Saumu ya al-Wisal

Kutoka wikishia

Saumu ya al-Wisal (Kiarabu:صوم الوصال) ni funga ya Saumu ya usiku na mchana (kuanzia adhana ya al-fajiri mpaka usiku wa siku inayofuata) au kufunga Saumu siku mbili mfululizo (kuanzia adhana ya alfajiri mpaka magharibi ya siku inayofuata); bila ya kufuturu hapo katikati. [1] Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Kishia, Saumu ya Wisal (ya kuunganisha bila ya kufuturu) ni miongoni mwa aina za Saumu ambazo zinahesabiwa kuwa ni haramu. [2] Ushahidi wa hukumu hii ni Aya ya 187 katika Surat al-Baqarah ambayo inabainisha muda wa kufunga Saumu (yaani kuanzia wakati gani mpaka wakati gani kisha mfungaji anapaswa kufuturu), [3] hadithi na makubaliano na kauli moja ya mafakihi (ijmaa). [4]

«وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ»


Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.



(Surat al-Baqarah: Aya: 187)


Kwa mujibu wa fat’wa za baadhi ya Marajii, endapo mtu atakuwa hana ufahamu na maarifa ya hukumu ya Saumu na kisha akafunga Saumu siku mbili mfululizo Saumu yake itakayokuwa sahihi na itakayokubaliwa ni ile tu ya siku ya kwanza. [5] Marajii Taqlidi wanasema, endapo mtu hatafuturu baada ya jua kuzama, lakini akawa hana nia ya kuendelea kufunga, hawezi kuhesabiwa kuwa ni kielelezo cha Saumu ya al-Wisal. [6]

Wafafanuzi wa hadithi wa madhehebu ya Kisuni kama Mahmoud Subki wamesema wazi kwamba, Ahlu-Sunna wametoa mitazamo mitatu kuhusiana na hili: Haramu mutlaki, haramu kutokana na kuweko taabu na mashaka kwa Saumu kama hiyo na makuruhu. [7]

Mafakihi kama Muhaqqiq Hilli na Shatibi ambaye ni mmoja wa mafakihi wa madhehebu ya Maliki ameihesabu Saumu hii kuwa ilikuwa inajuzu kwa Mtume (s.a.w.w) na inahesabiwa kuwa miongoni mwa sifa maalumu za Nabii Muhammad (s.a.w.w.) [8]

Mtume (s.a.w.w) amesema: [9]

«لا وِصالَ في صیامٍ»


Saumu ya al-Wisal haijuzu.


Saumu pekee ambayo imeashiriwa katika torati ni Saumu ya Yom Kippur ambapo katika siku hii Mayahudi hufunga kwa saa 25 kuanzia kuzama jua hadi kuzama jua siku inayofuata. [10]

Rejea

Vyanzo