Qur'an Kareem

Kutoka wikishia
Nakala ya Qur'an, kati ya karne ya 4 au 5

Qur'an kareem (Kiarabu: القرآن الكريم ) ni maneno ya Mwenyezi Mungu na kitabu kitakatifu cha Waislamu, ambacho ameteremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Mola wake kupitia malaika Jibril. Waislamu wanaamini ya kwamba; matini pamoja na maana au uelewa wa Qur'an, vyote vimeteremshwa na Mungu. Pia wanaamini ya kwamba; Qur'an ni muujiza na ithibati ya utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ndio kitabu cha mwisho cha Mwenyezi Mungu kuwateremkia waja wake. Kitabu hichi kimejisisitizia muujiza wake huku kikizingatia ithibati ya muujiza wake, ni kuwa hakuna mtu anayeweza kuja na mfano Aya, Sura na kitabu kinachofanana nacho.

Kwa mara ya kwanza kabisa Aya za Qur'an ziliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), akiwa kwenye pango la Hiraa lililoko kwenye Mlima Noor. Maoni ya watu wengi ni kwamba; Aya zake ziliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupitia Malaika wa Wahyi (Jibril) na moja kwa moja bila ya kuwepo wakala mwingine yeyote yule katikati. Waislamu wengi wanaamini kwamba Qur'an iliteremshwa hatua baada ya hatua, Lakini wengine wanaamini kwamba, pamoja na Aya kuteremshwa kwa hatua baada ya hatua, ila Mwenyezi Mungu alikuwa akimteremshia katika usiku wa Qadri (Lailatul-Qadri) kiwango chote kilichokuwa kimekadiriwa kuteremshwa katika kipindi cha mwaka mzima.

Katika zama za Mtume (s.a.w.w), Aya za Qur'an zilikuwa zikiandikwa kimtawanyiko; kwenye ngozi za wanyama, makozi ya mitende, karatasi na vitambaa. Baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), Aya na sura za Qur'an zilikusanywa na Maswahaba; Lakini ilikuwa na nakala au matoleo mengi yaliyotofautiana katika mpangilio wa sura zake na namna ya visomo vyake (usomekaji wake). Hatimae kupitia amri ya Othman, matoleo na nakala mbali mbali za Qur'an zikakusanywa na kutokomezwa, na badala yake kukatayarishwa nakala moja tu ya Qur'an. Mashia nao wakiwafuata Maimamu wao, wanaamini ya kwamba; Qur'an hii tuliyonayo ni Qur'an sahihi isiyo na aina yoyote ile ya kasoro au mapungufu.

Qur'an, Furqan, Al-Kitab na Mus-haf ni miongoni mwa majina maarufu ya Qur'an. Qu'ran ina sura 114 na Aya zaidi ya 6000 na imegawanywa katika sehemu (juzuu) 30 na vifungu (hizbu)120. Katika suala la vifungu ambavyo huitwa "hizbu", kila juzu ima hugawiwa vifungu viwili au vinne. Hivyo basi iwapo kila juzu itagawiwa vifungu viwili, jumla tutakuwa na hizbu 60 za Qur'an, ila kama kila juzu itagawiwa vifungu vinne, hapo tutapata idadi ya hizbu 120 Katika Qur'an. Kuna mada kadha zilizozungumzwa ndani ya Qur'an, miongoni mwazo ni: Tauhidi, ufufuo, vita vilivyopiganwa katika zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w), visa vya Manabii, matendo ya kisheria katika kidini ya Kiislamu, maadili mema na maovu na vita dhidi ya ushirikina na unafiki.

Hadi karne ya nne Hijiria, kulikuwa na aina mbalimbali maarufu za usomaji wa Qur'an miongoni mwa Waislamu. Kuwepo kwa matoleo na nakala tofauti za maandishi ya Qur'an, ukiongezea na kuwepo aina mbalimbali za visomo miongoni mwa Waislamu, kunatokana na mambo kadha; Yakiwemo uchanga maandishi ya Kiarabu katika zama hizo, kuwepo kwa lahaja mbalimbali za lugha ya Kiarabu pamoja na mapenzi ya wasomaji kuisoma Qur'an kwa mitindo tofauti ya usomaji. Katika karne ya nne, kulikuwa na visomo saba vilichaguliwa miongoni mwa visomo tofauti vya Qur'an. Kisomo mashuhuri mbele ya Waislamu walio wengi duniani, ni kisomo cha Qur'an kupia mfumo wa usomaji wa Asim uliyonukuliwa kutoka kwa Hafs.

Tafsiri kamili ya kwanza ya Qur'an kwa Kiajemi iliandikwa mnamo karne ya 4 Hijiria, huku tafsiri Kilatini ikiwa imeandikwa mnamo karne ya 6 Hijiria, sawa na  karne ya 12 Miladia. Tafsiri ya Qur'an ya Kilatini kwa mara ya kwanza kabisa ilichapishwa nchini Italia mnamo mwaka  950 Hijiria sawa na mwaka 1543 Miladia. Chapa ya kwanza ya Qur'an iliyochapishwa na Waislamu, ni chapa ya mwaka 1200 Hijria iliyochapwa mjini St. Petersburg Urusi. Iran ilikuwa ni nchi ya kwanza ya Kiislamu kuchapisha Qur'an katika mwaka wa 1243 Hijiria na mwaka 1248 Hijiria. Qur'an inayojulikana leo kwa jina la chapa ya Othman Taha, ni Qur'an inatokana na chapa ya Misri.

Qur'an imekuwa chanzo cha elimu nyingi miongoni mwa Waislamu. Tafsiri na sayansi (elimu) za Qur'an kama vile historia ya Qur'an, sayansi (elimu) ya maneno ya Qur'an, sayansi (fani) ya nahau na balagha (sanaa ya lugha) ya Qur'an, visa vya Qur'an pamoja na miujiza ya Qur'an ni miongoni mwa sayansi (elimu) mbalimbali za Qur'an.

Qur'an ina nafasi maalumu katika mila na sanaa za Kiislamu. Kukhitimisha Qur'an kwa ajili ya maiti na kusoma Quran katika sherehe ya ndoa ni miongoni mwao Mila za Waislamu kwa jumla. Mashia nao wana mila kama hizo ukiongezea na ile mila ya kuweka Qur'an juu ya vichwa vyao katika usiku wa Lailatul-Qadri. Miongoni mwa sanaa zilizokolea rangi zaidi kuhusiana na Qur'an, ni sanaa ya uchoraji wa hati za Qur'an, nakshi za Qur'an na kipamba Qur'an kupitia ngozi yenye nakshi zenye kuvutia fasihi na usanifu wa kimajenzi kupitia hati za Qur'an.


Maneno ya Mwenyezi Mungu

Kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu, Qur’an ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupitia njia ya wahyi. [1] Pia Waislamu wanaamini ya kwamba; Maana na maneno yake yote yametoka kwa Mwenyezi Mungu. [3] Imeelezwa ya kwamba; Aya za mwanzo zilizoteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w), zilikuwa ni Aya za Surat 'Alaq, na Sura ya kwanza iliyoteremshwa kwa ukamilifu wake kamili, ilikuwa ni Surat Al-Fatiha. [4] Kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu, Mtume wa Muhammad (s.a.w.w), ndiye Mtume wa mwisho, na Qur'an ndicho kitabu cha mwisho cha Mwenyezi Mungu kuwateremshia waja wake. [5]


Jinsi ya Kupokea Wahyi wa Quran

Qur’an ikizungumzia suala la uwezekano wa manabii na mitume kupokea wahyi, imeta njia  tatu za mfumo ushuswaji wa wahyi: Kwa njia ya ilhamu (kupokea kiini cha ujumbe bila ya kupitia maneno na bila ya kutumwa mjumbe), njia ya nyuma ya pazia (kupitia sauti iumbwayo na Mwenyezi Mungu) na kupitia kwa Malaika.” [6] Baadhi ya wanazuoni wasemasema ya kwamba, Mtu amereremshiwa Qur'an kwa njia ya wahyi wa Jibril tu, na hakupokea kupitia nji zaidi ya hiyo. Wao katika kuthibisha maoni yao wameitegemea Aya Ifuatayo: «قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ» ; “Sema: Yeyote yule mwenye uadui na Jibril (aelewe ya kwamba) kwa hakika yeye ameiteremsha Qur'an moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu." [7] Yaani mwenye Uaduia na Jibril atakuwa na uadui na Mwenye Ezi Mungu, kwa sababu yeye katumwa na Mola wake kuiteremsha Qur'an. [8] Maoni mashuhuri ni kwamba; Qur'an iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa njia tofauti, ikiwemo njia ya moja kwa moja (njia ya ilhamu) na pia kwa njia ya kushushiwa ujumbe kupitia jibril. [9]


Kushuka Kiujumla na Kushuka kwa Hatua kwa Hatua

Kwa mujibu wa baadhi ya Aya za Qur’an, kitabu hichi kiliteremshwa ndani ya mwezi wa Ramadhani na ndani ya usiku wa Qadri. [10] [Maelezo1] Kwa hiyo, kuna khitilafu baina ya Waislamu kuhusu je, Qur’an yote kwa pamoja, au ilimeteremshwa polepole (hatua kwa hatua). 11] Kuna waliosema: Qur’an imeteremshwa mara moja tu yote kwa jumla, [12] huku kundi jengine likiamini kwamba; Mwenyezi Mungu alimteremshia Mtume wake (s.a.w.w), kiwango cha mwaka mmoja cha Qur'an katika kila mwaka ndani ya usiku wa Lailatul-Qadri. [13] Baadhi ya watu pia wanaamini kwamba Qur'an iliteremshwa polepole tu ambapo mwanzo wa kuteremshwa kwake ulikuwa katika mwezi wa Ramadhani ndani ya usiku wa Lailatul-Qadri. [14]

Majina maarufu ya Qur'an

Majina mengi yaliyometajwa kuhusiana na Qur'an, Miongoni mwayo ni: Qur'an, Furqan, Al-Kitab na Mus-haf. Jina la Al-Mus-haf ndilo mashuhuri zaidi miongoni mwa majina hayo. [15] Jina la Mus-haf ni jina alilolitumia Abu Bakar katika kuiita Qur'an, lakini majina mengine yaliyobaki ni majina yametajwa katika Qur'an yenyewe. [16] Qur'an ndilo jina maarufu zaidi la kitabu hichi. Neno hili kihalisi lina maana ya "kusomwa kwa wingi au kinachosomwa kwa wingi", Neno hili limekaririwa mara 50 ndani ya Qur'an, huku mwanzoni mwake likiwa limeanzia na alifu na lamu, katika matumizi hayo yote,  neno hili lina maana ya kitabu cha Qur'an. Neno Qur'an pia likiwa halijaanzia na alifu na lamu, limekaririwa ndani ya Qur'an mara 20, ambapo mara 13 limetumika likimaanisha kitabu cha Qur’an. [17] Qur’an pia ina lakabu nyingi ambazo zinaashiria maana ya Qur’an, kama vile: Majid, Karim, Hakim na Mubeen. Mwandishi wa kitabu cha Qur'an wa  Qur'an Pazuhiy, ambaye ni Bahau Al-Din Khoramshahi anaamini ya kwamba; katika utamaduni wa Uislamu na Shia, watu wa madhehebu ya Sunni siku zote huita Qur'an kwa jina la "Qur'an Karimu" yaani kwa kupitia kivumishi "Karimu" na watu wa madhehebu ya Shia daima huita Qur'an kwa jina la "Qur'an Majidu" yaani wao hutumia kivumishi cha "Majidu", na vivumishi vyote viwili vina asili ya Qur'an. [18] Sadru Al-Mutalahin mwandishi wa kitabu Al-Asfar, katika sura ya (15) mlango wa saba wa sura hiyo ameutewa maalumu kwa ajili ya lakabu za Quran, malngo ambao ameuita "Faslun Fi Al-Qab Al-Qur'an wa Na'utihi" yaani: Mlango wa Majina na Sifa za Qur'an. Ndani ya mlango huo ameorodhesha zaidi ya majina na lakabu ishirini za Qur'an, lakabu na majina ambayo ameyafafanua akitegemea Aya za Qur'an katika ufafanuzi wake huo. [19] [Maelezo 2]

Nafasi mbele ya Waislamu

Qur'an ni chanzo muhimu zaidi cha fikra za Waislamu na ndiyo kigezo kikuu cha vyanzo vingine vya fikra za Kiislamu kama vile Hadith na Sunnah mbalimbali. Hii ina maana kwamba mafundisho yote ambayo yamepokewa kupitia vyanzo vingine vya Kiislamu hayotakuwa sahihi endapo yanapingana na mafundisho misingi mikuu ya Qur’an. [20] Kwa kuzingatia maelekezo ya Hadith za Mtume na Maimamu wa Kishia (a.s), ni lazima Hadith zipokewazo kupiti vyanzo mbalimbali  zipimwe kupitia dhana na misingi ya Qur'an, na iwapo hazitawafikiana nayo, basi hazitakuwa na mashiko wala hadhi. [21]

Kwa mfano, imepokewa kutoka kwa Mtume wa Uislamu Muhammad (s.a.w.w) akisema: “Kila neno linalosimuliwa na kunasibishwa kwangu mimi, basi lipimeni kwa kigezo cha Qur'an, ikiwa litawafikiana nayo, basi hilo litakuwa nimelisema mimi, na iwapo likipingana na Qur'an, basi hili sijalisema mimi". [22] [Maelezo 3] Pia kuna Hadithi kutoka kwa Imam Swadiq (a.s), isemayo kwamba; Hadith yoyote inayopingana na Qur'an ni Hadithi ya uwongo. [23]

Historia ya Qur'an

Kuandika na Kuhaririwa

Makala asili: Kuandikwa kwa Qur'an

Mtume wa Uislamu Muhammad (s.a.w.w) amesisitiza sana kuhifadhi Qur'an na kuzisoma Aya zake kwa njia usahihi. Bwana Mtume (s.a.w.w) alifanya jitihada kubwa katika kuhimiza na kuhakikisha kuwa hakuna kipingele au Aya ya Qur'an itakayopotea. Kutokana na kuwepo kwa watu wachache wanaojua kusoma na kuandika na ukosefu wa vifaa vya kuandikia katika miaka ya mwanzo ya Utume. Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa kuogopa kwamba neno fulani la Qur'an lisije likasahauliwa au kuandikwa kimakosa, alisisitiza sana kuzisoma na kuzihifadhi Aya zote za Qur'an kwa njia sahihi. [24] Pale Aya fulani ilipoteremshwa , yeye Aliwaita waandishi wa wahyi ili waiandike na kuirikodi. [25] Aya za Qur'an ziliandikwa kwenye vitu mparaganyiko, kama vile; Kwenye vipande vya ngozi za wanyama, makozi ya mitende, nguo pamoja na karatasi. [26]

Mtume mwenyewe alikuwa ndiye msimamizi wa uandishi wa wahyi. Baada ya Mtume (s.a.w.w) kuwasomea waandishi wake Aya za Qur'an, aliwataka waandishi hao wa wahyi wasome waliyoyaandika ili kusahihisha makosa yanayoweza kutokea katika maandishi. [27] Suyuti ameandika akisema: Katika zama za Mtume (s.a.w.w), Qur'an yote ilikuwa imeshaandikwa, ila hakuwa katika sura ya mjumuiko mmoja, pia Sura zake nazo zilikuwa bado hazijabainishwa na kuwekwa katika mfumo na mpangilio maalumu. [28]

Tendo la ukusanyaji na uhariri wa Qur'an katika hali yake ya sasa halikufanyika katika zama za Mtume (s.a.w.w). Kwa mujibu wa maelezo ya mwandishi wa kitabu Al-Tamhidu fi Ulumi Al-Qur'an, ni kwamba, katika zama za Mtume, ilikuwa tayari Aya na majina ya surah za Qur'an zimeshabainishwa. Hata hivyo, mkusanyo wa mwisho wa Qur’an na mpangilio wa Sura zake, pamoja na kuwekwa katika mfumo wa kitabu, ulifanyika baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w) kupitia uamuzi wa Maswahaba. [29] Kwa mujibu wa maelezo ya kitabu hichi, mtu wa kwanza aliyeikusanya Qur'an alikuwa ni Imam Ali (a.s), yeye Alizikusanya surah za Qur'an kwa kuzingatia tarehe ya kuteremshwa kwake. [30]


Kukusanywa kwa Misahafu

Baada ya kifo cha Mtume, Maswahaba wake wakubwa, kila mmoja wao, alianza kukusanya Qur'an. Misahafu mingi ilikusanywa katika zama hizo, ambayo ilikuwa ikitofautia katika mpangilio wa Sura na usomekaji wake. [31] Hili lilifanya kila kundi miongoni mwao lione usomaji wao wa Qur'an kuwa ni sahihi na kuuhisabu usomaji mwingine kuwa sio sahihi. [32]

Kupitia pendekezo la Huzaifa kwa Othman la kuunganisha Misahafu, pendekezo ambalo lilikubaliwa na Masahaba wa Mtume, Othmani aliagiza kundi la Masahaba maalumu kufanya kazi hiyo. [33] Alituma watu katika ardhi tofauti za Kiislamu na akakusanya Qur'an zote zilizopo, Kisha akaamuru ziangamizwe. [34] Kwa mujibu wa maandishi ya Kitabu cha Al-Tamhid ni kwamba; Kuna uwezekano mkubwa kuwa kazi hiyo ya kuunganishwa kwa Qur'an ilifanyika mnamo mwaka wa 25 wa Hijiria. [35]


Maimamu wa Kishia Kuuwafiki Msahafu wa Othman

Tazama pia: Msahafu wa Othmani "مصحف عثمانی"

Kwa mujibu wa Hadithi, Maimamu wa Shia walikubaliana na tendo la kukusanywa kwa Qur'an, na pia wameukubali Msahafu uliokusanywa kwa amri ya Othmani. Siyuti amekuu kutoka kwa Imam Ali (a.s) ya kwamba; Othmani alikwenda kushauriana naye kuhusu kuzikusanya Qur'ani zote zilizokuwepo mikononi mwa Waislamu katika zama hizo, naye akakubaliana naye juu ya jambao hilo. [36] Vile vile imesimuliwa kwamba; Imamu Swadiq (a.s) alimuona mtu aliyekuwa akiisoma Qur'an kinyume na kisomo rasmi kinachotumiwa na Waislamu, naye akamkataza kuisoma Qur'an katika mtindo huo [37] Kwa mujibu wa kitabu cha Al-Tamhid, Mashia wote wanaiamini Qur'an ilioko mikononi mwa Waislamu wa leona wanakubaliana nayo kuwa ni Quran sahihi na kamili isiyo nadosari. [38]


Visomo vya Quran

Makala asili: Wasomaji saba na riwaya Kumi na nne

Hadi karne ya 4 Hijiria, ilikuwa ni kawaida miongoni mwa Waislamu kuisoma Qur'an kupitia njia na visomo tofauti. [39] Mambo muhimu yaliyopelekea kuwepo kwa visomo tofauti vyya usomaji, ni kuwepo kwa nakala tofauti za Qur'an miongoni mwa Waislamu, uchanga wa mfumo na fani ya uandishi wa Lugha ya Kiarabu, kukosekana kwa nukta kwenye maandishi ya Kiarabu, kukosekana kwa irabu (vokali) ambazo ni herufi tamfu, kuwepo kwa lafudhi tofauti, na ushabiki wasomaji wa Qur'an (walimu wa Quran). [40]

Katika karne ya nne Hijiria, Abu Bakar bin Mujahid bingwa wa wasomaji wa Baghdad (aliyezaliwa mwaka 324 na kufariki 245 Hijiria), alichagua visomo saba miongoni mwa visomo vyote. Wasomaji wa visomo hivi wanajulikana kwa jina la Qura'aa Sab-'a. Kwa vile kila moja kati ya visomo hivi vimesimuliwa kwa Riwaya mbili tofauti, hivyo basi jumla ya visomo hivyo itakuwa ni visomo 14 vya Qur'an. Hivyo basi ndivyo visomo vilikubaliwa na Waislamu. [41]

Masunni wanaamini kuwa maneno ya Qur'an yana njia na miundo mbalimbali, na watu wanaweza kuisoma Qur'an hiyo kwa mujibu wa muundo na njia yoyote ile waitakayo. [42] Kwa upande wa pili, wanazuoni wa Kishia wanasema kwamba: Qur'an iliteremshwa kwa usomaji mmoja tu, na kama Maimamu wa Kishia wameruhusu kuisoma Qur'an kwa visomo tofauti, wamefanya hivyo kwa ajili ya kuirahisisha dini tu. [43]

Kisomo maarufu zaidi miongoni mwa Waislamu, ni kisomo cha Asim kupitia Riwaya ya Hafs. Kuna kundi miongoni mwa wanazuoni na watafiti wa Qur'an wa Kishia wanaoamini kwamba; Kisomo hichi cha Asim ndio kisomo pekee sahihi kilichopokewa kwa njia ya tawatur (kupitia matabaka wapokezi walioishi katika zama tofauti). Pia wanaamini kuwa; Visomo vyingine vyote vilivyobakia havikunukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), bali ni natija ushabiki wa wasomaji tu. [44]


Kutiwa Irabu (Vokali) Qur'an

Picha ya nakala ya Qur'an yenye tafsiri ya Kiajemi, inayohusiana na kipindi cha Taymurii

Vokali au irabu zina nafasi muhimu katika kuelewa maana ya maneno lugha ya Kiarabu, suala hili huwa na umuhimu maradufu pale tunapozungumzia umuhimu wa irabu katika kuilewa Qur'an. Hii inatokana na kwamba; Kutoelewa irabu (vokali) za maneno ya Qur’an, husababisha kutoelewa maana, ua hupelekewa mabadiliko ya uwelewa katika kufahamu maana za maneno ya Qur'an. Jambo hili wakati mwingine husababisha kuelewa maana isiyokusudiwa na Mwenyezi Mungu. [45] Hapo mwanzo waandishi wa wahyi waliyaandika maneno ya Qur’an bila ya nukta wala irabu (vokali), na hilo halikuwa tatizo kwa wale walioishi zama za Mtume (s.a.w.w), bali kwa vizazi vya baadae, na hasa Waislamu wasiokuwa Waarabu, wakati mwingine ilisababisha kupatikana visomo tofauti vya Qur'an. Katika hali hiyo jambo pekee ambalo litaweza kumaliza tatizo hilo, ni suala la kutia irabu (vokali) Qur'an, jambo ambalo lilipelekea kumaliza migogoro katika kuainisha maana za maneno ya Qur'an, na pia kuzuiya upotoshaji na usongomanishaji wa Qur'an. [46] Ripoti za kihistoria zimekhitalifiana kuhusu tukio la kwanza la utiaji vokali wa  wa Qur'an. Kwa kawaida Abu al-Aswad Dueli (aliye fariki mwaka 69 Hijiria), ndiye anayetambulika kama ni wa kwanza kabisa aliyefanya kazi ya kutia irabu maneno ya Qur'an Kareem, suala ambalo alilifanya kwa msaada wa Yahya bin Ya'amar. [47] Uwekaji wa awali wa irabu za Qur'an, ulikuwa kama ifuatavyo: Kuliwekwa alama ya nukta juu ya herufi ya mwisho ya neno ikimaanisha au kuwakilisha vokali ya "fat'ha", nukta chini ya herufi ya mwisho wa neno, ikimaanisha vokali ya "kasra", nukta kabla ya herufi ya mwisho ikimaanisha vokali ya "dhumma". [48] Karne moja baadaye, Khalil bin Ahmad Farahidi (aliye fariki mwaka 175 Hijiria), alikuja na alama nyingine ambazo zilichukuwa nafasi ya nukta, na ni: mstatili au mraba juu ya herufi ambayo ni alama ya vokali ya "fat'ha", mstatili au mraba chini ya herufi ambayo ni vokali ya "kasra", alama ya wau (kama alama ya koma) ndogo juu ya herufi ambayo ni vokali ya "dhumma". Yeye alipotaka kuonesha alama ya tanwini (ambazo ni fat'ha mbili au kasra mbili au dhumma mbili, ambazo huwakilisha nasasi ya nuni sakina) alikariri alama hizo mara mbili, yaani ima aliweka miraba miwili juu au chini au aliweka viwau (vikoma) viwili juu ya herufi ya mwisho wa neno. Yeye pia alitumia ala ndogo inayofanana na alama ya "w" kwa ajili ya vokali yenye mkazo (shadda), alitumia ziro ndogo iliyo nyumbuka kwa ajili ya vokali ya "sukun". [49] Kisha katika nusu ya pili ya karne ya pili ya Hijiria, wakaja wataalamu wa nadharia za fani ya sarufi wa mji wa Basra, kama vile: Siibawaihi, na wannadharia wa fani ya sarufi wa Kufa wakiongozwa za mwanadharia wao maarufu ajulikanaye kwa jina la Kisai, na katika katikati ya karne ya 3 ya Hijria, kukazaliwa wananadharia wa fani ya nahau wa mji wa Baghdad, jambo ambalo lilipelekea kuchanua na kuimarika elimu ya irabu za lugha, jambo ambalo lilileta mabadiliko makubwa katika fani ya irabu za Qur'an. [50]


Tafsiri

Makala asili: Tafsiri ya Qur'an

Tafsiri ya Qur'an ina historia ya kale mno na asili yake imeanza tokea mwanzoni mwa Uislamu. [51] Ila tafsiri ya kwanza kamili ya Qur'an katika lugha ya Kiajemi ilifanyika katika karne ya nne Hijiria. [52] Pia imesemwa ya kwamba; Mfasiri wa kwanza wa Qur'an alikuwa Salman Farsi, ambaye aliifasiri بسم الله الرحمن الرحیم (kwa jina la Yazdan, Mwingi wa Rehema). Neno Yazdan neno la Kiajemi lenye maana ya Mungu [53]

Tafsiri ya Qur'an katika lugha za Ulaya hapo awali ilifanywa kupitia makasisi wa Kikristo na watawa. Wao walifanya hivyo Ili kuukosoa Uislamu katika mijadala ya kitheolojia, wao walitafsiri baadhi tu ya ibara za Qur'an. [54] Tafsiri ya kwanza kamili ya Qur'an kwa Kilatini iliandikwa katika karne ya 6 Hijiria, sawa na karne ya 12 Miladia. [55]


Kuchapishwa kwa Qur'an

Kwa mara ya kwanza kabisa Qur'an ilichapishwa nchini Italia mnamo mwaka wa 950 Hijiria, sawa na mwaka 1543 Miladia. Chapa hii iliharibiwa na kutokomezwa kwa amri ya mamlaka ya kanisa. Baada ya hapo, mnamo mwaka wa 1104 Hijiria sawa na mwaka 1692 Miladia, kisha mnamo mwaka 1108 Hijiria swana na mwaka 1696 Miladia, Qur'an ilichapishwa tena huko Ulaya. Toleo la kwanza la Qur'an lilitolewa na Muislamu ni toleo la mwaka 1200 Hijiria. Moula Othman aliifanya kazi hiyo huko St. Petersburg Urusi. Nchi ya kwanza ya Kiislamu kuchapisha Qur'an ilikuwa Iran. Iran ilitoa nakala mbili nzuri kutoka kwake mnamo mwaka 1243 na 1248 Hijiria. Katika miaka iliyofuata, nchi nyingine za Kiislamu kama vile Uturuki, Misri na Iraq zilitoa matoleo tofauti ya Qur'an. [56]

Qur'an iliyochapishwa nchini Misri ilitayarishwa mwaka 1342 Hijiria chini ya usimamizi wa maprofesa wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar na kwa kuzingatia nukuu ya riwaya ya Hafs kutoka kwa Asim, Qur'an ambayo ilikubaliwa na ulimwengu mzima wa Kiislamu. Qur'an, ambayo leo hii inajulikana kwa jina la Othman Taha, imeandikwa na mwandishi na mchoraji wa hati za Kiarabu kutoka nchini Kisiria, Qur'an ambayo imechapwa kulingana na vigezo vya uchapishaji wa Misri. Qur'an hii imechapishwa katika nchi nyingi za Kiislamu. Sifa ya chapa hii ni mpangilio wa Aya kwenye kurasa na mgawanyo wa vikundi au vifungu (hizbu) na katika mpangilio wake wa juzu thelathini za Qur'an. [57]

Leo, uchapishaji wa Qur'an unafanywa chini ya usimamizi wa mashirika yanayohusiana suala la uchapaji wa Qur'an, chini ya sheria maalum. [58] Nchini Iran, shirika la Dar A-Qur'an Al-Karim ndilo shirika lenye jukumu la kusahihisha na kusimamia uchapishaji wa Qur'an. 59]

Muundo na mjengeko wa Qur'an

Qur'an imejengeka kupitia; Surah 114 na takriban Aya elfu sita. Kuna khitilafu ya maoni juu ya idadi kamili ya za Qur'an Kareem. Baadhi wamenukuu kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba; Qur'an ina Aya 6236.[60] Qur'an imegawika katika juzu 30 na vifungu (hizbu) 120. [61] Ugawanyikaji wa vifungu (hizbu) vya Qur'an unategemea zama au tamaduni za Waislamu katika kuisoma Qur'an, katika zama za Masahaba Qur'an ilikuwa ikigawiwa katika namna tofauti; Wengine walikuwa wakiigawa vifungu vitatu, wengine vifungu vitano, wengine saba, wengine tisa, wengine kumi na moja na wengine kumi na tatu.

Katika zama za leo, ima hugawiwa vifingu 60 au 120. [61] Falsafa ya kuigawa Qur'an kwa vifungu, ni kwa ajili ya kurahisisha khitimisho la Qur'an. Kwahiyo, wanaoigawa vifungu vitatu, huwa wanasoma kila siku kifungu kimoja, kwa maana hiyo kila siku 3 huwa wanahitimisha khitma moja ya Qur'an.


Sura

Makala asili: Surah

Kila Sura za Qur'an hujengeka kupitia idadi fulani za Aya za Qur'an, Sura huwa na idadi za Aya zenye maudhui moja au zaidi, ambazo huwa zimefungika katika mfungo maalumu unaoitwa Sura. [62] Sura za Qur'an, isipokuwa Surat Tauba, huwa zinaanzia kwa: بسم الله الرحمن الرحیم ; Yenye maana ya: (Ninaaza kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. [63] Sura hizo huwa zimegawika makundi mawili, nazo ni Sura zilizoshuka Makka na zilizoshuka Madina. Sura zilizoteremshwa kabla ya kuhama Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) kwenda Madina zinaitwa Makkiyyah, na Sura zilizoteremshwa baada ya Mtume (s.a.w.w) kuhama kwenda Madina zinaitwa Madaniyyah. [64]


Aya

Makala Asili: Aya

Aya ni neno, vifungu vya maneno au sentensi za Qur'an zinazounda Sura za Qur'an. [65] Kila Sura huwa na idadi fulani ya aya. [66] Aya za Qur'an hutofautiana katika ukubwa au urefu wake. Aya ya 282 ya Surat al-Baqarah ndio aya refu zaidi katika Qur'an. Miongoni mwa Aya fupi za Qur'an, ni kama vile:  "Modhammatan" "«مُدهامَّتان»" (Aya ya 64 ya Surat al-Rahman, "Wal-Dhuhaa" «والضُّحی» ambayo ni Aya ya kwanza ya Surat al-Dhuhaa), "Wal-Fajri" ambayo ni Aya ya kwanza ya Surat al-Fajri pamoja na Aya ziloanza kwa herufi tupu. [67]

Aya za Qur'an katika mfumo wa viwango vya uwelewa na ufahamikaji wake zimegawanyika katika kategoria mbili: Aya tata, zenye sura ya uwelewa zaidi ya mmoja (Ayatu Mutashabihati) na Aya zenye uwelewa ulio wazi na unaofahamika bila ya utata (Ayatu Muhkamati). Kwa hiyo, Aya zisizo tata ni Aya ambazo maana yake iko wazi kiasi yakwamba hakupatikani shaka juu welewa wa dhana yake. Aya tata nazo ni zile Aya ambazo kiuhalisia wake, zina uwezekano wa kuwa na zaidi ya maana moja, jambao ambalo huleta utata katika dwelewa wa dhana yake. [68] Uainishaji wa kategoria hizi umeelezewa na Qur'an yenyewe. [69]

Pia kuna kategoria nyingine ilizotumika katika kuzigawa Aya za Qur'an, nayo ni kategoria iliyozigawa Aya katika makundi yafuatayo: Aya inayobatilisha hukumu ya Aya nyingine, ambayo huitwa "Naasikh" yenye maana ya "mfutaji", namna ya pili ni Aya iliyobatilishwa hukumu yake, ambayo imepewa jina la "Mansuukh" yenye maana ya "mfutwaji". [70]


Juzu na Hizbu (Kivungu) cha Qur'an

Makala asili: Juzu na Hizbu (Kifungu)

Juzu na Hizbu (kifungu), ni aina mbili za mgawanyo wa Qur'an uliobuniwa na Waislamu wenyewe. Imedhaniwa kuwa Waislamu wamefanya hivyo ili kujipangia mfumo wa kusoma au kuhifadhi Qur'an kila siku. Migawanyo hiyo ilikuwa ni migawanyo binafsi na haikuwa sawa katika viwango vyake, bali kila mmoja alikuwa na kigao chake maalumu kinachotofautiana na vigao vya watu wengine. [71] Inasemekana kwamba: Wakati wa zama za Mtume (s.a.w.w), Qur'an iligawanwa katika vifungu saba, ambapo kila kundi kilijumuisha Sura kadhaa za Qur'an. Pia katika baadhi ya zama, Qur'an ilionekena kukawiwa kuanzia vifungu viwili hadi vifungu kumi. Katika zama zetu za leo, Qur'an imegawiwa katika juzu thelathini, ambapo kila juzu imegawiwa katika Hizbu (vifungu) nne. [72]

Mada za Qur'an

Ndani ya Qur’an kuna mada mbalimbali, kama vile mada za masuala ya kiitikadi, maadili, kanuni za sheria, visa vya watu wa zama zilizopita na kupambana dhidi ya wanafiki na washirikina. Baadhi ya dhana na mada muhimu za Qur'an ni: tauhidi, ufufuo, matukio yaliyotokea katika zama za awali ya Uislamu kama vile vita vilivyopiganwa katika zama za Mtume (s.a.w.w), visa vya ndani ya Qur'an, kanuni za namna ya kuabudu, kanuni za kimahakama za dini ya Kiislamu, kanuni na sheria kuhusiana na maadili mema na maovu na kanuni juu ya kukataza ushirikina na unafiki. [73]

Uimara wa Kutopotosheka

Makala asili: Upotoshaji wa Qur'an

Linapozungumziwa suala la upotoshwaji wa Qur'ani, mara nyingi huwa linalenga suala la upotoshaji wa uongezaji au upunguzaji wa neno au ibara fulani ndani ya Qur'ani. Abul Qasim Khui ameandika akisema: Waislamu wote kwa jumla wanakubaliana ya kwamba, suala la upotoshaji kupitia maana ya kwanza (kuongeza neno au ibara) halijawahi kuthibiti katika Qur'an. Hata hivyo, kuna tofauti ya maoni kuhusiana na kuondolewa kwa neno au maneno kutoka katika Qur'an [74] Kwa mujibu wa maoni yake, rai za wanazuoni wa Kishia ni kwamba, upotoshaji katika maana hii ya pili pia haujafanyika ndani ya Qur'an. [75]

Changamoto na muujiza wa Qur'an

Makala asili: Changamoto na Muujiza wa Qur'an

Katika baadhi ya Aya za Qur'an, Mwenyezi Mungu amewataka wapinzani wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), iwapo hawamtambui Mtume wa Mwenyezi Mungu, kuwa ni mjumbe wa Mungu, basi walete kitabu kama Qur'an au sura kumi au angalau sura moja mfano wake. [76] Waislamu wamelihisabu suala hili kuwa ni miongoni mwa changamoto za Qur'an. Neno hangamoto linatokana na neno "تحدی" ambalo ni neno la Kiarabu lenye maana ya kutoa tangazo la kujidhatiti katika kukabiliana na mpinzani, yaani kumtaka mpinzani ajitokeze na aoneshe uhodari wake. Kwa mara ya kwanza kabisa, neno hili lilitumika katika maandishi ya kitheolojia ya karne ya tatu, katika kuthibitisha changamoto ya Qur'an dhidi ya wapinzani wake. [77] Kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu ni kwamba; Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuleta kitabu kama Qur'an, na hii ni ithibati ya muujiza huo wa Qur'an na utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Qur’an yenyewe nayo ni yenye kusisita kwamba, Qur'an ni maneno ya Mungu, na pia imejidhatiti ya kuwa hakuna awezaye kuleta mfano wake. [78] Miujiza ya Qur’an ni miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika fani ya sayansi (elimu) za Qur’an inayochunguza na kutafiti ithibati zinazothibitisha kuwa Qur’an ni muujiza wa Mungu. [79]

Sayansi (Elimu) zinazohusiana na Qur'an

Qur'an imekuwa ndio chanzo cha elimu nyingi miongoni mwa Waislamu. Tafsir na fani ya (elimu) za Qur'an (علوم القراَن), ni mojawapo wa elimu hizo mbalimbali za Qur'an.


Tafsiri

Makala aslili: Tafsiri

Tafsiri ni  elimu ya kufafanua na kubainisha maana zaq Aya za Qur’an. [80] Fani ya tafsiri ya Qur’an imeanza tokea zama za bwana Mtume (s.a.w.w), na yeye mwenyewe alikuwa ndiye mfasiri wa kwanza wa Qur'an. [81] Imam Ali (a.s), Ibn Abbas, Abdullah bin Masoud na Ubi bin Ka'ab, walikuwa ndio wafasiri wa kwanza wa Qur'an baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). [82] Qur'an Karimu imefasiriwa kwa njia na mifumo tofauti. Baadhi ya njia na mifumo hiyo ni: Tafsiri ya kimaudhui "تفسیر موضوعی", tafsiri kwa taratibu za Aya na Sura "تفسیر ترتیبی", tafsiri ya Qur'an kwa Qur'an "تفسير القراَن بالقراَن", tafsiri kupitia Hadithi "تفسير الروائي", tafsiri ya kisayansi "تفسير العلمي", tafsiri ya kifiqhi "تفسير الفقهي", tafsiri ya kifalsafa "تفسير الفلسفي", na tafsiri ya ki'irfani au kisufi "تفسير العرفاني".


Sayansi (Elimu) za Qur'an

Makala asili: Fani ya Sayansi (Elimu) za Qur'an

Mkusanyo wa elimu zinazoijadili Qur'an, unaitwa sayansi za Qur'an "علوم القراَن". Historia ya Qur'an, tafiti juu Aya zinazohusiana na sheria, fani ya lugha ya Qur'an, fani ya irabu na sanaa ya lugha ya Qur'an, sababu za kushuka Aya za Qur'an, visa vya Qur'an, miujiza ya Qur’an, fani ya usomaji, tafiti juu ya Aya na Sura za Makka na Madani, tafiti juu ya Aya tata na Aya bayana na tafiti juu ya Aya zilizofuta hukumu na Aya za kabla yake, ni miongoni mwa mada za sayansi (elimu) za Qur’an "علوم القراَن". Vyanzo muhimu vya sayansi (elimu) za Qur'an ni:


  • Kitabu Imla-i Maa Manna Bhii Al-Rahmanu "إملاءُ ما مَنَّ بِه الرحمن" cha    Abu Al-Baqqaa Akbariy (aliyefariki mwaka 616 Hijiria)
  • Kitabu Al-Burhanu fii Ulumi Al-Qur'an "البرهان فی علوم القرآن" cha Zarkashi (aliyefariki mwaka 794 Hijiria)
  • Kitabu Al-Itqanu fii Ulumi Al-Qur'ani cha Jalal Al-Din Suyuti (aliyefariki mwaka 911 Hijiria)

Mila, sanaa na tamaduni

Qur'an ina umuhimu mkubwa katika maisha ya kijamii ya Waislamu. Vikao vya kukhitimisha Qur'an hufanyika katika hadhara mbali mbali misikitini, majengo ya makaburi ya Maimamu na wana wa Maimamu, pia kuna hadhara mbali mbali za kidini ninazofanyika majumbani. [86] Uwekaji wa Qur'an juu ya vichwa, ni miongoni mwa mila za ibada zinazozifanywa na Mashia katika mikesha ya Lailatul-Qadri. Katika ibada hii, huku wakiiweka Qur'an kichwani, wanaapa kwa haki ya Mwenyezi Mungu, kwa haki ya Qur'an na Maasumina, ili Mola wao awasamehe dhambi zao. [87]

Qur'an huwa na nafasi na hadhi maalumu katika mikusanyiko mingi rasmi ya Waislamu, kama vile mikusanyiko ya mawaidha, pamoja na mikusanyiko inayohusiana na mila tofauti za kijamii, ikiwemo mikusanyiko katika sherehe za harusi. Mara nyingi ndani ya mikusanyiko ya aina hiyo, Aya za Qur'an husomwa kama ni utangulizi wa kufungulia shughuli za mikusanyiko hiyo. [88] Mojawapo ya taratibu za kawaida nchini Iran ni kuingia na Qur'ani, pale mmoja wao anapoingia katika nyumba mpya au anapohama. Wairani wanapoingia katika nyumba mpya, kwanza kabisa huiingiza Qur'an, kisha huingiza vitu vingine vilivyobakia nyumbani humo. [89]

Qur'an ina uhusiano mkubwa na mila za Wairani za Nowruz (Sherehe za Mwaka Kogwa). Katika sherehe hizo, Wairani wanaweka Qur'an juu ya meza ya Haftsin (Meza yenye vitu saba vinavyoanzia na herufi ya siin ambayo ni herufi ya "s"). Woa huuanza mwaka mpya kwa kusoma Aya za Qur'an. Pia katika baadhi ya familia, wazee hutoa Eid kupitia Qur'an, yaani wazee huweka pesa katika Qurani na watoto wanaifungua na kuchukua Eid yao. [90]

Qur'an katika sanaa

Qur'an imekuwa ni chanzo cha tafakuri na nadharia nyingi katika sanaa za Kiislamu. Dhihiriko lake kubwa zaidi linaweza kuonekana katika sanaa za: uchoraji wa hati za Qur'an, nakshi, utengenezaji wa mijalada ya ngozi zenye nakshi za kuvutia, fasihi pamoja na uchongaji na urembaji wa majengo ya nyumba. Kwa vile uchapaji wa Qur'an huambatana na fani ya sanaa ya uandishi na uchoraji, jambo hili limepelekea kukua na kunawiri vyema kwa fani hiyo ni miongoni mwa Waislamu wengi duniani. [91] Jambo hilo pia limepelekea Qur'an kuandikwa katika maandishi tofauti, kama vile: Maandisho ya mtindo wa hati za Naskh, hati za Kufi, hati za Thulth, hati za Shekaste na hati za Nastaliq. [92] Aya Qur'an pia zimetumika sana katika fasihi ya Kiajemi na Kiarabu. Qur'an imekuwa na nafasi maalumu katika kila sanaa ya lugha, katika nathari, katika mashairi ya Kiajemi na Kiarabu, misemo na mada nyingine tofauti. [93]

Sanaa ya usanifu katika fani ya ujenzi wa Kiislamu imefinyangwa zaidi kwa mfinyango wa Aya za Qur'an kuliko kitu chochote ndani ya sanaa za na tamaduni za Kiislamu. Katika majengo mengi ya kihistoria ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na misikiti na majumba, utakuta yamesarifiwa kwa mapambo ya Aya za Qur'an. Pia, baadhi ya dhamira za Qur'an, kama vile maelezo ya Qur'an kuhusu Pepo na Moto, zimetumika katika usanifu wa majengo hayo. [94] Ibara za Qur'an zinazopatikana katika jengo la msikiti maarufu wa "قبة الصخرة" lililoko Jerusalem, zinahisabiwa kuwa ni mojawapo ya matumizi ya kuvutia zaidi ya Aya za Qur'an katika majengo yaliyojengwa katika nchi mbali mbali. Katika nakshi na maandishi ya jengo hili, lilijengwa mnamo mwaka 71 hijiria sawa na mwaka 691 Miladia, zinadhihirika wazi Aya kuhusu imani kuu za Uislamu, baadhi sehemu za Aya za Surat an-Nisa, al-Imran pamoja na Surat Maryam. [95]

Nafasi ya Qur'an juu ya kudumu kwa lugha fasaha ya Kiarabu

Inasemekana kuwa; Lugha ya Qur'an ilikuwa ni lugha fasaha na bora zaidi kuliko lugha ya Kiarabu na fasihi ya zama za kuteremka kwake. Miongoni mambo ya msingi yaliyoiimarisha na kuilinda lugha ya Kiarabu, ni: Muujiza wa Qur'an uliopo katika maneno yake, uandishi wa Qur'an na baadae kukua kwa hati na uwekaji wa irabu kwenye Qur'an, tafsiri (kama vile istilahi na kumbukumbu na ithibati kupitia mashairi ya zama za Ujahilia), uandishi wa sheria za lugha na sarufi ya lugha Kiarabu (kwa ajili ya kuilinda Qur'an dhidi ya kupotoshwa na kuepusha usomaji usio sahihi), sayansi (elimu) za Qur'an, kuenea kwa Uislamu katika nchi nyingine na kadhalika.

Yote hayo kwa jumla ni miongoni mwa mambo yaliyopelekea lugha hii kuhifadhiwa na kuwa ni lugha ya kilimwengu. Hivyo basi kuna wanaosema ya kwamba, kama si Qur'an, basi lugha fasaha ya Kiarabu, kama ilivyokuwa lugha ya Kilatini na Sanskrit, ingelikuwa ni lugha mfu na ya kale isiyo na uhai wowote. [96]

Mtazamo wa watafiti wa Mashariki (Mustashriqina)

Wataalamu wasiokuwa Waislamu wamefanya tafiti nyingi kuhusiana na fasihi, dhana na uhakika kuhusu ukweli juu ya ufunuo (wahyi) wa Qur'an. Baadhi ya Wanamashariki (watafiti wa Mashariki) wanaichukulia Qur'an kuwa ni maneno ya Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) na wamesema: maudhui na dhana zake zimetoholewa kutoka katika vyanzo vya Kiyahudi, Kikristo na mashairi ya zama za Jahilia. Ingawaje wengine hawajaichukulia Qur'an kuwa inatokana na chanzo cha wahyi, ila waisifu kwa kusema kuwa, iabara na maneno yake yapo juu zaidi ya ibara na maneno ya kibinadamu. [97]

Richard Bell [Maelezo 4] amesema: Mtindo wa kifasihi wa Qur'an, ambamo ndani yake kuna marudio mengi ya tashibiha na vibwagizo, umeathiriwa kutoka katika maandiko ya Kiyahudi na Kikristo na dini ya Kihanifa (dini iyendayo na matakwa ya maumbile ya mwanadamu). Kwa upande mwingine, Noldeke amezihisabu Sura za Qur'an, hasa Surah zilizoteremshwa Makka, kuwa ni Sura zenye miujiza wa kifasihi. Yeye amezilinganisha Aya za Qur'an na sauti ya naghama za malaika wanaotumbuiza roho za waumini. Mtaalamu wa mambo ya mashariki wa Ufaransa Maurice Bocay ameumulika muujiza wa kisayansi wa Qur'an, kisha akaandika kwa kusema: Baadhi ya Aya za Qur'an zinaendana sawa na kukubaliana moja kwa moja na uvumbuzi mpya wa kisayansi. Yeye Amehitimisha ya kwamba, Qur'an inatokana na chanzo cha Kiungu. [98]

Masuala yanayofungamana

Taurati


Vyanzo

  • Abbāsī, Mihrdād. "Tafsir." In Dānishnāma-yi jahān-i Islām, volume 7. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Islāmī, 1382 Sh.
  • "Ādāb-i khatm-i Qurʾān dar māh-i Ramaḍān". Gulistān-i Qurʾān 91, 1380 Sh.
  • Ādharnūsh, Ādhartāsh. "Tarjuma-yi Qurʾān bi Fārsī." In Dānishnāma-yi jahān-i Islām, volume 7. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Islāmī, 1382 Sh.
  • Group of authors. "Āya-yi basmala". In Farhangnāma-yi ʿUlūm-i Qurʾānī. Qom: Daftar-i Tablīghāt-i Islāmī, 1394 Sh.
  • Grabar, Oleg, "Art and Architecture and the Qurʾān." In Encyclopaedia of the Qurʾān. Edited by Jane Dammen McAuliffe, Georgetown University, Washington DC, [n.d].
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa ilā taḥṣīl masāʾil al-sharīʿa. Edited by ʿAbd al-Raḥīm Rabbānī Shīrāzī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1412 AH.
  • Iskandarlū, Muḥammad Jawād. ʿUlūm-i Qurʾānī. Qom: Sazmān-i Ḥuwza-hā wa Madāris-i ʿIlmīyya-yi Khārij az Kishwār, 1379 Sh.
  • Jabbārī Rād, Ḥamīd. "Nūrnigārān-i muʿāsir." Bishārat 58 (1386 Sh).
  • Khurramshāhī, Bahāʾ al-Dīn. "Qurʾān-i majīd". In Dānishnāma-yi Qurʾān wa Qurʾān pazhūhī, volume 2. Tehran: Dūstān-Nāhīd, 1377 Sh.
  • Khoei, Abū l-Qāsim al-. Al-Bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Muʾassisat Iḥyāʾ Āthār al-Imām al-Khoei, 1430 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Maʿmūrī, ʿAlī. "Taḥaddī." In Dāʾirat al-maʿārif-i buzurg-i Islāmī, volume 14. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Buzurg-i Islāmī, 1385 Sh.
  • Maʿrifat, Muḥammad Hādī. Al-Tafsīr wa l-mufassirūn fī thawbih al-qashīb. Mashhad: Dānishgāh-i ʿUlūm-i Islāmī-yi Raḍawī, 1418 AH.
  • Maʿrifat, Muḥammad Hādī. Al-Tamhīd fī ʿulūm al-Qurʾān. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1412 AH.
  • Maʿrifat, Muḥammad Hādī. "Pīshīna-yi chāp-i Qurʾān-i karīm". On Dānishnāma-yi Muwzūʿī-yi Qurʾān (4 May 2019)
  • Maḥmūdzāda, Mihrdād. "Hunar-i khat wa tadhhīb Qurʾānī." Kitāb-i māh-i hunar 3 (1377 Sh).
  • "Marāsim-i Qurʾān bi sar giriftan". Pāygāh-i Ittilaʿ Risānī-yi Hawza (4 May 2019)
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1374 Sh.
  • Miṣbāḥ Yazdī, Muḥammad Taqī. Qurʾān shināsī. Qom: Muʾassisa-yi Imām Khomeinī, 1389 Sh.
  • Mīr Muḥammadī Zarandī, Sayyid Abū l-Faḍl. Tarīkh wa ʿulūm-i Qurʾān. Qom: Daftar Intishārāt-i Islāmī, 1363 Sh.
  • Motahhari, Morteza. Majmūʿa-yi āthār. Tehran: Ṣadrā, 1389 Sh.
  • Muḥammadī Riyshahrī, Muḥammad et. al. Shinākhtnāma-yi Qurʾān bar pāya-yi Qurʾān wa ḥadīth. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1391 Sh.
  • Mujtahid Shabistarī, Muḥammad. "Āya." In Dāʾirat al-maʿārif-i buzurg-i Islāmī, volume 2. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Buzurg-i Islāmī, 1370 Sh.
  • Musawī Āmulī. "Qurʾān dar rusūm-i Irānī." Bisharat 51 (1384 Sh).
  • Mustafīd, Hamīd Riḍā. "Juzʾ." In Dānishnāma-yi jahān-i Islām, volume 10. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Islāmī, 1385 Sh.
  • Nāṣiḥīyān, ʿAlī Aṣghar. ʿUlūm-i Qurʾānī dar maktab-i Ahl-i Bayt. Mashhad: Danishgāh-i Ulūm-i Islāmī-yi Raḍawī, 1389 Sh.
  • Raḥmatī, Muḥammad Kāẓim. "Tarjuma-yi Qurʾān bi zabānhā-yi dīgar." In Dānishnāma-yi jahān-i Islām, volume 7. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Islāmī, 1382 Sh.
  • Rāmyār, Maḥmūd. Tārīkh-i Qurʾān. Tehran: Amīr Kabīr. 1369 Sh.
  • Rāstgū, Sayyid Muḥammad. "Tajallī-yi Qurʾān dar adab-i Fārsī." Bishārat 30 (1381 Sh).
  • Suyūṭī, Jalāl al-Dīn al-. Al-Itqān fī ʿulūm al-Qurʾān. Qom: al-Raḍī-Bīdār-Azīzī, 1363 Sh.
  • Yūsufī Gharawī, Muḥammad Hādī. ʿUlūm-i Qurʾānī. Qom: Daftar-i Nashr-i Maʿarif, 1393 Sh.