Nenda kwa yaliyomo

Kuchinja kisheria

Kutoka wikishia

kuchinja kisheria (Kiarabu: الذبح الشرعي) Ni kukata kichwa cha wanyama kwa njia inayokubalika kisheria. Sharti ya kuhalalika nyama ya wanyama halali kuliwa, ni kuchinywa kwa mfumo maalumu uliowekwa na sheria ya dini. Kwa hiyo wanyama wote wanaoishi ardhini (isipokuwa nzige na ngamia, ambao nyama zao huhalalika kwa njia tofauti), ni lazima wahalalishwe kupitia machinjo ya kisheria. Pia wanyama walioharamishwa nao hutoharika nyama na viungo vyao baada ya kuchinjwa kisheria. Kwa mujibu wa fatwa ya mafaqihi, inajuzu kutumia nyama na viungo vyao vya wanyama ambao ni haramu kuliwa, iwapo watachinjwa kupitia mfumo wa kisheria. Bali si halali kula nyama zao, badala yake nyama na viungo vyao vinaweza kutumika katika matumizi yasiokuwa ya chakula. Na pia haifai kutumia ngozi au viungo vya mnyama huyo katika ibada ya sala.

Masharti ya kuchinja kisheria kwa sheria ya Uislamu ni kama ifuatavyo: Kifaa cha kuchinjia ni lazama kiwe cha chuma au mfano wa choma, (chuma ndicho kilichotajwa katika Hadithi) mnyama awe ameelekea Qibla, mnyama awe hai kabla ya kuchinjwa, mchinjaji awe ni Muislamu, mchinjaji atamke jina la Mungu wakati wa kukata kichwa cha mnyama, na ya mwisho ni kukata kiukamilifu mishipa minne mikuu ya shingo kutoka chini ya koo ya mnyama. Pia Katika dini ya Kiyahudi, kuna masharti maalumu yanayozingatiwa kwatika sheria za kuchinja wanyama.

Katika dini ya Kiislamu, kuna desturi maalumu zinazofuatwa katika sheria za kuchinja wanyama, ili kumpunguzia mnyama maumivu kwa kiasi fulani. Hata hivyo, katika baadhi ya nchi zisizo kuwa za Kiislamu, hairuhusiwi kuchinja kwa mfumo wa Kiislamu na ni marufuku kufanya hivyo. Kulingana na baadhi ya tafiti za kisayansi, kuchinja kwa njia ya sheria za kidini husababisha ubora wa nyama, na husababisha nyama hiyo kudumu kwa muda mredu zaidi.

Utafiti wa dhana na hadhi yake

Katika sheria za Kiislamu, kuchinja ni mojawapo ya njia za kuihalalisha nyama, tendo la kuchinja kisheria hutimia kwa kukata mishipa minne ya shingo ya mnyama.[1] Wanyama halali wanaoishi ardhini (isipokuwa ngamia na nzige) [Maelezo 1] ambao wana damu inayochuruzika (inayofoka wakati wa kuchinjwa kwao), na wanyama wa waoishi majini (inayofoka damu yao wakati wa kuchinjwa kwao), huhalalika kupitia chinjo la kisheria. [2] Mnyama aliyechinjwa kwa njia ya kidini huitwa مذکّی (aliyetoharishwa kisheria), ambapo kinyume chake ni mnyama aliyekufa au kuuliwa au kuchinjwa bila kujali sheria za machinjo ya kidini. Mchinja wa mnyama huitwa «ذابح» (mchinjaji) na kichinjwacho huitwa «مذبوح» "Mazbouh".[4]

Qur'ani Tukufu imekataza Waislamu kula nyama ya wanyama ambao hawajachinjwa kihalali [Maelezo 2] [5] Katika vitabu vya fiqhi, mada ya kuchinja wanyama imejadiliwa katika malngo unaohusiana na masuala ya kuwinda na kuchinja. [6]

Masharti kuchinja

Katika dini ya Kiislamu, kuna masharti kadhaa yanayozingatiwa kwa ajili ya kutekeleza uchinja wa kisheria. Masharti hayo ni:

  • Kukatwa Mishipa minne mikuu ya shingo ya mnyama kutoka chini ya koo. [7]
  • Kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja. Kulingana na kauli ya Sahib Al-Jawaher, wanasheria (wanafiqhi) wote wameihisabu sharti hii kuwa ni shyarti ya lazima.[8]
  • Wakati wa kuchinja, mnyama aelekee Qiblah [9] Kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi wa Kishia, kama mtu anayechinja mnyama na atakuwa kuwa hii ni miongoni mwa sharti za kichinja, kisha akamchinja kwa makusudi mnyama bila ya kumuelekeza Qiblah, nyama ya mnyama huyo itaharamika. [10]
  • Kifaa cha kuchinjia kiwe kimetengenezwa kwa chuma; Bila shaka, ikiwa ni kutakhofiwa mnyama mnyama huyo kufa bila ya kuchinjwa, basi hati jiwe au kifaa chengine chochote kile chengine chenye ncha kali kinaweza kutumika kumchinja myama huyo. [11]
  • Mchinjaji lazima awe Muislamu [12] Kwa mujibu wa kauli ya Shahidi Al-Thani, mwanasheria wa Shia katika karne ya 10, yeye anasema; Fatwa za wanasheria wote wa Kiislamu zimesisitiza ya kwamba, mchinjaji hawezi kuwa kafiri asiye muamini Mungu, aliyeritadi, au miongoni mwa Maghulati (waoamini uungu wa Ali). [13] Bila shaka, kuna nadharia mbili kuhusiana na uchinjaji wa Ahlul Al-Kitabi (Mayahudi na Wakiristo); Wengi miongoni mwa mafaqihi wa Kishia hawakubaliani na uchinjaji wa Wakiristo na Wayahudi, na vichinjwa vyao wanavihisabu kuwa haramu na najisi. [14] Pia Mafakihi wa Kishia wanaviharamisha vichinjwa vya Nawasib (wenye uwadui na Ahlu Al-bait) na wanavihisabu vichinjwa vyao kuwa ni najisi na haramu. [15]
  • Mnyama lazima awe hai kabla ya kuchinjwa. Kuna kundi la mafaqihi wasemao kwamba; ni lazima mnyama huyo autikise mwili wake au apige miguu yake baada ya kuchinjwa ili kuonyesha kwamba alikuwa hai kabla ya kuchinjwa. [16]
  • Kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi wa Kiislamu, ni sahihi kuchinja wanyama kwa vifaa vipya (yaani kupitia teknolojia za mashine za kuchinjia); Lakini ni lazima litajwe jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, na sharti zingine za kuchinja pia zizingatiwe, kama vile kukatwa kwa mishipa minne mikuu. [17] Pia, wanazuoni wamejuzisha kula nyama tusizokuwa na uhakika nazo kuhusiana na uchinjwaji wake wa kisheria, ila ni lazima ziwe zimenunuliwa kutoka kwa Muislamu au kutoka katika soko la Waislamu. [18]

Nidhanu za uchinjaji wa kisheria

Kuna nidhamu kadhaa zilizotajwa katika vitabu vya fiqhi kuhusiana na sheria za uchinjaji wa kisheria:

Nidhamu pendekezwa (Mustahabbu)

  • Mchinjaji aelekee Qibla. [19]
  • Chombo cha kuchinjia kiwe kikali na tendo la uchinjaji lifanyike kwa haraka (yaani mnyama asikeketwe).
  • Kabla ya kumchinja mnyama , kwanza mnyama huyo apewe maji.
  • Mnyama aandaliwe kwa upole kabisa kwa ajili ya kuchinjwa.
  • Wakati wa kuchinja kondoo, yatakiwa miguu miwili yake ya nyuma ifunganishwe na mguu wake mmoja wa mbele. Yaani mguu wake mmoja wa mbele ubaki huru.
  • Wakati wa kuchinja ng'ombe, miguu yake yote minne inatakiwa kufungwa na mkia wake uwe huru.
  • Baada ya kumchinja kuku, aachwe ili apige mbawa zake. [20]

Yasiopendekezwa kutendwa (Makruhu)

  • Kukata uti wa mgongo kabla ya mnyama kutoka roho yake.
  • Kumchinja mnyama mbele ya wanyama wengine.
  • Kumchinja ambaye umemlea mwenyewe, na una urafiki naye.
  • Kuchinja mnyama wakati wa usiku.
  • Chinja siku ya Ijumaa kabla ya kukingiuka kwa jua .
  • Kutumbukiza kisu nyuma ya koo na kukivuta mbele, ili koo ikatwe kutoka nyuma. [21]

Faida za chinjo la kisheria

Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi wa Kiislamu, baada ya mnyama halali kuchinjwa kupitia chinjo la kisheria, nyama yake huwa ni halali na viungo vyake huwa ni safi na ni halali kuvitumia; Ila akiwa aliyechinjwa atakuwa ni myama ambaye si halali kumla, nyama yake na viungo vyake vitasafika na kutoharika, ila nyama yake haitageuka kuwa ni halali. Yaani itabakia ni haramu kama ilivyokuwa mwanzo.Kwa mujibu wa fat'wa za baadhi ya mafaqihi, ngozi na shamau zao zinaweza kutumika katika kazi mbali mbali, [22] ila katika sala tu haitajuzu kuvitumia vitu hivyo. [23]

Kulingana na baadhi ya tafiti, kumchinja mnyama kwa njia ya kidini kuna athari chanya kwenye ubora wa nyama ya mnyama huyo. Ubora huo unatokana na kule nyama kusafika na kutokuwa na damu ndani yake. Kiuimara nyama hiyo huwa na ubora wa hali ya juu zaidi, na hudumu zaidi bila ya kuharibika, ukulinganisha na nyama ya mnyama aliyechinjwa kupitia njia nyingine zisizokuwa za kidini (Kiislamu). [24]

Uchinjaji wa kiyahudi na kikiristo

Katika Dini ya Kiyahudi, kuna maagizo maalumu yanayohusiana na sheria za kuchinja wanyama. Miongoni mwazo sheria zilizoashiriwa ndani ya Talmud (Kitabu cha Kiyahudi) ni kwamba; Kabla ya mnyama kuchinjwa, ni lazima mnyama huyo asiwe na fahamu au asiweze na uwezo wa kusimama kabla ya kuchinjwa kwake. [25] Pia, kuchinja kunapaswa kutekelezwe na mtu ambaye amefunzwa na wasomi wa Kiyahudi (marabi) jinsi ya kuchinja wanyama, na anatakiwa kumpiga pigo lililo sahihi na la haraka. [26] Mfumo na njia ya kuchinja wanyama katika dini ya Uyahudi inaitwa Shahiita (Shechita) [27] Lakini katika Ukristo, hakuna sheria maalum inayohusiana na kuchinja wanyama. [28]

Marufuku ya kuchinja kidini katika baadhi ya nchi

Katika baadhi ya nchi kama vile Uholanzi, [29] Denmark [30] na Ubelgiji [31] kuchinja wanyama kwa njia za Kiislamu na Kiyahudi ni marufuku. Sababu ya sheria hii ni kuzuia maumivu na mateso ya wanyama wakati wa kuwachinja. [32] Bila shaka, falsafa ya baadhi ya desturi za Kiislamu katika kuchinja wanyama, kama vile ukali wa kisu na kasi ya uchinjaji, inahisabiwa kuwa ni moja ya njia za kumpunguzia maumivu ya mnyama katika machinjo yake. [33] Katika baadhi ya nchi za Kikristo, kwatoa fahamu mnyama kabla ya kuwachinja ni moja ya kanuni za uchinjaji wa wanyama. [34] Kulingana na nadharia za mafaqihi wa Kishia, hakuna tatizo kuwatoa fahamu wanyama kabla ya kuwachinja, iwapo jambo hilo halitapelekea mnyama kufariki kabla ya kuchinjwa kwake. [35]

Orodha ya vitabu

Kuna vitabu na maandishi mengi yalioandikwa kuhusiana na uchinjaji wa kidini na sheria zake. Ikiwa ni pamoja na:

  • Barresi Tatbiiqiy Dhibhi Shar'ii Dar Islam: Katika kitabu hiki, kumelinganishwa maoni ya wanasheria wa Kishia wa karne ya 12 na maoni ya madhehebu manne ya fikra za Kisunni. [36]
  • Dhibhe Dar Islam, Aathare wa Ahkame Mutaabiq Baa Madhahibe Islami: Ni kitabu kilichoandikwa na Benyamin Shirkhani katika lugha ya Kiajemi. Chapa ya Majma Jihaniy Taqriib Madhahibe Islami. Kitabu hichi kilichapisha mwaka wa 1398 Shamsia. [37]
  • Pazuuhesh Tatbiiqiy Dar Ahkame Fiqhiy Dhibh: Kilichoandikwa na Mohammad Rahmani. Chapa ya Markaze Mutaaliate wa Tahiqiiqate Hawze Namaayandegiy Walii Faqiih, Wizarate Kishawarziy. Kitabu hichi kilichapishwa mnamo mwaka 1377 Shamsia. [38]
  • Kitabu cha Raweshehaye Mukhtalif Dhibhe wa Aathare Aan Bar Kaifiyyate Gusht, cha Sayyid Said Farhi, ambacho kilichapishwa katika lugha ya Kiajemi mwaka wa 1394 Shamsia. [39]

Rejea

  1. Shāhrūdī et al, Farhang-i fiqh, vol. 3, p. 701.

Maelezo

  1. شتر با نَحر (کارد را در گودی بین گردن و سینه شتر فروکردن)(امام خمینی، رساله توضیح‌المسائل، ص۴۱۲، مسأله۲۵۹۵.) و ملخ با صید (زنده‌گیری) تذکیه می‌شوند.(امام خمینی، رساله توضیح‌المسائل، ص۴۱۸، مسأله۲۶۲۲.)
  2. حُرِّمَتْ عَلَيْکُمُ الْمَيْتَةُ وَ الدَّمُ وَ لَحْمُ الْخِنْزيرِ وَ ما أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ وَ الْمُنْخَنِقَةُ وَ الْمَوْقُوذَةُ وَ الْمُتَرَدِّيَةُ وَ النَّطيحَةُ وَ ما أَکَلَ السَّبُعُ إِلاَّ ما ذَکَّيْتُمْ وَ...؛ برای شما مؤمنان گوشت مردار و خون و گوشت خوک و آن ذبیحه‌ای که به نام غیر خدا کشتند. همچنین هر حیوانی که به خفه کردن یا به چوب زدن یا از بلندی افکندن یا به شاخ زدن به هم بمیرند و نیم‌خورده درندگان، جز آن را که قبلًا تذکیه کرده باشید حرام است و...

Vyanzo

  • Cohen, Abraham. Everyman's Talmud: the major teaching of the rabbinic sages. Translated into Farsi by Amir Firiydūn Gurgānī. Tehran: Nashr Yahūdā, 1350 AH.
  • Daftar-i Intishārāt-i Islāmī. Tawḍīh al-masāʾil marājiʿ, Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1392 SH.