Kujikurubisha Kwa Mwenyezi Mungu

Kutoka wikishia

Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Kiarabu: استجابة الدعاء) ni kufanya ibada au jambo kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kujikurubisha Kwake. Nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la lazima tu katika Wajibaat Taabudi kama Swala, Swaumu na Hija na bila ya hilo ibada hizo hazisihi. Lakini katika Wajibat Tawassuli hakuna haja ya nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi. Baadhi wanaamini kuwa, nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu sambamba na imani ni miongoni mwa masharti ya kupata thawabu.


Utambuzi wa maana (conceptology)

Makusudio ya kufanya amali ya ibada kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni kutekeleza agizo na amri ya Mwenyezi Mungu na kumridhisha Mola Muumba. [1] Mafakihi (wanazuoni wa fikihi) wa Kishia wanaamini kuwa, kutekeleza amali mbalimbali za ibada kwa lengo na msukumo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kutaka kupata radhi zake, kufikia na kupata thawabu, kuwa mbali na adhabu na kufikia maslahi na manufaa katika ibada ni miongoni mwa njia za kupatikana hali ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. [2] Baadhi wanaona kuwa, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na imani ni sharti la kupata ujira ambapo bila ya hilo ujira huo hauwezi kumfikia aliyefanya amali hiyo. [3]

Kigezo cha kugawanywa wajibu katika taabudi na tawasuli

Amali na matendo ya wajibu kwa mujibu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu yanagawanywa katika makundi mawili.

  • Wajibaat Taabudi: Hizi ni amali za wajibu ambazo ni sharti ndani yake kuweko na nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na bila ya sharti hilo amri ya Mwenyezi haitakuwa imetekelezwa. Kama Swala na Swaumu. [4] Ayatulllah Makarem Shirazi, fakihi (mwanazuoni wa fikihi) mtajika wa Kishia anasema, ubora wa kitendo na ubora wa mtendaji ni katika nguzo za ibada. Makusudio ya ubora wa mtendaji ni kwamba, mtendaji wa ibada hiyo anapaswa kuifanya amali hiyo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kutaka radhi Zake, na sio kwa ajili ya ria, kujionyesha, kutaka kumfurahisha fulani na kadhalika. [5] Hata hivyo wanazuoni wa fikihi wa Kishia wametofautiana kimitazamo kuhusiana na je, wajibu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika Wajibaat Taabudi ni jambo la kiakili au la kisheria; [6] kuna misingi mitatu jumla kuhusiana na jambo hili:
  1. Mtazamo wa Ayatullah Khui: Wajibu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la kisheria na muwekaji sheria (Mwenyezi Mungu) amezingatia pia suala la kujikurubisha Kwake katika suala la ibada.
  2. Mtazamo wa Mirza Naini: Wajibu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la kisheria na muwekaji sheria (Mwenyezi Mungu) amezingatia suala la wajibu wa kujikurubisha Kwake katika suala jingine lisilokuwa la ibada. [7]
  3. Mtazamo wa Akhund Khorasani: Wajibu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la kiakili na linategemea namna ya utekelezaji wa amali na kumtii Mwenyezi Mungu. [9] Kama lengo la aliyeweka sheria ni kutekelezwa tu jambo hilo katika sura yake ya nje kama vile wajibu wa kuzika maiti, akili haitambui ulazima wa kuweko suala la kujikurubisha. Lakini kama lengo la muweka sheria ni kwamba, kwa kufanyika amali apate pia Yeye hiyo ‘hali ya kujikurubisha” katika sura hii, akili inatambua ulazima wa kujikurubisha. [10]
  • Wajibaat Tawassuli: Ni wajibu ambazo katika kuzitekeleza wajibu hizi, nia ya kujikurubisha (kwa Mwenyezi Mungu) sio sharti la lazima. Ni kama vile: Kumuokoa mtu ambaye anazama, kumzika maiti na kulipa deni. [11]


Kigezo cha kugawanywa wajibu katika Taqarrubi na Tawassuli

Katika kitabu chake cha Tahdhib al-Usul, Imamu Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) amezigawa wajibu katika makundi mawili ya Wajibaat Taqarrubi na Wajibaat Tawassuli. [12] Katika wajibaat taqarrubi nia ya kujikurubisha ni sharti humo na zenyewe ziko makundi mawili.

  • Wajibu ambazo anuani ya ibada inasadikika kwazo kama vile Swala, Swaumu, Hija na kadhalika. [13]
  • Wajibu ambazo licha ya kuwa kujikurubisha ni sharti, lakini hazihesabiwi kuwa ni ibada. Kama vile kutoa Zaka. [14]

Rejea

Vyanzo


  • Ākhund Khurāsānī, Muḥammad Kāẓim. Kifāyat al-uṣūl. Qom: Muʾassisa-i Āl al-Bayt(a) li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1409 AH.
  • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Tahdhīb al-usūl. Qom: Muʾassisa-i al-Nashr al-Islāmī, 1405 AH.
  • Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Ajwad al-taqrīrāt. 2nd Edition. Qom: Kitāb furūshī Muṣṭafawī, 1368 SH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Ḥīlahā-yi sharʿī wa chāra jūʾīhā-yi ṣaḥīḥ. 2nd Edition. Qom: Madrisa al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib(a), 1428 AH.
  • Muʾassisa-i Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī. Farhanq-i fiqh fārsī. Qom: Muʾassisa-i Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī, 1387 SH.
  • Muzaffar, Muḥammad Riḍā al-. Uṣūl al-fiqh. Qom: Daftar Tablīghāt Islāmī, 1370 SH.
  • Pazhūhishgah ʿUlūm wa Farhang Islāmī.Farhangnāma-yi usūl-i fiqh. Qom: Pazhūhishgah ʿUlūm wa Farhang Islāmī, 1389 SH.