Fiqhi

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Fikihi)

Fiqhi (Kiarabu: الفقه الإسلامي) ni elimu yenye juhudi ya kuhakiki vyanzo vya sheria (Qur’an, Sunna, Akili na Ijmaa) kwa ajili ya kupata hukumu za kisheria kuhusiana na majukumu ya kidini ndani ya dini ya Kiislamu. Mada na mlengwa wa elimu ya fiqhi ni matendo ya hiari kwa wale waliopewa jukumu ya kisheria, yaani kwa wale wanao andamwa na sheria kulingana na masharti ya yaliowekwa juu uandwamaji huo. [Maelezo: Matendo ya mwanadamu ya yamegawika sehemu mbili; metendo ya hiari na matendo yasio ya hiari. Kinachokusudia kwenye suala la matendo ya hiari katika makala hii, ni yale matendo ambayo hatamu za utendekaji wake ziko mikononi mwako, kama vile kula kutembea, kuchukua kitu fulani, kuuza, kununua, kuoa, kuacha na kadhalika. Matendo ya hiari pia yana ambatanisha majukumu yote ya kisheria, kama vile; kusali na kufunga, kutoa Zaka, kuhiji na kadhalika.

Wanazuoni wanaona kuwa lengo la kuandaa fiqh ni kuzalisha masuala ya kuandaa maisha ya kidunia ya wale waliopewa jukumu (waliokuwa tayari wamesha andamwa au wamesha elekewa na kivuli cha sheria) pamoja na kuwapa mwisho wa kufuzu siku ya Kiama. Kwa mujibu wa maoni ya baadhi yao, elimu ya fiqh inashika nafasi ya pili baada ya kumjua Mwenyezi Mungu (elimu ya tauhidi). Kulingana na hadhi yake hiyo, wanazuoni wamesema kwamba; kujifunza elimu ya fiqhi, ni wajibu kifaya.

Kuna nadharia mbili zilizotajwa kuhusu mipaka ya uwanja wa elimu ya fiqh; Katika nadharia ya kwanza, fiqh inachukuliwa kuwa ni fani inayo angaza nyanja zote za kijamii, kisiasa, kijeshi na kitamaduni kwa ajili ya wale waliokamilisha masharti ya kuandamwa na sheria za Kiismamu. Kwa mujibu ya nadharia pili, elimu ya fiqh ina jukumu la kufafanua baadhi tu ya hukumu za kisheria zinazo husiana na masuala ya maisha ya mwanadamu. Inasemekana kwamba wakati wa maisha ya Mtume (s.a.w.w) ambao ndio wakati ulio anzishwa fiqhi, au enzi ya kuanzishwa kwa sheria, Waislamu walipokea hukumu zao za kisheria kutoka kwenye Qur'an na Sunna za Mtume (s.a.w.w). Baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Waislamu waligawika katika madhehebu mawili ya Shia na Sunni, kuzaliwa kwa madhehebu haya ndio sababu msingi ya kuiibuka kwa mielekeo miwili mkubwa ya kifiqhi katika fiqhi ya Kiislamu.

Mashia waliamini kwamba Imam Ali (a.s) pamoja na Maimamu Maasumu wa kutoka kizazi chake ni katika mwendelezo wa uwepo wa Mtume (s.a.w.w) (Mwendelezo wa kazi ya utume) na wafasiri wa Qur'an na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w). Mashia wanachukua hukumu zao za kisheria (fiqhi) kutoka kwa Maimamu hao, wakati Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaelekea kwa masahaba, masahaba nao walitoa fatwa kwa kurejelea Qur'an na Sunna za Mtume (s.a.w.w) pamoja na kupitia juhudi za kijitahadi.

Madhehebu ya fiqh ya Shia baada ya ya kumalizika enzi za kuanzishwa kwa sheria na enzi ya uwepo wa Maimamu maasumu (a.s.), wameweza kuendeleza fani ya fiqhi katika vyuo mbalimbali vya kifiqh vilivyopa katika miji kama vile; Qom, Ray, Baghdad, Hilla, Jabal al-Amil, Esfahani, Karbala na Najaf. Kuanzia wakati huo hadi zama za sasa, vyuo hivi vimepita nyakati tofauti za maendeleo na udhaifu katika juhudi zake za kiijitahidi katika fiqhi. Madhehebu ya fiqhi kwa upande wa Sunni pia nayo baada ya zama za masahaba na taabi'in (kuanzia mwanzo wa karne ya pili hadi mwanzoni mwa karne ya nne) yalipita katika hatua tofauti. Wao katika katika hatua hizo, waliweza kuzalisha madhehebu mengi ya fiqhi, ambayo mwishowe kupatika madhehebu manne maarufu ya fiqhi, ambayo ni; Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hanbali. Ukiachana na madhehebu ya fiqhi ya Shia na Sunni, pia kuna madhehebu mawili ya fiqh ambayo ni madhehebu ya Kiibadhi na Zaidiyyah, nayo pia ni madhehebu yenye fiqhi iliyoandikwa na hadi leo madhehebu hayo yana wafuasi wake maalumu.


Umuhimu

Sayansi ya fiqhi ni miongoni mwa elimu zilizo pewa mazingatio makubwa na kuwavutia wafuasi wa madhehebu ya Kiislamu. [1] Hajwa Tha'alabi (faqihi na mtaalamu wa fani ya usuli al-fiqhi wa madhehebu ya Maliki), anaichukulia elimu ya fiqhi kuwa ni miongoni mwa fani yenye fakhari (fahari) kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa maoni yake ni kwamba; maisha ya jamii ya Kiislamu yamehuika kupitia fiqhi na ni elimu tegemezi katika jamii ya Wislamu. [2] Allama Hilli katika utangulizi wa kitabu chake "Tahrir al-Ahkam", akibainisha umuhimu wa elimu ya fiqhi alisem; elimu yenye hadhi zaidi baada ya elimu ya tauhidi (kumjua Mungu), ni elimu ya fiqhi; Kwa sababu ya kwamba; elimu hiyo ndio inayo panga na kunadhimu mambo yanayohusiana na maisha ya kidunia, pamoja na baada ya ufufuo. [3] Vile vile alizingatia suala la kujifunza elimu ya fiqhi, kuwa ni faradhi tosheleza (faradhi kifaya) kwa mujibu wa Aya ya Nafar [4].

Sahib al-Maalam (Hassan bin Zeinu al-Ddiin pia aliichukulia elimu ya fiqhi kuwa ndiyo elimu tukufu na bora na yenye nafasi ya pili baada ya elimu ya kumtambua Mwenyezi Mungu; Kwa sababu hii ni elimu inayohusiana na amri za Mwenyezi Mungu, na kuwa na wewe juu ya amri za Mwenye Ezi Mungu jambo ashimu adhimu sana. Na kwa kuwa welewa huo hufikiwa kupitia elimu ya fiqhi, jambo hili huifanya elimu hii kuwa ni elimu yenye hadhi kubwa mno. Kwa upande mwengine, elimu ya fiqhi hupanga maisha ya kivitendo ya mwanadamu katika nyanja za mtu binafsi na za kijamii, na ndio chimbuko la ukamilifu na maendeleo ya mwanadamu. [5]

Imam Khomeini, katika kueleza umuhimu na nafasi ya fiqhi, alisema kwamba; elimu hii ndiyo nadharia halisi na kamilifu ya uwendesha na utawala wa mwanadamu kuanzia utotoni hadi kaburini. [6]

Maana ya Fiqhi

Mafaqihi wa Kiislamu [7] wameifafanua fani ya fiqhi kama elimu ya sheria za kidini inayo chopoa hukumu za vitawi vya sheria (sheria reja reja) kutoka katika hoja zake kuu au vyanzo vyake vikuu. [8] Tunaposema vyanzo vikuu tunakusudia sehemu mnamotolewa au kuzaliwa hukumu za kifiqhi, nazo ni;Qur’an, Sunna, Ijmaa na Akili. [9] Katika ufafanuzi mwingine, fiqhi imearifishwa kama elimu inayo shughulikia aina mada za aina mbili:

  • Kueleza na kutoa huku juu ya vitendo vya wajibu na kurekebisha uhusiano uliopo baina yao na Muumba wao, kama vile ibada zinazomfunganisha mja na Mola wake, ambazo mfano wake ni kama: sala, saumu, zaka na hija.
  • Kueleza, kufafanua na kurekebisha mahusiano baina ya mja ambaye tayari amesha andamwa na sheria na jamii na watu wengine, kama vile uuzaji, ununuzi, ndoa na talaka. [10]

Mada ya fiqhi na lengo lake

Fiqhi ni elimu inayo jadili hukumu tano za msingi, ambazo ni; wajibu, haramu, mustahabbu (la sunna ambalo ni vyema kulitenda), makruhu (linalo chukiza kulitenda) na mubaha (tende huru ambalo limenyamaziwa na sheri). Pia elimu hii inajadili usahihi na ubatilikaji wa matendo mbali mbali yanayo huisiana na kufungamana na misingi hiyo mitano. [11] Hii ndio sababu ya kusemwa kwamba; mada ya elimu ya fiqhi, ni kujadili vitendo na tabia hiari za watu waliopewa majukumu ya kisheria (walio kuwa tayari wamesha andamwa au wametandwa na kivuli cha sheri). [12]

Kulingana na kauli za wanazuoni wa fiqhi, lengo la sayansi ya fiqhi ni kweka kwenye meza ya jamii masuala muhimu yenye uwezo na dhamira kudhibiti na kunadhimu maisha ya kidunia (ya mtu binafsi na kijamii) na kwa ajili ya kufikia furaha ya siku ya mwisho (katika maisha ya Akhera). [13]

Vyanzo vya fiqhi

Kwa mujibu wa mafaqihi wote wa Kiislamu, chanzo muhimu zaidi cha kupata hukumu za Sheria ni Qur'an [14] Kuhusu vyanzo vingine vya fiqhi, kuna tofauti za maoni kati ya madhehebu mbali mbali:

Shia

Mbali na Qur'an, Mafakihi wa Kishia pia wanategemea Sunnah, Ijmaa na Akili, kama ni vya kupata hukumu za Sheria. [15] Bila shaka Akhbari ni moja ya kundi la Mafakihi wa Kishia wanaozingatia Qur'an na Sunna tu, kama ndio vyanzo vya hukumu za Sheria. [16] Baadhi yao, kama vile Muhammad Amin Istar-abadi, alikuwa na shaka juu ya kushikamana na Qur'ani Tukufu na anaamini kwamba hadhira (wanaohutubiwa) ya Qur'an ni Ahlul-Bayt (a.s) na mujtahid hawezi kutegemea Qur'ani katika kufikia hukumu ya sharia. [17] Kwa upande mwingine, baadhi kama vile Muhammad Sadiqiy Tehraniy (faqihi na mfasiri wa Kishia, aliye zaliwa mwaka 1305 na kufariki 1390 Shamsia) anaichukulia Quran kuwa chanzo pekee cha kupata hukumu za Sharia na kuizingatia Sunna kuwa ni sahihi kwa msingi wa Quran (ikiwa itawafikiana na Qur'ani). [18]

Tofauti baina ya Sunni na Shia

Mbali na Qur'an, mafaqihi wa madhehebu manne yanayo shikamana na fikra za Kisunni wanatumia Sunna, Ijmaa (makubaliano ya wanazuoni), na Qiasi (kukihukumu kitu kimoja kupitia hukumu ya kitu chengine chenye malingano na tabia inayo fanana nacho) ili kutoa hukumu za Sheria. [19] Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kisunni, Sunna ni ni jambo makhsusi liliruhusiwa kwa maneno, vitendo na takriru (ukimya wa Mutme (s.a.w.w) mbele ya amali fulani iliyotendeka mbele yake na akawa hakuikemea). [20] Kwa upande wa pili maafaqihi wa Kishia wanayachukulia maneno, matendo na takriru za maimamu maasumu (a.s) kuwa ni sawa na takriri ya Mtume (s.a.w.w), na chanzo cha kuaminika cha kufikia hukumu za Shariah ya Mwenyezi Mungu. [21] Mafaqihi wa Kisunni wanaamini ya kwamba; Ijmaa kama Ijmaa ni hoja na kielelezo tosha na ni chanzo kinacho jitegemea katika kuzifikia au kuchopoa hukumu za sheria. [22] Lakini kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi wa Kishia, Ijmaa ni sahihi iwapo tu itaweza kutoa mwongozo wa kuifikia kauli ya Imamu Maasumu itayopelekea kuifikia hukumu ya sheria. [23]

Waislamu wa Madhehebu ya Sunni pia hutumia vyanzo vingine vya ziada kama vile istihsan, masalihu mursala, na saddu al-dhari'a ili kupata hukumu za kisheria. [24] Hata hivyo, Muhammad bin Idris al-Shafi'i (mwanachuoni na mwanzilishi wa madhehebu ya Shafi'i katika fiqhi ya Sunni), anakubaliana na sadd al-dhari'a tu kati ya vyaza hivyo vitatu vya ziada. [25] Kwa mujibu mtazamo wa wanachuoni wa madhehebu ya Shia, hakuna hata chanzo kimoja kati ya hivyo chenye uhalali katika kuzifikia hukumu za kisheria. [26]

Kulingana na maelezo ya Muhammad Abu Zahra (aliyafariki mwaka wa 1395 Hijiria), ambaye ni mwanachuoni na mwanahistoria wa madhehebu ya Sunni, ni kwamba; wanachuoni wa madhehebu ya Zaidiyyah, ambao ni miongoni mwa madhehebu ya Shia, wamegungamana na madhehebu ya Hanafi katika kutumia kiasi, istihsan, na masalih al-mursala katika kupata baadhi ya hukumu za kifiqi. [27]

Mipaka ya elimu ya fiqhi

Kulingana na maelezo ya mwanachuoni wa Kiirani na mtafiti wa fiqhi, Mehdi Mihrizi (aliyezaliwa 1341 Shamsia) ni kwamb; hakuna tofauti ya maoni kwamba fiqhi inashughulikia vitendo vya kibinafsi na vya kijamii vya wale wanao andamwa na hukumu za Kiislamu. Hata hivyo, kuna khitilafu ya maoni iwapo fiqhi inahusisha mambo yote ya kijamii ya mwanadamu na kueleza hukumu zake, au inashughulikia tu baadhi ya mambo hayo.[28]

Kulingana na mtazamo wa Imam Khomeini, hukumu za fiqh zinaangazia nyanja zote za maisha ya kijamii ya waliopewa majukumu ya kisheria. Yeye anaamini kwamba; serikali ni akisiko linalo onyesha uso wa vitendo vya kifiqhi katika kukabiliana na changamoto zote za kijamii, kisiasa, kijeshi na kitamaduni. [29] Pia, katika kitabu "Al-Mawsoo'ah al-Fiqhiyyah al-Kuwaitiyyah" (ensiklopidia ya fiqhi ya Sunni katika juzuu ya 45), inadaiwa kuwa elimu ya fiqhi ina suluhisho juu ya masuala yote ya mwanadamu na ina uwezo wa kutibu matatizo yote maishani mwake. Hii ni kwa sababu hakuna hata kitendo kimoja anacho kifanya mwanadamu ambacho hakina uamuzi wa kifiqhi, na elimu ya fiqhi inawajibika katika kutoa hukumu juu ya uhalali au uharamu wa kitendo hicho. [30]

Kinyume na maoni haya, wanamageuzi wa kidini wa kisasa, kama vile Abdulkarim Soroush na Muhammad Mojtahid Shabistari wamekataa kwamba elimu ya fiqhi inajibu mahitaji yote ya kibinafsi na kijamii ya maisha ya binadamu. [31] Soroush anaamini kwamba; ni sehemu ndogo tu ya masuala ya jamii ambayo kiasili yanahusiana na elimu ya fiqhi, bali kuna masuala mengi mengine ambayo yanayohusiana na elimu ya siasa na uchumi, ambayo fiqhi haina mpango wa kuyashughulikia masuala hayo, na kupata suluhisho katika jamii juu yake, panahitaji kuwepo elimu ambazo ni bidhaa na zao la tafakuri na uzoefu wa binadamu. [32]

Mojtahed Shabestari pia amesema kwamba maandishi ya kidini kuhusu siasa, yaani mambo yanayohusu na adhabu mbalimbali za kifiqhi, fidia, kisasi na hukumu nyingine za kifiqhi, yanapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa kihistoria; kwa kuwa mengi yao yanalenga maswali yaliyokuwapo katika enzi za kuzaliwa kwa sheria, na dalili zake haziashirii hukumu za enzi ya sasa na wala haziendi sawa na zama hizi, pia haziwezi kufanya kazi katika zama zetu za leo. [33]

Mipaka ya fiqhi katika mada mbalimbali

Mada ambazo hujadiliwa na hukumu za kifiqhi zimegawanywa katika makundi mawili makuu:

  • Mada kuhusiuana na vitu “sirfatun صرفه” au “a’ayanu اعیان”: Mada ambazo utambuzi wake hauhitaji hoja, na ni wazi kabisa kwamba kila mtu anaelewa maana yake, [34] kama vile dhana ya maji ambayo ni wazi kwa kila mtu na ijtihadi haisaidii chochote katika kuielewa dhana ya maji. [35] Kulingana na maoni ya wanachuoni wote wa Kiislamu, ufafanuzi wa mada hizi uko nje ya uwanja wa mwanazuoni. [36]
  • Mada “mustanbata مُستنبطه: Mada ambazo haziko wazi kwa watu wote katika welewa na utambuzi wa dhana yake, pamoja na utambuzi wa mipaka yake. Mada hizi kikawaida huwa zinahitaji hoja na vielelezo. [37] Mada hizi zinagawanywa katika makundi matatu:
  1. Mada za kisheri: Mada ambazo mtengenezaji wa sheria ameziunda na kuzianzisha mwenyewe; kama vile sala, Udhu, ghusli (kogo au josho) na tayammum (kutayamamu). [38] Kulingana na maoni ya wanazuoni wote, ufafanuzi wa kundi hili pamoja na hukumu zake za kisheria, huwa ni jukumu la mwanachuoni. [39]
  2. Mada zinazotegemea welewa wa jamii: Mada ambazo welewa wa dhana yake na utambuzi wa mipaka yake huwa ni jukumu la wanajamii. [40]
  3. Mada za lugha: Mada ambazo utambuzi wa mipaka yake sio rahisi kwa kila mtu na inahitaji kurejea kwenye sheria za lugha na kanuni zilizowekwa na wanalugha maalum. [41]

Kuna tofauti ya maoni kuhusu wajibu wa mwanachuoni juu ya kutambua mada zinazotegemea welewa wa jamii na mada za zinazohusiana na lugha. [42] Wanachuoni kama vile Mirzai Qomiy, [43] Muhammad Kadhim Tabatabaei Yazdiy [44] na Sahib al-Jawahir [45] wamesema kuwa ufafanuzi wa mada hizi ni nje ya majukumu ya mwanachuoni. Kwa upande mwingine, wanachuoni kama vile Sayyid Mohsin Hakim na Sayyid Abu al-Qassim Khui, wamesisitiza juu ya jukumu la mwanachuoni katika ufafanuzi wa aina hii ya mada. [46]

Kashifu al-Ghataa amegawanya mada za sehemu mbali; mada ngumu ambazo si rahisi kueleweka, na mada za kawaida za lugha ambazo ni nyepesi kueleweka, na akasema kuwa aina ya kwanza haiwezi kutambuliwa isipokuwa kwa kurejea kwenye hoja na vielelezo vya kisheria. Kwa hivyo, mada hizo ni kama mada za kisheria, ziko katika jukumu la mwanachuoni. [47]

Madhehebu za kifiqhi

Kuna madhehebu mawili makuu ya kifiqhi katika ulimwengu wa Kiislamu, ambayo ni madhehebu ya fiqhi ya Shia na madhehebu ya fiqhi ya Sunni. Kila moja kati yake ni yenye kutofautiana kimisingi. [48]

Madhehebu ya kifiqhi ya Shia

Madhehebu ya kifiqhi ya Shia, baada ya zama za kuwepo kwa Maimamu maasumu (baada ya kughibu kwa Imamu Mahdi Ghaiba yake Kubwa), [49] ni kama ifuatavyo:

Namba Jina Tarehe ya kuanishwa Mafaqihi mashuhuri Vanzo muhimu vya fiqhi Sifa maalumu
1 Qom wa Rai (ray) Mwanzoni mwa karne ya 4 hadi nusu ya kwanza ya karne ya 5 Ali bin Ibrahim Qummiy, Muhammad bin Ya’aqub Kulainiy, Ali bin Babawaihi Qummiy, Sheikh Saduq Al-Kafi, al-Sharai’I, Man laa Yahdhuhulfaqiif,

Al-Muqni’i

Kuhariri na kupanga kwa milango vyanzo vya Hadithi, kuenea kwa fiqhi iliyo tegemea Hadithi
2 Baghadi Karne ya 4

Hijiria

Ibnu ‘Aqil Omaniy, Ibnu Junaid Iskani, Sheikh mufidu, Sayyid Murtadha, Sheikh Tusi al-Ahmadi fil Fiqhi al-Muhammadi, al-Mutamassik Bihabli Aali al-Rasuli, al-Muqni’a, al- Mabsut Mwanzo wa kuhaririwa fani ya usulu al-fiqhi, kutumika kwa dalili za kiakili katika kuchopoa hukumu za fiqhi
3 Hilla Mwishoni mwa karne ya 6 Hijiria Ibnu Idris Hilliy, Muhaqqiqu Hilliy, Ahmad bin Taawus Hilliy, Yahya bin Said Hilliy, Allama Hilliy Al-Saraairu, al-Mu’utabar, Sharai’u al-Islam, al-Jami’u al-Sharai’u, Tahriru al-Ahkam, Mukhtalafu al-Shia Uandishi wa fiqhi kwa vielelezo vya hoja (fiqhu al-Istidlali), kukua kwa usulu al-Fiqhi, mpangilio mpya wa milango ya kifiqhi
4 Maktabu Jabalu ‘Aamil Karne ya 8 Hijiria Shahidu Awwal, Shahidu al-Thani, Hassan bin Zainuddin ‘Aamili, Sayyid Muhammad Musawi ‘Aamili Al-Lum’atu al-Damashqiyya, Masaliki a-Afham, Madariku al-Ahkam, Muntaha al-Jamaan. Kuhaririwa kwa kanuni za kifiqhi, kupambazua Hadithi za Kutubu al-Arba’a, kuanzisha upya utafiti wa elmu alrijali, kupambazua na kunadhimu tafiti za fani ya sulu al-fiqhi, kutilia mkazo juu ya milolongo ya wapokezi wa Hadithi
5 Maktabu ya Isfahani Karne ya 10 Hijiria Muhaqqiq Karaki, Sheikh Bahai, Muhammad Taqi Majlisi, Muhammad Baqir Majlisi, Muhaqqiq Khansari, Fadhil Hindi, Muhaqqiq Ardabili, Faidh Kashani Jaami’u al-Maqasid, raudhatu al-Muttaqiin, Majma’u al-Faida wa al-Burhan, Mafatihu al-Sharaai’I, Kashfu al-Litham Kuhaririwa kwa Insiklopedia za Hadithi, kupewa kipau mbele fiqhi ya kisiasa
6 Maktabu Karbala Karne ya12 Muhammad Baqir Wahid Bahbahani, Sayyid Ali Tababai, Sayyid Jawad Husseini ‘Amili, Mulla Mahdi Nairaqi, Mulla Ahmad Nairaqi, Mirzai Qummi, Sayyid Muhsin A’araji Riadhu al-Masail, Mustanadu al-Ahia, Jami’u al-Shitaati, Mafaatihu al-Karama Kupambana dhidi Ikhbariyyuna, kufufua fiqhi ya ijitihadi, kufikia upeni fani ya usuli al-fiqhi
7 Maktabu al-Najaf Karne ya 13 Hijiria Muhammad Hassan Najafi, Sheikh Ansari, Akhund Khurasani, Sayyid Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi, Agha Ridha Hamadani, Sayyid Muhsin Hakim, Sayyid Abu al-Qasim Khui Jawahiru al-Kalam, Makasib, ‘Urwatu al-Wuthqa, Misbahu al-Faqih, Mustamsaku fi Sarhi al-‘Urwatu al-Wuthqa, al-Tanqiih Mabadiliko katika fiqhu al-Istidlali, uvumbuzi mpya katika fiqhi na usuli al-fiqhi, kuanza kwa kufumo uwandishi juu ya mihadhara ya masomo ya fiqhi na usulu al-fiqhi
8 Maktabu Qum Karne ya 14 Sheikh Abdu al-Karim Hairi, Sayyid Muhammad Burjurdi, Sayyid Ruhu al-llahi al-Khomeini, Muhammad Ali Araaki,Sayyid Muhammad Ridha Gulpaigani, Muhammad Fadhil Lankaarani, Hussein Ali Muntadhari Tahriru al-wasila, al-Durru al-Mandhud fi Ahkami al-Hudud, Dirasatu fi Wilayati al-Faqihi wa Fiqhu al-Ddaulati al-Islamiyya, Tafsilu al-Shari’a Kupewa kipau mbele juu ya fiqhu al-Siasa (fiqhi ya kisisa), kuingia kwa masuala ya fiqhi kwenye sheria za nchi, kujadili masuala mapya kama vile bink, bima na masuala mapya kuhusiana na afya katika fiqhi

Madhehebu ya kifiqhi kwa upande wa madehebu ya Sunni

Madhehebu ya Kisunni pia ulikuwa na madhehebu kadhaa ya kifiqhi za ambayo baadhi yake yametoweka. [50] Madhehebu ya fiqhi yaliosalia hadi leo ni Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hambali. [51]

Namba Jina Mwanzilishi Mafaqihi mashuhuri Vyanzo vya fiqhi Wasifu wake
1 Hanafi Abu Hanifa (aliye fariki mwaka 150 Hijiria Abu Yusuf, Muhammad bin Hassan Shaibani, Abdu al-llahi bin Ahmad Nasafi, Muhammad bin Ali Hasgafi, Shamsu al-Aimma Sarkhisi Al-athar, al-Mabsut, Kanzu al-Daqaiq (fil Fiqhi al-Hanafi), al-Durru al-Mukhtar Kupewa kipau mbele, Qiasi, Istihsanu, na Maslihu al-Mursala, iwapo patakosekana hukumu ya qur’ni, Sunna za Mtume (s.a.w.w) na masahab
2 Maliki Malik bin Anas (aliyefariki mwaka 179 Hijiria) Abdurrahman bin Qasim, Asad bin Furat Tunisi, Abu Bakar Baqalani, Ibnu Rashdi, Shatibi, Abu al-Barakat Ahmad bin Muhammad Dardir Muwattau, al-Asadiyyah, al-Insaf, Bidayatu al-Mujtihid wa Nihayatu al-Muqtasid, al-Muwafaat, al-Sharhu al-Kabir Kupewa kipau mbele fatwa za watu wa Madina sambamba na Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya wanazuoni katika kusaka hukumu, hatua ya pili ni kufutu kwa kutumia Kiasi na Masalihu Mursala
3 Shafi’i Muhammad bin Idrisa Shafi’I (aliye fariki mwaka 2040 Hijiria) Ismail bin Yahya Muzani, Ibn Hajr Haitami, Ibrahim bin Muhammad Dasoqi, Jalaluddin Siyuti, Ali bin Muhammad Mawaridi, Yahya bin Sharaf Nawawi Al-Ummu, Mukhtasaru al-Muzani, al-Hawi al-Kabeer, al-Iqna'i fi fiqhi al-Shafi’i, al-Tanbiih fi fiqhi al-Shafi’i, Raudhatu al-Talibin Kufutu kwa misingi ya analogia (Kiasi), ikiwa kutapatika ashirio la hukumu katika Qur-aan na Sunnah, kuto toa fatwa kupitia Istihsanu na Masalihu Mursala
4 Hambali Ahmad bin Hambali (aliye fariki mwaka 241 Hijiria) Abul Khattab Baghdadi, Ibn Qudamah Maqdisi, Ibn Taimiyyah Harrani, Mansour Bin Yunus Bahuti Al-Hadaiya, Al-Mughni, Kashaf al-Qina'a Kuelemea zaid katika Hadith na kufuata fatwa za masahaba, Hadithi kupewa kipau mbele zaid; hata hadithi dhaifu na hadithu Mursala zilipewa kipau mbele kuliko kutumia Kiasi. [52]

Muundo au mjengeko wa fiqhi

Elimu ya fiqhi imekusanya ndani yake masuala tofauti [53] na ili kuwasilisha dhana sahihi juu ya masuala ya elimu hii, ilibidi ipangwe kwa utaratibu maalumu na sahihi, katika vitabu vukuu vya fani hii. Hatua hiyo ilitimia kwa kuyapanga masuala yake chini ya vichwa na sura zilizokusanya mada hizo za. [54]

Uainishaji wa milango ya fiqhi uliofanywa na Muhaqqiqq Hilli katika kitabu chake kiitwacho Sharai'u al-Islam, ni mojawapo ya kategoria mashuhuri katika fiqhi ya Shia ilioacha athari hata kwa wanafiqhi waliokuja baada yake. [55] Yeye aliigawanya fiqhi yote katika makundi manne ya jumla; fiqhi ya matendo ya ibada, mikataba, iqa'aat (mahakikisho ya haki fulani zenye kutegemea maamuzi ya pande moja tu; kama vile talaka, wakfu, zawadi...) pamoja na hukumu za kifiqhi, na akaweka kila moja chini ya kila kategoria yake. [56]

Abu Hamid al-Ghazali katika kitabu "Ehiyau Ulumu al-Din", [57] Ibn Jizyu Kalbi (faqihi wa madhehebu ya Maliki wa karne ya 8) katika kitabu "Al-Quwaaninu al-Fiqhiyyah", [58] Mahmoud Shaltut katika kitabu "Islam 'Aqida wa Shariah", [59] Mustafa Ahmad al-Zarqa katika kitabu "Mad-khalu al-Fiqhi al-Aam", [60] na Wahbah Zuhaili katika kitabu "Al-Fiqhu al-Islami wa Adillatuhu", [61] ni miongoni mwa wanachuoni na mafaqihi wa Kisunni ambao wamewasilisha sura za masuala ya fiqhi na kuipangilia kwa mfumu wa mada zake.

Historia ya sheria za fiqhi ya Kiislamu

Sheria za kifiqhi zilipatikana na kuzaliwa kwa ujio wa Uislamu. [62] Waislamu wa zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w) walifuata Qur'an na Sunnah (maneno, matendo na taqriru ya Mtume (s.a.w.w) katika kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu. Katika kipindi hicho, Mtume (s.a.w.w.) alihesabiwa kuwa ndiye mwenye mamlaka pekee ya kutoa hukumu za Sheria. [63] Kwa hiyo, baadhi ya wanazuoni wameziita zama za Mtume (s.a.w.w) kuwa ni zama za kuanzishwa kwa fiqhi au zama za kutungwa kwa sheria. [64] kufuatia kifo cha Mtume (s.a.w.w) na kwa kupita muda mrefu baada ya zama hizo, ambapo masuala mapya yalijitokeza, Masunni walirejea kwa masahaba na wafuasi wa bwana Mtume (s.a.w.w), na masahaba nao wakawabainishia hukumu za sheria kupitia Qur'an na Sunnah za bwana Mtume (s.a.w.w). Pale masahaba hao waliposhindwa kupata hukumu ya jambo fulani katika Qur'an na Sunnah, walifanya ijtihadi na kutoa fatwa kupitia ijitihadi zao. [65]

Kwa upande wa Mashia; mbali na Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume (s.a.w.w), wao wanawarejea Maimamu wao na wanayachukulia maneno yao kuwa ni sawa na maneno ya Mtume (s.a.w.w). [66] Kuanzia hapa, madhehebu mawili makubwa ya sheria ya fiqhi ya Kiislamu yalijitokeza, yaani fiqhi ya Imamiyyah (ya Mashia) na fiqhi ya Kisunni. [67]

Baada ya Sahaba na Tabi'in (tangu mwanzo wa karne ya pili hadi mwanzoni mwa karne ya nne) Madhehebu ya kifiqhi ya Kisunni ulitoka kwenye sakata za uzaaji wa madhehebu mbali mbali ya kifiqhi na hatimae kubakia na madhehebu manne maarufu za ambayo ni; Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hambali. [68] Baada ya hapo, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 4 hadi karne ya 13 Hijiria, harakati za ijtihad katika fiqhi ya Kisunni ilidumaa kwa sababu ya ufungikaji wa kufuata na kuiga fikra za madhehebu manne hayo. Licha ya ukweli kwamba; kulikuwa na wanazuoni kadhaa wa fiqhi walio jitokeza na kuandika vitabu mbali mbali vya fiqhi, ila suala hilo halikuweza haikuleta maendeleo makubwa katika uwanja wa ijitihadi. [69]

Kwa kuibuka kwa utawala Othmani katika karne ya 13 Hijiria, ilioshika hatamu kuanzia mwaka 1387 Hijiri, [70] na kutokana na upeo kwa uwanja na mamlaka kitengo maalumu cha kusimamia utunzi wa sheria ya uendeshaji wa mambo ya jamii na serikali, jambo hili liliweza kuleta mafuu kwa ajili yao. Kwa kuanzishwa kwa jarida la "Al-Ahkam al-Adliyyah", [Maelezo: Jarida hili lina idadi ya makala 1,851 za kisheria na linajumuisha vitabu 16 kuhusianan na mauzo, kodi, udhamini, utumaji fedha (mabadilishano ya mali na fedha), rehani, dhamana, zawadi, unyang'anyi (kufosi), upotevu (uharibifu na ubadhirifu), ushirikiano, wakala (uwakili), mawafikiano, kusamehe, maombezi, hajru (kumzuia mtu kutumia mali yake kutokana na tatizo fulani), kulazimishwa kutenda jambo, kukiri, ugomvi, haki, utoaji hukumu, usimamishaji wa hoja na viapo. Jarida hili lilianzishwa kwa amri ya serikali ya Othmaniyyah ili kupata nyenzo za mahakama na sheria za kiraia zenye nidhamu kutoka kwenye vyanzo vya fiqhi ya Hanafi na kuzitumia katika mahakama. (Zarqaa, Al-Madkhalu al-Fiqhi al-Aam, chapa ya mwaka 1425 Hijiria, Juzuu ya 1, ukurasa wa 226-227). 1] fiqhi ya Kihanafi ilipata hadhi maalumu na kupiga hatu muhimu katika nyanja mbali mbali. Kwas muda wa miaka mingi vitengo vya fiqhi, mafunzo na hatamu za maamuzi katika sekta za utoaji wa hukumu, zilishikwa na madhehebu ya Hanafi, ambapo madhehebu hayo ndiyo yaliokuwa madhehebu rasmi ya dola ya Othmaniyyah. Wao ndio waliokuwa wakitoa fatwa kwa muda mrefu, hadi kundi la wanamageuzi na wanafikra walipo vunja kizuizi hichi na hatimae kutumia madhehebu yote katika utunzi wa sheria za Kiislamu. [72]

Kwa mujibu wa nadharia za baadhi ya watafiti; fiqhi ya Shia imepitia vipindi saba vya kihistoria baada ya kumalizika enzi za utunshi wa sheri, yaani baada ya zama za Maimamu maasumu (a.s), hadi zama za sasa. Vipindi saba hivyo ni; Zama za kunadhimu milango ya fiqhi, ambayo ni katikati mwa karne ya 4 katikati mwa karne 5 Hijiria, enzi ya mabadiliko katika uwanja wa sheria (kifiqhi) na ijtihadi (karne ya 5), enzi ya kuzorota na kufuata mafaqihi waliotangulia (kutoka nusu ya pili ya karne ya 5 hadi mwisho wa karne ya 6), enzi za uamsho (mwamko) wa fiqhi (kutoka mwisho wa karne ya 6) hadi mwanzoni mwa karne ya 11), kuibuka kwa vuguvugu la Ikhbariyyuna (karne ya 11 hadi mwishoni mwa karne ya 12), enzi ya uamsho wa ijtihad (karne ya 13), enzi ya uvumbuzi wa mambo mapya ya kifiqhi (kutoka karne ya 13) na enzi ya fiqhi iliyoingia katika nyanja mbalimbali za kijamii (karne ya 14 hadi leo). [74]

Mbali na madhehebu mawili ya fiqhi; Shia na Sunni, pia kuna madhehebu mengine muhimu ndani ya Uislamu, nayo ni madhehebu ya Ibadhiyyah na Zaidiyyah nao pia wameratibu fani ya fiqhi kulingana na nadharia zao nazo zimebaki hadi zama za hivi sasa. [75] Mostafa Ahmad al-Zarqaa, mwanasheria na mwanachuoni wa Kisunni, anayazingatia madhehebu ya fiqhi ya Abadhiyyah na Zaidiyyah kuwa ni madhehebu yanayo karibiana na fiqhi ya Kisunni. [76]

Rejea

Vyanzo

  • Farāhīdī, Khalīl b. Aḥmad. Kitāb al-ʿayn. 2nd edition. Beirut: Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Gurjī, Abu l-Qāsim. Tārīkh-i fiqh wa fuqahā. Tehran: Intishārāt-i Samt, 1385 Sh.
  • Group of authors. Dāʾirat al-maʿārif-i fiqh-i muqārin. [n.p]. [n.d].
  • Jannātī, Muḥammad Ibrāhīm. Manābiʿ-i ijtihād az dīdgāh-i madhāhib-i Islāmī. [n.p]. [n.d].
  • Khurramshāhī, Bahāʾ al-Dīn. Dānishnāmah-yi Qurʾān wa Qurʾān pazhūhī. Tehran: Dūstān wa Nāhīd, 1377 Sh.
  • Mishkīnī, ʿAlī. Iṣṭalaḥāt fiqhī wa uṣūlī. 6th edition. Qom: al-Hādī, 1416 AH.
  • Muzaffar, Muḥammad Riḍā al-. Uṣūl al-fiqh. 5th edition. Qom: Muʾassisa-yi Ismāʿīlīyān, 1375 Sh.
  • Muzaffar, Muḥammad Riḍā al-. Uṣūl al-fiqh. 4th edition. Qom: Intishārāt-i Daftar-i Tablīghāt-i Islāmī-yi Ḥawza-yi Ilmīya-yi Qom, 1370 Sh.
  • Rabbānī, Muḥammad Ḥasan. Fiqh wa fuqahā-yi imāmīyya dar guzar-i zamān. Tehran: Chāp wa Nashr-i Bayn al-Milal, 1386 Sh.
  • Shahābī, Maḥmūd. Adwār-i fiqh. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād-i Islāmī, [n.d].