Nenda kwa yaliyomo

Kibaba cha chakula

Kutoka wikishia


Kibaba cha chakula (Kifarisi: مُدِّ طَعام) ni kiwango cha kibaba kimoja cha chakula ambacho makadirio yake ni gramu 750 (kilo kasorobo), chakula hicho kinaweza kuwa; unga, mchele, ngano au tende, kinacho tolewa kama ni fidia ya Swaumu na kafara katika fikihi.

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Kishia, watu ambao kutokana na uzee au ugonjwa hawawezi kufunga Swaumu ya mwezi wa Ramadhani au mwanamke mjamzito au anayenyonyesha ambaye hafungi Swaumu akihofia kwamba, kufunga Swaumu huenda kukamdhuru uhai wake yeye au mtoto aliye tumboni, na udhuru wake ukaendelea mpaka mwezi wa Ramadhani wa mwaka ujao, kisheria wanapaswa kutoa kafara ya kibaba kimoja cha chakula kila siku kwa anuani ya fidia na kumpatia masikini.

Kadhalika mtu ambaye siku kadhaa katika masiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yamempita na hakufunga kutokana na udhuru wa kisheria kama kuwa safarini n.k… kama baada ya kuondoka udhuru wake wa kisheria na kisha hakulipa kadhwa za siku hizo mpaka ikawadia Ramadhani ya mwaka mwingine, anapaswa kulipa kibaba cha chakula kwa kila siku zilizompita na hakuzilipa ikiwa ni kafara kwa anuani ya kuchelewesha. Kafara ya kufanya baadhi ya mambo ambayo mtu hapaswi kuyafanya akiwa amevaa vazi la ihramu pia ni kulipa fidia ya kibaba kimoja cha chakula.

Kiwango na Umuhimu

Lililo mashuhuri baina ya mafakihi ni kwamba, kiwango cha kila kibaba ni gramu 750 (kilo kasoro) na makusudio ya chakula ni ngano, mchele, ngano, unga na kadhalika. [1] Baadhi wamesema, kiwango cha kibaba pia ni mithqal 153.5 sawa na gramu 719 [2] na baadhi wamesema kiwango chake ni takribani gramu 900. Kiwango cha kibaba katika fikihi kinatumika kama kipimo cha kupimia kiwango cha kafara (fidia) na hilo limekuja na kuzungumziwa katika vitabu vya fikihi katika hukumu za swaumu, [4] dhihar (mtu kufananisha mgongo wa mkewe na mgongo wa mamake), Hija (mambo ya haramu kufanya kwa aliyevaa vazi la ihramu), [5] na kafara mbalimbali (fidia).

Kigezo cha kipimo cha fidia

Fidia au kafara ya kuchelewesha, ni kitu kinacholipwa kama mbadala wa siku ambayo mtu hakufunga swaumu. [6] Maeneo ambayo mtu anapaswa kutoa [7] kibaba kimoja au viwili vya chakula kwa anuani ya fidia ya swaumu ya kuchelewesha ni:

  • Kuchelewesha kadhwa ya swaumu ya mwezi wa Ramadhani mpaka kuwadia Ramadhani ya mwaka mwingine; mtu ambaye amechelewesha kadhwa ya swaumu ya mwezi wa Ramadhani bila udhuru wa kisheria mpaka ikawadia Ramadhani nyingine, anapaswa kumpatia masikini kibaba kimoja cha chakula katika kila siku ambayo ilimpita na hakulipa kadhwa yake mpaka ikawadia Ramadhani nyingine na hali ya kuwa hakuwa na udhuru wa kisheria. [8]
  • Mwanamke mjamzito na anayenyonyesha ambaye hafungi swaumu akihofia kwamba, kufunga Saumu huenda kukamdhuru uhai wake yeye au mwanawe aliyeko tumboni. [9]
  • Mtu ambaye ana maradhi ya kiu na hawezi kufunga swaumu.
  • Wazee ambao hawawezi kufunga swaumu au kufunga kwao swaumu kuna mashaka na tabu kubwa. [11]

Hukumu

Kuhusiana na kwamba, katika hili ni wajibu kutoa kibaba kimoja cha chakula au viwili kuna tofauti za kimitazamo [12], licha ya kuwa kutoa vibaba viwili kunaafikiana na ihtiyat(tahadhari) [13]. Pamoja na hayo, Marajii Taqlidi wanaona kuwa, kutoa kibaba kimoja cha chakula kunatosheleza. [14] Kadhalika kwa mujibu wa fat’wa ya Marajii Taqlidi kutoa fedha na thamani ya kibaba kimoja cha chakula kwa masikini haitoshi, bali maskini anapaswa kupatiwa asili ya chakula, isipokuwa kama kutakuwa na yakini kwamba, masikini atazitumia fedha hizo kwa ajili ya kununua chakula. [15]

Kigezo cha Kipimo cha Kafara

Kutoa kibaba kimoja cha chakula kumejaaliwa pia ni kafara ya kufanya baadhi ya mambo ambayo ni haramu kuyafanya kwa mtu ambaye yuko ndani ya vazi la ihramu kama vile:

  • Kuua ndege hali ya kuwa ndani ya vazi la ihramu. [16]
  • Kukata kila kucha kama katika majimui itakuwa ni chini ya kucha kumi katika hali ya ihramu. [17]
  • Kushindwa kulipa kafara na kutotekeleza ahadi na nadhiri. [18]

Kadhalika wamesema, mtu ambaye kwake ni tatizo na mushikili kuswali swala za sunna za kila siku ili anufaike na thawabu zake atoe kibaba kimoja cha chakula kwa ajili ya masikini. [19]


Rejea

Vyanzo