Usiku wa mwezi 23 Ramadhani

Kutoka wikishia

Usiku wa mwezi 23 Ramadhani (Kiarabu: ليلة ثلاث وعشرين من شهر رمضان) ni moja kati ya masiku ambayo yawezekana ukawa ni usiku wa cheo kitukufu (Laylatul Qadr). Kwa msingi huo, Waislamu wa madhehebu ya Shia hukesha katika usiku huu wakifanya ibada na kuomba dua. Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa Kishia imesisitizwa zaidi juu ya uwezekano wa usiku mwezi 19 na 21 kuwa moja ya nyusiku za Laylatu Qadr. Kadhalika amali mahususi za usiku huu ni nyingi zaidi ikilinganishwa na nyusiku nyingine mbili (usiku wa kumi na tisa na usiku wa ishirini na moja). Kuna ripoti pia kutoka katikak sira ya Ahlul-Bayt (a.s) zinaoeleza kwamba, walikuwa wakiwafanya watu wao wa nyumbani kubakia macho katika usiku huu. Kukamilika kazi za uandishi wa baadhi ya vitabu vya Maulamaa wa Kishia pia umetajwa katika usiku huu.

Uwezekano wa Laylatul Qadr Kuwa Usiku wa Mwezi 23

Ibada za usiku wa ishirini na tatu wa Ramadhani huko Karbala (Ramadhan 1443 AH) [1]

Usiku wa mwezi 23 Ramadhani ni moja ya nyusiku ambazo yawezekana ikawa ni Laylatul Qadr (usiku wa cheo kitukufu). [2] Kwa msingi huo Waislamu wa madhehebu ya Shia hukesha katika usiku huu wakifanya ibada na kuomba dua. [3]

Kwa mujibu wa Allamah Majlisi, mtazamo na maoni ya wanachuoni wa Shia Imamiyyah, Usiku wa Qadr unapatikana katika mojawapo ya nyusiku za 19, 21, na 23 za Ramadhani. [4] Hata hivyo, Sheikh Sadouq amesema kwamba, walimu wetu wameafikiana kwamba, usiku wa Qadr (Laylatul Qadr) ni usiku wa mwezi 23 Ramadhani. [5] Kuna hadithi pia zilizonukuliwa ambazo zinautaja usiku wa mwezi 23 Ramadhani kuwa ni Laylatul Qadr. [6] Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, katika usiku wa 19, mambo hukadiriwa, katika usiku wa 21 hukamilika na kupasiishwana usiku wa 23, saini ya mwisho hutiwa. [7] Muhammad Taqi Majlisi, Sheikh Sadouq na akthari ya Maulamaa wa Kishia wakitegemea riwaya kama hadithi ya Juhani wanautambua usiku wa mwezi 23 Ramadhani kuwa ni Laylatul Qadr; pamoja na hayo Majlisi wa Kwanza akitegemea baadhi ya hadithi anaamini kwamba, kila moja ya mikesha mitatu, 19, 21, na 23, imejumuishwa katika sifa za Usiku wa Qadr, na ni bora kujaalia zote tatu kwamba, mojawapo inaweza kuwa ndio ule usiku wa cheo kitukufu. [8]

Umashuhuri wa usiku wa mwezi 23

Usiku wa mwezi 23 Ramadhani umeondokea kuwa mashuhurii kwa jina la Usiku wa Juhani kutokana na hadithi ya Imamu Baqir (a.s). Kwa mujibu wa hadithi hiyo mtu mmoja aliyejuliakana kwa jina la Juhani (Abdallah bin Anis Ansari) alimwambia Bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba: Nyumba yangu iko mbali na Madina, hivyo nitajie usiku ambao ili nije huku. Mtume (s.a.w.w) akamwambia aje Madina katika usiku wa 23. Aidha kisa cha usiku wa Juhani kimeelezewa hivi katika hadithi kwamba: Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Abdallah bin Unais Ansari ambaye alikuwa ni mkazi wa Juhani alifika kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na kumwambia: Nyumba yangu iko mbali na Madina, na nina ngamia, kondoo na wajakazi, ningependa unijulishe usiku fulani ili katika usiku huo nije Madina na katika Masjdu an-Nabi kwa ajili ya kufanya ibada. Mtume (s.a.w.w) akamwambia amkaribe, kisha akamnong'oneza kitu masikioni, kisha baada ya hapo na kuendelea, Bwana yule akawa kila mwaka anakuja Madina katika usiku wa 23 wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kubakia usiku wote katika Masjdu al-Nabi akifanya ibada kisha asubuhi yake alikuwa akirejea alikotoka. [9] Baada ya kushuhudiwa mazungumzo hayo na mwenendo wa Abdallah bin Unais Ansari katika usiku wa 23 wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, usiku huu ukapewa jina la Laylatul Juhani (usiku wa Juhani) na jina hilo likawa moja ya majina ya Laylatul-Qadr kiasi kwamba, masahaba na wafuasi wa Maimamu wakawa wakiuliza kuhusiana na Usiku wa Juhani. [10]

Sira ya Ahlul-Bayt (a.s) katika Usiku wa Mwezi 23

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s) katika kitabu cha Daa'im al-Islam ni kuwa, katika usiku wa mwezi 23 Mtume (s.a.w.w) alikuwa akiwafanya watu wa nyumbani kwake kubakia macho na alikuwa akiwamwagia maji usoni wale waliokuwa na usingizi ili waamke. [11] Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba, Mtume (s.a.w.w) lilipokuwa likiwadia kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani alikuwa akikusanya tandiko lake na alikuwa akiondoka na kuelekea msikitini kwa ajili ya itikafu. Licha ya kuwa Msikiti wa Madina haukuwa na paa, lakini hakuwa akiondoka msikitini hapo hata wakati ambao mvua ilikuwa ikinyesha. Mtindo wa Fatma (a.s) ulikuwa huu kwamba, katika nyusiku za Laylatul Qadr alikuwa akifanya ibada mpaka asubuhi na alikuwa akiwataka watoto na familia yake nao wabakie macho kwa ajili ya kufanya ibada; na alikuwa akilitatua tatizo lao la usingizi kwa kuwapa chakula kidogo na kuwalaza mchana. Alikuwa akisema, aliyenyimwa (mnyimwaji) ni yule aliyenyimwa mema ya usiku huu. [12] Maasumina (a.s) hawakuwa wakiacha suala la kuhudhuria msikiti na kukesha wakifanya ibada. Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ni kuwa, alikuwa mgonjwa sana katika moja ya nyusiku za Laylatul Qadr, lakini pamoja na hayo aliwataka watu wake wa karibu wampeleke msikitini ili akafanyie ibada huko. [13] Sheikh Abbasi Qumi ameinukuu hadithi hii katika kitabu chake cha Mafatihu al-Jinan chini ya amali makhsusi zinazofanywa katika usiku wa mwezii 23 Ramadhani. [14]

Vitabu vya Maulamaa wa Kishia katika Usiku wa Mwezi 23 Ramadhani

Kwa mujibu wa Muhammad Muhammadi Rayshahri, baadhi ya wanazuoni wa Kishia wamemaliza kuandika vitabu vyao maarufu katika usiku wa mwezi 23 Ramadhani; [15] Jawahir al-Kalam (1254 H) cha Muhammad Hassan Najafi, Sharh Manzoomah (1261 H) cha Mollahadi Sabzevari na Al- Mizan (1392 H) cha Allama Tabatabai ni mojawapo ya matukio haya. [16] Aidha Rayshahri mwenyewe alikamiliisha uandishi wa kitabu cha Mizan al-Hikmah katika usiku wa mwezi 23 Ramadhani 1405 Hijria. [17]

Ibada na Amali za Usiku wa Mwezi 23 Ramadhani

Sheikh Abbas Qomi amebainisha amali na ibada za kufanya katika usiku wa mwezi 23 Ramadhani katika Mafatih al-Jinnan [14] Amepokea kutoka kwa Allama Majlisi kwamba, katika usiku huu isomwe Qur'ani kadiri iwezekanavyo na dua zilizoko katika Sahifa Sajjadiyya hasa Dua Makarim al-Akhlaq na Dua ya Toba. [18] Pia, katika usiku huu, imeusiwa na kukokotezwa sana kukariri dua ya Allahuma Kun Liwaliyyika katika hali yoyote (kusimama, kukaa au kusujudu). [19]

Amali za Usiku wa 23 Mwezi wa Ramadhani

AMALI ZA PAMOJA ZA NYUSIKU
  • Kuoga.
  • Kusali Sala ya rakaa mbili, baada ya Surat al-Fatiha husomwa Surat Tawhid (Qul-Huwallah) mara 7, na baada ya anayesali kukamilisha Sala hiyo atasema: (اَسْتَغْفِرُ اللّهَ وَاَتُوبُ اِلَیهِ) mara 7
  • Kukesha katika nyusiku hizi.
  • Kusali Sala ya rakaa 100 (Sala 50 za rakaa mbili mbili).
  • Kusoma dua ya (...اَللهمَّ اِنّی اَمسیتُ لَکَ عَبداً)
  • Kusoma dua ya Jawshan Kabir.
  • Kusoma Ziyara ya Imam Hussein (a.s).
  • Kuweka msahafu kichwani na kuapa kwa Mwenyezi Mungu na kwa Maasumina 14. [20]
HUKUMU MAKHSUSI ZA USIKU WA MWEZI 23
  • Kusoma dua zinazohusiana na kumi la mwisho la Ramadhani.
  • Kusoma sura za Ankabut, Rum na Dukhan.
  • Kusoma Surat al-Qadr mara 1000.
  • Kuoga mwanzo na kuoga mwishoni mwa usiku.
  • Dua: (...اَللَّهُمَّ امْدُدْ لِی فِی عُمُرِی وَ أَوْسِعْ لِی فِی رِزْقِی)
  • Dua: (...اَللَّهُمَّ اجْعَلْ فِیمَا تَقْضِی وَ فِیمَا تُقَدِّرُ مِنَ الْأَمْرِ الْمَحْتُومِ)
  • Dua: (...یا بَاطِنا فِی ظُهُورِهِ وَ یا ظَاهِرا فِی بُطُونِهِ)
  • Kusoma dua ya kumuombea afya njema Imam Mahdi (a.t.f.s). [21]
  • Kukesha (kuhuisha) kwa kufanya mazungumzo ya kielimu. [22]

Rejea

Vyanzo