Nenda kwa yaliyomo

Abdallah Jawadi Amoli

Kutoka wikishia
Ayatullah Abdallah Jawadi Amuli

Abdallah Jawadi Amuli (Kiarabu: عبد الله جوادي الآملي)(alizaliwa 1933) ni mwanafalsafa, faqihi, mfasiri wa Qur’an, mhadhiri wa Chuo kikuu cha kidini katika mji wa Qom (Hawza)-Iran na mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia. Yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Ayatullah Borujerdi, Imamu Khomeini na Allama Tabatabai na amefundisha kwa takribani miaka 60 masomo mbalimbali ya vyuo vya kidini katika miji ya Tehran na Qom kama falsafa, irfan, fiq’h na tafsiri. Jawadi Amuli ameandika vitabu vingi ambapo Tafsiri ya Tasnim na ar-Rahiq al-Makhtum (sherh ya al-Asfar al-Arba'a) ni miongoni mwa vitabu hivyo.

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Sheikh Jawadi Amuli alishika nyadhifa mbalimbali kama mjumbe katika Baraza kuu la Mahakama, Baraza la Wanazuoni Wataalamu wa Sheria na katiba, Jumuiya ya walimu (Jami' modarrisin) wa Hawza Qom, na Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu na kusimamia kazi zake. Pia, alikuwa Khatibu na Imamu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Qom katika muongo wa 70 na 80. Mnamo mwaka wa 1989, alifanya safari katika uliokuwa Muungano wa Sovieti kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Imam Khomeini kwa Mikhail Gorbachef, kiongozi wa wakati huo wa nchi hiyo.

Katika falsafa Jawadi Amuli ni mfuasi wa nidhamu na mfumo wa falsafa wa Mulla Sadr unaojulikana kama (Hekmat al-Muta'aliya). Anakubali kuwepo kwa elimu ya dini katika uwanja wa elimu ya ubinadamu (inayohusu binadamu na mahitaji yake au humanities) na jarabati. Baadhi ya Fat’wa zake tofauti ni: Kuruhusu wanawake kumkalidi na kumfuata Marjaa mwanamke, kuruhusu kubadilisha jinsia na kwamba Ahlul-Kitab sio najisi bali ni tohara.

Maisha yake

Abdallah Jawadi Amuli alizaliwa mwaka 1933 katika mji wa Amul-Iran. [1] Baba yake alikuwa mmoja wa Maulamaa wa mji huo. .[2] Mnamo mwaka wa 1946, alianza kusoma masomo ya dini katika Hawza ya Amul na katika miaka mitano alisoma fasihi ya lugha ya Kiarabu, mantiki, Usul al-Fiq’h, Fiqhi, tafsiri ya Qur’an na hadithi katika ngazi ya kati ya uwanja huo.[3]

Mnamo mwaka 1950, alikwenda Tehran na akaendelea kusoma elimu mbalimbali za dini na kwa miaka mitano alisoma katika shule ya Marvi. Katika muda huu, alihudhuria darsa na masomo ya Muhammad Taqi Amuli, Abul-Hassan Sha'arani, Mahdi Elahi Qomshaei na Muhammad Hussein Tuni. Pamoja na elimu ya fiq’h na usul, alikuwa akisoma pia falsafa na irfani na wakati huohuo, alijishughulisha na kufundisha masomo ya Hawza. [4] Alienda kwenye chuo kikuu cha dini cha Qom (Hawza) mwaka wa 1955 na akashiriki masomo ya ngazi za juu kwa wanazuoni kama vile Ayatullah Boroujerdi, Ayatullah Sayyid Muhammad Moqqiq Damad, Mirza Hashim Amuli, Imam Khomeini na Allama Tabatabai. [5]

Kufundisha

Kitabu cha Tafsiri Tasnim

Jawadi Amuli alianza kufundisha masomo ya Hawza tangu alipokuwa kijana mdogo na ni wakati alipokuwa akisoma katika Chuo cha Kidini cha Tehran.[6] Alianza kufundisha masomo mbalimbali ya Hawza tangu kipindi alipoanza kuishi Tehran. Katika faili lake la ufundishaji kuna miaka takribani 60 ya tajiriba ya kufundisha masomo mbalimbali kama fiq’hi, falsafa, irfan na tafsiri ya Qur'an. Katika kipindi hiki, amefundisha mara tatu kitabu cha al-Asfar al-Arba'a cha Mulla Sadra katika chuo kikuu cha kidini cha Qom. [7] Masomo yake ya Tafsir alianza kuyafundisha tangu 1976. .[8] Mafunzo ya tafsir ya Jawadi Amuli na darsa ya kharij ya fikihi (masomo ya juu kabisa ya fikihi yanafanyika katika Msikiti A’dham Qom. [9]

Wanafunzi

Katika miaka mingi ya kufundisha ya Ayatullah Jawadi Amuli - zaidi ya miaka 55 - maelfu ya watu wamefaidika na masomo yake; ikiwa ni pamoja na:

  1. Mahdi Shabzendedari, [10]
  1. Sayyid Muhammad Reza Modarresi Yazdi, [11]
  2. Ghulam Reza Fayazi,
  3. Abdul-Hussein Khosropanah,
  4. Hamid Parsaniya,
  5. Mahdi Hadavi Tehrani.

Umarjaa

Ofisi za Marjaa Jawadi Amuli zimefunguliwa katika miji mbalimbali ya Iran kama Qom, Tehran, Shahr Rey, Tabriz, Orumieh, Zanjan, Amol na Shiraz. [12] Kitabu chake cha fat’wa na sheria za Kiislamu pia kimesambazwa.

Fikra

Baadhi ya wanafunzi Jawadi Amuli wanaamini kuwa, mhimili wa kifikra wa mwanazuoni huyu ni nidhamu na mfumo wa kifalsafa wa Hekmatul al-Muta'aliya (ambao ni wa Mulla Sadra). Kwa hiyo, yeye anaamini juu ya kuweko uratibu baina ya akili, irfani na Qur'an, na haoni kama maarifa yao yana hali ya kukinzana. [13] Kwa mtazamo wake ni kuwa, akili haipingi dini; bali ni nuru ya dini na inaweza kutumika kuelewa mafundisho ya kidini na kimaadili na sheria za kifiq’h na kisheria za dini. [14]

Elimu ya Dini

Jawadi Amuli anaamini umuhimuu wa elimu ya dini. Katika fikra na mtazamo wake makusudio ya akili, sio akili ya kinadharia tu; inajumuisha pia "akili ya jarabati” kwa muktadha huo, elimu jarabati inajumuisha sayansi asilia na elimu ya ubinadamu (humanities). [15] Anasema: Elimu katika dhati yake yenyewe haipingani na dini. [16] Elimu jarabati zinatuonyesha ulimwengu wa asili na kwa sababu ulimwengu huu umeumbwa na Mwenyezizi Mungu, elimu hizi zinatuonyesha matendo ya Mungu. Kwa hiyo, elimu hizi zinapaswa kuchukuliwa kuwa za kidini. [17]

Kupitia ujengeaji hoja huu, anatoa natija kwa kusema, ikiwa elimu itakuwa ni elimu ya kweli basi haiwezi kuwa isiyo ya kidini na isiyoamini Mungu. [18]

Fikra za Kisiasa

Jawadi Amuli ni miongoni mwa wanaoamini nadharia ya Wilayat al-Faqih (uongozi wa faqih au uongozi wa mwanachuoni). Katika kitabu chake cha: Velayat Faqih; Velayat Faqahat va Adalat” ametoa dalili kuu tatu za kuthibitisha Wilayat al-Faqih. [19] Hoja hizo ni "Aqli Mahdh", inayoundwa na "akili na nakili" (hadithi) na "Naqli Mahdh". Hoja yake kuundwa akili na nakili ni hii kwamba, katika Uislamu kuna hukumu na sheria za kijamii na kisiasa kama Hija, [20], Jihad, [21] hudud (adhabu) na Taazirat (makosa ambayo katika Uislamu adhabu zake hazijaanishwa na jukumu hilo lipo mikononi mwa mtawala wa kisheria) [22] na sheria za kimali mithili ya anfal na khumsi [23] ambazo utekelezaji wake katika kipindi cha Ghaiba ya Maasumu unatimia tu kwa usimamizi na uongozi wa Faqihi aliyetimiza masharti. [24] Kwa upande mwingine akili inahukumu kwamba, Mwenyezi Mungu katika kipindi cha Ghaiba ya Maasumu hawezi kuiacha jamii ya Kiislamu bila ya msimamizi. Mintarafu hiyo, katika zama hizi, mafakihi waliotimiza masharti wana jukumu la uongozi wa jamii kwa anuani ya viongozi badala ya Imamu Maasumu. [25]

Fat’wa Maalumu

Katika kitabu cha Tawdhih al-Masail (ufafanuzi wa sheria za Kiislamu) cha Ayatullah Jawadi Amuli, tofauti na vitabu vingine vya ufafanuzi wa hukumu za Kiislamu, kuna maudhui kama vile makundi, uchaguzi, kuandika Qur'an kwa maji ya dhahabu, haki za uandishi na uchapishaji, utoaji wa haki ya kukopa, malipo ya deni kulingana na mfumuko wa bei, kubadilisha jinsia, maombolezo, msaada na utoaji huduma katika ajali na hukumu za Ahlul-Kitab ambazo zimezungumziwa na kuja katika kitabu hiki.[26]

Miongoni mwa fat’wa zake tofauti na za kipekee ni: Kuruhusu wanawake kumkalidi na kumfuata Mujtahidi mwanamke ambaye ni msomi zaidi, [27] kujuzu na kufaa kubadilisha jinsia [28] na kuwa na itibari haki ya kuchapisha, tarjuma, usambazaji na uzalishaji na utengenezaji wa programu ya kompyuta. [29]

Harakati za Kisiasa na Kijamii

Uwasilishaji wa ujumbe wa Imam Khomeini kwa Gorbachef, kiongozi wa mwisho wa zamani wa Usovieti, na Ayatullah Jawadi.

Ingawa harakati za kielimu ndizo zilizogubika shughuli jumla za Jawadi Amuli, katika miaka ya kabla na baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, lakini alishiriki pia katika shughuli za kisiasa na kijamii. Kabla ya mapinduzi, alikuwa mmoja wa wasambazaji wa fikra za Imam Khomeini, na kwa sababu hii, alipigwa marufuku mara kadhaa kuhubiri na kuhutubia kama ambavyo pia alitiwa mbaroni na kushikiliwa mara kadhaa. [30] Kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Mahakama, [31] kuandaa miswada ya mahakama, [32] kuwa mjumbe katika duru mbili kwenye Baraza la wataalamu linalomchagua kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusimamia kazi zake na ujumbe katika Jumuiya ya walimu wa Hawza ya Qom (Jami' Modarresin) ni miongoni mwa harakati zake baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [33]

Mwaka 1997 Jawadi Amuli baada ya hotuba ya Ayatullah Monzateri alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokusanyika katika msikkiti wa A'dham Qom kulalamikia hotuba hiyo. [34] Aidha mwaka 2000 alihutubia watu waliofanya mgomo wa kuketii kulalamikiai kuchapishwa katuni na kibonzo kilichokuwa kikimvunjia heshima Ayatullah Misbah Yazdi. Katika hotuba yake hiyo, Ayatullah Jawadi Amuli alikosoa sera za kiutamaduni za serikali ya wakati huo ya Iran. [35]

Katika muongo wa 70 na 80 Hijiria Shamsia, Jawadi Amuli alikuwa mmoja wa makhatibu na Maimamu wa Sala ya Ijumaa katika mji wa Qum. [36] Alijiuzulu wadhifa huo mwaka 2009.[37]

Safari ya Umoja wa Kisovieti na Marekani

Mnamo mwaka wa 1989, Jawadi Amuli, pamoja na Muhammad Javad Larijani na Marzieh Hadidachi (Dabbagh) [38], alipewa jukumu la kuwasilisha ujumbe wa Imam Khomeini kwa Mikhail Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Muungano wa Sovieti, na kumsomea ujumbe huo. [39] Baada ya safari hiyo, Ayatullah Javadi Amuli aliandika maelezo na ufafanuzi kuhusu ujumbe wa Imam Khomeini ambao aliupa jina la "Sauti ya Tawhidi" na akautoa kama zawadi kwa baadhi ya viongozi wa kidini wa nchi za Ulaya. [40] Mwaka 2000 Jawadi Amuli alifanya safari New York Marekani kwa ajili ya kwenda kusoma ujumbe wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran katika kongamano la Dini la Milenia.[41]

Kituo cha Esra na Taasisi ya Imamu Hassan Askary (a.s)

Taasisi ya Esra International Foundation of Revelatory Sciences ni moja vituo vya kielimu katika mji wa Qom Iran ambacho kinaendeshwa chini ya usimamizi wa Ayatullah Jawadi Amuli. Lengo la kituo hikii ni kubainisha na kueneza elimu za Uislamu kwa mtazamo wake na vilevile kutoa mafunzo na kozi kwa watafiti wa elimu hizi. [42] Jawadi Amuli pia ni Msimamizi wa Kituo cha Mafunzo ya juu ya Hawza cha Imamu Hasssan Askary (a.s) ambacho kilianzishwa 1387 Hijria Shamsia. [43]

Athari

Makala Kuu: Orodha ya athari za Ayatullah Jawadi Amuli

Jawadi Amuli ameandika vitabu katika nyanja mbalimbali kama vile fiq'h, tafsiri, falsafa na hadithi. Kituo cha Kifalme cha Jordan cha Mafunzo ya Kimkakati kimeorodhesha zaidi ya makala na vitabu 300 vya Jawadi Amuli. [44] Kitabu chake cha tafsiri ambacho ni matokeo ya darsa zake za tafsiri kinaitwa Tasnim [45] na juzuu zake 62 zimechapishwa hadi kufikia Juni 2022. [46]

Kitabu chake kingine ni ar-Rahiq al-Makhtoum ambacho ni natija ya duru ya tatu ya kufundisha kitabu cha al-Asfar Arba'a kilichoandikwa na Mulla Sadra [47], ambapo hadi kufikia mwaka 2021 juzuu yake ya 35 ilikuwa imechapishwa. [48]

Mafatih al-Hayat, Zan dar ayine-yi jamal wa jalal, Shari'a dar Ayine Maarifat, Adab dar Fanay Moqaraban (ufafanuzi wa ziara ya Jami'at al-Kabira) na Tawdhih al-Masail (ufafanuzi wa sheria za Kiislamu) ni miongoni mwa vitabu vingine vya Jawadi Amuli.

Athari teule

Kitabu cha Din Shenasi (kutambua dini) kiliteuliwa na majaji kama mojawapo ya kazi teule katika Kongamano la 5 la Kitabu cha Mwaka cha Hawza lililofanyika mwaka wa 2002. [49]. Kitabu cha Hayat Haqiqi Insan Dar Qur'an (Maisha ya Kweli ya Mwanadamu katika Qur'an) nacho kilikuwa miongoni mwa athari bora za mwaka katika kongamano la sita kitabu cha mwaka cha Hawza la mwaka uliofuata. [50]

Kitabu cha Tahreer Iqaz al-Na'imi kilichaguliwa na majaji kama mojawapo ya kazi bora na teule za mkutano huo katika Kongamano la 18 la kitabu cha mwaka cha Hawza. [51]

Rejea

  1. «زندگی‌نامه حضرت آیة الله جوادی آملی از زبان خودشان»، وبگاه پایگاه اطلاع‌رسانی حوزه.
  2. «زندگی‌نامه حضرت آیة الله جوادی آملی از زبان خودشان»، وبگاه پایگاه اطلاع‌رسانی حوزه.
  3. Bandali, Mehr Ostad, 1391, uk.37.
  4. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء.
  5. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء.
  6. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء.
  7. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین‌المللی علوم وحیانی اسراء.
  8. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء.
  9. «برنامه دروس آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه پایگاه اطلاع‌رسانی حوزه.
  10. «شب‌زنده‌دار کیست؟»، خبرگزاری فارس.
  11. «زندگی‌نامه حضرت حجه الاسلام والمسلمین سید محمد رضا مدرسی یزدی»، سایت جامعه مدرسین حوزه علمیه قم.
  12. «دفاتر آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین‌المللی علوم وحیانی اسراء.
  13. مصطفی‌پور، «منظومه فکری آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه پژوهشگاه معارج.
  14. Waazi, "Sayansi ya kidini kwa mtazamo wa Ayatollah Javadi Amuli", uk.10.
  15. Waazi, "Sayansi ya kidini kwa mtazamo wa Ayatollah Javadi Amuli", uk. 11 na 12.
  16. Waazi, "Sayansi ya kidini kwa mtazamo wa Ayatollah Javadi Amuli", p. 15.
  17. Waazi, "Sayansi ya kidini kwa mtazamo wa Ayatollah Javadi Amuli", p. 16.
  18. Waazi, "Sayansi ya kidini kwa mtazamo wa Ayatollah Javadi Amuli", uk. 16.
  19. Angalia Javadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, uk. 150-184.
  20. Angalia Javadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, p. 168.
  21. Angalia Javadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, uk. 168.
  22. Angalia Jawadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, uk. 170.
  23. Angalia Javadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, uk. 171 na 172.
  24. Angalia Jawadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, p. 168.
  25. Angalia Javadi Amuli, Velayat Faqih, 1378, p. 168.
  26. Gazeti la Jamhuri ya Kiislamu, Oktoba 12, 2016, ukurasa wa 12.
  27. Javadi Amuli, Hati ya vitendo, Beta, juzuu ya 1, uk.22.
  28. Javadi Amuli, Abdullah, Risaleh Pramiyah, Juz. 1, uk. 401.
  29. Javadi Amuli, Hati ya vitendo, Beta, juzuu ya 1, uk.390.
  30. Bandali, Mehr Ostad, toleo la kielektroniki, 1391, uk. 191 na 192.
  31. Bandali, Saeed, Mehr Ostad, toleo la kielektroniki, 1391, uk. 201.
  32. Bandali, Saeed, Mehr Ostad, toleo la kielektroniki, 1391, uk.204.
  33. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  34. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  35. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  36. نگاه کنید به «خطبه‌های نماز جمعه»، وبگاه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء.
  37. «آخرین خطبه نماز جمعه آیت‌الله جوادی آملی قرائت شد»، وبگاه خبرگزاری فارس.
  38. «ماجرای نامه امام به گورباچف به قلم حضرت آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه پایگاه اطلاع‌رسانی حوزه.
  39. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  40. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  41. مدرسی، «تاریخچه زندگی آیت‌الله شیخ عبدالله جوادی آملی».
  42. «اساسنامه بنیاد بین المللی علوم وحیانی اسراء»، وبگاه مرکز پژوهش‌های مجلس.
  43. «نیم‌نگاهی به بنیاد بین‌المللی علوم وحیانی اِسراء»، افق حوزه، ص۱۲.
  44. The Muslim, 500, 2023, p114
  45. Angalia Javadi Amuli, Tasnim, 2008, vol.1, p.25.
  46. « تسنیم: تفسیر قرآن کریم جلد ۶۲»، مرکز بین المللی نشر اسراء.
  47. «حیات علمی و قرآنی آیت‌الله جوادی آملی»، وبگاه بنیاد بین‌المللی علوم وحیانی اسراء.
  48. «رحیق مختوم: شرح حکمت متعالیه جلد 35»، مرکز بین‌المللی نشر اسراء.
  49. «همایش طبیب روحانی؛ بزرگداشت آیت‌الله جوادی آملی »، خبرگزاری صداوسیما.
  50. «حضرت آیت الله جوادی آملی در فهرست ۵۰۰ شخصیت برتر مسلمان جهان»، خبرگزاری بین المللی شفقنا.
  51. Sekretarieti ya Mwaka wa Kongamano la Kitabu cha Hoza, toleo maalum la Mwaka wa 15 wa Mkutano wa Hoza Book, 1392, uk. 78-80

Vyanzo