Ya Aliyu Ya Adhim (Dua)

Kutoka wikishia

Ya Aliyu Ya Adhim ni katika dua mashuhuri sana katika mwezi wa Ramadhani ambayo imetiliwa mkazo kuisoma kila baada ya Sala za kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni kutokana na ukweli huo ndio maana Waislamu wa madhehebu ya Shia huisoma dua hii kwa pamoja baada ya Sala za kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Dua hii imenukuliwa katika vitabu vya Iqbal al-A’mal, Misbah Kaf’ami na Zad al-Maad kutoka kwa Maimamu Sadiq na Kadhim (as) na katika dua hii kuna mafunzo ya kumtambua Mwenyezi Mungu, mwezi wa Ramadahni, Qur’an, Laylatul Qadr (usiku wenye heshima na cheo) na mafunzo ya adabu za dua.

Nafasi yake

Dua’ ya Ya Aliyu Ya Adhim ni miongoni mwa dua ambazo Ayatullah Makarim Shirazi anaamini kwamba, zina maana na madhumuni ya juu sana. [1] Kwa mujibu wa kile kilichosimuliwa na Allama Majlisi (aliyeaga dunia: 1110 H) katika kitabu cha Zad al-Maad kutoka kwa Imamu Sadiq (as) na Imamu Kadhim (as) ni kwamba, dua hii imeusiwa kusomwa kila baada ya kila Sala ya wajibu katika Sala za kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. [2] Ni kutokana na ukweli huo ndio maana Waislamu wa madhehebu ya Shia huisoma dua hii kwa pamoja baada ya Sala za kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Dua hii inaweza kuwa na athari muhimu kwa mtu za kumtambua Mwenyezi Mungu, kuufahamu vyema mwezi wa Ramadhani, kuitambua Qur’ani, kuutambua usiku wa cheo (Laylatu-Qadr) na adabu za kuomba dua. [3]

Nyaraka

Dua’ ya Ya Aliyu Ya Adhim, kwa mara ya kwanza ilinukuliwa na Sayyid Bin Tawus (aliyeaga dunia: 664 H) katika kitabu cha Iqbal al’Amal na akainasibisha na Maimamu Sadiq na Kadhim (as). [4] Kadhalika dua hii imenukuliwa na Kaf'ami (aliaga dunia: 905 H) katika kitabu cha Misbah [5] na Allama Majlisi (aliaga dunia: 1110 H) katika kitabu cha Zad al-Maad. [6] Hata hivyo dua ambayo imetajwa katika kitabu cha Misbah ina tofauti kidogo na ile iliyonukuliwa katika kitabu cha Iqbal al-A'mal na Zad al-Maad. Kwa mfano ibara ya:

«وَ هَذَا شَهْرٌ عَظَّمْتَهُ وَ كَرَّمْتَهُ وَ شَرَّفْتَهُ وَ فَضَّلْتَهُ عَلَى الشُّهُورِ»

“Na huu ni mwezi umeuadhimisha na umeutukuza, umeuthaminisha na umeufadhilisha kuliko miezi yote", imenukuliwa namna hii katika kitabu cha Iqbal al-A'mal na Zad al-Maad. [7]

Lakini katika kitabu cha Misbah imenukuliwa namna hii:

[8]«وَ هَذَا شَهْرٌ شَرَّفْتَهُ وَ عَظَّمْتَهُ وَ كَرَّمْتَهُ وَ فَضَّلْتَهُ عَلَى الشُّهُور

“Na huu ni mwezi umeuthaminisha, umeuadhimisha na umeutukuza, na umeufadhilisha kuliko miezi yote". Kadhalika ibara ya:

يا عَلِيُّ يا عَظِيمُ يا غَفُورُ يا رَحيم... ‏»[9]

Ewe Mtukufu, Ewe Mkuu, Ewe Msamehevu, Ewe Mrehemevu Imekuja katika nakala ya zamani ya kitabu cha Iqbal al-A'mal kwa sura hii:

[10]«يَا عَلِيُّ يَا عَظِيمُ يَا غَفُورُ يَا شَكُورٌ يَا رَحِيم‏...»

Ewe Mtukufu, Ewe Mkuu, Ewe Msamehevu, Ewe mshukurivu, Ewe Mrehemevu

Maudhui ya Dua

Ayatullah Makarem Shirazi anaamini kwamba, kila moja kati ya kipande cha dua hii ya "Ya Aliyu Ya Adhim" kina ujumbe. [11] Mwanzo wa dua kunabainishwa suala la kumtambua Mwenyezi Mungu na sifa zaa Muumba, na katika sehemu inayofuuata kunaashiriwa sifa maalumu za mwezi wa Ramadhani. Kuweko aina tatu za uongofu katika Qur'ani, kuashiriwa kuwa bora Laylatul Qadr kuliko miezi elfu moja na mafunzo ya adabu za dua ni miongoni mwa mafundisho mengine yanayopatikana katika dua hii ambayo Ayatullah Makarem Shirazi ameyabainisha. [12]

Matini ya Dua

يا عَلِيُّ يا عَظِيمُ يا غَفُورُ يا رَحيمُ، انْتَ الرَّبُّ الْعَظِيمُ، الَّذي لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْ‏ءٌ وَ هُوَ السَّميعُ الْبَصِيرُ، وَ هَذا شَهْرٌ عَظَّمْتَهُ وَ كَرَّمْتَهُ وَ شَرَّفْتَهُ وَ فَضَّلْتَهُ عَلَى الشُّهُورِ، وَ هُوَ الشَّهْرُ الَّذي فَرَضْتَ صِيامَهُ عَلَيَّ، وَ هُوَ شَهْرُ رَمَضانَ، الَّذي انْزَلْتَ فيهِ الْقُرْآنَ، هُدىً لِلنّاسِ وَ بَيِّناتٍ مِنَ الْهُدى‏ وَ الْفُرْقانِ، وَ جَعَلْتَ فيهِ لَيْلَةَ الْقَدْرِ وَ جَعَلْتَها خَيْراً مِنْ الْفِ شَهْرٍ. فَيا ذَا الْمَنِّ و لا يُمَنُّ عَلَيْكَ، مُنَّ عَلَيَّ بِفَكاكِ رَقَبَتي مِنَ النّارِ، فيمَنْ تَمُنُّ عَلَيْهِ، وَ ادْخِلْني الْجَنَّةَ بِرَحْمَتِكَ يا ارْحَمَ الرَّاحِمِينَ [13]

Tarjumi

“Ewe Mtukufu, Ewe Mkuu, Ewe Msamehevu, Ewe Mrehemevu. Ndiwe Bwana Mlezi Mkuu, Asiyefanana na chochote, Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. “Na huu ni mwezi umeuadhimisha na umeutukuza, umeuthaminisha na umeufadhilisha kuliko miezi yote. Nao ni mwezi ambao umenifaridhia kufunga, nao ni mwerzi wa Ramadhani. Ambamo umeiteremsha humo Qur’ani yenye kuwaongoa watu na yenye kudhihirisha wazi uwongofu na upambanuzi. Na umejaalia humo Usiku wa Cheo na umejaalia kuwa ni bora kuliko miezi elfu. “Basi Ewe Mwenye kuneemesha usiyeneemeshwa, nineemeshe kwa kuniachilia huru mbali na Moto nikiwa pamoja na unaowaneemesha. Na Uniingize Peponi kwa rehema Zako Ee Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. [14]