. Tehran: Nashr-e Jahan, Chapa ya Kwanza, ۱۳۷۸Q/1958M.
  • Suri Laki, Husayn. «فلسفه وجوب روزه» (Falsafa ya Kuwajibishwa kwa Funga). Jarida la Pasdar-e Islam, Namba 228, Azar ۱۳۷۹H/2000M. Imetembelewa: Septemba 12, 2026
  • Tabarsi, Hasan bin Fadhl. Jawami' al-Jami'. Utafiti: Muassasa Nashr Islami. Qum: Jami'at al-Mudarrisin.
  • Tabarsi, Hasan bin Fadhl. Makarim al-Akhlaq. Qum: Intisharat Sharif Radhi, Chapa ya Nne, ۱۴۱۲Q/1991M.
  • Tabataba'i Yazdi, Sayyid Muhammad Kadhim. Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha) Jz. 1. Qum: Daftar Intisharat Islami, Chapa ya Kwanza, ۱۴۱۹Q/1998M.
  • Tabataba'i Yazdi, Sayyid Muhammad Kadhim. Al-Urwatu al-Wuthqa (Muhashsha) Jz. 3. Qum: Daftar Intisharat Islami, Chapa ya Kwanza, ۱۴۲۰Q/1999M.
  • Tabataba'i, Sayyid Muhammad Husayn. Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an. Qum: Daftar Nashr Islami.
  • Tabataba'i, Sayyid Muhammad Husayn. Ta'alim-e Islam. Ukusanyaji: Hadi Khusrowshahi. Qum: Intisharat Bustan-e Kitab, ۱۳۸۷H/2008M.
  • Tamimi Amidi, Abdulwahid bin Muhammad. Ghurar al-Hikam wa Durar al-Kalim. Usahihishaji: Sayyid Mahdi Raja'i. Qum: Dar al-Kitab al-Islami, Chapa ya Pili, ۱۴۱۰Q/1989M.
  • Tusi, Muhammad bin Hasan. Al-Amali. Qum: Dar al-Thaqafa, Chapa ya Kwanza, ۱۴۱۴Q/1993M.
  • Ya'qubi, Ahmad bin Ishaq. Tarikh Ya'qubi. Beirut: Dar Sadir, Bita.
  • «کاهش ۵ تا ۳۳ درصدی جرایم در ماه رمضان» (Kupungua kwa Asilimia 5 hadi 33 ya Uhalifu Mwezi wa Ramadhani). Shirika la Habari la Aftab. Imewekwa: 17 Julai 2013. Imetembelewa: 7 Septemba 2026.
  • «نظر مراجع عظام تقلید پیرامون روزه‌داری با ضعف جسمانی» (Maoni ya Maraji'i Kuhusu Kufunga kwa Udhaifu wa Mwili). Shirika Rasmi la Habari la Hawzah. Imewekwa: 7 Julai 2014. Imetembelewa: 7 Septemba 2026.
  • «نقش روزه در تعالی انسان از منظر عرفان اسلامی» (Nafasi ya Funga katika Kuinuka kwa Mwanadamu kwa Mtazamo wa Irfani ya Kiislamu). Tovuti ya Shirika la Habari la Shabestan. Imewekwa: 27 Aprili 2022. Imetembelewa: 7 Septemba 2026.
  • «Fasting» (Funga). Encyclopedia Iranica. Imewekwa: 15 Desemba 1999. Imetembelewa: 7 Septemba 2026.

Viungo vya Nje