Sala ya Usiku wa Laylatul-Qadr (Rakaa 100)

Kutoka wikishia
Kwa ajili ya matumizi mengine angalia Sala ya Usiku wa Laylaytul-Qadr (kuondoa hali ya kutoeleweka)

Sala ya rakaa 100 ya usiku wa Laylatul-Qadr Ni Sala 50 za rakaa mbili mbili ambayo husaliwa katika usiku wa Laylatul Qadr. Katika Sala hii, katika kila rakaa, baada ya kusoma Surat al-Fatiha (al-Hamd) husomwa Surat al-Tawhid mara 10.[1] Sheikh Abbasi Qummi ameiileta na kuitaja Sala hii katika kitabu chake cha Mafatihul al-Jinan kwamba, ni miongoni mwa amali za pamoja za nyusiku za Laylatul Qadr na anaona kuwa ni bora kusoma Surat Tawhid (baada ya al-Hamd) mara 10 katika kila rakaa.[2]

Kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa na Imam Baqir (a.s) ni kuwa, mtu ambaye atahuisha usiku wa 23 wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na akaswali rakaa 100, riziki yake huongezwa na atahifadhiwa kunako woga wa malaika Nakir na Munkar.[3]

Katika baadhi ya misikiti ya Kishia katika kila usiiku wa 19, 21 na 23 wa mwezi wa Ramadhani husaliwa kwa jamaa rakaa 100 za Sala ya kadhaa za wajibu (siku sita). Kwa mujibu wa fatwa ya Ayatullah Makarim Shirazi mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia, mtu anaweza katika usiku wa Laylatul; Qadr akaswali Sala za kadhaa ya wajibu na akafaidika na thawabu za amali za usiku huu.[4]

Rejea

  1. Sayyid Ibnu Tawus, Al-Iqbal bi al-A'mal, juz. 1, uk. 313.
  2. Qummiy, Kuliyat Mafatih al-Jinan, Amali Mushtarake Shab-haye Qadr, 1384 S, uk. 365.
  3. Ibnu Tawus, Iqbal bi al-A'mal, juz. 1, uk. 386.
  4. Adam Jaiguzin Shudan Namaz Shab Qadr be Ja-e Namaz Qadha, Tovuti ahkam.makarem.ir.

Vyanzo

  • Ibnu Tawus, Ali bin Mussa. Iqbal bi al-A'mal al-Hasanah. Mhariri: Jawad Qayumi Isfahani. Qom: Daftar Tablighat Islami, Chapa ya kwanza, 1376 HS.
  • Qummiy, Sheikh Abbas. Kuliyat Mafatih al-Jinan. Qom: Matbuat Dini, 1384 HS.
  • Adam Jaiguzin Shudan Namaz Shab Qadr be Ja-e Namaz Qadha, Tovuti ahkam.makarem.ir. Tarikh Bazdid: 14 Farvardin 1403 HS.