Nenda kwa yaliyomo

Ayaatul Ahkaam

Kutoka wikishia

Ayaatul Ahkaam au Fiqh ul Qur’an (Kiarabu: آيات الأحكام، أو فقه القرآن) : Ni Aya za Qur’ani ambazo zinaelezea au zinazochopolewa kutoka ndani yake hukumu za kisheria. Hukumu za kisheria zinamaanisha hukumu zinazo husiana na matendo mwanadamu, kama vile: Sala, zaka, na jihadi, sio hukumu za imani na maadili. Inajulikana kuwa ndani ya Qur’ani kuna idadi ya Aya 500 ambazo ni Ayaatul Ahkaam.

Qur'an ni chanzo cha kwanza cha fiq'hi. Kulingana na Hadithi, kurudi kwenye Qur’an ili kupata hukumu za vitendo vya dini, ilikuwa ni jambo la kawaida na mashuhuri miongoni mwa masahaba tangu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Katika hali nyengine ni kwamba, Maimamu walifutu na kutoa hukumu za kisheria kwa kutegemea Aya za Quran. Kitabu cha kwanza kilicho andikwa kuhusisna na Ayaatul Ahkaam, kiliandikwa na Muhammad bin Sa'ib Kalbi (aliye fariki dunia mwaka 146 Hijiria) ambaye alikuwa ni miongoni mwa Masahaba wa Imamu Baqir (a.s) na Imamu Swadiq (a.s).

Kuna vitabu vingi vilivyo andikwa kuhusu Fiqh ul Quran, ambavyo vingi vyao vimepewa jina la "Ayaatul Ahkaam". Waandishi wa kazi hizi, kulingana na sifa za Ayaatul Ahkaam, wamegawanya Aya zinazo zungumzia sheria za kifiqhi katika makundi kadhaa; kwa mfano, wameweka zile Aya zenye hukumu zaidi ya moja katika kundi moja na Aya zenye hukumu moja katika kundi lingine. Inasemekana kuwa; baadhi ya Ayaatul Ahkaam (Aya zinazo zungumzia sharia), zimefutwa na hukumu mpya zimekuja badala yake; kama vile Aya ya Najwa isemayo:

﴾یا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا إِذا ناجَیْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَیْنَ یَدَیْ نَجْواکُمْ صَدَقَةً ذالِکَ خَیْرٌ لَکُمْ وَ أَطْهَرُ فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللهَ غَفُورٌ رَحِیمٌ﴿


Enyi mlio amini! mkizungumza kwa faragha na Mtume (s.a.w.w) basi toeni sadaka kabla hamjafanya hivyo, hiyo ni kheri kwenu na ni jambo takatifu zaidi; na mkishindwa basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.



(Surat al-Mujadila, Aya ya 12).


Ufafanuzi

Ayat al-Ahkam, [1] ambazo pia hujulikana kwa jina la Fiq'hu al-Quran, [2] ni zile Aya za Qur’an zinazozungumzia hukumu za kidini (kifiqhi), au ambazo hukumu za kisheria zinaweza kutolewa na kuchopolewa kutoka kwake. Neno "hukmu za sharia" linarejelea kwenye hukumu za vitendo; kama vile hukumu za sala, saumu, jihadi na zakat, na sio hukumu zinazohusiana na maadili au imani. [3] Ikumbukwe kwamba neno «Ayatu al-Ahkam» limetumika kama jina la vitabu vingi vinavyo zungumzia hukumu za vitendo vya Waislamu. Agha Bozorge Tehrani, mwandishi wa al-Dhari'ah, ametaja kazi 30 chini ya jina la Ayat al-Ahkam katika kitabu chake hicho kiitwacho Al-Dhari'ah. Ingawa vitabu hivi wakati mwingine vilikuwa na majina mengine tofauti na jina Ayatu al-Ahkam, ila Agha Bozorge amevitambulisha vyote kwa jina la Ayatu al-Ahkam, kama vile kitabu cha Amir Ibrahim Qazvini kuhusiana na Ayatu al-Ahkam, ambacho jina lake ni «Tahsilu al-Itminaan» na Sherhe Zabdatu al-Bayan cha Maqsud Ardebili. Kwa hiyo kuna vitabu vingi vilivyo orodheshwa kwa jina la Ayatu al-Ahkam. Orodha nzima ya mwanazuoni huyu, utaipata kwenye kitabu chake hicho kiitwacho Al-Dhari'ah, juzuu ya 1, uk. 41 na juzuu ya 3, uk. 396. [4] Mifano mengine ya vitabu hivyo ni pamoja na; Ayat al-Ahkam cha Qutb Ravandi, chenye jina la Fiqh al- Quran, na Ayat al-Ahkam cha Maqadas Ardebili, kilichoitwa Zubdatu al-Bayan. [5] {{Maelezo | Mfano wa Ayatu al-Ahkam katika Qur’ani, ni ile Aya mashuhuri ya inayo husiana naudhu isemayo:

﴾یا أَیهَا الَّذینَ آمَنُوا إِذا قُمْتُمْ إِلَی الصَّلاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَ أَیدِیكُمْ إِلَی الْمَرافِقِ وَ امْسَحُوا بِرُؤُسِكُمْ وَ أَرْجُلَكُمْ إِلَی االْكَعْبَین﴿


Enyi mlioamini mnaposimama kwa ajili ya Swala, osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye viwiko, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka viungo...'. Mnaposimama kwa ajili ya Swala, osheni nyuso zenu na mikono yenu kwa Al-Marafiq, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu kwa Al-Ka'bain...'



(Suratu Ma'idah, Aya ya 6).


Qur'an ni Chanzo cha Kwanza cha Hukumu

Qur'an ndiyo chanzo cha kwanza na muhimu zaidi cha sheria za Kiislamu. [6] Kuna Aya na Hadithi nyingi zinazoelezea kuwa; Qur'an ndio chanzo cha kuelewa dini na ndio kitabu kinachojumuisha ndani yake ibara fafanuzi juu ya halali na haramu. [7] Hata hivyo, baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaoitwa Ikhbaariyyun wanaamini kwamba; Chanzo pekee cha kupata hukumu za kisheria ni Hadithi, na kwamba Qur'an inapaswa kufahamika kupitia Hadithi. Pia wanaamini kuwa ni marufuku kurudi katika Qur'an moja kwa moja bila ya tafsiri ya Ahlul Bayt (a.s). [8]

Ieleweke kwamba; sio fafanuzi zote za hukumu za kisheria zimefafanuliwa katika Qur'an. Bali kile ambacho kimekuja katika Qur'an ni hukumu za jumla, na ni sheria ambazo maelezo yake yanaweza kupatikana katika Hadithi za Maimamu watakatrifu (a.s). [9] Kwa mfano, hukumu ya wajibu wa sala inaweza kupatikana katika Aya za Qur'an, lakini ni rakaa zake, nguzo zake, na nyiradi zake, vyote hivyo vinakuja katika Hadithi.

Historia ya Kuitumia Qur’ani katika Kutoa Hukumu za Kifiqfi

Kwa mujibu wa yale yaliyotajwa katika riwaya, [10] ni kwamba suala la kurejea kwenye Qur'ani na kuchopoa hukumu za kisheria katika Aya zake, lilianza tangu zama za bwana Mtume (s.a.w.w), na tokea zama za kuteremshwa kwa Qur'ani. Pia ilikuwa ni desturi miongoni mwa Maswahaba na wafuasi wa Maimamu (a.s). Mara nyingi, maimamu walikuwa wakieleza hukumu za sharia kwa watu kwa kurejelea Aya za Qur'ani; Kwa mfano, imepokewa kwamba; Abdul A’ala alimwambia Imamu Swadiq (a.s): Nilianguka na ukucha wa kidole chang cha mguu ukang'olka, hivyo ikabidi niufunge kidoke changu, sasa nifanyaje kwa ajili ya udhu? Imamu akasema: Hukumu hii na inayofanana nayo inaweza kufahamika kutokana na Aya isemayo: Mungu hakukufanyieni ugumu katika dini, [11] basi futa juu ya sehemu ulioifunga kutokana na jeraha lako [12].

Mafaqihi wa Kishia nao pia katika zama zote, walikuwa na kawaida ya kurejea katika Qur’an na kwenye Aya zinazo zungumzia hukumu za kisheria ili kuchopoa hukumu za sharia kutoka katika Aya hizo. Lakini suala la kukusanya na kuandika kazi zinazojitegemea katika uwanja wa Ayat al-Ahkam ulianzia mnamo karne ya pili Hijria. Inasemekana kwamba; kitabu cha kwanza juu ya mada hii kiliandikwa na Muhammad bin Saaib Kalbi (aliyefariki mwaka 146 Hijiria), ambaye ni mmoja wa Masahaba wa Imamu Baqir (a.s) na Imamu Swadiq (a.s). [13]

Idadi ya Aya za Kisheria na Maudhui Zake

Kuna maoni tofauti kuhusu idadi ya Ayatu al-Ahkam (Aya zeneye kujadili msuala ya kifiqhi. Katika baadhi ya Hadithi, kwamba robo ya Qur'ani inahusu hukumu za kidini, [14] na katika nyengine inasemekana kwamba theluthi moja ya Aya ni yenye kujadili Aya zinazo husiana na masuala ya kisheria. [15] Miongoni mwa mafaqihi wa Kishia, inajulikana kwamba idadi ya Ayatu al-Ahkam katika Qur’ani, ni Aya mia tano. Pia inasemekana kwamba hakuna idadi kamili katika suala hili, kwa sababu faqihi fulani anaweza kutoa sheria kutoka katika Aya moja huku faqihi mwengine akaacha kuchopoa hukumu katika Aya hiyo. Inawezekana kwamba; mtu wa kwanza kutaja idadi ya Aya 500 ni Muqatil bin Suleiman (aliye fariki mnamo mwaka 150 Hijiria). [17] Aya refu zaidi ya Qur'an kuhusiana na Ayatu al-Ahkam ni aya ya 282 ya Surat al-Baqarah, inayojulikana kama ni Aya ya Daini, ambayo kiuhalisia, pia ndio Aya refu zaidi katika Qur’an.

Kuhusu idadi ya maudhui za Aya za kisheria katika vitabu vya Ayatu al-Ahkam na Fiqh al-Qur'an, Inasemekana kwamba; kwa mtazamo wa haraka haraka, idadi yake ni sawa na idadi ile ile iliojadiliwa katika vitabu vya fiqhi, ambazo mfano wake ni kama vile; tohara, sala, kufunga saumu, Khums, Zakat, ndoa na urithi. (Rejea pia: Abwabu Fiqhi. [18]

Mfano wa Aya Wazi katika Uwanja wa Kisheria

Makala Asili: Orodha ya Aya za Ahkam

Mfano wa Aya maarufu zilizo beba ndani yake sheria waziwazi za kidini ni:

  1. Aya ya udhu isemayo: «Enyi mlioamini! Mkiinuka kuelekea katika sali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu hadi viwikoni, na futeni baadhi sehemu ya vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni».[19]
  2. Aya ya tayammum isemayo: «Na ikiwa ni wagonjwa au mko safarini, au mmoja wenu ametoka kwenye haja kubwa au ndogo, au mmewagusa wanawake (mmekutana nao kimwili), na mkawa hamkupata maji (ya kujisafishia), basi tayamamuni kupitia udongo safi, na muzipake uso zenu na mikono yenu. Mwenyezi Mungu hataki kukusumbueni, bali anataka kukutakaseni na kukutimizieni neema zake juu yenu, hwenenda mkamshukuru». [20]
  3. Aya ya khums isemayo: «Jua kwamba kila mali (ghanima) mnayoipata, basi khums yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na kwa ajili ya jamaa wa karibu, na mayatima, na maskini, na ibnu sabili (wasafiri wa waislamu waliokwama njiani) ....».[21]
  4. Aya ya Saumu isemayo: «Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa saumu juu yenu, kama ilivyokuwa ni faradhi juu ya waliotangulia kabla yenu, ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu».[22]

Upangiliaji wa Aya

Wanazuoni wa Shia wameainisha na kuzigawa Ayatu al-Ahkam kulingana na sifa zake. Kwa mfano, wao wamezigawanya Aya za kisheria katika makundi manne, kulingana na aina ya hukumu zake:

  1. Aya zinazoeleza hukumu makhususi.
  2. Aya zinazoeleza hukumu ya jumla.
  3. Aya zinazotoa chimbuko la msingi fulani wa kisheria (kifiqhi).
  4. Aya zinazotoa chimbuko la msingi maalumu wa usuli al-fiqhi. [23] [Maelezo 1]

Mfumo mwingine wa upangiliaji kulingana na jinsi ya hukumu inavyoelezwa:

  1. Aya zinazoeleza waziwazi hukumu.
  2. Aya zinazoashiria na kutoa mwelekeo wa hukumu kwa njia ya lawama, vitisho, au kwa kutoa bishara na ahadi juu ya tendo na amali fulani.
  3. Aya zitoazo hukumu kwa njia amri au makatazo.
  4. Aya zinazotoa hukumu kwa njia ya kutoa habari. [24] [Maelezo 2]

Aya za ahkam pia zimeainishwa kulingana na kama zina shuhratul-nuzuul au la, na kama zinajumuisha hukumu moja au zaidi. [25]

Kufutwa kwa hukumu za baadhi ya Aya

Makala Asili: Nasuh na Mansuh"

Wanazuoni wa Shia wanaamini kwamba; baadhi ya hukumu za Aya za Qur'ani zimeghairiswa, ingawa wanazuoni hao ni wenye kutofautiana kuhusu ni Aya zipi ambazo hukumu zake zimeghairishwa. Kughairishwa kunamaanisha kuondolewa kwa hukumu moja kwa kuja kwa hukumu nyingine badala yake. Qur'ani imezungumzia suala la kughairishwa kwa hukumu za baadhi ya Aya katika aya mbili; nazo ni (Aya ya 106 ya Surat al-Baqara na Aya ya 101 ya Surat al-Nahli). [26] Wanazuoni wa Shia wamekubali uwepo wa suala la kughairishwa kwa hukumu ya Aya moja ya Qur'ani na hukumu ya Aya nyingine lushika nafasi yake, lakini wachache tu wanao kubali uwezekano wa Hukumu Aya ya Qur'ani kughairishwa kupitia Hadithi. [27]

Baadhi ya aya ambazo zimesemwa kuwa hukumu zake zimeghairishwa ni:

  1. Katika surat al-Anfal, Aya ya 65 ilimtaka kila mujahid wa Kiislamu asimame na kukabiliana na makafiri kumi, kisha Aya inayofuata ikapunguza kwa kutoa takhfifu na kusema kwamba; kila mtu anapaswa kusimama na kukabiliana na makafiri wawili.
  2. Suala la kubadilishwa kwa qibla, ambalo linapatikana katika Aya ya 144 ya Surat al-Baqara.
  3. Aya ya sadaka, ambayo ililazimisha kutoa sadaka kwa sahaba atakaye taka kufanya mazungumzo ya faragha na bwana Mtume (s.a.w.w), kisha hukumu hii ikaiondolewa. [28]

Seti ya orodha ya vitabu vya Aya za Hukumu (bibliographia)

Vitabu vingi vimeandikwa kuhusiana na Aya zilizo beba Hukumu za kisheria ndani yake, ambazo nyingi zimeiandikiwa vibu vingi kwa jina la «Ayatu al-Ahkamu» au «Ahkam al-Qur'an». Kitabu kiitwacho Daaneshname kinaorodhesha vitabu 108 katika uwanja huu, vilivyo rikodiwa kutoka kwa waandishi wa Shia na Sunni. [29] Inasemekana kwamba mtu wa kwanza kuandika kuhusiana na mada hii ya Ayatu al-Ahkamu, katika karne ya pili Hijria, alikuwa ni Muhammad bin Sa'ib Kalbi (aliyezaliwa mwaka 146 Hijiria), ambaye ni mmoja wa masahaba wa Imamu Baqir (a.s) na Imamu Swadiq (a.s). [30] Pia kitabu kiitwacho "Tafsiri Khamsamiah Aya fi al-Ahkami" cha Muqatil bin Suleiman (aliyezaliwa mwaka 150 Hijiria), anacho kiliandikwa katika kipindi hicho hicho. [31] Miongoni mwa kazi zilizoandikwa katika uwanja huu ni; Fikh al-Qur'an cha Qutubu al-Ddin Rawandi (aliyezaliwa mwaka 573 Hijiria), Kanz al-Irfan fi Fiqhi al-Qur'ani cha Faadhil Miqdaad (aliyezaliwa mwaka 826 Hijiria) na Zubdatu al-Bayan cha Muqaddas Ardebili (aliyezaliwa mwaka 993 Hijiria). Hizo ndio kazi zilizochaguliwa kuwa ni miongoni mwa kazi maarufu na muhimu zaidi kuhusu mada ya Ayatu al-Ahkamu. [32]

Maelezo

  1. (A). Mfano wa kesi kwanza ni kwamba; "Kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ni wajibu kwa watu kwenda kuhiji na kutembelea Nyumba Takatifu ya Mwenye Ezi Mungu, kwa kila mwenye uwezo wa kufika huko." (Sura ya Al-Imran, aya ya 97). (B). Mfano wa kesi ya pili ni Aya isemayo: “Lazima msaidiane katika mambo mema na uchamungu” (Suratu al-Ma’idah, Aya ya 2). Aya hii inaeleza hukumu ya jumla ambayo ndani yake inayojumuisha hukumu ya kurudisha vitu vilivyopotea kwa wamiliki wake. (C). Mfano kwa kesi ya tatu: Ni Aya isemayo: “Mwenyezi Mungu amekufanyieni wepesi katika hukumu zake na wala hakuifanyieni ugumu ndani yake” (Sura Baqarah, aya ya 185). Aya hii inahusiana na kanuni ya kifiqhi inayo kanusha na kuepusha shida na dhiki, ambayo inatumika katika fiqhi na sura zake mbalimbali. (D). Mfano wa kesi ya nne: ni Aya isemayo “Enyi mlio amini, anapokuleteeni muovu habari fulani, basi ichunguzeni, msije mkawasababishia watu mateso kwa ujinga (bila ya kujua), kisha mkajuta kwa mliyoyatenda” (Suratu al-Hujurat, Aya ya 6) au pia Aya ya Nafr ilioko katika Suratu Tauba Aya ya 123).
  2. (1). Mfano wa kigao cha mwanzo mwanzo, ni Aya isemayo: “Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ni marafiki wenu, na mkawaacha waumini. Je, mnataka kujitayarishia hoja za wazi dhidi yenu mbele Mwenye Ezi Mungu? (Suratu al- Nisaa, Aya ya 144). (2). Mfano wa kigao cha pili ni Aya isemayo: “Wale waliotangulia kuamini kisha wakakufuru, kisha wakaamini tena na wakawa makafiri tena, kisha wakawazidishia ukafiri wao, Mwenyezi Mungu hatawasamehe na wala hatawaongoza kwenye njia (ya haki). Wape bishara wanaafiki kwamba watapata adhabu chungu” (Suratu al-Nisaa, Aya ya 138 na 139). (3). Mfano wa kigao cha tatu ni Aya isemayo: “Na wapeni mayatima mali zao baada ya wao kubaleghe, wala msibadilishe mali zenu mbaya na duni kuwa mali (zao) nzuri, wala msitumie mali zao kwa kuzichanganya na mali zenu, kwani hii ni dhambi kubwa. ' (Suratu al- Nisa, Aya ya ya 2) ). (4). Mfano wa kigao cha nne ni Aya isemayo: “Wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma, kwa hakika wao wanatumbukiza moto wa Jahannamu matumboni mwao, na hivi karibuni wataingia kwenye moto unaowaka” (Suratu al-Nisaa, Aya ya 10).

Rejea

Vyanzo

  • Āqā Buzurg Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-Shīʿa. Edited by Aḥmad b. Muḥammad Ḥusaynī. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, [n.d].
  • Fakhlaʿī. 1379 Sh. "Justārī dar tārīkh-i tafsīr-i āyāt al-aḥkām." Muṭāliʿāt-i Islāmī, 49-50.
  • Fākir Miybudī, Muḥammad. 1383 Sh. "Dar āmadī bar āyāt al-aḥkām". Payām-i Jāwīdān 3.
  • Fākir Miybudī, Muḥammad. 1390 Sh. "Barrasī-yi naskh wa aqsām-i ān dar āyāt-i qurʾān." Muṭāliʿāt-i Tafsīrī 7.
  • Īrawānī, Bāqir. Durūs tamhīdīyya fī tafsīr āyāt al-aḥkām. Qom: Dār al-Fiqh, 1423 AH.
  • Islāmī, Ridā. Madkhal-i ʿilm-i fiqh. Qom: Markaz-i Mudīrīyāt-i Ḥawzahā-yi ʿIlmīyya, 1384 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Muʿīnī, Muḥsin. 1376 Sh. "Āyāt al-aḥkām". Taḥqīqāt-i Islāmī, 1-2.
  • Muttaqī al-Hindī, ʿAlī b. Ḥisām al-Dīn al-. Kanz al-ʿummāl fī sunan al-aqwāl wa l-afʿāl. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1409 AH.
  • Ṣādiqī Fadakī, Sayyid Jaʿfar. 1390 Sh. "Panj dīdgāh-i maṭraḥ darbāra-yi tiʿdād-i āyāt al-aḥkām." Pazhūhishhā-yi Fiqhī 4.
  • Ṭabāṭabāyī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Shīʿa dar Islām. Sixth edition. Kitābkhāna-yi Buzurg-i Islāmī, 1354 Sh.