Nenda kwa yaliyomo

Udhu

Kutoka wikishia
Picha inayoonesha mtu akitia udhu

Udhu (Kiarabu: الوضوء) ni aina ya tohara katika dini ya Uislamu, inayopatikana kwa kuosha uso na mikono pamoja na kupangusa kichwa na miguu kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu tu, kwa nia ya kufanya ibada maalumu. Yapendekezwa Muislamu kuwa na udhu kwa kadri iwezekanavyo, na udhu kama udhu ni sunna, hata kama udhu huo hautakuwa umefungamanishwa na ibada nyingine. Lakini kwa upande mwingine, udhu ni moja ya sharti za ibada kadhaa kama vile; sala, tawafu pamoja na ibada nyinginezo ambazo hazipati uhalali wala usahihi bila ya kutawadha. Haijuzu mtu kugusa maandishi ya Qur'an wala majina ya Mwenyezi Mungu bila ya kutawadha. Inapendekezwa mtu kuwa na udhu pale aendapo msikitini au akitaka kusoma Qur'an tukufu. Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, hukumu ya udhu ilishuka Makka tokea mwanzoni mwa ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Bayana na ithibati kuhusiana udhu zimetajwa ndani ya Aya ya sita ya Surat al-Maida na pia ndani zaidi ya riwaya 400 zitokazo kwa Maasumina (watu watoharifu). Imeelezwa katika Hadithi ya kwamba; kutawadha na kukariri udhu juu ya udhu, hupelekea; mtu kutakasika kutokana na dhambi, kutoweka kwa hasira, maisha marefu, kung'aa kwa uso siku ya Kiama na kuongezeka kwa riziki.

Yawezekana mtu kutia udhu kupita moja kati ya mifumo miwili ya udhu; Kwa mfumo wa kuchirizisha maji juu ya viungu vipaswavyo kuoshwa na ksiha kuviosha kwa kupitisha mkono wake juu yake. Mfumo huu wa udhu unajulikana kwa jina la “udhu wa tartibi”. Mfumo wa pili ni mfumo wa kuchovya au kupitisha na kuvitelezesha viongo vya udhu vinavyostahiki kuoshwa kwenye maji. Mfumo huu wa kutawadha, huwa unajulikana kwa jina la “udhu wa irtimasi (udhu wa mchovyo)”. Katika mfumo wa kwanza (udhu wa tartibi), kwanza kabisa huanza kuoshwa uso, kisha huoshwa mkono wa kulia na halafu mkono wa kushoto. Baada ya hapo, hupanguswa kichwa kisha miguu kupitia unyevunyevu wa mabaki ya maji yaliomo katika mikono hiyo ualiopatikana baada ya kutiwa udhu mikononi humo. Udhu wa irtmasi (udhu wa mchovyo) ni sawa na udhu wa kawaida (wa tartibi), ila tu badala ya kuosha uso na mikono kwa kuchirizisha maji juu yake, uso na mikono mikono hiyo huchovya kwenye maji na kutelezeshwa ndani yake, kisha kichwa na miguu hupanguswa kupitia unyevunyevu wa mapaki ya maji yaliomo mikononi. Jambo muhimu la kukumbushana hapa, ni suala la kuchunga utaratibu katika kutekeleza udhu; katika aina zote mbili za udhu, yatakiwa mtu kuanza kuosha uso, kisha mkono wa kulia, kisha wa kushoto, na baada ya hapo apanguse kichwa chake, kisha mguu wake wa kulia halafu amalizie kwa kupangusa mguu wake wa kushoto. Ikiwa kutatokea dharura ya vidonda au majaraha ndani ya maeneo ya viungo vya udhu, hapo itabidi kutia udhu kupitia mfumo wa 'jabira'. Katika udhu wa jabira mtu hutakiwa kuoshwa zile sehumu zisikuwa na majaraha tu, na zile sehemu za majaraha hufungwa kwa kitambaa au plastiki juu yake, kisha hupanguswa kwa unyevunyevu wa maji tu.

Mashia na Masunni wanatofautiana katika suala la utiaji wa udhu, khitilafu hizo zipo katika namna ya kukosha mikono na namna ya kupangusa kichwa na miguu. Shia wanaamini ya kwamba; Ni wajibu katika kutia udhu, mtu aanze kuosha mikono yake kuanzia juu ya viwiko na kumalizia kumalizia vidoleni. Sunni wao wanaamini kwamba; Ni wajibu katika udhu mtu kuosha mikono yake kuanzia chini (vidoleni) na kumalizia juu (juu ya viwiko viwili). Kwa mujibu wa vyanzo vya Hadithi, hadi mwisho wa ukhalifa wa Omar bin Khattab, hapakuwa na tofauti kubwa katika suala la kutawadha miongoni mwa Waislamu, na wote walikuwa wakitawadha kupitia mfumo ule ule unaoaminiwa na Mashia Ithnaashariyyah. Khitilafu juu ya suala la udhu baina ya Sunni na Shia limeonekana kuripotiwa kuanzia zama za ukhalifa tatu (Othmani bin Affan).


Welewa wa dhana ya udhu

Maana ya udhu ni kuosha uso na mikono na kupangusa kichwa na miguu kwa namna maalum na kwa kwa madhumuni na nia ya kujikaribisha na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu. [1] Ibada hii ni miongoni sharti za usahihi wa sala na tawafu (kutufu), na vile vile ni sharti inayomruhusu mtu kuigusa Qur'an.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria; Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipokea mafunzo ya udhu kutoka kwa Jibril huko Makka. Mtume (s.a.w.w) alipokea mafunzo hayo ya udhu tokea mwanzoni mwa kutangaza ujumbe wake mtakatifu, naye aliwafunza watu jinsi ya kutawadha tokea wakati huo. [3]

Hukumu za udhu

Makala Asili: Aya ya Udhu

Namna ya kutawadha pamoja na umuhimu wake umetajwa wazi wazi ndani ya Qur'an na Hadithi. [4] Katika Qur'an hukumu na mfumo wa kutawadha unapatikana katika Aya ya sita ya Suratu Al-Maidah. Aya hii ni maarufu kwa jina la Aya ya wudhuu, [5] nayo ni kama ifuatavyo: ((یا أَیُّها الَّذینَ آمَنوا إِذا قُمتُم إِلَی الصَّلاةِ فَاغسِلوا وُجوهَكُم وَ أَیدیَكُم إِلَی الْمَرافِقِ وَ امسَحوا بِرُءُوسِكُم وَ أَرجُلَكُم إِلَی الكَعبَینِ)) ; "Enyi mlioamini mnapoinuka kwa ajili ya kusali, osheni nyuso zenu na mikono yenu hadi viwikoni, na -panguseni kwa maji- baadhi ya sehemu ya vichwa vyenu na -panguseni kwa maji- miguu yenu mpaka kwenye vifundo viwili. [7]

Kutawadha kama kutawadha -bila ya kuzingatia ibada nyingine zinazofanya kwa udhu- ni jambo lililopendekezwa, yaani ni mustahabu. [8] Pia kuna ibada kadhaa zinazoshurutishwa kutendwa kwa udhu, miongoni mwazo ni; sala zote (isipokuwa sala ya maiti), ibada ya tawafu, kugusa Aya za Qur'an pamoja na kugusa majina ya Mwenyezi Mungu. Kupitia nadharia ya “msingi wa tahadhari (ihtiat)”, ni kwamba; haifai mtu asiyekuwa na udhu kushika jina la Mtume (s.a.w.w), jina bibi Fatima Zahraa(a.s) pamoja na majina ya Maimamu 12 watakatifu. Ni jambo lililopendekezwa mtu kutia udhu kwa ajili ya mambo yafuatayo: Kwa ajili ya kwenda msikitini, kuzuru makaburi ya Maimamu, kusoma na kubeba Qur'ani, kugusa sehemu ya Qur'ani hata kama ni kava au ukingo wa Qur'an pamoja na kuzuru makaburi ya Waislamu. [11]


Sharti za udhu

  • Maji ya udhu yanapaswa kuwa safi (yasiwe najisi).
  • Maji ya udhu yasiwe na mchanganyo wa kitu chengine (kama vile marashi au manukato).
  • Maji na nafasi ambayo anatawadhia juu yake isiwe ni ya kufosi.
  • Chombo cha maji ya kutawadhia kisiwe cha wizi cha kufosi.
  • Chombo cha maji ya udhu kisiwe cha dhahabu au fedha.
  • Viungo vya udhu viwe safi (visiwe na najisi).
  • Kusiwe na kiszuizi juu ya viongo vya udhu kinachozuia maji kuingia viungoni.
  • Anatakiwa kutawadha kwa nia ya kujikurubisha bila ya unafiki.
  • Kufuata mpangilio wa viungo katika udhu kama ilivyoelezwa na Qur'ani.
  • Kuzingatia muwala (yaani kusipite pengo refu -la wakati- baina ya kuosha kiungo kimoja hadi chengine).
  • Usichukue msaada kutoka kwa mwengine katika kutawadha.
  • Maji yasiwe na madhara kwa anayetawadha.
  • Kuwepo wakati tosha kwa ajili ya udhu. [12]

Aina za udhu

Udhu hutimia kwa kupitia moja kati ya mifumo miwili ya udhu. [13] Mifumo miwili hiyo ya udhu ni; mfumo wa kuchururisha maji juu ya viungo vya udhu na kuvikosha kwa mujibu wa sharia kimoja baada ya kingine, mfumo huu unaitwa "mfumo wa tartibi". Mfumo wa pili wa kutawadha, ni mfumo wa "irtimasi” (udhu wa mchovyo), katika mfumo huu, mtu huchovya viungo vipaswavyo kuoshwa ndani ya maji na kuvitelezesha ndani yake. Iwapo mtu atakuwa na dharura ya majaraha, basi atatakiwa kutia udhu wa "jabira" ambapo yeye atakosha sehemu za viungo -zisizo na majaraha- vipaswazo kuoshwa, kisha ataweka kizuizi kama vile kitambaa au plastiki juu ya sehemu za majaraha, kisha atapangusa juu kiziwizi hicho kwa kupitisha mkono wenye umaji maji juu yake. Udhu kama huu huitwa udhu wa "jabira". [14]


Ufafanuzi zaidi juu ya udhu wa Tartibi

Mafunzo ya kutia nia na namna ya kuosha uso

Udhu wa tartibi: Katika mfumo huu wa udhu, ni lazima kwanza uanze kuoshwa uso; Ni wajibu kuuosha uso kuanzia maoteo ya nywele hadi mwisho wa kidevu, kwa kiwango cha upana wa kiganja cha mkono mmoja. Baada ya kukosha uso, huoshwa mkono wa kulia kisha hufuatia mkono wa kushoto, kuanzia juu kidogo ya viwiko viwili hadi vidoleni. Baada ya hapo, kupitia unyevu nyevu uliosalia mikononi katika kuosha mikono, hupanguswa mbele ya kichwa, yaani na juu ya paji la uso, kisha kwa unyevu huo huo uliobakia mokononi, hupanguswa mguu wa kulia kisha mguu wa kushoto . [15]


Ufafanuzi zaidi juu ya udhu wa Irmatasi

Makala Asili: Udhu wa Irtmasi (Mchovyo)
Mafunzo juu ya namna ya kuosha mikono

Katika udhu wa "irtmasi" baada ya mtu, kutia nia ya udhu, [16] huuchovya uso wake kwenye maji na kuutelezesha kwa nia ya kutawadha, kisha mikono yake. [17] Njia ya pili ya udhu wa "irtmasi" ni kwamba; kwanza atazamisha uso wake na mikono yake ndani maji, kisha atatia nia ya kutawadha hali viungo vyake vikiwa ndani ya maji, kisha atoe viungo vyake hivyo nje ya maji, kimoja baada ya kingine kama ulivyo utaratibu wa udhu. Kwa maana hiyo, kwanza kabisa yeye atatakiwa kuutoa uso wake, kisha mkono wake wa kuli na kisha mkono wake wa kushoto. [18] Katika udhu wa "irtimasi", baada ya mtu kumaliza kuosha uso na mikono yake, hapo ndipo atakapopangusa kichwa na mguu yake kupitia mabaki ya maji yaliomo mikononi mwake, kwanza atapangusa kichwa chake, kisha mguu wake wa kulia na kumalizia mguu wake wa kushoto. [19] Ni lazima ieleweke ya kwamba udhu wa “irtimasi” (udhu wa mchovyo) pia nao hufuata uratibu wa udhu wa kawaida. Kwa maana hiyo mweye kutia udhu wa “irtimasi”, hutakiwa kuanza kwa uso, kisha mkono wa kulia, kisha wa kushoto, halafu apanguse kichwa chake, kisha mguu wa kuumeni kwake na kumalizia kwa mguu wa kushoto. [20]

Mafunzo kuhusu kupangusa kichwa na miguu


Udhu wa Jabira

Udhu wa jabira: Iwapo mtu atakuwa na majaraha au kidonda katika moja ya sehemu viongo vyake vinavyostahiki kuoshwa au kupanguswa wakati wa kutia udhu, kiasi ya kwamba itakuwa haiwezekani kuoshwa au kupanguswa viungo hivyo, basi yeye atapaswa kutia udhu wa “jabira”. [21] Neno "jabira” lina maana ya kizuizi kinachowekwa kwenye majaraha wakati wa kutia udhu. [22] Katika udhu huu wa "jabira", yeye atatia udhu wake kwa kadiri iwezekanavyo, na zile sehemu ambazo hazitawezekana kuoshwa au kupanguswa kwa maji, atatakiwa kuziziba kwa kizuizi cha kitambaa au plastiki, na badala ya kuosha au kupangusa sehemu hizo, yueye atatakiwa kupitisha mkono wake juu ya kizuizi hicho alichoweka juu ya majaraha hayo. Yaani atapangusa kwa umaji maji tu bila ya kuchuruzisha maji juu yake. [23]

Si halali mtu kutia udhu wa jabira, sipokuwa katika hali ya kuwepo dharura ya kutowezekana kutia udhu wa kawaida, ambapo pengine maji yanaweza kuwa ni hatari, au kwa kuhofia kueneza najisi kupitia maji hayo, kutokana kuvunjika kwa moja sehemu za viungo vya udhu... au kutokana na dharura nyingine ambayo imepelekea mtu kutoweza tumia maji na kutawadha kama kawaida. [24]

"Katika baadhi ya dharura na hali fulani, Tayammum (udhu mkavu) huchukua nafasi ya udhu wa kawaida (udhu wa maji); kwa mfano; ikiwa muda wa kusali unakukimbia na ukwa huna muda wa kutosha wa kutia udhu wa kawaida kabla ya muda wa sala kuisha. Kiasi ya kwamba; iwapo yeye atakwenda kutia udhu, basi ya sala yake au sala nzima itakiuka wakati halisi wa sla hiyo. katika hali kama hiyo, utawajibika kutayamamu badala ya kutia udhu wa kawaida. [25] Zaidi ya hilo, pia iwapo maji yatakosekana, au iwapo maji yatakuwa na madhara kwa mtiaji udhu, hapo yeye atatakiwa kutayamamu. [26] Iwapo mtu atakuwa amekoga josho la janaba, hatakuwa na haja tena ya kutia udhu kwa ajili ya sala, na josho hilo litatosheleza na kukaa na fasi ya udhu. [27] Wanazuoni wamekhitalifiana juu ya aina nyengine za majosho (kama vile; hedhi, istihadha na nifasi), kwamba je majosho hayo hutosheleza au hayatoshelezi katika sula la udhu.


Vipi udhu hubatilika?

Udhu hubatilika katika sura kadhaa, katika vitabu vya fiqhi, vitu au mambo yabatilishayo udhu hujulikana kwa jina la hadathu al-asghar (tukio dogo). [28] Miongoni mwa hadathu al-asghar ni:

  • Kutokwa na mkojo, kinyesi au upepo kutoka katika moja ya sehemu zake za siri (tupu mbili).
  • Usingizi (ambao utakao pelekea masikio yasisikie na macho yasione), wazimu, ulevi na kukosa fahamu. [29]
  • Mambo yanayopelekea josho la wajibu; kama vile janaba na kugusa wafu. [30]

Kwa mujibu wa kauli ya Fadhil Moqdad; Baadhi ya mafaqihi wa Kisunni wanaamini ya kwamba, pia udhu hubatilika kupitia njia kugusana kwa ngozi kwa ngozi, kati ya mwanamume na mwanamke wasiokuwa maharimu. Tegemeo lao juu ya nadharia hiyo, ni kisomo cha Qur'an cha Kisaai, ambapo kwa kupitia kisomo chake yeye, Aya ya Surat al-Maida na Aya 43 ya Surat al-Nisaa, badala ya kusomwa "Laamastum", husomwa "Lamastum". [31] Ikiwa neno "لامَسْتُمُ" liliko katika Aya mbili hizo, litasomwa "Laamastum" litakuwa na maana ya kumuingila mwanamke (kutenda tendo la ndoa). Ila iwapo neno hilo litasomwa "Lamastum" litakuwa na maana ya "kumgusa mwanamke tu" hata kama hukufanya tendo hilo la ndoa. Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kishia, neno "لامَسْتُمُ" ni sitiari yenye maana ya kutenda tendo la ndoa. [32]

Tofauti kati ya udhu wa Shia na Sunni

Makala Asili: Aya ya udhu na namna ya kuosha mikono, na kupangusa juu ya khofu mbili (viatu maalumu)

Katika suala la kutawadha, kuna tofauti kati ya Shia na Sunni kuhusu namna ya kuosha mikono na pia jinsi ya kupaka kichwa na miguu. [33] Tofauti kati ya Shia na Sunni kuhusiana na udhu inatokana zaidi na tofauti ya kufasiri maana ya Aya ya sita ya Surat al-Maida, au tofauti ya usomaji wake. [34]

Mashia, wakitegemea riwaya kutoka kwa maasumina ambao ni Mtume (s.a.w.w), Maimamu watoharifu pamoja na bibi Fatima (a.s), [34] wameifasiri ibara ya Qur'an isemayo: ((و أیدیکم إلی المراف)) "Na osheni (mnapotia udhu) mikono yenu hadi viwikoni" wakisema kwamba; maana iliyokusudiwa katika Aya hiyo ni kwamba; Ni wajibu kuikosha mikono kuanzia juu, yaani kuanzia viwikoni na kuishia vidoleni. Madhehebu yote manne ya Kisunni yanaamini kinyume na imani ya Kishia katika suala hilo. Masunni wanaamini ya kwamba ni wajibu kuosha mikono kutoka chini kuelekea juu. [36]

Pia, kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi wa Kishia, ni kwamba; katika kutawadha, ni lazima (wajibu) kwanza kuuoshwa mkono wa kulia kisha mkono wa kushoto. [37] Hukumu hii mbele ya Masunni inachukuliwa kuwa ni mustahabu, na sio lazima kufanya hivyo. [38]

Katika suala la udhu, ni wajibu mbele ya Madhehebu manne ya Sunni kuosha miguu pamoja na vifundo vya miguu. [39] Ila katika suala hilo, Mashia wanaamini ya kwamba; lililo waji kuhusiana na miguu, ni kupaka miguu kuanzia ncha ya vidole hadi juu ya kinundu cha mguu. [40] Suala la kupangusa miguu na kichwa kupitia unyevu wa mabaki ya maji yaliobaki kwenye mikono, ni makhususi kwa madhehebu ya Shia tu peke yao. [41] Watu madhehebu ya Maliki na Hanafi, hawaamini kuwepo ulazima wa kutawadha kwa utaratibu maalumu (yaani kuaza uso kisha mkono wa kulia kisha..). Kwa upande wa pili madhehebu ya Shafi hawaoni kuwepo ulazima wa muwalat; yaani hawaoni ulazilima wa kufuluzisha kutoka kiungo kwenda kingine, bali waona kuwa mtu anaweza kutia udhu kiungo kimoja kisha akasubiri kidogo, halafu akaendelea kwenye kiungo kingine. [42]

Pia Shia na Sunni wamehitalifiana kuhusu namna ya kupaka kichwa. Mojawapo ya hitilafu hizo ni kwamba, kwa mujibu wa fikihi ya Mashia, yatosha kupaka kiwango kidogo tu, ilimradi ihisabike kuwa mtu amepaka sehemu ya kichwa chake, ila imependekezwa (ni sunna) kupaka kwa kiwango cha ukubwa wa vidole vitatu vilivyofungwa pamoja, na si zaidi hapo. [43] Na haijuzu mtu kupangusa (kupaka) kichwa chake kwa maji mapya, bali kupitia unyevu uliobaki mikononi mwake. [44] Hata hivyo, wanazuoni wa madhehebu ya Sunni wana maoni tofauti kuhusiana na jinsi ya kupangusa kichwa. [45] Kwa mujibu wa fiqhi ya Hambali, ni wajibu kupangusa kichwa kizima pamoja na masikio yote mawili ni [46] na ni lazima kutumia maji mapya katika kupangusa kichwa, na sio unyevu wa maji uliobaki mikononi. [47] Kwa maoni ya fiqhi ya Maliki, ni lazima kupangusa kichwa kizima, [48] na katika fiqhi ya Hanafi, ni wajibu kupangusa robo ya kichwa. [49] Mashafi wanaamini kuwa; inatosha kupangusa sehemu ndogo tu ya kichwa, ilimradi ieleweke tu kuwa mtu amepaka sehemu ya kichwa chake kwa maji, ila ni lazima kutumia maji mapya. [50]

Kupangusa juu ya khofu (viatu) ni moja ya kesi nyengine za mzozo ambazo Mashia hawaoni kuwa ni sahihi. [51] Mashia wameitegemea Aya ya 6 ya Surat al- Maida katika kukataa suala hilo. [52] Ingawaje Mashia wanakhitilafia katika namna ya kutawadha, ila kuna baadhi ya sehemu fulani, utakuta kuwa wao walikuwa wakitawadha kama Masunni, ila kufanya kwao hivyo kunatokana na kukhofia kugunduliwa madhahebu yao, kwa hiyo walifanya hivyo kutokana na taqiyyah (khofu). Jambo hili linadhihirika katika jawabu ya Imamu Kadhim (a.s), akijibu barua ya Ali bin Yaqtin, ambaye alikuwa na nafasi maalum katika serikali ya ukhalifa wa Bani Abbas. Katika jawabu ya barua hiyo, Imamu Kadhim (a.s) alimuamuru Ali bin Yaqtin kutawadha kama wanavyotawadha Masunni ili kwamba Harun al-Rashid asijue kuwa yeye ni Mshia. [53] Imamu Musa bin Jafar (a.s) alimtaka Ali bin Yaqtin aendelee kubaki katika serikali ya Bani Abbas na kuwatumikia Mashia. [54] Huku akiwakataza Mashia wengine kushirikiana na Bani Abbas. [55]

Mwanzo wa khitilafu za udhu ulianza zama za Othman

Baadhi ya wanazuoni wanaamini ya kwamba; katika kipindi chote cha zama za bwana Mtume (s.a.w.w), hapakuwa na tofauti katika suala la udhu miongoni mwa Waislamu. [56] Wao wanaamini kwamba; Mtume (s.a.w.w)) alitawadha kwa kupangusa miguu badala ya kuosha. [58] Hata katika wakati wa zama za ukhalifa Abu Bakar, hapakuonekana wala kurikodiwa khitilafu katika suala linalohusiana na namna ya kutawadha. Katika kipindi cha utawala wa Omar bin Khattab palitokea khitilafu moja tu juu ya suala hilo, nayo ni khitilafu juu ya suala la kupangusa juu ya khofu mbili (viatu viwili). Kwa upande mwingine ni kwamba; Hakuna hata riwaya moja katika zama hizo inayoonesha kuwepo kwa mzozo juu ya namna ya kutawadha. [59]

Kulingana na kile kilichoelezwa katika Kanzu al-Ummal [60] na baadhi ya vyanzo vingine, [61] baadhi ya watafiti wanaamini kwamba tofauti juu ya suala la udhu zimedhihirika miongoni mwa Waislamu kuanzia wakati wa Khalifa wa tatu (Othman). [62] [Maelezo 1] Sayyied Ali Shahrashtani Akizungumzia tofauti kati ya Imam Ali (a.s) na Omar bin Khattab kuhusu suala linalohusiana na udhu wa kupaka juu ya khofo mbili (viatu), anaamini ya kwamba; Khalifa wa pili, tofauti na Othman bin Affan, hakuwa akiosha miguu yake katika udhu, bali alikuwa akiipaka miguu yake. [63]

Kwa kuegemea Aya ya udhu, na pia Hadith kuhusu suala hilo, Mashia wanaamini kuwa; Mtume (s.a.w.w) na masahaba zake walikuwa wakipangusa miguu yao kama wafanyavyo Mashia Imamiyyah, na hawakuwa wakiosha kama wanavyo fanya Masunni. [64] Hata katika suala la namna ya kuosha mikono, pia kuna Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w)), inayoonesha kuwa yeye alikuwa akiikosha mikono yake kama vile Mashia wanavyo osha mikono yao wakati wa kutawadha, yaani alikuwa akiosha mikono yake kutoka juu (kutoka kwenye viwiko viwili) na kumalizia chini (vidoleni). [65] Kwa mtazamo wa Mashia, riwaya zitegemewazo na Masunni katika suala la kuosha miguu katika udhu, ni riwaya dhaifu na hazina msingi, mbali na ukweli wa kwamba; riwaya hizo zinapingana na Aya ya Qur'an iliyokuja kufafanua suala la udhu. [66]

Nidhamu, sunna na faida za udhu

Mambo kadhaa yamezingatiwa kuwa ni sunna katika kutawadha; Ikiwa ni pamoja na:

  • Kupiga mswaki kabla ya kutawadha: Mtume (s.a.w.w) katika wosia wake kwa Imam Ali (a.s), alipendekeza kupiga mswaki kabla ya kila udhu (a.s). [67]
  • Kupiga Bismillahi mwanzoni mwa udhu. [68]
  • Kusukutua na kuungiza maji puani. [69]
  • Kuuhudhurisha moyo wakati wa kutawadha
  • Kusoma Surat al-Qadri wakati wa kutawadha
  • Kusoma Ayatul Kursi baada ya kutawadha
  • Kuweka chombo cha maji cha udhu upande wa kulia. [70]

Kwa mujibu wa Hadithi za Imam Ali (a.s) ni kwamba; Imamu Ali alikuwa akisoma dua maalumu wakati wa kutia udhu. Kwa mujibu wa Hadithi hizo ni kwamba; Atakayesoma dua hizo wakati wa kutawadha, Mwenye Ezi Mungu atamuumbia Malaika kutoka katika kila tone la maji yake ya udhu, atakayefanya kazi ya akimtukuza, kumtakasa na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa niaba yake, kisha thawabu za amali ya malaika hao huendelea kuandikiwa mtia udhu huyo hadi Siku ya Qiyaamah. [71] Dua zisomwazo katika kila moja miongoni matendo ya udhu ni kama ifuatavyo:


Vipengele vya udhu Dua
Wakati utakapoona maji الْحَمْدُ للَّهِ الذی جَعَلَ الْماءَ طَهُوراً وَ لَمْ یَجْعلْه نَجِساً ; Sifa njema na shukurani ni za Mwenyezi Mungu aliyeyafanya maji kuwa safi na yenye utakaso na hakuyafanya kuwa najisi. [72]
Atakapotia maji puani na mdomono kwa ajili ya kuyasukutua اللّهم لا تُحَرّم عليَّ ريحَ الجنّة و اجعلني ممّن يَشمّ ريحها و طيبها و ريحانها ; Ewe Mwenyezi Mungu, usininyime harufu ya Pepo na nijaalie niwe mwenye kunusa harufu yake, ya manukato yake na harufu ya mauwa ya bustani zake. [73]
Wakati wa kusukutua اللّهمّ أنطق لساني بذكرك و اجعلني ممّن ترضى عنه ; Ewe Mwenyezi Mungu, ifanye dhiri yako iwe ndio uradi wa ulimi wangu na unijaalie niwe ni miongoni mwa unaowaridhia. [74]
Wakati wa kuosha uso اللّهم بيّض وجهي يوم تَسوّد فيه الوجوه و لا تُسَوّد وجهي يوم تبيضّ فيه الوجوه ; Ewe Mwenyezi Mungu! Ufanye uso wangu kuwa mweupe siku ambayo nyuso zitakuwa nyeusi, wala usiufanye uso wangu kuwa mweusi siku ambayo nyuso zitakuwa nyeupe. [75]
Wakati wa kuosha mkono wa kulia اللّهمّ أعطني كتابي بيميني و الخلد بيساري ; Ewe Mwenyezi Mungu, nipe kitabu changu kwa mkono wangu wa kulia na umilele wa milele kwa mkono wangu wa kushoto. [76]
Wakati wa kuosha mkono wa kushoto اللّهمّ لا تعطني كتابي بشمالي و لا تجعلها مغلولة إلى عنقي و أعوذ بك من مقطّعات النّيران ; Ee Mungu, usinipe kitabu cha matendo yangu kwa mkono wa shoto na usiufunge mkono wangu shingoni mwangu, na najikinga kwako kwako kutokana na nguo za moto. [77]
Wakati wa kupangusa kichwa اللّهمّ غشّني برحمتك و بركاتك و عفوك، اللهم غشّني برحمتك و بركاتك و عفوك ; Ee Mungu, nigubike kwa rehema zako, kwa baraka zako, na kwa msamaha wako.. [78]
Wakati wa kupangusa miguu اللّهمّ ثبّت قدميّ على الصّراط يوم تزلّ فيه الأقدام و اجعل سعيي فيما يرضيك عنّي ; Ewe Mola, iimarishe miguu yangu kwenye "Sirati" (njia ilionyooka) wakati wa kuvuka njia ya "Sirati", siku ambayo miguu itatetema katika njia hiyo, na zijaalie juhudi zangu ziwe kwenye yale yanayokupendeza. [79]


Kuna zaidi ya Hadithi 400, katika vyanzo vya Hadithi za Shia na Sunni, zilizo pokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Kishia, zinazohusiana na sheria za udhu, sifa zake pamoja na faida zake. [80] Kwa mujibu wa mafunzo ya Hadithi hizo, udhu hupelekea; utakaso wa dhambi [ 81] kuondokewa na asira, [82] kuwa na maisha marefu, [83] kung'aa kwa uso huko siku ya Kiama, [84] na kuongezeka kwa riziki [85]. Pia, katika masimulizi ya Hadithi nyengine kuhusiana na faida ya udhu, kuna Hadithi zinazoelezea faida ya kukariri udhu, [86] na Hadithi nyingine zimesema ya kwamba; kutia udhu ni sawa na kutubia. [87]

Masuala yanayo fungamana

Vyanzo

  • Āmadī, Muḥammad Ḥasan al-. Al-Masḥ fī wuḍūʾ al-rasūl. Beirut: Dār al-Muṣṭafā li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1420 AH.
  • Anṣārī, Shaykh Murtaḍā al-. Kitāb al-ṭahāra. Qom: Kungira-yi Jahānī-yi Shaykh al-Anṣārī, 1415 AH.
  • Bihbahānī, ʿAbd al-Karīm. Masḥ-i pā dar wuḍūʾ. Qom: Majmaʿ-i Jahānī-yi Ahl al-Bayt, 1395 Sh.
  • Markaz-i Farhang wa Maʿārif-i Qurʾān. Dāʾirat al-maʿārif al-Qurʾān. Qom: Būstān-i Kitāb, 1382 Sh.
  • Fallāḥzāda, Muḥammad Ḥusayn. Aḥkām-i dīn. Tehran: Mashʿar, 1386 Sh.
  • Fallāḥzāda, Muḥammad Ḥusayn. Darsnāma-yi aḥkām-i mubtalā bih-i ḥajj. Tehran: Mashʿar, 1389 Sh.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i fiqh muṭābiq-i madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif-i Fiqh-i Islāmī, 1426 AH.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Muḥammad Muḥsin al-. Muʿtaṣim al-Shīʿa. Edited by Masīḥ-i Tawḥīdī. Tehran: Madrisa-yi ʿĀlī-yi Shahīd Muṭahharī, 1429 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Ḥusaynī, Ḥamīd. 1388 Sh. "Wuḍūʾ az dīdgāh-i madhāhib-i Islāmī." Faṣlnāma-yi Muṭāliʿāt-i Taqrībī-yi Madhāhib-i Islāmī 17:6-14.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Edited by Muṣṭafā al-Saqā & Ibrāhīm al-Abyārī. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Rijāl. Mashhad: Dānishgāh-i Firdusī-yi Mashhad, 1409 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh Mufīd, 1413 AH.
  • Muttaqī al-Hindī, ʿAlī b. Ḥisām al-Dīn al-. Kanz al-ʿummāl fī sunan al-aqwāl wa l-afʿāl. Edited by Bakrī Ḥayyānī & Ṣafwa al-Saqā. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1405 AH.
  • Qummī, ʿAlī. 1393 Sh. "Chigūnigī-yi anjām-i wuḍū nazd-i farīqayn". Miqāt-i Ḥajj 87-90.
  • Sayyid Sābiq. Fiqh al-sunna. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1397 AH.
  • Shahristānī, Sayyid ʿAlī. Limādhā al-ikhtilāf fī l-wuḍūʾ. Edited by Fiys ʿAṭṭār. Tehran: Mashʿar, 1426 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. 1383 Sh. "Wuḍūʾ dar kitāb wa sunnat." Faṣlnāma-yi Fiqh Ahl al-Bayt 38:3-50.
  • Yazdī Ṭabāṭabāyī, Sayyid Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwa al-Wuthqā. Edited by Aḥmad Muḥsinī Sabziwārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.