Kuingiliana

Kutoka wikishia

Kujamii au kujamiiana (Kiarabu: الجماع) ni kukutanisha utupu wa mwanadamu na mwanadamu mwingine au na mnyama. Kwa maneno mengine ni kukutanisha tupu mbili. Katika fiqh ya Kiislamu, maneno kama jimai, kuingilia, kukutana kimwili na kadhalika yatumika kwa maana ya kujamii au kujamiiana. Hukumu za fikihi kuhusiana na jambo hili zinahusika pale kuingilia kunathibitka (kwa akali kwa kiwango cha kichwa cha uume yaani kwa kiwango cha sehemu ya kutahiriwa). Mafakihi wamegawanya jimai na kukutana kimwili katika makundi matatu: Kukutana kimwili kwa njia ya halali kama kwa njia ya ndoa, kwa njia ya haramu kama zinaa na sehemu ya tatu ni shubha (kimakosa) na wanazungumzia hukumu za kila mojawapo. Kwa mujibu wa fat'wa yao, kuingilia kimwili kwa mbele au kwa nyuma yote mawili yanasabisha janaba na ili kutoharisha janaba ni lazima kuoga josho la janaba. Ni haramu kufanya mapenzi watu wa jinsia moja, hakuna ndoa ya watu wa jinsia moja. Kwa maana kwamba, ni haramu kwa mwanaume na mwanaume kufanya mapenzi (liwati / اللواط) na wanawake kwa wanawake ni haramu kufanya mapenzi baina yao yaani (kusagana / المُساحقة) kama ambavyo ni haramu mwanadamu kumuingilia mnyama. Aidha ni makuruhu mume kumuingilia mkewe kwa nyuma. Hizi ni baadhi ya hukumu za kisheria zinazohusiana na kujamiiana.

Maana na nafasi ya kifiq'h

Katika fiqh ya Kiislamu, kujamii kunatambulika kwa maneno kama jimai, kuingilia, kukutana kimwili na kadhalika na hiyo ina maana ya kukutanisha mtu tupu yake na ya mwingine au na ya mnyama. [1] Hukumu za kujamiiana zinazungumziwa sana katika milango ya fiq'h kama tohara, Swaumu, itikafu, Hija, ndoa, talaka na kadhalika. [2] Hata hivyo hukumu hizi ni makhsusi kwa maudhui ya kujamiiana ambako ndani yake kumethibitika kwa uchache kuingia uume kwa kiwango cha mpaka sehemu ya kutahiriwa. [3]

Aina za kujamii

Kwa mujibu wa fiq'h, jimai au kujamii na kukutana kimwili kumegawanyika makundi matatu:

  1. Kujamii (kuingilia) kwa njia ya halali.
  2. Kujamii kwa shubha (utata na kimakosa).
  3. Kujamii kwa njia ya haramu. Na kila mojawapo ina hukumu zake tofauti. [4]

Kujamii kwa njia ya halali

Kujamii kwa njia ya halali hutimia pale panapokuweko sababu za kisheria. Sababu za kisheria za kujamii na kukutana kimwili kwa njia ya halali ni: Ndoa ya daima, ndoa ya mutaa (ya muda) umiliki (mwenye kumiliki kanizi yaani binti au mwanamke asiye Muislamu aliyechukuliwa mateka katika vita baina ya Waislamu na makafiri) na kuhalalisha (mwenye kumiliki mwanamke au binti asiye Mwislamu aliyepatikana katika vita baina ya Waislamu na makafiri atakapomhalalishia mtu mwingine kunufaika na binti au mwanamke huyo kijinsia). [5]

Kujamii kwa njia ya shubha (kimakosa)

Kujamiiana mwanamke na mwanauume wakidhani kwamba, sababu za kisheria zimetimia. Aina hii ya kujamiiana katika istilahi ya kifikihi inajulikana kama Wat'i Shubha (kukutana kimwili au kuingiliana kimakosa); ni kama vile mwananaume amuingilie mwanamke fulani akidhani kwamba, ni mkewe kumbe sivyo. Hii inaweza kutokea kwa mfano kama kuna giza na yeye ameingia ndani akitokea kazini au safarini akijua yuko mkewe tu kumbe kuna ndugu wa mkewe kwa mfano amekuja na yeye akamuingia kimakosa. [6] Kwa mujibu wa fat'wa za mafakihi kujamii au kumuingilia kimakosa mwanamke hakuna adhabu ya kisheria. [7]

Kujamii kwa njia ya haramu

Kujamiiana au kukutana kimwili mwanaume na mwanamke hali ya kuwa wana ufahamu kamili kwamba; sababu za kisheria kama ndoa hazijatimia baina yao na wamefanya hivyo kwa hiari yao, aina hii ya kujamiiana inafahamika kuwa ni kujamiiana kwa njia ya haramu. [8] Baadhi ya mifano ya kujamiiana kwa njia ya haramu ni kama: Zinaa, liwati, kusagana na kujamiiana na mnyama. [9] Aidha kujamiiana mke na mume hali ya kuwa mke yupo katika hali ya hedhi (siku zake), damu ya nifasi (damu ya uzazi) na kujamiiana katika hali ya Swaumu ni haramu. [10]

Kupatikana janaba baada ya kujamiiana

Kadhalika angalia: Janaba

Kwa mujibu wa fat'wa ya mafakihi, kujamiiana iwe ni kwa nyuma au kwa mbele ni kitendo kinachopelekea kupatikana janaba. [11] Kufanya mapenzi ya jinsia moja yaani mwanaume kwa mwanaume na vilevile kujamiiana na mnyama pia kunapelekea kupatikana janaba. [12] Kuna hukumu mbalimbali kuhusiana na kujamiiana na janaba pia; na miongoni mwazo ni kuwa haramu kugusa maandishi ya Qur'an, jina la Mwenyezi Mungu na kwa mujibu wa tahadhari ya wajibu (ihtiyat wajib) kugusa pia majina ya Maimamu, kubakia misikitini na kusoma sura za Qur'an ambazo zina sijida ya wajibu. [13] Mwanaume ambaye amefanya jimai na akaingiza utupu wake mpaka kwa kiwango cha sehemu iliyotahiriwa [14] anapaswa kuoga janaba anapotaka kuswali na kufunga swaumu. [15]

Baadhi ya hukumu za kujamiiana

Kwa mujibu wa fat'wa za Marajii taqlidi, hukumu za kujamii zinathibiti pale mtu anapoingiza uume lwa uchache mpaka katika sehemu iliyotahiriwa. ]16] Baadhi ya hukumu za kujamii kama zilivyonukuliwa katika vitabu vya fiq'h ni:

  • Ni haramu kuacha kufanya tendo la ndoa katika ndoa ya daima kwa muda wa zaidi ya miezi minne. [17]
  • Ni haramu kujamiiana na mnyama na kitendo hiki kina adhabu za taazir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo). [18]
  • Ni haramu kumuingilia binti ambaye hajafikisha umri wa kubaleghe. [19]
  • Ni haramu kuingiliana mwanaume kwa mwanaume ambako kunafahamika kama liwati na kufanya mapenzi mwanamke na mwanamke ambako kunajulikana kwa jina la kusagana na kitendo hiki kina adhabu. [20]
  • Kama mwanaume atamuingilia mwanaume mwenziwe ni haramu kwake kumuoa mama, dada au binti wa huyu mwanaume. [21]
  • Kumuingilia mwanamke kwa nyuma inajuzu; lakini ni makuruhu sana (inachukiza sana). ]22]
  • Ni mustahabu kufanya tendo la ndoa usiku wa Jumatatu, Jumanne, Alkhamisi na Ijumaa na vilevile adhuhuri ya siku ya Alkhamisi. [23]
  • Ni makuruhu kufanya tendo la ndoa kwa mtu ambaye amewasili usiku akitokea safari. [24]
  • Ni makuruhu kufanya tendo la ndoa hali ya kuwa mtu ameelekea kibla kama ambavyo ni makuruhu kujamiiana hali ya kuwa na shibe. [25]

Rejea

Vyanzo

  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf, Mukhtalaf al-Shiah fi Ahkam al-Syari'ah, Qom: Kantor penerbitan Islami, cet. II, 1413 H.
  • Bani Hashimi Khomaini, Sayyied Muhammad Hussein, Taudhih al-Masail Maraji Muthabiq Ba Fatawa Shanzdah nafar Maraji' Muazham Taqlid, Qom: Kantor penerbitan Islami, cet. VIII, 1424 H.
  • Muassasah Dairatul Ma'arif Fiqh Islami bar Mazhab Ahle Beyt, Farhange Fiqh Muthabiqe Mazhab Ahle Beyt as, Qom: Muassasah Dairatul Ma'arif fiqh Islami, cet. III, 1392 HS.
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan, Shara'i al-Islam fi Masail al-Halal wa al-Haram, Riset dan editor: Abdul Hussein Muhammad Ali Baqqal, Qom: Ismaililyan, cet. II, 1408 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam fi Sharhi Sharai' Islam, Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, cet. VII, 1404 H.
  • Shahid Awal, Muhammad bin Makki, Al-Qawaid wa al-Fawaid, Riset: Sayyied Abdul Hadi Hakim, Qom: toko buku Mufid, cet. I, 1400 H.
  • Shahid Tsani, Zainuddin bin Ali, Al-Raudhah al-Bahiyah fi Sharhi al-Lum'ah al-Dimishqiyah. Syarah: Sayyied Muhammad Kalantar, Qom: toko buku Mufid, cet. I, 1410 H.
  • Tabatabai Yazdi, Sayyied Muhammad Kazhim, Al-Urwah al-Wutsqa, Beirut: Muassasah al-A'lami lilmathbu'at, cet. II, 1409 H.