Nenda kwa yaliyomo

Mirathi

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Urithi)

Mirathi au Urithi (Kiarabu: الإرث) ni mali au haki maalumu inayotolewa kwa warithi baada ya kifo cha mtu fulani ambaye wao wana husiana na kwa uhusiano maalumu wa kifamilia. Mali hii huwafikia wao baada ya wahusika wa maiti huyo kulipa haki na madeni ya marehemu. Warithi humilikishwa kisheria sehemu yao ya mirathi kulingana na tofauti zao katika daraja za mirathi. Mambo mawili kisheria (kifiqhi) ni lazima yazingatiwe katika sula la ugawaji wa mali ya urithi; la kwanza ni ukoo (uhusiano wa kifamili kupitia uzawa), na la pili ni kupitia mafungamano ya kisababu (uhusiano unao tokana na ndoa). Mawili hayo ndio mambo yaliyo tambulishwa kuwa ndio sababu zinazo pelekea mtu kuwa na haki ya urithi. Haki ya urithi inaweza kupikuliwa kupitia mambo kama vile; Uasherati, mauaji, utumwa, uzinzi, na kiapo cha kuapizana baada ya tuhuma ya uzinzi. Haya ni ambayo kulingana na mazingira maalumu, huwa ni vikwazo vya urithi.

Sheria za mirathi pamoja na kiwango cha fungu la kila mmoja wa warithi zimeelezwa katika Qur'ani na zinapatikana katika vyanzo vya Hadithi. Katika vitabu vya fiqhi kuna ufafanuzi wa kina kuhusiana na masula ya mirathi. Sifa mojawapo ya sheria za mirathi katika Uislamu ni kule mtoto wa kiume kuongezwa mara dufu (mara mbili) katika sehemu ya haki ya mirathi yake ikilinganishwa na fungu la mtoto wa kike. Katika katiba ya baadhi ya nchi, kama vile Iran na Afghanistan, sheria ya mirathi inadhibitiwa kwa kuzingatia sheria za kifiqhi (Kiislamu).

Nafasi ya Mirathi na Ufafanuzi wake Katika Fiqhi

Suala la mirathi linachukuliwa kuwa ni miongoni mwa masuala muhimu ya kifiqhi.[1] Kuna milango maalumu inayo pambazuka kiurefu na mapana katika kujadili masuala na kanuni za mirathi kwa kina kabisa ndani ya vyanzo vya fiqhi.[2]Qur'an pia imefafanua kanuni na vigao vya mirathi na kuelezea viwango vya kila mmoja kati ya warithi wa mali ilio achwa na maiti.[3] Pia kuna riwaya nyingi kuhusiana na masuala ya mirathi na hukumu zake katika vitabu mbali mbali vya Hadith. Kwa mfano, katika kitabu cha Wasailu al-Shia, katika mlango uitwayo "Faraidhu wa Mawaariithu", katika sura kumi na mbili ya mlango huo, kumetajwa Riwaya mbalimbali zinzohusiana na mirathi. Miongoni mwa masuala yaliotajwa katika Riwaya hizo ni pamoja na masuala kama vile; vikwazo vya mirathi, sababu za mirathi, na urithi wa wazazi kwa watoto wao na watoto kwa wazazi wao.[4]

Dhana ya Urithi

Neno Urithi, katika fafanuzi na maana za kisheria, limefafanuliwa kwa maana ya mali ambayo ilio salia kutoka kwa mtu aliyekufa, ambayo hugawiwa na kupewa watu maalumu walio baada yake.[5] Mbali na mali, urithi pia hujumuisha vitu kama vile; haki ya kubadili mawazo katika ushika fulani na haki ya shuf'a (haki ya kumiliki mali iliouzwa na mshirika bila ya ushauri, ila kwanza ni lazima arushe fedha za mnunuzi wa mali hili).[6] Mtu anayestahiki urithi huitwa waarithu na mtu aliyeacha urithi huitwa muwarrithu na mali na haki zilizoachwa na marehemu huitwa tarakah au miirathu.[7] Katika fiqhi kwa kuzingatia utambulisho uliotolewa na Qur'an, mali iliocha na maiti huitwa faradh au faridha.[8]

Umiliki wa kumilikishwa mali kwa warithi wa mali ya marehemu, huanzishwa baada ya kulipa haki na madeni ambayo kisheria inabidi kulipwa kutoka katika mali ya urithi; Yaani, kwanza kabisa ni lazima kulipa gharama za kumtayarisha na kumkafini maiti, kisha madeni na wajibu mwengine wa kifedha. Wasia wa marehemu kuhusiana na thuluthi moja ya mali (ikiwa ameusia), itabidi kukatwa katika mali hiyo bila kuhitaji idhini ya warithi, ila wasia wa marehemu wa zaidi ya theluthi moja ya mali hiyo, itabidi kukatwa baada ya kupata muwafaka na idhini ya warithi wake, na kile kinachokwenda kwa mtoto mkubwa (ambacho hujulikana kwa jina la hab-wah) hukatwa kutoka katika mali ya marehemu, baada ya hapo, kilicho baki katika mali hiyo ya urithi hupewa warithi warithi wake.[9]

Sababu za Kurithi

Makala Asili: Vyenye Kuwajibisha Mirathi

Kuna sababu mbili ambazo husababisha mtu kuwa na haki ya kurithi, nazo ni:

  • Nasaba (warithi wa kinasaba): Nasaba ni uhusiano wa kiuzaliwakati ya pande mbili za wanao rithiana, kama vile baba na mwana na dada na kaka.[10]
  • Kisababu (warithi wa kisababu): Urithi wa kisababu hutokana na uhusiano usio wa kiujamaa kati ya pande mbili za wanao rithiana, kuna sababu mbili zinazo pelekea urithi wa aina hii, ni:
A. Ndoa: Ndoa ya kudumu au ndoa ya muda ilio shurutishwa ndani yake haki ya urithi (kulingana na maoni ya wanazuoni walio wengi)
B. Walaa au Kiswahili kuwa na haki ya uwalii (haki ya usimamizi na maamuzi): Walaa katika ngazi tunayo izungumza hapa ni tofautia na uwalii wa wazazi kwa watoto wao. Nalo ni lile fungamano lisilo la kinasaba wala la kuzaliwa au kupitia ndoa. Kuna aina tatu, za mafungamano ya kiurithi kupitia kwayo kwa kuzingatia masharti maalum:
  1. Walaa ‘Atiq (inayohusiana na sheria za utumwa na masuria).
  2. Walaa Dhaamin Jarirah (mkataba wa dhamana kwa masharti ya urithi).
  3. Walaa wa Imamah (Uimamu) (Haki ya Imamu katika kumrithi mtu asiye kuwa na mrithi yeyote yule wa kurithi mali yake).[11]
Kwa maelezo zaidi juu ya haya, pia angalia: Mahrumiyat Nasabii na Mahrumiyat Sababii

Matabaka ya Warithi

Makala Asili: Matabaka ya Mirathi

Warithi wa kinasaba wamegawanywa katika tabaka tatu kuu , na kwa ujumla, tabaka la chini haliwezi kuwa na haki ya kurithi, na kurithi kwao hutegemea kuto kuwepo kwa warithi wa tabaka tabaka la juu yao. Pia kila moja kati ya matabaka lina jumla ya masuala na makadirio yake maalumu:

  • Tabaka la kwanza: ni baba, mama, mtoto, mjukuu (mjukuu hurithi katika kesi ya kutokuwepo au kufariki kwa mtoto).
  • Tabaka la pili: ni babu wa baba na mama na mababu wanaoendelea juu zaidi, kaka na dada (watokao upande wa baba) au (watokao upande mama) au (upande wa baba na mama) na watoto wao (katika hali ya kuto kuwepo kwao).
  • Tabaka la tatu: ni ami, shangazi, wajomba na makhaloo na watoto wao katika hali ya wao wenyewe kuto kuwepo. Kwa kukosekana na kuto kuwepo kwa matabata haya ya awali, urithi wa mali ya maiti utakwenda kwa; ami wa marehemu, shangazi, mjomba na kahloo wa marehemu huyo.[12]

Sehemu au Hisa ya Urithi wa Kila Mmoja wa Warithi

Imesemwa ya kwamba; haki ya urithi ima huwa ni haki "kadirio" au haki "ainisho"; Yaani ima ni haki ilio ainishwa na kubinishwa ndani ya Qur'ani, au ni haki ambayo hikubainishwa ndani ya Qur'ani. Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba; ndani ya Qur-aan, hakuna sehemu ya haki yoyote ile maalumu iliyo ainishwa na jamaa wa mbali wa maiti, badala yake Qur'ani imewataja tu kwa jina la “Ulu al- Arham", bila ya kuashiria wakusudiwa kundi hilo la "Ulu al- Arham" au kutaja kiwango cha hisa zao. Miongoni mwa jamaa wa mbali wa maiti ambao hawakutajwa wazi ndani ya Qur'aniwa ni maami na mashangazi. [13] Hisa za "wajibu" au za faradhi zilizotajwa katika Qur'an ni kama ifuatavyo:

  • Nusu: Ikiwa binti ni mtoto pekee na hana kaka, yeye anapata nusu ya urithi wa mali ya marehemu. Pia, ikiwa ana dada wa upande baba au dada wa upande wa baba na mama, haki ya urithi wake itakuwa ni nusu ya mali ya urithi huo, na pia mume, ikiwa hana watoto kutoka kwa mkewe, naye pia haki yake ni nusu ya urithi.
  • Theluthi mbili: Binti wawili au zaidi, ikiwa hawana kaka, watapata theluthi mbili ya urithi. Pia urithi wa dada wawili wa upane baba tu, au wa upande wa baba na mama, ikiwa hawana kaka, haki yao katika urithi wa mali ya marehemu ni thuluthi mbili.
  • Theluthi moja: Mama ikiwa marehemu hana watoto wala ndugu, na pia dada na kaka wa upande wa mama wakiwa ni zaidi ya mmoja, hupokea thuluthi moja ya urithi wa mali ya marehemu.
  • Moja ya sehemu ya nne (robo): Robo ni hisa ya mke ikiwa mumewe hana watoto, na pia fungu la mume ikiwa mke wake hana mtoto kutoka kwake au kwa mume mwingine ni robo.
  • Moja ya sita: Kila mmoja wa wazazi (baba na mama), ikiwa marehemu alikuwa na mtoto, na hali wakiwa baba na mama ni wahai, wao watarithi moja ya sehemu ya sita, na iwapo mtu atafariki na kuaacha ndugu, huku mama yake akiwa hai, basi mama huyo atarithi moja ya sehemu yasita. Sehemu ya kaka au dada wa upande wa mama ni moja ya sita ikiwa atakuwa yupo peke yake.
  • Moja ya sehemu ya nane: Sehemu ya mke, ikiwa mumewe amefariki na kuacha watoto, ni moja ya sehemu ya nane.[13]

Haki ya Mirathi Kati ya Mume ma Mke

Kila mmoja kati ya mume na mke hurithiana baada mmoja kati yao kufariki huku mwengina akiwa hai, wao hurithiana mali ya mmoja kati yao huku wakishirikina na warithi wengine katika mali hiyo. Hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kurithi mali yote ya mwingine, isipokuwa kama mrithi atakuwa ni mume baada ya mke kufariki hali akiwa hana mrithi mwengine ispokuwa mumewe tu. Katika hali hii, mume hurithi mali yote iliochwa na mke.[14] Iwapo mume atafariki na mke akawa ndiye mrithi pekee kwa upande wa mumewe, haki ya mke huyo itakuwa ni robo ya mali hiyo, na sehemu iliyo baki itarudi kwa Imamu au kiongozi wa dini ambaye anastahiki na ana hadhi ya kutoa fatwa (faqihi au kwa jina jengine ni mujitahid).[15]

Hisa ya Mwanaume ni Mara Mbili Zaidi Ukilinganisha na Mwanamke

Makala Asili: Mirathi ya Mwanamke

Kuna sehemu mbili ambazo mwana mke ana haki ya kurithi nusu tu ya hisa ya mwanamme:

  1. Iwapo dada na kaka ni halisa, haki ya urithi wa dada ni nusu ya urithi wa kaka yake, yaani hisa ya kaka huwa ni mara mbili zaidi ya hisa ya dada: hati ya hukumu hii ni aya isemayo: ((لِلذَّکَرِ‌ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَیَیْنِ ; Haki ya mume ni sawa na hisa ya wanawake wawili)).[16] Kulingana na Aya hii, fungu la mwanamme ni sawa namafungu mawili ya mwanamke.[17]
  2. Dada wa kalaala: Kalala ni mtu aliye fariki hali akiwa hakuacha baba, mama wala mtoto, kiasi ya kwamba aweze kurithiwa na watu hao. Katika hali hii iwapo dada wa kalala atakuwa na kaka na dada wa baba mmoja na mama mmoja (halisa), yeye atakuwa na haki ya kurithi nusu ya hisa ya mwanamme. Hukumu hii inapatika katika Aya ya 176 Surat al-Nisaa.[18]

Vikwazo vya Urithi

Makala Asili: Vikwazo vya Urithi

Kuna matukio maalumu ambayo huzuia na huwa ni vikwazo vya mtu kupata haki ya urithi, vikwazo hivi vimejadiliwa vya kutosha katika vitabu vya fiqhi. Vikwazo hivyo vya urithi ni kama ifuatavyo:

  • Kukufuru: Kwa mujibu wa makubaliano (ijmaa) ya Waislamu, kafiri hawezi kumrithi Mwislamu; Lakini kwa upande wa pili, mujibu wa makubaliano ya mafaqihi wa madhehebu ya Imamiyya, Mwislamu hurithi kutoka kwa kafiri. [18] Pia imesemwa ya kwamba; Katika sheria za urithi, aliye ritadi bado huhesabiwa kama ni Mwislamu, hivyo basi kafiri hawezi kumrithi aliye ritadi.[19]
  • Mauaji: Ikiwa mrithi ni muuaji wa kukusudia na akawa ameua kidhalimu hali akiwa ni miongoni mwa warithi wa aliyeuawa, mtu huyo hunyang'anywa haki urithi wake, na ikiwa ameua kimakosa, basi yeye atakosa tu haki ya kurithi mali iliyotolea kwa kufidia maauaji hayo. Watoto na jamaa wa muuaji hawanyimwi haki urithi kutokana na kosa lake yeye.[20]
  • Utumwa: Mtumwa hana haki ya kumrithi mtu yeyote, hata kama aliyekufa pia ni mtumwa kama yeye. Iwapo mtumwa atafariki, mali yake yote huenda kwa mtu huru (asiye mtumwa).[21]
  • Li’an (kiapo cha kimahakama cha kulaaniana katika ya kuto wepo ushahidi): Ikiwa li'an itatokea baina ya mume na mke, kwa vile Lia'an husababisha kukatika kwa fungamano la ndoa na kuachana kwa mume na mke, hili hupelekea kuto rithiana baina ya mume na mke;[22] ila yule mtoto aliye pelekea wazee wake kulaaniana, huwa na haki ya kumrithi mama yake tu, na hana haki ya kumrithi baba yake aliye laaniana na mama yake.[23]
  • Mimba: Mtoto aliye tumboni mwa mama yake huwa na haki ya kurithi iwapo tu mimba yake ilitungwa katika zama za uhai marerehemu, na siao baada ya kifo marehemu, na ni lazima mtoto huyo awe amezaliwa akiwa hai, la muhimu ni kwamba mtoto huyo alipozaliwa ali bado yuhai. Mtoto huyu huwa na haki ya urithi hata kama atafariki mara tu baada ya kuzaliwa kwake.[24] Mtoto hawezi kurithi maadamu yuko tumboni mwa mamaye (bali baada ya kuzaliwa kwake) Lakini yeye huwa ni kizuizi cha warithi wa matabaka yanalofuata baada ya tabaka lake.[25]
  • Aliyepotea (Asiye julikana habari zake au asiyejulikana alipo): Mtu alipotea na asiye julikana alipo wala habari zake, huwa ni kizuiza cha wengine kurithi, ila yeye anarithi kutoka kwa wengine. Baada kupatikana kwa habari za kifo chake, au kiongozi wa kisheria kutoa hukumu kufariki kwa mtu huyo, mali yake huenda kwa warithi wake.[26] Isipokuwa ikibainika kuwa mtu huyo aliye potea alifariki kabla ya kufa kwa yule aliyemrithi, mali hiyo aliyo irithi itarudi kwa warithi wa yule maiti wa mwanzo ambaye yeye alirithi mali hiyo kutoka kwake.[27]
  • Uzinzi: Mtoto aliyezaliwa kupitia tendo la zinaa, hana haki ya kurithi kutoka wa wazazi wake hao waliye mzaa kinyume na sheria. Pia wazazi wake pamoja na jamaa zake hawana haki ya kumrithi mtoto huyo.[28]
  • Deni: Wengine wamesema kwamba; ikiwa marehemu alikuwa na deni kubwa sawa na mali aliyo iacha baada ya kufariki kwake, warithi wake hawatakuwa na haki ya kurithi mali hiyo, katika hali kama hiyo deni huwa ni kizuizi kinacho wazuia warithi wasiweze kuwa na haki ya urithi.[29]
  • Hajbu (kizuizi): Hajbu katika urithi humaanisha uwepo wa mrithi fulani huwa ni kizuizi cha warithi wengine kuweza kurithi mali ilio achwa na marehemu. Mzuia huyu wa urithi anaweza kuwazuiwa warithi wote au kuzuia sehemu ya warithi wa marehemu huyo. Ikiwa atakuwa ni kiziuizi kwa kwapinga warithi wote, yeye huitwa "Hajbu Hirman" na katika hali ya pili huitwa "Hajbu Nuqsan".[30] Uwepo wa tabaka la juu la warithi kati ya matabaka matatu ya warithi, huwa ni kizuizi cha matabaka yote matatu ya warithi walio katika matabaka ya chini.[31]

Sheria ya Kiraia za Nchi za Kiislamu

Ibara ya 861 hadi Ibara ya 949 katika Kanuni za Kiraia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni ibara maalumu kwa ajili ya masuala mbalimbali ya mirathi kama. Miongoni masuala yanayojadiliwa katika ibara hizo ni vile; matabaka ya warithi, sababu na vikwazo vya mirathi kwa mujibu wa fiqhi ya Kishia.[32] Pia katika kanunu za Kiraia za Afghanistani, masula ya mirathini miongoni mambo yaliyo jadilawa ndani ya kanuni hizo. Kanuni za mirathi nchini Afghanistani zimepangwa kulingana na fiqhi ya madhehebu ya Kihanafi. Ibara ya 1993 hadi 2102 katika Kanuni za Kiraia za nchi hii, ni maalumu kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali ya urithi, ambapo ndani yake mna masuala kadhaa kuhusiana na mirathi, kama vile; kanuni za kiujumla za mirathi, sababu na vikwazo vya mirathi.[33]

Rejea

  1. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  2. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  3. Tazama: Surat an-Nissa: Aya ya 7, 11, 12, 19, 176.
  4. Tazama: Hurri Amili, Wasā'il as-Shī'ah, juz. 26, uk. 11-320.
  5. Hashimi Shahrudi na wenzake, Mausū'ah al-Fiqh al-Islāmī al-Muqāran, juz. 2, uk. 121-122.
  6. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  7. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  8. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  9. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 375.
  10. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'a al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 15-16.
  11. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'a al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 18-19; Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 378 & 379.
  12. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 378 & 379.
  13. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 378 & 379.
  14. Fadhil Lankarani, Tafsīl as-Sharī'a (al-Mawārīth), 1421 H, uk. 455.
  15. Rejea: Tahzib al-Ahkam, Sheikh Tusi, juz. 9, uk. 294, Hadithi ya 15, Chapa ya Darul-e-Kitab al-Islamiya, Tehran.
  16. Jawadi Amuli, Zan Dar Ayine-e Jalal wa Jamal, 1382 S, uk. 346.
  17. Jawadi Amuli, Zan Dar Ayine-e Jalal wa Jamal, 1382 S, uk. 346.
  18. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 21 & 22.
  19. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 31 & 32.
  20. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 54 & 55.
  21. Shahid Thani, ar-Raudhat al-Bahiyyat, juz. 8, uk. 38.
  22. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 80.
  23. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 80.
  24. Shahid Thani, ar-Raudhat al-Bahiyyat, juz. 8, uk. 47; Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 92.
  25. Subhani, Nidhām al-Irth Fī Sharī'ah al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 89.
  26. Tazama: Sheikh Tusi, al-Khilāf, juz. 4, uk. 119; Ibn Idris, as-Sarā'ir, juz. 2, uk. 298; Allamah Hilli, Mukhtalaf as-Shī'a, juz. 9, uk. 110; Allamah Hilli, Tabsirat al-Muta'allimīn, uk. 177; Najafi, Jawāhir al-Kalām, 1362 H, juz. 39, uk. 63; Makarim Shirazi, al-Fatāwā al-Jadīdah, juz. 2, uk. 362.
  27. Katuziyan, Daure-e Muqaddamati- Huquq Madani, uk. 222.
  28. Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 39, uk. 275.
  29. Tazama: Subhani, Nidhām al-Irth Fī as-Sharī'a al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 95.
  30. Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 39, uk. 75; Subhani, Nidhām al-Irth Fī as-Sharī'a al-Islāmiyyah al-Gharrā', uk. 97.
  31. Muasase Dayirat al-Ma'arif Fiqh-e Eslami, Farhangg Fiqh, juz. 1, uk. 378.
  32. «Qanun Madani»، Markaz Pezhuhesh Majlis Shurah Islami.
  33. «Qanun Madani Afghanistan»، Muasase Farhang Bisharat..

Vyanzo

  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf. Mukhtalaf as-Shī'a Fī Ahkām as-Sharī'ah. Qom: Daftar Entesharat Islami, 1413 H.
  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf. Tabshirat al-Muta'allimīn Fī Ahkām ad-Dīn. Mhakiki: Muhammad Hadi Yusufi Ghurawi. Tehran: Wizarat Farhang wa Irshad Islami. Sazman Cap wa Intesharat, 1411 H.
  • Fadhil Lankarani, Muhammad. Tafsīl as-Sharī'a Fī Sharh Tahrīr al-Wasīlah at-Talāq, al-Mawārīth. Qom: Markaz Fiqhi Aimat At-har (a.s). Chapa ya kwanza, 1421 H.
  • Hashimi Shahrudi, Mahmud & Wenzake. Mausū'at al-Fiqh al-Islāmī al-Muqāran. Qom: Muasase Da'yirat al-Ma'arif Fiqh Islami Bar Madhab Ahlul-Bait (a.s). Chapa ya kwanza, 1433 H.
  • Hurri Amili, Muhammad bin Hassan. Wasā'il as-Shī'ah. Mhakiki na mhariri: Guruhe Pezhuhesh Muasase Āhlul-Bait. Qom: Muasase Āhlul-Bait. Chapa ya kwanza, 1409 H.
  • Ibn Idrisi, Muhammad bin Ahmad. As-Sarāir al-Hāwī Li Tahrīr al-Fatāwā. Qom: Muasase an-Nashr al-Islami, 1410 H.
  • Jawadi Amuli, Abdullah. Zan Dar Ayine-e Jalal Wa Jamal. Mhakiki na mhariri: Mahmud Latifi. Qom: Nashr Isra'. Chapa ya saba, 1382 HS/2004.
  • Katuzian, Nashir. Daure Muqaddamati Huquq Madani Darsihaye Az Shuf-e, Wasiyat wa irth. Tehran: Nashr Mizan, 1386 HS/2007.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Al-Fatāwā al-Jadīdah. Qom: Madrasat al-Imam Ali bin Abi Talib (a.s), 1385 HS/2006.
  • «Qanun Madani»، Markaz Pezhuhesh Majlis Shurah Islami.
  • «Qanun Madani Afghanistan»، Muasase Farhang Bisharat..
  • Najafi, Muhammad Hassan. Jawāhir al-Kalām Fī Sharh Sharā'i' al-Islām. Mhakiki: Abbas Quchani & Ali Akhundi. Beirut: Dar Ihya' at-Turath al-'Arabi. Chapa ya saba.
  • Subhani, Ja'far. Nidhām al-Irth Fī as-Sharī'at al-Islāmiyyah al-Gharrā'. Mhakiki: Sayyid Ridha Peiyambar-Pur Kashani. Qom: Muasase Imam Sadiq (a.s). Chapa ya kwanza, 1415 HS.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Ar-Raudhat al-Bahiyyah Fī Sharh al-Lum'ah ad-Damishqiyyah. Sherh: Sayyid Muhammad Kalantar. Qom: Kitab Furushi Dawari. Chapa ya kwanza, 1410 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan. Kitāb al-Khilāf. Qom: Muasase an-Nashr al-Islami.
  • Muasase Da'yirah al-Ma'arif Fiqh Islami. Farhang Fiqh Mutwabiq Madhab Ahlul-Bait (a.s). Chini ya uangalizi wa Sayyid Mahmud Hashimi Shahrudi. Qom: Muasase Da'yirat al-Ma'arif Fiqh Islami. Chapa ya kwanza, 1385 HS/2006.