Mwanzo

Kutoka wikishia
WikiShia
Ensaiklopidia ya Maktaba Ahlul Bayt (a.s.), inayosimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s.)
570 Makala / mabadiliko 11,879 kwa Kiswahili

Makala ya Wiki

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani (Kiarabu: شهر رمضان المبارك) ni mwezi wa tisa katika kalenda ya kiislamu ya Hijiria ambapo ndani yake Waislamu wamefaradhishiwa funga ya swaumu. Katika Hadithi zimeelezwa fadhila mbalimbali za mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo mwezi huu umetajwa kuwa ni mwezi wa kualikwa na Mwenyezi Mungu, mwezi wa rehema, maghufira, baraka na machipuo ya Qur’an. Kwa mujibu wa hadithi, katika mwezi huu milango ya mbinguni na ya peponi hufunguliwa huku milango ya motoni ikifungwa. Usiku wa cheo kitukufu (Laylatul-Qadr) ambapo Qur’an ilishushwa ndani ya usiku huo, unapatikana katika mwezi huu.

Baadhi ya vitabu vingine vya mbinguni kama Taurati na Injili pia vilishushwa ndani ya mwezi huu. Ramadhani ndio mwezi pekee ambao jina lake limetajwa ndani ya Qur’an. Mwezi huu unaheshimiwa sana na Waislamu na una nafasi maalumu kwa wafuasi wa dini hii. Katika mwezi huu Waislamu huzingatia zaidi masuala ya ibada, dua na kuomba maghufira. Katika vitabu vya dua kumenukuliwa na kuelezwa amali na ibada mbalimbali zinazopaswa kufanywa katika mwezi huu.

Read more ...


Je, wajua ...
  • ... Kifo cha Fatima Zahra, binti ya Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa vifo vilivyo na utata zaidi katika Uislamu na hata kaburi lake halijulikani lilipo?
  • ... Kitendo cha kusengenya kimefananishwa na mtu kula nyama ya nduguye aliyekufa?
  • ... Ramadhani, ndio mwezi pekee jina lake limekuja katika Qur'an?
  • ... Aya ya 7 ya Surat al-Bayyinah ni miongoni mwa Aya ambazo zilizoteremka kuelezea fadhila na ubora wa Ali bin Abi Talib (a.s)?
  • ... Shia ndio madhehebu inayoamini na kuitikadi kuwa Khalifa au Kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w) anapaswa kuchaguliwa na M.mungu kisha kuainishwa na Mtume?
Makala Zilizo Pendekezwa


  • Futari « Ni mlo wa kwanza unaoliwa na mtu aliyefunga Saumu au ni mlo ambao mtu anautumia kufungulia Saumu yake.»
  • Daku «Ni chakula chochote ambacho huliwa na Waislamu wenye nia ya kufunga Swaumu kesho yake mchana, na imesisitizwa zaidi kuliwa chakula hicho muda kidogo kabla ya adhana ya Alfajiri.»
  • Akhera «Ni ulimwengu baada ya kifo na mauti na ni ulimwengu ujao baada ya maisha ya dunia.»
  • Sadaka za lazima «Ni wajibu wa kimali unaoelezewa katika Uislamu ambao unabeba maudhui mbalimbali kama vile zaka ya mali, zakat al-fitr na kafara.»
  • Kafara ya swaumu «Ni adhabu ambayo huwekwa kutokana na kubatilisha na kuharibu funga ya mwezi wa Ramadhan, funga ya nadhiri ya muda maalumu na pia kadhwaa au malipo ya funga ya mwezi wa Ramadhan ikiwa itaharibiwa na kubatilishwa baada ya adhana ya adhuhuri, funga ambayo ilikuwa ni wajibu kwa mukallaf (mwenye kuwajibishwa).»
  • Safari ya Kisheria «Ni safari ambayo ndani yake msafiri analazimika kusali sala zake kwa kupunguza (Sala za rakaa nne azisali rakaa mbili) na hapaswi kufunga Swaumu.»
Kategoria Kuu
Jamii inayoitwa Beliefs‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Culture‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Geography‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa History‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa People‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Politics‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Religion‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Sciences‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Works‎ haikupatikana