Waqfu

Kutoka wikishia

Waqfu (Kiarabu: الوقف) Ni mkataba maalum ambapo mali hukabidhiwa au huwasilishwa ili watu wa kikundi au tabaka fulani waweze kunufaika nayo. Katika waqfu hakuna hata mmoja mwenye haki ya kuuza au kutoa mali ya waqf na kuihamishia kwa watu wengine, si mweka waqfu wala si waliokusudiwa kunufaika na mali hiyo ya waqfu. Qur'an haikuzugumzia suala la waqfu kwa uwazi. Katika Hadithi, mali ya waqfu imezingatiwa kama ni "sadaka inayoendelea (sadaqatu al-Jaria)". Historia ya waqfu inarudi kwenye zama za kabla ya Uislamu. Hata hivyo, suala la watu kuweka waqfu lilikuwa ni maarufu kati ya masahaba tokea wakati wa maisha ya bwana Mtume (s.a.w.w). Mifano ya mali ziliyowekwa kwa ajili ya bwana Mtume (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s) imerikodiwa katika vyanzo kadhaa vya Kiislamu.

Waqfu ni mojawapo ya aina za mikataba katika Uislamu. Mkataba huu umejadiliwa na kutafitiwa katika vitabu vya fiqh, ambapo masharti ya uhalali na hukumu zake zimefafanuliwa ndani yake. Waqfu imegawanywa katika aina mbili: waqfu maalumu na waqfu wa kiujumla (waqfu huria).

Ufafanuzi na maana ya waqfu

Maana ya waqfu katika istilahi za wanazuoni ni aina ya mkataba ambao kupitia mkataba huo, mali fulani hutolewa ili tu watu wanufaike na faida yake. [1] Kwa mfano, mahali fulani huwekwa kwa ajili ya maskini, ili maskini hao wapate wanufaike na faida ya mahali hapo, huku hati ya kuweza kuuza au kununua mahali hapo ikiwa imefutwa moja kwa moja (yaani hapauziki wala kununulika kisheria). [2] katika mkataba wa waqfu, mali hutoka katika umiliki wa mwekaji waqfu, [3] kwa hiyo sio yeye wala wale waliowekewa waqfu, mwenye haki ya kuuza au kutoa mali hiyo. [4]

Waqfu inachukuliwa kuwa ni sadaka inayoendelea (صدقة الجارية), imeitwa hivyo kwa sababu katika hadithi; [6] imeelezwa kuwa faida zake ni zenye kubaki daima. [7]

waqfu maalumu na waqfu wa kiujumla

Makala asili: waqfu maalumu na waqfu wa kiujumla

Katika vitabu vya fiqh, waqfu umegawanywa katika aina mbili: waqfu wa umma (waqfu huria) na waqfu makhususi (waqfu kwa walengwa maalumu). Waqfu ulio wekwa kwa lengo la umma au kwa ajili ya umma huitwa waqfu wa umma, kama vile waqfu wa skuli na hospitali na waqfu wa mali kwa ajili ya maskini au wanazuoni. Wakfu unaowekwa kwa lengo la walengwa makhususi, au kwa ajili ya kikundi maalum huitwa wakqu makhususi, kama vile waqfu wa mahali fulani kwa mtu au watu na walengwa maalumu. [8]

Nafasi ya waqfu na umuhimu wake

Waqfu ni mojawapo ya masuala ya kisheria ndani ya fiqhi ya Kiislamu. Katika vitabu vya fiqhi; masharti ya uhalali na sheria za waqfu zinajadiliwa vya kutosha ndani. [9] Katika vitabu vya Hadithi, suala la waqfu limeorodheshwa sambamba na masuala ya sadaka, zawadi, na masuala mengine yanayo fanana nayo. [10]

Katika Qur'an, neno waqfu halikutajwa kabisa ndani yake, lakini katika vitabu vyenye kujadili Aya zinazozungumzia sheria za kifiqhi, suala la waqfu limeorodheshwa katika orodha sawa na masuala ya sukna (سُکنیٰ) (matumizi ya faida ya mali kwa muda maalum), sadaka, na zawadi, na imeainishwa chini jumla ya masuala yanayo husiana na misaada inayo tolewa bila ya malipo (mali ambayo hupewa watu bila ya kupokea ujira wowote kutoka kwa watu hao). Nafasi ya waqfu katika vitabu hivyo imefanana na baadhi ya dhana za misaada mingine ilioko kwenye Aya za Qur'ani, kama vile infaq (kutoa sadaka) na kutoa zawadi mali. [11] Kulingana na Hadithi, sadaka inayoendelea (waqfu وقف) ni mojawapo ya mambo ambayo hueendelea faida zake hata baada ya kifo cha mtoaji wa sadaka hiyo. [12] Bila shaka, katika Hadithi hizi, neno waqfu limetumika mara chache tu, ila neno sadaka ndilo neno liliokoza rangi zaidi katika uwanja wa Hadithi. [13] hata hivyo, katika Hadithi zinazohusiana na sheria za waqfu, neno waqfu limeonekana kumetumika ndani yake. [14]Mada ya waqfu ni mojawapo ya mada zinazojadiliwa sana miongoni mwa Waislamu. Mbali na maandishi ya kifiqhi juu ya mada hii, pia kuna vitabu na makala nyingi zilizo jitenga katika kujadili suala la waqfu. Katika kitabu kiitwacho Maakhadh Shenasi Waqf, kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Sajjadiy, mmeorodheshwa ndani yake idadi ya kazi 6239 kuhusiana na mada ya waqfu; zikiwemo vitabu, makala, tasnifu, nakala zilizo andikwa kwa njia hati za mkono, habari pamoja na ripoti za majarida. [15]

Enzi za kunzishwa kwake

Kuna maoni tofauti kuhusu asili ya waqfu na inaaminika kwamba; amali ya waqfu ina historia refu na kwamba iliibuka kabla ya Uislamu. [16] Hata hivyo, baada ya Uislamu, amali ya waqfu ilianza kuenea haraka miongoni mwa Waislamu. [17] Mtume Muhammad (s.a.w.w) mwenyewe aliwahi kumiliki mali na kuitoa waqfu. [18] Mara ya kwanza bwana Mtume (s.a.w.w), alitoa ardhi ya kwa ajili kutumiwa na wasafiri waokwama katika safari zao (ibnu sabiil). [19] Pia, kuna Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kwa Jabir bin Abdullah Ansari, inayosema kwamba; hakuna mtu miongoni mwa Maswahaba ambaye alikuwa na uwezo wa kifedha akawa hakuwahi kutoa kitu chochote kwa ajili ya waqfu. [20]Miongoni mwa Maimamu, Imam Ali (a.s) alikuwa na waqfu nyingi zaidi. [21]

Kulingana na maelezo ua Ibnu Shahre Ashub; Imam Ali (a.s) alijenga visima mia katika mji wa Yanbu na kuviweka waqfu kwa ajili ya mahujaji. Pia, alichimba visima njiani kuelekea mji wa Kufa na Makka, na akajenga misikiti katika miji ya Madina, Miqat, Kufa, na Basra, kisha kuweka waqfu. [22] Hatimaye, mali za waqfu kwa Waislamu zilikua mno, kiasia ya kwamba katika utawala wa Bani Umayyah, ilibidi kuanzisha taasisi makhususi kwa ajili ya kusimamia mali za waqfu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, serikali za Kiislamu zilikuwa na jukumu la kusimamia mali za waqfu. [23]

Utendaji kuhusiana na waqfu

Katika baadhi ya maandishi yanayo husiana na waqfu, pia kuna mazungumzo juu ya athari za waqfu katika nyanja za kiuchumi na kijamii. [24] Kulingana na ripoti za kihistoria, baadhi ya masuala ambayo mali za waqfu huweza kutumika ni: Ujenzi wa misikiti, maskuli, maktaba na hospitali, jela za wendawazimu, visima, misingi ya maji na huduma kwa maskini, yatima, walemavu na wafungwa, na utoaji wa gharama za maisha kwa wanazuoni. [25] Kwa hivyo wanazuoni wamesema kuwa; waqfu ilikuwa na jukumu la kuhudumu katika maeneo ya utoaji wa huduma za kijamii, afya na matibabu na kueneza kwa elimu na teknolojia. [26]

Wengine, kwa msingi wa tafiti za kihistoria, wamegawanya kazi za waqfu katika maeneo manne yafuatayo:

  • Masuala ya kitamaduni: kama vile kuanzisha skuli, vitabu na maktaba.
  • Masuala ya afya: kama vile kuanzisha hospitali, jela za wendawazimu na bafu.
  • Masuala ya kijamii na ustawi: kama vile ujenzi wa karakana, daraja, ngome, visima, misingi ya maji na viwanda.
  • Masuala ya kidini: kama vile kujenga misikiti na makaburi ya watu wema. [27]

Leo, maeneo kahdhaa ya kidini kama vile; haramu za Maimamu (a.s), misikiti na vyuo vya kiislamu yanaendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia mapato yanayotokana na waqfu.

Uendeshaji wa mali za waqfu

Utukukaji wa mali za wakfu katika nchi za Kiislamu, umesababisha kuanzishwa kwa mashirika ya umma katika nchi za Kiislamu. Suala hili lina historia refu, na kulingana na ripoti za kihistoria linarudi katika enzi za utawala wa Bani Umayya. Katika kipindi hiki, Toba bin Namir, hakimu wa mji wa Basra, aliamuru mashamba yaliyowekwa waqfu yasajiliwe. Pia alianzisha ofisi ya mashamba yaliyowekwa waqfu katika jiji hilo. [28]

Katika enzi za utawala wa Ilkhinaan wa Mongol, kulikuwa na idara iniitwayo Hukumat Mauquufat ambalo lilifanya kazi chini ya mamlaka ya kadhi mkuu. [29]

Nchini Iran, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wafalme wa Safawi, ilianzishwa idara huru kwa ajili ya kusimamia mashamba ya waqfu. Idara hii ilikuwa na wawakilishi katika miji yote mikubwa. Mawakili wa idara hii walikuwa wakijulikana kwa jila "Waziri Auqaaf". [30] Katika nchi za Kiislamu, kuna mashirika kahdaa na maalum kwa ajili ya kusimamia mashamba yaliyowekwa wakfu, ikiwa ni pamoja na:

  • Idara ya Mali za Waqfu na Masuala ya Kheri ya Iran. [31]
  • Ofisi ya mali za waqfu za Shia na Ofisi ya mali za waqfu za Sunni ya Iraq. [32]
  • Wizara ya Waqfu ya Misri. [33]
  • Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait. [34]
  • Baraza Kuu la Wakfu la Saudi Arabia. [35]

Masharti za Uhalali wa waqifu

Wanazuoni wametaja masharti manne kuhusiana na uhalali wa waqifu ambayo ni: kuwepo kwa mali inayowekwa waqfu, mweka waqfu, wanao wekewa wakfu na tendo la kuweka waqfu.

Mali inayowekwa waqfu

Mali inayowekwa waqfu ni lazima iwe na masharti manne yafuatayo:

  • Iwe na uwepo unaohisiwa ambayo imehusishwa na kuonekana kimwili. Kwa mujibu wa sharti hii, hatuwezi kuweka waqfu mali ambayo iko kwa mtu mwingine, au nyumba ambayo hatujaifafanua ni ipi tunayoizungumzia katika waqfu huo.
  • Iwe ina uwezo wa kumilikika kisheria (iwe inahisabiwa ni mali kisheria). Kwa mujibu wa sharti hii, kwa mfano, hatuwezi kuweka waqfu nguruwe; kwani nguruwe hawezi kumilikiwa na Mwislamu.
  • Iweze inawezekana kutumiwa manufaa yake bila mali hiyo kutalifika. Kwa mujibu wa sharti hii, hatuwezi kuweka wakfu pesa; kwani kutumia manufaa yake kunamaanisha kutalifika na kumaliszika kwa mali yenyewe.
  • Iwezekane mali hiyo kuchukuliwa kutoka kwa mweka waqfu. Kwa hivyo, mwekaji waqfu hawezi kuweka waqfu mali ya mtu mwingine; kwani kuchukua mali hiyo ni haramu. [36]

Mweka waqfu

Mweka waqfu awe amebaleghe, awe amepevuka kiakili na pia awe na idhini ya kutumia mali yake. [37]

Wanao wekewa waqfu

Anaye wekewa waqfu lazima awepo, awe mtu au watu mahususi, na kuwekewa waqfu kwake isiwe haramu. Kwa mujibu wa masharti haya, hatuwezi kuweka waqfu kwa mtu ambaye hajazaliwa. Pia hatuwezi kuweka wakfu kwa majambazi na makafiri wapinzani; kwani kuwawekea waqfu kama hao ni haramu. [38]

Tendo la kuweka waqfu

Tendo la kuweka waqfu ni halali iwapo lina masharti yafuatayo:

  • Kudumu; yaani, waqfu haupaswi kuwa na muda maalumu. Kwa hivyo, kuweka wakqu kwa muda maalumu, si sahihi. Pia kuweka waqfu kwa mtu maalum si sahihi; kwani kwa kifo chake, wakfu huisha na kusimama.
  • Nia amilifu shikamanifu itendekayo bila ya kuchelewa; yaani, haiwezekani kupitisha maneno ya kuweka wakfu (nia) kwa ajili ya kuweka waqfu mali katika siku zijazo (kwa mfano, mwanzoni mwa mwezi iingie kwenye waqfu).
  • Kuchukua mali; Yaani mpaka pale ambapo kitu kilichowekewa waqfu kitakuwa bado hakijachukuliwa kutoka kwa mwakifi, wakfu huo utakuwa bado haujafanyika, kitu hicho kinahisabiwa kuwa badi ni mali yake.
  • Kutoka nje ya umiliki wa mweka waqfu; Kwa mujibu wa sharti hii, mtu hawezi kuweka waqfu mali yake kwa ajili yake mwenyewe. [39]

Hukmu za waqfu

Baadhi ya hukmu za uwaqifu, kwa misingi ya vitabu vya fiqhi ni kama ifuatavyo:

  • Mali ya waqfu inatoka nje ya umiliki wa mweka waqfu na mweka waqfu huyo hawezi kuiuza au kuigawa, na wala mtu yeyote hawezi kurithi mali hiyo kutoka kwake.
  • Mali ya waqfu haiwezi kununuliwa au kuuzwa.
  • Kulingana na Fatwa za baadhi ya mafaqihi ni kwamba; katika suala la waqfu, lazima katika uwekaji waqfu kusomwe maneno ya tungo ya waqfu; lakini si lazima yawe kwa lugha ya Kiarabu; lakini baadhi ya mafaqihi wengine hawaoni kusoma maneno ya kufunga tungo ya waqfu kuwa ni lazima. Kwa mtazamo wao ni kwamba; hata kama tutaandika kitu au kufanya jambo ambalo maana yake litamaanisha kuweka waqfu, basi waqfu huo utakuwa ni sahihi.
  • Kulingana na fatwa ya baadhi ya mafaqihi, katika katika suala la uwekaji waqfu ni kwamba; Hakuna haja ya kukubali na kuridhika kwa wale wanao wekewa waqfu, iwe ni waqfu binafsi wa jumla jamala (waqfu huria). Ila kulingana na fatwa za baadhi ya wanazuoni wengine ni kwamba; Katika uwekaji waqfu binafsi (waqfu kwa watu maalumu), ni sharti kwa mtu au watu ambao wamewekwa wakfu kukubali, na ridhaa yao ni sharti katika uhalali wa waqfu huo.
  • Haiwezekani kuweka waqfu mali kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe. Hata hivyo, ikiwa mtu ataweka waqfu mali kwa ajili ya watu fulani, kwa mfano kwa ajili ya maskini, kisha baadae mwenyewe akawa maskini, katika hali hiyo, anaweza kutumia manufaa ya mali hiyo.
  • Ikiwa mali ya waqfu itaharibika, haitatoka nje ya waqfu; lakini ikiwa inaweza kutengenezwa, basi inapaswa kutengenezwa. Ikiwa haiwezi kutengenezwa, inapaswa kuuzwa na pesa zake zitumike katika kazi inayokaribiana na maoni ya mwekaji waqfu. Ikiwa hii pia haiwezekani, basi pesa hizo zinapaswa kutumika katika kazi ya hisani. [40]

Seti ya Orodha ya vitabu (bibliografia)

Baadhi ya vitabu katika uwanja wa waqfu ni kama ifuatavyo:

  • Uwakifu katika Fiqhi ya Kiislamu na Nafsi Yake Katika Ustawi wa Uchumi وقف در فقه اسلامی و نقش آن در شکوفایی اقتصاد, kilichoandikwa na Muhammad Hassan Hairi Yazdi. Kitabu hichi kimejadili ndani yake masuala kadhaa kuhusiana na mada ya waqfu, miongoni mwayo ni; Umuhimu wa waqfu katika Uislamu, historia yake kabla ya Uislamu, waqfu kwenye jamii ya wasiokuwa Waislamu, mali za waqfu za bwana Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu (a.s), hukumu za fiqhi za waqfu kulingana na mtizamo ya madhehebu ya Kiislamu, istilahi za waqfu, jinsi ya kutumia mapato ya waqfu, nafasi ya waqfu katika kufanikisha malengo ya uchumi wa Kiislamu.
  • Hukumu za Waqfu Katika Sheria ya Kiislamu احكام الوقف فى الشريعة الاسلاميه, kilichoandikwa na Muhammad Abed al-Kabisi. Kitabu hichi kimechapishwa kwa jina la "Ahkame waqfu Dar Shari’at Islami", baada ya kufasiriwa na Ahmad Sadiqi Goldar. Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1397 Hijria/1977 Miladia nchini Iraq. [41] Katika kitabu hichi, mmejadiliawa maoni ya wanazuoni wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu (Jaafaria, Hanbali, Hanafi, Shafi'i, Zaidi, Dhahiriyya na Maliki) kisha mwandishi akaelezea maoni yake katika kila nyanja zilizo tafitiwa ndani yake. [42]
  • Kamusi ya istilahi za uwakifu فرهنگ اصطلاحات وقف. Kitabu hichi ni tafsiri ya المصطلحات الوقفیه, kilichoandikwa na Abdullah Atiiq, Izzuddin Tuuni na Khalid Shuaib, ambacho kimetafsiriwa na Abbas Ismailizadeh. Katika kitabu hichi, mna mada 106, zilizo jadili masuala ya waqfu kupitia mitazamo ya madhehebu manne maaru ya Kisunni. [43]
  • Hukumu za uwakifu katika sheria tukufu ya Kiislamu احکام الوقف فی الشریعة الاسلامیة الغراء, kilichoandikwa na Jaafar Sobhani. Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi, ni kwamba; katika kitabu hichi, mmetumika juhudi kubwa ili kutatua baadhi ya masuala ya waqfu, ambayo husababisha ugumu kwa wasimamizi wa waqfu. [44]