Kifo cha Imamu Ali (a.s)

Kutoka wikishia

Kifo cha Imamu Ali (a.s) (Kiarabu: استشهاد الإمام علي عليه السلام) ni tukio la karne ya kwanza Hijria ambalo lilikuwa na athari kubwa kwa Waislamu wa madhehebu Shia. Kifo cha Imamu Ali (a.s) kilisababisha kuanza kwa mauaji na mateso ya Waislamu wa Shia na kusababisha kuvunjika kuparaganyika kwa jeshi la Imamu Ali (a.s). Baada ya kifo cha Imamu Ali (a.s), tofauti za mitazamo, kutokubaliana, na chuki kati ya watu wa Kufa zilianza kuibuka. Baadhi ya wafuasi wa Iamu Ali (a.s) walifananisha jeshi la Kufa baada ya kifo cha Imamu na kundi la kondoo lilimepoteza mchungaji wake na kuvamiwa mbwa mwitu kutoka kila pande. Kikundi cha Khawarij kilikusanyika baada ya Hija na kulalamikia kuhusiana na hali ya Waislamu. Hatimaye, watu watatu walikubaliana kutekeleza mauaji ya kumuua Ali (a.s), Muawiya, na Amru bin Aas. Ibnu Muljim akajitolea kumuua Ali (a.s). Imamu Ali (a.s) katika usiku wa kumi na tisa wa mwezi wa Ramadhani alikuwa ni mgeni wa binti yake Ummu Kulthum, kabla ya adhana ya alfajiri, alielekea msikitini, aliwaamsha waliokuwa wamelala msikitini humo kwa ajili ya swala, akiwemo Ibnu Muljim, naye (Imamu Ali) akasimama kwenye mihrabu na kuanza kuswali. Ibnu Muljim akampiga kichwani mwake pigo moja kwa kutumia upanga, tendo ambalo alilifanya pale Imamu Ali (a.s) alipokuwa katika hali ya kusujudu au alipokuwa akiinuka kutoka kwenye sijda. Imamu alipelekwa nyumbani na tabibu stadi aitwaye Athir bin Amr alimpima ili kujua hali yake. Athir, ambaye alikuwa ni mmoja wa Matabiina, baada ya kugundua kuwa pigo lile limefika kwenye ubongo wa Iamu Ali (a.s), alimwambia Imamu aandae wsia wake, kwa sababu hataishi tena kwa muda mrefu kutokana na pigo hilo. Kabla ya kifo chake, mara kwa mara Imamu alikuwa akipoteza fahamu. Alikuwa akisali sala zake akiwa ameketi na akawa anawausia wasia wake wa mwisho. Maiti ya Imamu Ali (a.s) ilioshwa na Imamu Hassan (a.s), Imamu Husayn (a.s.), Muhammad ibn al-Hanafiyyah, na Abdullah bin Ja'afar. Imamu Hassan (a.s) ndiye aliye chukuwa jukumu za kummsalia baba yake sala ya maiti. Ali (a.s) alizikwa usiku na mahali pa mazishi yake palihifadhiwa ili kuzuia kuchimbuliwa kaburi la na kundi la Khawarij na maadui wa upande wa Bani Umayya, hali hiyo iliendelea pale Imamu Sadiq (a.s) alipokuja kufichua mahali pa kaburi hilo wakati katika zama za utawala wa Bani Abbas.

Athari za Kifo cha Imamu Ali (a.s) Juu ya Hali ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia

Imamu Ali (a.s) aliuawa katika mwezi wa Ramadhani mwaka 40 Hijria. [1] Kifo chake kilitokea wakati ambapo kulikuwa na matatizo mengi ndani ya jamii; wanajeshi hawakuwa wakimtii kikamilifu na walikuwa wazembe katika kumsaidia kiongozi wao. Kinyume chake, jeshi la Sham (Syria) chini ya uongozi wa Muawiya bin Abi Sufian, lilikuwa limeimarika mno. [2] Katika kipindi hichi, Muawiya, akiwa na ufahamu wa hali iliyokuwepo ndani ya wafwasi wa Imamu Ali, alishambulia maeneo mbalimbali ya utawala wa Imamu Ali (a.s.) na kuua pamoja na kupora mali za wafuasi wa Ali bin Abi Talib (a.s). [3] Pale Imamu Ali (a.s) aliposhambuliwa na Ibnu Muljim alikuwa katika hali ya akijiandaa kwa ajili ya kuunda jeshi la kwenda Sham na kupigana na Muawiya. [4] Kifo cha Imamu Ali (a.s) kilileta mgawanyiko mkubwa katika jeshi la watu wa Kufa. Kama alivyo simulia Nauf al-Bakali, mmoja wa wafuasi wa Imamu Ali (a.s), akisema; Wanajeshi walikuwa wakijiandaa kwenda Sham, na mara tu Imamu aliposhambuliwa na Ibnu Muljim, wanajeshi hao walirejea mjini Kufa. Nauf alifananisha hali ya jeshi la Imamu Ali (a.s) na hali ya kundi la kondoo lililopoteza mchungaji wake huku mbwa mwitu wakiwavamia kutoka kila pande. [5] Baada ya kifo cha Imamu Ali (a.s), watu wa Kufa walimpa Imamu Hassan (a.s) kiapo cha utiifu kama ni Khalifa baada ya baba yake; lakini kama wasemavyo baadhi ya watafiti, hali halisi ya Kufa ilikuwa na khitilafu kadhaa, kutokubaliana, na chuki wazi baina ya watu wenyewe kwa wenyewe. Kwa hivyo, jeshi la Imamu Hassan (a.s) halikuweza kupingana au kusimama dhidi ya jeshi la Sham. [6] Ayatollah Subhani, mtafiti wa historia ya Shia, anaamini kwamba kifo cha Imams Ali (a.s) kilikuwa ni pigo kubwa kwa jamii ya Kiislamu na ndio chanzo cha kuanza mauaji, mashambulio, na mateso dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka upande wa maadui zao. [7] Baada ya kifo cha Imamu Ali (a.s) na baada ya kipindi kifupi cha utawala wa Imamu Hassan (a.s), enzi hizi za Bani Umayya, zilikuwa ni enzi na nyakati mgumu zaidi kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia. [8] Hali ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ilizidi kuwa ngumu baada ya Muawiya kupata madaraka. Ibn Abi al-Hadid amesimulia akisema kwamba; Waislamu wa Kishia popote pale walipokuwa wakiishi, ima walikuwa wakiuawa, kukatwa mikono na miguu yao, au kuporwa mali zao na kufungwa magerezani. [9] Waislamu wa Shia hukusanyika misikitini na maeneo ya ibada katika usiku wa ishirini na moja wa mwezi wa Ramadhani, ambao huenda usiku huo ukawa ndio ni usiku wa Laylatu al-Qadri [10] kwa mtazamo wa Kishia, kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s). [11] Maeneo kadhaa nchini Iran, katika usiku huu, hushuhudia tamasha la maombolezo liitwa "Tamasha la Qanbar na Imamu Ali (a.s)". [12] Pia baadhi ya Waislamu wa Kishia husambaza sadaka zao, futari, na daku katika usiku huu. [13] Mashia hufanya amali maalumu ya kukariri mara mia moja dhikri isemayo: "Allahumma il'an qatalata Amiru al-Mu'minina" yaani "Ewe Mungu, walaani wauaji wa Ali (a.s)". Hii ni miongoni mwa amali za usiku wa kumi na tisa na usiku wa ishirini na moja wa mwezi wa Ramadhani. [14]

Je, Imam Ali Alikuwa na Khabari Kuhusiana na Kifo Chake?

Kulingana na baadhi ya Riwaya, Imamu Ali (a.s) alikuwa na habari tosha kuhusiana na kifo chake, ikiwemo wakati na jinsi kitakavyotokea. [15] Katika kitabu Al-Kafi, mojawapo ya vitabu vinne maaruf vya Shia, kuna sehemu isemayo kuwa; Maimamu (a.s) huwa wanaelewa nyakati za vifo vyao. [16] Sheikh Mufid, Allama Hilli, na Sayyid al-Murtadha pia wamelizungumzia jambo hili katika vitabu vyao. [17] Kulingana na maelezo ya Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 Hijria), ambaye ni mwanatheolojia wa Shia, ni kwamba; Riwaya zilizopokewa kuhusiana na jambao hili, ni Riwaya mutawatir (zenye mfululizo wa wapokezi wengi kupitia watu wa kuaminika kutoka matabaka tofauti). [18] Sheikh Mufid alitoa majibu mawili juu ya swali lisemalo kwamba; kama Maimamu, wakiwemo Imam Ali, walikuwa wakijua wakati wa kifo chao, ni kwa nini basi hawakujilinda kuotakana na jambo hilo? Jawabu zake juu ya swali hili ni kama ifuatavyo:

  • Kwanza, huenda ikawa ujuzi wao kuhusiana na wakati na mahali pa kifo chao au pia kuhusiana na muuaji wao haukuwa ni ujuzi wa kina.
  • Pili, kama itakuwa walikuwa na ujuzi wa kina juu ya vifo chao, basi huenda ikawa wao walikuwa na wajibu wa kuvumilia jambo hilo. [19]

Sayyid al-Murtadha (aliyefariki mwaka 436 Hijria), mwanatheolojia mwingine wa Shia, alijibu akisema kwamba; Imamu Ali alikuwa akijua jinsi atakavyokufa na pia alikuwa akimjua muuaji wake, ila hakujua ni wakati gati kifo chake kitakapo wadia; kwa sababu kama angelijua, ingelimbidi kujiepushe na tukio hilo la kuuawa. [20] Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa makala iitwayo "Ujuzi wa Imamu Kuhusiana Kifo na Shaka ya Kutoendana kwake na iamani ya Isma", aliandika akisema kuwa; Katika hali ambapo Maimamu walikubali kujitoa muhanga na kukubaliana kifo chao, hali hiyo haikukiuka hukumu ya wajibu wa mtu kuihifadhi nafsi yake. Kulingana na maoni ya mwandishi huyu, elimu hiyo ya Maimamu haukupatikana kwa njia za kawaida. Hivyo basi, elimu hiyo huenda usiwawajibishe kuzihifadhi nafsi zao, na hata kama ingeliwajibisha, pia Maimamu wanaweza kuwa na jukumu maalumu kwa ajili ya ustawi wa jamii, jukumu ambalo waliwajibika kulitekeleza. [21] Pia Imamu Ridha (a.s) alisimulia akisema kuwa; Imamu Ali (a.s) katika usiku wa kumi na tisa alikubali kuyaweka mambo mikononi mwa Mwenye Ezi Mungu. [22] Mulla Saleh Mazandarani, mfasiri wa kitabu Usul al-Kafi, alieleza akisema kuwa; Imamu Ali (a.s) katika usiku wa kumi na tisa wa mwezi wa Ramadhani alipewa hiari mbili kati ya kubaki duniani na kukutana na Mwenye Ezi Mungu, ila yeye alichagua kukutana na Mola wake ili mipango ya Mwenye Ezi Mungu itimie. Na ikiwa jambo hilo lilifanyika kwa amri na ridhaa ya Mwenye Ezi Mungu mwenyewe, basi sio tu jambo hilo ni la halali, bali ni jambo la wajibu, kama vile Imamu Hussein (a.s) alivyofanya, na sisi pia tunafanya hivyo hivyo wakati wa kupigana jihad dhidi ya maadui zetu. [23]

Nafasi ya Qatam katika Kifo cha Imam Ali (a.s)

Kulingana na ripoti za kihistoria, Qatam binti Shajna alihusika katika kifo cha Imam Ali (a.s). Pale Qatam alipokubali ombi la ndoa au posa ya Ibnu Muljim, alisharitisha mahari yake yawe ni dirham elfu moja, mtumwa mmoja, kijakazi mmoja, na kuuawa kwa Ali (a.s). [24] Ibnu Muljim naye alikubaliana na masharti hayo na akaoana Qatam. [25] Baba [26] na ndugu wa Qatam [27] ni watu walio uawa katika vita vya Nahrawan. Katika ibada ya Hija ya mwaka 39 Hijria, kulizuka mgogoro kati ya mtendaji wa Imamu Ali (a.s) na mtendaji wa Muawiya. Baada ya kumalizika ibada ya Hija, kundi la Khawarij walikusanyika huko Makka na kusema kwamba hawa hawakuheshimu utukufu wa Kaaba. [28] Walilalamikia hali ya Waislamu na kuwakumbuka waliouawa katika vita vya Nahrawan. [29] Hatimaye, watu watatu alikubaliana kutekeleza mauaji ya kuwaua watu watatu ambao ni: Imamu Ali (a.s), Muawiya, na Amr bin Aas. Ibnu Muljim Muradi aliahidi kumuua Imamu Ali (a.s). [30] Ibn Muljim aliwasili Kufa [31] tarehe 20 Shaaban mwaka 40 Hijria na huko ndipo alipokutana na Qatam. [32]

Kupigwa Dharuba kwa Imam Ali (a.s)

Imamu Ali (a.s) alipigwa upanga katika usiku wa kumi na tisa wa mwezi wa Ramadhani alipokuwa mgeni kwa binti yake, Ummu Kulthum, aliye mwalika kwa ajili ya futari. [33] Kwa mujibu wa mwandishi Jafarian, ambaye ni mtafiti wa historia ya Kishia, ni kwamba; Kuna Riwaya nyingi kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s) pamoja na Ahlus-Sunnah zinazoshuhudia hali maalum ya kiroho na kisaikolojia aliyokuwa nayo Imamu Ali (a.s) katika usiku wa kuuawa kwake. [34]

Kulingana na ripoti alizo nukuu Ibnu Athir, ambaye ni mwanahistoria wa madhehebu ya Kisunni katika kitabu chake kiitwacho "Al-Kamil," pamo na Rriwaya kutoka kitabu cha "Al-Kafi" ni kwamba, Imamu alipokuwa akitoka nyumbani katika usiku wa kuuliwa kwake, mabata mzinga walimsimamia mbele yake na watu waalipo jaribu kuwafukuza, Imamu Ali (a.s) aliwaambia akisema; waacheni kwa kwani wao ni wenye kulia na kuomboleza kutokana na huzuni. Allama Majlisi ameihisabu Riwaya hii kutoka katika kitabu "Al-Kafi" kuwa dhaifu. [37] Kwa mujibu wa Allama Majlisi katika "Bihar al-Anwar," ni kwamba; Imam Ali (a.s) alikwenda msikitini na akaadhini yeye mwenyewe, [38] baada ya kuadhini aliwaamsha wale waliokuwa wamelala msikitini kwa ajili ya sala. Pia alimwamsha Ibnu Muljim ambaye aliyekuwa amelala kifudifudi msikitini na kumkanya kutokana na kulala hivyo. [39] Kisha aliingia kwenye mihrabu na kuanza kusali. Ibn Muljim alimsubiri akiwa kwenye sijda [40] na kumpiga panga kichwani mwake, [41] au pale Imamu Ali (a.s) alipokuwa akiinuka kutoka katika sijida [42] Baadhi ya Riwaya zinasema kuwa: Imamu Ali (a.s) alishambuliwa alipokuwa akiingia msikitini, [43] huku Ibn Muljim akisaidiwa au akiwa ameongozwa na Shabib bin Bujra al-Ashja'i [44] pamoja na Wardan. [45] Baada ya Ibnu Muljim kumpiga Imamu Ali (a.s), alisema: "Hukumu ni ya Mwenye Ezi Mungu peke yake na si yako wewe wala wafuasi wako." [46] Riwaya inasema kwamba baada ya Imamu kupigwa upanga huo, Malaika Jibril aliapa mbele ya Mwenye Ezi Mungu akisema kwamba; Kwa hakika misingi ya uongozi imesha poromoshwa na nyota za mbinguni na alama za uchaji Mungu zimezimika. [47] Riwaya hii haipo katika vyanzo vya awali na imepokewa tu katika baadhi ya vyanzo vya vilivyo fuata baadaye. [48] [Maelezo 1: Wa Llahi, nguzo za uongozi zimevunjika, nyota za mbinguni na alama za uchaji Mungu zimezimika, na kamba ya imani ambayo ilikuwa kati ya Muumba na viumbe wake imekatika. Mtoto wa ami yake Muhammad Mustafa (s.a.w.w) ameuawa, Ali Al-Murtadha ameuawa kupita mtu muovu zaidi kuliko wote ulimwenguni."]

Fuztu wa Rabbil Ka'aba

Kwa mujibu wa Ibn Qutaybah Dainawari, ambaye ni mwanahistoria wa karne ya tatu, ni kwamba; Baada ya Imamu Ali (a.s) kupigwa alisema, "Fuztu wa Rabbil Ka'aba", yaani "Naapa kwa Mola wa Ka'ba kuwa nimefaulu" [49] Hadithi imenukuliwa na wanazuoni wa pande zote mbili. Miongoni mwa wanazuoni wa Kishia wailionukuu Hadithi hii ni; Sayyid Radhii [50] na Ibn Shahr Ashub, [51] na kwa upande wa wanazuoni wa Ahlus-Sunnah ni Ibnu Athir [52] na Baladhuri. [53] Ibn Abi al-Hadid anasema kwamba; Baada ya Imamu Ali (a.s) kupigwa upanga huo, waganga wa mji Kufa walikusanyika kwa ajili ya kumpima hali yake ilivyo. [54] Athir bin Amr, baada ya kukagua jeraha la Imamu Ali (a.s), aligundua kwamba pigo lile lilikuwa limefika hadi kwenye ubongo wake. Hivyo, alimtaka Imamu Ali (a.s) kuandika wasia wake wa mwisho, kwa kuwa hali yake haita mruhusu keuendelea kubaki hai kwa muda mrefu. [55]

Wasia wa Imam Ali Baada ya Kupigwa na Upanga

Kuna wasia na maneno tofauti yalio nukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s), katika kipindi cha baada ya kupigwa na upanga hadi kufariki kwake. Mara kadhaa Imamu Ali (a.s) alipoteza fahamu katika kipindi hicho hadi kufariki kwake. [57] Sala zake alizsali hali akiwa amekaa kitako, na alikawausia wanawe kwa kuwapa wasia maalumu. [58] Alitoa wasia maalum ulio nukuliwa katika Nahjul Balagha kwa ajili ya Imamu Hassan na Imam Hussein (a.s). [59] Akiwa katika kipindi hicho, Imamu Ali (a.s) alitoa mazungumzo maalumu kuhusiana na kifo. [60] Imam Ali (a.s) alifariki dunia mnamo 21 Ramadhani mwaka wa 40 Hijiria. [61] Baadhi ya vyanzo vimetaja tarehe nyingine isiokuwa hiyo kuhusiana na kifo chake. [62]

Wasia Kuhusiana na Kisasi kwa Ibnu Muljim

Imamu Ali (a.s) aliwausia watu wake kwa kuwaambia kuwa; ikiwa yeye atafariki kwa pigo hilo alilompigwa na Ibnu Muljim, basi nao wanatakiwa kumpiga Ibnu Muljim kwa pigo moja tu na sio zadi ya hilo, [63] na wala wasije kumkatakata viungo vya mwili wake. [64] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, Imamu aliagiza Ibnu Muljim apewe chakula na maji na kuamiliwa kwa muamala mwema. [65] Hata hivyo, katika vyanzo vingine imeelezwa kwamba baada ya kisasi dhidi ya Ibnu Muljim kutimizwa kupitia mkono wa Imam Hassan (a.s), [66] watu waliuchukua mwili wake na kuuchoma moto. [67] Pia baadhi ya vyanzo vimenukuu tendo la kukatwa kwa viungo vya Ibnu Muljim. [68]

Kukafiniwa Pamoja na Mazishi ya Imamu Ali (a.s)

Mwili wa Imamu Ali (a.s) uliandaliwa na Imamu Hassan (a.s), Imamu Hussein (a.s), Muhammad Hanafiyya na Abdullah bin Ja'afar. [70] Imamu Hassan (a.s) ndiye aliyechukua jukumu la kuusalia mwili wa baba yake. [71] Imamu Ali (a.s) alizikwa usiku na maeneo kadhaa yaliandaliwa kwa ajili ya mazishi yake ili kuficha mahali pa kaburi pake na kubakisha kuwa ni siri isiojulikana na watu ya wakati huo. [72] Mahali alipozikwa Imamu Ali (a.s) palifichwa ili kuepusha kufukuliwa na kundi la Khawarij [73] au uadui wa kutoka upande wa Bani Umayyah. [74] Idadi ndogo ya Waislamu wa upande wa madhehebu ya Shia ndio waliokuwa wakijua mahali pa kaburi la Imamu Ali (a.s). Siri hii iliendelea mpaka pale Imamu Sadiq (a.s) alipoifichua suiri hiyo wakati wa zama za utawala wa Bani Abbas. [75] Mahali pa mazishi ya Imamu Ali (a.s), palikuwa ni ndani ya mji wa Najaf, ila vyanzo vya kidini na kihistoria vimepataja mahala hapo kwa majina tofauti, [76] ila Waislamu wa Kishia wamewafikiana hukusiana na kua kaburi lake ndio lile lililopo hivi sasa mjini Najafa. [77]

Tasnifu ya Pekee (Makhususi)

Maqtal al-Imam Amir al-Mu'minin Ali bin Abi Talib; ni kitabu cha Kiarabu kilichoandikwa na Ibn Abi al-Dun’a (aliyefariki mwaka 281 Hijria), ambaye ni mmoja wa wanahadithi wa Ahlus-Sunnah. [78] Kitabu hichi kimekusanya ndani yake habari maalumu zinazohusiana na mauaji ya Imamu Ali (a.s), habazi ambazo zimekusanya kupitia nukuu za Hadithi zianazohusiana na mauaji hayo. Kitabu hichi kilitafsiriwa kwa Kifarsi na Mahmoud Mahdavi Damghani. [79] Shahidi Tanhaa (Maqtal Amir al-Mu'minin Ali a.s) ni kitabu kilicho andikwa na Sayyid Muhammad Ridha Hosseini Motlaq. [80]

Mada Zinazohusiana:

Haram ya Imamu Ali (A.S), Msikiti wa Kabud Mazar Sharif, Gharat

Rejea

Vyanzo