Nenda kwa yaliyomo

Istighfaru

Kutoka wikishia

Istighfar au Toba (Kiarabu: الاستغفار): Ni neno la Kiarabu lenye maana ya kuomba maghufira kutoka kwa Mungu kupitia matamshi kwa kusema (استغفرالله) au vitendo vinavyo ashiria jambo hilo. Qur'an na Hadithi hutoa mifano mingi na mwongozo wa faraja juu ya ujira wa kuomba msamaha. Ndani ya Qur’an Karim kuna kiasi cha Aya 30 zinazo husiana na istighar za Mitume kwa Mola wake. Miongoni mwa faida zilizotajwa ndani ya Qur’an na Hadithi kuhusiana na istighfar ni pamoja na; kusamehewa dhambi, na kupata ongezeko la rizki.

Kuomba toba -ambayo ni Sunnah- ni miongoni mwa dua na ibada bora mno. Lakini katika hali fulani, toba huwa ni wajibu na wakati mwingine huchukuwa nafasi ya fidia kutokana na dhambi fulani. Kwa mfano mtu aliyomo katika ihiramu kwake ni wajibu. Kulingana na mafundisho ya Qur'an, toba kwa washirikina haikubaliki na Mtume (s.a.w.w).

Imam Ali (a.s) amesema: Kujuta kwa dhambi za zamani, uamuzi wa kuto rudi tena kwenye dhambi, kutimiza haki za watu na kutekeleza matendo ya wajibu, ni masharti ya toba.

Toba inapendekezwa kufanywa wakati wote na mahali popote hata kama mtu hakufanya dhambi; lakini usiku wa manane ni wakati ndio wakati mzuri zaidi wa kufanya toba. Toba mara nyingi hufanywa kwa nia ya kuomba msamaha kutokana na dhambi na dhuluma juu ya nafsi ya mtu mwenyewe. Pia tendo la kuomba maghufira, linaweza kufanyika kwa nia kuomba msamaha juu dhambi za kudhulumu wengine, na mara nyingine kwa sababu ya dhambi za kijamii.

Welewa wa Dhana ya Toba

Neno istighfaru linamaanisha ombi linalo fanyika kupitia lugha ya maneno au vitendo kutoka kwa mja kwenda kwa Mola wake, kwa nia ya kuomba msamaha wa dhambi. [2] Lengo la lake hasa ni kuomba kinga na himaya kutokana na athari mbaya za dhambi na adhabu ya Mungu. [3]

Istighfaru ni ahadi na kauli inayo fanyika kupitia lugha na maneno maalumu, kama vile kusema; Astaghfirullah au kutenda matendo yanayo sababisha mja kupata msamaha. [4] Istighfar kupitia lugha ya maneno, imejadiliwa kwenye milango maalumu ya fani ya fiqhi kama vile: mlango wa tohara, sala, saumu, hija, biashara, udhu na kafara. [5]

Baadhi ya wafasiri wa Kisunni, kama Zamakhshari na Fakhru al-Razi, wamelifasiri neno "istighfaru" katika Aya za Qur'an kwa maana ya imani [6] au Uislamu. [7] Tabarsi, ambaye ni mmoja wa wafasiri wa Kishia wa karne ya tano Hijiria, katika kulifasiri neno istighfaru lililoko katika baadhi ya Aya za Qur'an tukufu, kama vile Aya ya 17 ya Surat Al-Imran, isemayo:((الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنْفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ ; Wenye subira, wakweli, wanyenyekevu, wasikivu, na wanaoomba msamaha karibu na alfajiri)). Yeye amelifasiri neno hili kwa maana ya "kusali au kusimamisha sala", na akaihisabu sala kuwa ni moja wapo ya mifano hai ya kuomba toba. Amefasiri hivyo kulingana na baadhi ya Hadithi zilizo itaja sala kuwa ni miongoni mwa matendo ya kuomba. [8]

Nafasi ya Istighfar au Toba

Dhana ya kutafuta msamaha imetajwa mara 68 katika Qur'an Tukufu, ambapo mara 68, 43 inatokana na mnyambuko halisi wa neno istighfaru, 17 kwa mfumo wa ighfir, tatu kwa mfumo wa yaghfiru, mbili kwa mfumo wa taghfiru, na mara moja kwa mfumo wa maghfira.

Kukuza dhana ya kuomba msamaha au amri ya kufanya hivyo pia imesisitizwa katika Aya nyingi za Qur'an Tukufu. [10] Pia katika badhi ya hali fulani, Qur'an imewakemea wale wasio na tabia ya kuomba msamaha.

Kulingana na mafundisho ya Qur'an, malaika huwaombea msamaha waumini, [12] pamoja na wakazi wa dunia kwa jumla. [13] Kwa upande mwingine, Qur'an imelihisabu tendo la kutafuta msamaha kuwa ni moja wapo ya sifa ya walio ongoka. [14] Pia moja ya mambo yanayo pelekea kuondoa shaka na pingamizi juu ya uhalali wa kuomba msamaha kupitia mitume na mawalii, na kufuta dhana ya ushirikina juu ya jambo hilo, ni yale maombi waovu ya kuwataka manabii wawaombee msamaha kutoka kwa Mungu. Maombi hayo ya waovu, ni miongoni mwa nyenendo zinaondoa mashaka na wasiwasi juu ya shirki inayo husishwa na ombi la msamaha kupitia watu wengine (mitume na mawalii). Pia watafiti wa madhehebu ya Kisunni kwa kuzingatia Aya za Qur'an, hawaoni ombi la msamaha kupitia Mtume kuwa ni miongoni mwa matendo ya kishirikina. [15] Watoto wa Nabii Yakubu, baada ya matendo yao dhidi ya mdogo wao (Yusufu), walimwomba baba yao awaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa niaba yao, naye pia akawaahidi kufanya hivyo. [Maelezo 1] Pia Mwenye Ezi Mungu akimhutubia Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Qur'ani Tukufu [Maelezo 2]

Kuna karibu ya Aya 30 ndani ya Qur'an Tukufu zinazo husiana na matukio ya msamaha wa manabii kuwaombea wengine. [16] Hata hivyo, Ayatullah Tabataba'i, akiaishiria utukufu wa Manabii, amelichukulia suala la kutenda dhambi kwa manabii, kuwa linakwenda kinyume na majukumu yao ya kulingani dini. Kwa hiyo; kule manabii kustaghafiru mara kwa mara, hakumaanishi kuwa wao wawefanya makosa, bali wanafanya hivyo kutokana na matendo halali walio yafanya ambayo hayapendezi wao kuyafanya kutokana na hadhi yao. [17] Nukta hii inaingia kwenye msamiati usemao Hasanatul Abrari Sayyiatu al-Muqarrabina. Yaani Mema ya watu wema, ni dhambi mbele ya walio wekwa ubavuni mwa Mola wao. Yaani si kwamba tu, baadhi ya mambo mahali kwa watu wa kaida huwa ni haramu kwa wachamungu, bali pia yawezekana jambo jema likawa ni haramu kutendwa na mchamungu. [18]

Baadhi ya matunda ya kuomba msamaha yaliyotajwa Katika Aya za Qur'an Tukufu, pamoja na Maasumina (a.s), ni pamoja na: msamaha wa dhambi, [21] kupata ongezeko la riziki na watoto, [22] pamoja na ongezeko la umri na kuishi maisha marefu. [23]

Katika moja ya simulizi za Hadithi, imeelezwa kuwa; kutafuta msamaha hupelekea kitabu cha amali za mwanadamu kuboreka na kupata hadhi zaidi Siku ya Kiama. [24] Katika simulizi za Riwaya nyingine kutoka kwa Zurara bin A'yyun, akinukuu kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), amesema kwamba: "Yeyote yule atendaye dhambi, basi aelewe kwamba; muhula wake wa kutubia ni kuanzia asubuhi hadi usiku. Kwa hiyo iwapo atatubia katika muhula huo, basi yeye hata andikiwa dhambi za kosa hilio."

Hukumu ya Toba

Kuomba msamaha (kuomba toba) kwa mujibu wa sheria za Kiislamu ni sunna; lakini pia jambo linaweza kuwa ni wajibu au haramu kwa sababu fulani.

  1. Msamaha wa sunna: Maombi ya kutafuta msamaha ni moja ya maombi na ibada bora mno miongoni mwa ibada, na imependekezwa kufanya hivyo katika hali mbali mbali; ikiwa ni pamoja na: [26] Kati ya sajdah mbili za sala, [27] Baada ya uradi wa tasbihi kusomwa baada ya sala za faradhi (Allahu Akbar, Alhamdulillahi, Subhaanallahi), [28] katika kunuti, hasa katika kunuti ya sala ya witri [29] inayo saliwa wakati wa alfajiri, [30] na katika mwezi wa Ramadhani. [31]
  2. Toba na msamaha wa wajibu: Kuomba msamaha huwa ni lazima na wajibu katika kesi fulani; ikiwa ni pamoja na; fidia kwa muhrimu aliye zozana na wengine kwa mara moja au mbili. [32]
  3. Msamaha haramu: Kulingana na Qur'an Tukufu, ni haramu kwa Waislamu kuwaombea msamaha washirikina. [33] Wafasiri wa Qur'an wamekhitalifiana juu maelezo ya Qur'an yanayo husiana na matakwa ya Ibrahimu ya kumwombea msamaha baba yake (au babu yake wa mzalia mama au ami yake) hali akiwa ni miongozi mwa mshirikina. [34] Lakini kulingana na Aya za Qur'an Tukufu, Ibrahimu alimwombea baba yake huyo (Aazar) msamaha, kwa sababu alikuwa amemwahidi kufanya hivyo, lakini alipogundua tu kwamba hakuwa miongoni mwa walio amini, alitengana naye na hakumwombea tena msamaha. Qur'an imelizungumzia suala hili kwenye Aya ya 114 ya Suratu al-Taubah: ((وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَنْ مَوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِلَّهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ; Na haikuwa ya Ibrahimu kwa ajili ya babaye isipokuwa kutokana na ahadi aliyo muahidi kwa ajili yake, ila baada baada ya kugundua kwamba yeye ni (baba yake) ni adui wa Mwenye Ezi Mungu, alijitenga naye. Kwa hakika Ibrahimu ni mnyeyekevu mno na mwenye huruma)).

Adabu za Toba

Kuna adabu kadhaa zilizosimuliwa kutoka katika Riwaya za Masumina (a.s) kuhusiana na toba. Miongoni mwazo ni kutoka katika Hadithi ya Imamu Ali (a.s), akimwambia mmoja ya watu aliye kuwa akiomba toba. Imamu Ali (a.s) ametaja sharti sita za toba halisi katika Hadithi hiyo, sharti hizo ni; Majuto juu ya dhambi iliyopita, dhamira madhubuti ya kuto rudia tena dhambi hiyo, kurejesha haki za watu, kutekeleza (kukidhi) wajibu aliyo upoteza, kujitahidi kuyayusha kilichoota mwilini mwake (nyama) kupitia mali ya haramu na kuuonjesha mwili wake taa ya Mwenye Ezi Mungu. [35]

Ingawaje kuomba toba hakuhitaji zama, mahala wala wakati maalumu, ila Qur'an imesisitiza zaidi toba ya usiku wa manane (Alfajiri kubwa). [36] Mwenye Ezi Mungu akiashiria sisitizo hili katika Qur'an katika Aya ya 18 ya Surat al-Dhariat amesema:((وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ))

Aina za Kuomba Maghufira

Kulingana na uhalisia wa dhambi na maudhui yake, toba hugawika sehemu tatu zifuatazo:

  1. Toba ya dhambi binafsi, ambapo mtu huwa amejidhulumu nafsi yake mwenyewe.
  2. Toba ya dhambi iyotendeka katika kukiuka haki za watu wengine, ambazo ni dhambi za makosa ya watu wanayo fanyiana wenyewe kwa wenyewe.
  3. Toba kutokana na dhambi za kukiuka na kuvunja haki za wengine. Ambazo ni dhambi za wakuu, waendesha na viongozi wa kisiasa na wa kijamii.

Maelezo

  1. قَالُوا يَا أَبَانَا اسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا إِنَّا كُنَّا خَاطِئِينَ Wakasema; Ewe baba yetu, tutakie msamaha (kwa Mola wetu), kwa hakika sisi tulikuwa makosani (watenda makosa)
  2. وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللهَ تَوَّابًا رَحِيمًا ; amesema: Na kwa hakika wao, lau pale walipo jidhulumu nafsi zao, wangelikujia na kukuomba uwambee msamaha, nawe ungelieaombea msamaha (na mtume angeliwaombea msamaha), basi wangelimwona Mungu kuwa ni Msamehevu na Mrehemevu.

Rejea

Vyanzo

  • Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1426 AH.
  • ʿAbd al-Bāqī, Muḥammad fuʾād. Al-Muʿjam al-mufahras li-alfāẓ al-Qurʾān al-karīm. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1412 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Al-Tafsīr al-kabīr. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Ḥimyarī, Nashwān b. Saʿīd al-. Shams al-ʿulūm wa dawāʾ kalām al-ʿarab min al-kulūm. Edited by Ḥusayn b. ʿAbd Allāh al-ʿAmrī. Damascus: Dār al-Fikr, 1420 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tafsīl Wasāʾil al-Shīʿa ilā taḥṣīl masāʾil al-sharīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1409 AH.
  • Ibn ʿĀshūr, Muḥammad Ṭāhir. Al-Taḥrīr wa l-tanwīr. Beirut: Muʾassisat al-Tārīkh, 1420 AH.
  • Ibn Athīr, Mubārak b. Muḥammad. Al-Nihāya fī gharīb al-ḥadīth wa l-athar. Qom: Ismāʿīlīyān, 1367 Sh.
  • Ibn Fahd al-Ḥillī, Aḥmad b. Muḥammad. ʿUddat al-dāʿī wa najāḥ al-sāʿī. Beirut: Dār al-Kutub al-Islāmī, 1407 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Beirut: Dār al-Ṣādir, 2000.
  • Iskandarānī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Kashf al-asrār al-nūrānīyya al-Qurʾānīyya. Edited by Aḥmad Farīd al-Mazīdī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 2001.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Fourth edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1380 Sh.
  • Muwaḥḥidī, ʿAbd Allāh. Tafsīr-i mawḍūʿī-yi Qurʾān. Qom: Daftar-i Nashr-i Maʿārif, 1386 Sh.
  • Najafī, Muḥammad Ḥasan al-. Jawāḥir al-kalām. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1362 AH.
  • Qurṭubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Qom: Markaz-i Iṭilāʿāt wa Madārik-i Islāmī, 1387 AH.
  • Rāghib al-Iṣfahānī, Ḥusayn b. Muḥammad al-. Mufradāt alfāẓ al-Qurʾān. Damascus: Dār al-Qalam, 1416 AH.
  • Ṣādiqī Tihrānī, Muḥammad. Al-Furqān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Farhang-i Islāmī, 1406 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jamiʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1392 AH.
  • Ṭabāṭabāyī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Terhan: Bunyād-i ʿIlmī wa fikrī-yi ʿAllāma Ṭabāṭabāyī, 1370 Sh.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān. Tehran: Nāṣir Khusru, 1372 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Miṣbāḥ al-mutahajjid. Tehran: al-Maktaba al-Islāmīyya, [n.d].
  • Yazdī, Sayyid Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwa al-wuthqā. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1409 AH.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Al-Kashshāf ʿan ḥaqāyiq ghawāmiḍ al-tanzīl wa ʿuyūn al-aqāwīl fī wujūh al-taʾwīl. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, [n.d].