Nenda kwa yaliyomo

Sala ya Eid

Kutoka wikishia
Sala ya Idul-fitr ikiongozwa na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Tehran, 2013

Sala ya Idi au Sala ya Idi mbili (Kiarabu: صلاة العيد أو صلاة العيدين) ni Sala ambayo Waislamu huisali katika siku ya Idi al-Fitr na Idul-Adh’ha. Ushiriki wa Waislamu katika Sala ya Idi hususan Idul-Fitr ni mubwa sana. Kwa mujibu wa fat’wa za mafakihi wa Kishia, Sala hii ni wajibu katika zama za uwepo wa Imamu Maasumu na inapaswa kusaliwa kwa jamaa. Aidha ni mustahabu kusali Sala hii katika zama za ghaiba ya Imamu ingawa kuna tofauti za kinadharia na kimitazamo kuhusiana na kwamba, inapaswa kusaliwa kwa jamaa au furada.

Kwa mujibu wa Tarikh Tabari ni kwamba, Sala ya kwanza ya Idi ilisaliwa tarehe Mosi Shawwal (Mfunguo Mosi) mwaka wa pili Hijria. Imamu Ridha (a.s) katika kipindi chake cha urithi wa kiti cha utawala katika zama za Maamum Khalifa wa utawala wa Bani Abbas alikubali ombi la mtawala huo la kusimamisha Sala ya Idul-Fitr na akafanya mambo ya utanguzli wa Sala hiyo, lakini Maamun akabadilisha uamuzi. Nchini Iran Sala ya Idul-Fitr ilisaliwa mwaka 1357 Hijiria Shamsia kwa Uimamu wa Mohammad Mofatteh na kwa hotuba ya Muhammad Jawad Bahonar na ikaishia kwa maandamano dhidi ya utawala wa Kipahlavi. Katika kipindi cha utawala wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran, Sala ya Idul-Fitr mjini Tehran mara nyingi husalishwa na Sayyid Ali Khamenei, kiongozi wa pili wa Jamhuri wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sala ya Idi ina rakaa mbili; rakaa ya kwanza ina kunuti 5 na rakaa ya pili ina kunuti nne. Kadhalika Sala ya Idi ina hotuba mbili ambazo hutolewa baada ya Sala. Wakati wa Sala ya Idi ni kuanza kuchomoza jua mpaka zawali (adhuhuri ya kisheria). Sala ya Idi ina adabu na hukumu zake maalumu na miongoni mwazo ni: Bora Sala hii ikasaliwa eneo la wazi lisilo na kizuizi juu na kuna dua maalumu inayosomwa katika kunuti.

Umuhimu na Nafasi Yake

Sala ya Idi ni Sala ambayo husaliwa na Waislamu katika siku ya Idul-Fitr na Idul-Adh’ha. Sala hii inatambulika katika vyanzo vya fikihi na hadithi kwa jina la Salat al-Idein (Sala ya idi mbili). [1] Muhammad bin Jarir Tabari, mwanahistoria wa karne ya tatu Hijiria anasema: Mtume (s.a.w.w) alisimamisha Sala ya Idi kwa mara ya kwanza tarehe Mosi Shawwal mwaka wa pili Hijiria. [2] Ushiriki wa Waislamu katika Sala ya Idi hususan Idul-Fitr ni mkbwa sana na Sala hii husimamishwa katika maeneo yote matakatifu ya Waislamu na ya Mashia. [3] Nchini Iran Sala ya Idi husaliwa kwa jamaa katika maeneo mbalimbali kwa kuhudhuriwa na waumini wengi. [4]

Katika mji wa Mash’had, Iran Sala ya Idi kila mwaka husaliwa katika Haram ya Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s). [5] Kwa mujibu wa ripoti katika kipindi cha utawala wa ukoo wa Qajar Sala hii katika mji wa Mash’had ilikuwa ikisaliwa katika musala. [6] Katika mji wa Najaf, Iran Sala ya idi husaliwa katika Haram ya Imamu Ali (a.s) [7] na katika mji wa Kufa husaliwa katika msikiti wa Jamia, [8] na katika mji wa Karbala Sala hii husaliwa katika eneo la Baina al-Haramein. [9]

Maamum Amzuia Imam Ridha Kusalisha Sala ya Idi

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha al-Kafi, Maamun Khalifa na kiongozi wa wakati huo wa ukoo wa Bani Abbas baada ya kumchagua Imamu Ridha (a.s) kuwa mrithi wa kiti cha utawala alimtaka asalishe Sala ya Idi na baada ya Maamun kulazimshwa sana hilo, Imamu akakaubali kwa sharti kwamba, Sala hiyo isaliwe kwa mujibu wa suna na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w). [10] Pamoja na hayo na kwa mujibu wa hadithi tajwa, Fadhl bin Sahl, waziri wa Maamun Abbas, wakati alipoona watu wamejitokeza kwa wingi, alimwambia Maamun, kama Imamu Ridha atafika sehemu ya kusalia Sala ya Idi watu watavutiwa na hivyo kuwa pamoja naye. Kwa muktadha huo, Maamun alituma ujumbe na kumtaka Imamu Ridha arejee. [11] Murtadha Mutahhari anasema: Sababu kuu ya Maamun kumzuia Imamu Ridha kusalisha Sala ya Idi siku hiyo ni hatari aliyoihisi ya watu kumpokea kwa wingi Imamu Ridha na kuonyesha huba na mapenzi makubwa waliyonayo kwake; hii ni kutokana na kuwa, Imamu Ridha (a.s) kinyume na mtindo wa maisha ya makhalifa wa Bani Abbas yeye alikuwa akiishi maisha ya kawaida yasiyo na mapambo na mambo ya anasa. [12]

Sala ya Idul-Fitr Tehran Mwaka 1978

Sala ya Idul-Fitr katika mji wa Tehran 4 Septemba 1978 ilisalishwa na Mohammad Mofatteh huku hotuba ikitolewa Muhammad Jawad Bahonar mmoja wa viongozi wa kidini aliyekuwa akiupinga utawala wa Kipahlavi. Sala hiyo ilisaliwa katika miinuko ya Qeytarieh [13] na ikaishia kwa kufanyika maandamano dhidi ya utawala wa Kipahlavi. [14] Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la It’laat, siku hiyo watu milioni 3 walishiriki katika maandamano ya baada ya Sala ya Idul-Fitr katika maeneo mbalimbali nchini Iran. [15] Inaelezwa kuwa, maandamano hayo yalipelekea kutokea maandamanao mengine 8 Septemba 1978 na kufanyika mauaji dhidi ya waandamanaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama vya utawala wa Kipahlavi. [16]

Kusalishwa Sala ya Eidul-Fitr Tehran na Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Baada ya Sayyid Ali Khamenei kuanza kuongoza kama Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (kuanzia mwaka 1989), Sala ya Idul-Fitr mjini Tehran husalishwa na yeye. Katika kipindi cha uongozi wa Imam Khomeini kama Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Khamenei alikuwa pia Imamu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran [17] na kuanzia 1982-1989 alikuwa akisalisha Sala ya Eidul-Fitr. [18] Kuanzia mwaka 1991 Sala ya Idul-Fitr ilikuwa ikisalishwa na Akbar Hashemi Rafsanjani. [19]

Kipindi fulani Sala ya Idul-Fitr ilikuwa ikisaliwa katika Chuo Kikuu cha Tehran, lakini kuanzia mwaka 1993 (Idul-Fitr 1403 Hijiria) [20] imekuwa ikisaliwa katika Musalla mkubwa wa Tehran. Kwa muda wa miaka mitatu mtawalia kuanzia mwaka 2020-2022 Sala ya Idul-Fitr haikusaliwa Musalla kutokana na kuenea maradhi ya Corona. [21).

Hukumu na Adabu za Sala ya Idi

Kwa mujibu wa fiq’h ya Kishia, Sala ya Idi ni wajibu katika zama za uwepo wa Imamu Maasumu [22] na inapaswa kusaliwa kwa jamaa. [23] Aidha ni mustahabu kusali Sala hii katika zama za ghaiba ya Imamu Maasumu [24] ingawa kuna tofauti za kinadharia na kimitazamo kuhusiana na kusaliwa kwa jamaa katika zama za ghaiba. [25] Kwa mujibu wa fat’wa ya Imam Khomeini, kama Walii Faqih (Fakihi Mtawala) au mtu ambaye ana idhini kutoka kwake ataongoza Sala ya Idi au ikasaliwa kwa nia ya rajaa na matarajio, hakuna tatizo katika hilo; kinyume na hivyo kwa tahadhari ya wajibu inapaswa kusaliwa kwa jamaa. [26]

Sala ya Idi ina rakaa mbili. Katika rakaa ya kwanza baada ya Surat al-Fatiha husomwa sura nyingine. Inaelezwa kuwa ni bora katika rakaa ya kwanza baada ya Hamdu ikasomwa Surat Shams na katika rakaa ya pili baada ya Hamdu ikasomwa Surat al-Ghashiyah au katika rakaa ya kwanza baada ya Hamdu ikasomwa Surat al-A’la na katika rakaa ya pili baada ya Surat al-fFatiha ikasomwa Surat Shams. Kadhalika katika rakaa ya kwanza baada ya Sura hutolewa takbira tano na kunuti tano (kunuti moja kila baada ya takbira moja) na katika rakaa ya pili kuna takbira 4 na na kunuti nne. Katika kunuti, inatosha kusoma dhikri na dua yoyote ile kama ilivyo katika Sala za kila siku. Hata hivyo ni bora kusoma dua makhsusi ambayo inaanza na: ((اَللّهُمَّ اَهْلَ الْکبْرِیاءِ وَالْعَظَمَةِ)) [ ]


Dua kamili ya kunuti ya Sala ya Idi:

اَللّهُمَّ اَهْلَ الْکبْرِیاءِ وَالْعَظَمَةِ وَاَهْلَ الْجوُدِ وَالْجَبَروُتِ وَاَهْلَ الْعَفْوِ وَالرَّحْمَةِ وَاَهْلَ التَّقْوی وَالْمَغْفِرَةِ اَسْألُک بِحَقِّ هَذَا الْیوْمِ الَّذی جَعَلْتَهُ لِلْمُسْلِمینَ عیداً وَ لِمـُحَمَّد صلی الله علیه وآله ذُخراً وَشَرَفاً وَ کَرامَةً وَمَزیداً أَنْ تُصَلِّیَ عَلی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ وَ اَنْ تُدْخِلَنی فی کُلِّ خَیرٍ أدْخَلْتَ فیهِ مُحَمَّداً وَآلَ مُحَمَّد وَ أَنْ تُخْرِجَنی مِنْ کلِّ سوُءٍ اَخْرَجْتَ مِنْهُ مُحَمَّداً وَ آلَ مُحَمَّد صَلَواتُک عَلَیهِ وَ عَلَیهِمْ اَللّهُمَّ إنّی اَسْألُکَ خَیرَ ما .سَألَکَ بِهِ عِبَادُکَ الصَّالِحوُنَ وَأَعوُذُ بِکَ مِمَّا اسْتَعَاذَ مِنْهُ عِبَادُکَ الْمـُخْلَصوُنَ



Khutba

Sala ya Idi kama ilivyo Sala ya Ijumaa ina hotuba mbili, ingawa kuna tofauti ambayo ni, hotuba za Sala ya Idi hutolewa baada ya kusali, tofauti na hotuba za Sala ya Ijumaa ambazo hutolewa kabla ya Sala yenyewe. [28] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) na ambayo imekuja pia katika kitabu cha cha Fiq’h cha Jawahir al-Kalam, tofauti hii ni kutokana na kuwa, Sala ya Ijumaa inasaliwa kila wiki na kama hotuba zitatolewa baada ya Sala, watu watachoka na kuondoka, lakini kwa kuwa Sala ya Idi inasaliwa kwa mwaka mara mbili tu, waumini waliohudhuria Sala hubakia hadi mwishoni mwa hotuba. [29] Kadhalika kuhusiana na kuwa wajibu au mustahabu hotuba za Sala ya Idi kuna tofauti za kimitazamo baina ya mafakihi. [30]

Wakati wa Sala ya Idi

Sahib al-Jawahir anasema, kwa mujibu wa nadharia na mtazamo mashuhuri wa mafakihi wa Kishia, wakati wa Sala ya Idi ni kuanzia kuchomoza jua mpaka zawali (adhuhuri ya kisheria) [31] na kama haikusaliwa kwa wakati, basi haina kulipa kadhaa. [32] Kwa mujibu wa fat’wa ya Imam Khomeini ni mustahabu kusali Sala ya Idi baada ya jua kuinuka. [33] Kadhalika Sahib al-Jawahir amenukuu kutoka katika kitabu cha Madarik al-Ahkam ya kwamba, Maulamaa wana mtazamo mmoja kwamba, ni mustahabu Sala ya Idul-Fitr isaliwe kwa kucheleweshwa kidogo ikilinganishwa na Sala ya Idul-Adh’ha, kwani katika Idul Fitr ni mustahabu anayesali afuturu kabla ya kusali na kutoa au kutenga kabisa Zaka yake ya Fitri. Lakini katika Idul Adh’ha ni mustahabu kuchinja na kula nyama ya kichinjwa hicho baada ya Sala. [34]

Adabu

  • Ni mustahabu baada ya Sala ya Idi kutamka dhikiri hii: [35] «اَللهُ اَکبرُ اَلله اَکبرُ، لا اِلهَ اِلّا اللهُ وَاللهُ اَکبرُ، اَلله اَکبرُ وَلِله الحَمدُ، اَلله اَکبَرُ عَلی ما هَدانا»
  • Sala ya Idi haina adhana na iqama, lakini ni mustahabu muadhini kabla ya Sala aseme mara tatu “Salaa”. [36]
  • Ni makuruhu Sala ya Idi kusaliwa katika sehemu ambayo ina kizuizi juu (paa). [37] Imenukuliwa katika hadithi ya kwamba, Imamu Ali (a.s) alikuwa akitoka nyumbani kwake siku ya Idi kwa ajili ya kwenda kusali Sala ya Idi nje ya mji (Kufa) na njia nzima alikuwa akitamka takbira mtawalia. [38] Aidha imenukuliwa kutoka kwa Abdallah bin Omar ya kwamba, Mtume (s.a.w.w) alikuwa akienda kusali Sala ya Idi akitembea kwa miguu na alikuwa akifanya hivyo pia wakati wa kurejea.[39] Imenukuliwa kutoka kwa Abu Rafi’ kwamba, wakati wa kurejea Mtume hakuwa akitumia njia ileile aliyoitumia wakati wa kwenda kusali Idi. [40]
  • Mtu ambaye anasali Sala ya Idul-Fitr anapaswa kutoa Zakatul-Fitr yake kabla ya kusali au kwa mujibu wa fat’wa ya baadhi ya marajii, awe ameitenga kando na mali zake nyingine; [41] kwani kwa mujibu wa hadithi mbalimbali makusudio ya: «تزکی» na «فَصَلَّیٰ» Katika Aya za: [42] «قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَکیٰ» na [43] «وَذَکرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّیٰ» . Ni kutoa Zakat al-Fitr na kusali Sala ya Idul-Fitr. [44]
  • Ni mustahabu kwa anayetaka kusali Sala ya Idi aoge josho na asome dua ambazo zimetajwa katika vitabu vya dua ambazo zinasomwa kabla na baada ya Sala ya Idi. [45]
  • Ni mustahabu kwa anayesali katika Sala ya Idi kusujudu juu ya ardhi [46] na wakati wa kusoma takbira anyanyue mikono na kusoma dhikri za Sala. [47]
  • Katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) imeusiwa kuvaa nguo bora kabisa na kutumia uturi bora kabisa katika Sala ya Idi. [48].

Vyanzo

  • Khomeini, Rūḥullāh. Taḥrīr al-wasīla. Tehran: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeini, 1387 Sh.
  • Khomeini, Rūḥullāh. Tawḍīḥ al-masāʾil. Tehran: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeini, 1386 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Mutaqī al-Hindī, ʿAlī b. Ḥisām al-. Kanz al-ummāl fī sunan al-aqwāl wa l-afʿāl. Beirut: Muʾassisa al-Risāla, 1413 AH.
  • Qāḍī Nuʿmān al-Maghribī. Daʿāʾim al-Islām. Edited by ʿĀṣif Fiyḍī. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1385 AH.
  • Ṭabāṭabāyī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, [n.d].