Kubakia na janaba
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Kubakia na janaba (البقاء على الجنابة) maana yake ni kuchelewesha kuoga janaba mpaka wakati wa adhana ya alfajiri (kuchomoza alfajiri). Wanazuoni wa fiq'h wanaamini kwamba, mukallaf (mtu anayepaswa kutekeleza ibada kwa mujibu wa sheria) hapaswi kuchelewesha kuoga janaba mpaka adhana ya asubuhi katika usiku wa mwezi wa Ramadhani au usiku mwingine wowote ambao kesho yake ameazimia kufunga kadha ya Saumu ya mwezi wa Ramadhani.
Mafakihi wanasema kuwa, Saumu ya mtu ambaye ndani ya mwezi wa Ramadhani au Swaumu ya Kadhaa (alibakia na janaba kwa makusudi au kwa kusahau) mpaka kufikia adhana ya asubuhi haisihi na wanaamini kuwa, inapaswa kulipa kadha ya siku hiyo.
Kadhalika wanasema, kubakia na janaba mpaka adhana ya asubuhi katika Saumu za mustahabu na Saumu zingine za wajibu kama Saumu ya kafara hakupelekei kubatilika Saum; lakini kwa mujibu wa Ihtiyat wajib (Tahadjhari ya Wajibu) haipasi kubakia na janaba kwa makusudi mpaka adhana ya asubuhi.
Fat'wa ya mafakihi inasema, mtu ambaye amepata janaba au amejiotea (kutokwa na manii usingizini) katika mwezi wa Ramadhani na anajua kwamba, kama atalala hatoweza kuamka mpaka asubuhi, hapaswi kulala pasi na kufanya ghusli na kama atalala na kisha asiamke mpaka asubuhi, Saumu yake itabatilika na anapaswa kulipa kadhaa na kutoa kafara; lakini kama amenuia na kukukusudia kwamba, baadaye ataamka kabla ya adhana ya asubuhi na kufanya ghusli lakini akapitiwa na usingizi, Saumu yake itakuwa sahihi.
Utambuzi wa maana
Kubakia na janaba maana yake ni kuchelewesha kuoga josho la janaba katika usiku wa mwezi wa Ramadhani mpaka kufikia adhana ya alfajiri au usiku wowote ule ambao kesho yake mukallaf amekusudia kufunga Swaum.
Hukumu ya kifikihi ya kubakia na janaba
Kuhusiana na Saum ya mwezi wa Ramadhani na kulipa kadha ya mwezi wa Ramadhan, akthari ya mafakihi wanaona kuwa ni wajibu kwa mtu mwenye janaba ajiepushe kubakia na janaba mpaka mpaka adhana ya asubuhi [2] na Saumu ya mtu ambaye amebakia na janaba kwa makusudi mpaka adhana ya asubuhi ni batili. [3] Kadhalika kama mtu jukumu lake ni kutayamamu na kisha asifanye hivyo, Saumu yake ni batili. [4]
Baadhi ya mafakihi kama Tabatabai Yazdi na Imamu Khomeini wanasema, kama mtu atabakia na janaba mpaka adhana ya asubuhi kwa kusahahu, basi Saumu yake inabatilika’ [5] lakini kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni na mafakihi wengine akiwemo Makarim Shirazi, kama mtu atabakia na janaba mpaka adhana ya asubuhi kwa kusahahu, Saumu yake itasihi. [6]
Kwa mujibu wa mafakihi ni kuwa, kuhusiana na Saumu zingine za wajibu (zisizokuwa na mwezi wa Ramadhan na kadhaa ya mwezi wa Ramadhani) hakuna dalili na hoja madhubuti iliyonukuliwa inayobainisha wajibu wa kuoga janaba kabla ya adhana ya asubuhi ili kuifanya Saumu isihi; [7] lakini wamesema kuwa, kwa mujibu wa Tadhahari ya Wajibu haipasi kubakia na janaba kwa makusudi mpaka adhana ya asubuhi. [8]
Kwa mujibu wa mtazamo mashuhuri baina ya mafakihi ni kwamba, katika Saumu za mustahabu kubakia na janaba mpaka adhana ya asubuhi hakubatilishi Saumu. [9]
Hukumu ya kulala baada ya kuwa na janaba au kujiotea
Kuna hukumu mbalimbali zilizobainishwa kuhusiana na kubakia na janaba kwa sababu ya mtu kupitiwa na usingizi katika usiku wa mwezi wa Ramadhani au kujiotea. Miongoni mwazo ni:
- Saumu ya mtu ambaye amepata janaba kisha akalala mpaka asubuhi bila ya kuwa na nia ya kuoga janaba anahesabiwa kuwa sawa na mtu aliyebakia na janaba kwa makusudi (yaani Saumu yake inabatilika na ni wajibu kwake kulipa kadhaa na kutoa kafara); [10] lakini kama alitia nia kwamba, baadaye ataamka (kabla ya adhana ya asubuhi) ili aoge janaba, na kisha akapitiwa usingizi, Saumu yake inasihi. [11]
- Mtu ambaye amepata janaba katika usiku wa mwezi wa Ramadhani na anafahamu kwamba, kama atalala, hawezi kuamka mpaka asubuhi, ikiwa atalala na asiamke mpaka asubuhi, Saumu yake inabatilika na ni wajibu kwake kulipa kadha na kutoa kafara. [12] Kwa mujibu wa mtazamo wa Marajii Taqlidi ni kwamba, anapaswa kukamilisha Saumu yake lakini wakati huo huo ni wajibu kwake kulipa kadha na kutoa kafara. [13]
- Kama mukallaf atapitiwa na usingizi lakini ni baada ya kuamka na kisha kulala mara mbili, hata kama atakuwa alitia nia ya kuoga janaba, Saumu yake inabatilika. [14] Sheikh Tusi anaamini kuwa, kafara ni wajibu kwake pia. [15]
- Kwa mujibu wa fatwa ya Imamu Khomeini, kama mtu atapata janaba usiku, kisha akaamka mara tatu na akalala bila ya kuoga janaba na kisha asiamke mpaka adhana yua asubuhi, anapaswa kulipa kadha ya siku hiyo tu na siku jukumu kwake kuto akafara. [16]
- Kwa mujibu wa mtazamo wa Imamu Khomeini makusukio ya kulala mara ya kwanza ni kulala ambako aliyejiotea analala tena baada ya kuwa ameamka. Hata hivyo Ayatullah Sistani anaona kuwa, usingizi ambao ndani yake mtu amejiotea ndio kulala kwa mara ya kwanza au usingizi wa kwanza. [17]