Mwaka wa Pili Hijria
Mandhari
Mwaka wa pili Hijiria (Kiarabu: سنة الثانیة للهجرة) ni mwaka wa pili katika kuhesabu miaka kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu ya Hijiria. Siku ya kwanza ya mwaka huu ilianza tarehe Mosi Muharram iliyosadifiana na Jumanne 16 Tir mwaka wa Pili Hijiria Shamsia ambayo ni sawa na tarehe 8 Julai 623 Miladia, na Siku yake ya mwisho yaani tarehe 30 Dhul-Hijja ilisadifiana na Jumamosi tarehe 5 Tir mwakak wa tatu Hijria Shamsia iliyokuwa mwafaka na tarehe 26 Juni mwaka 624 Miladia. [1]
Ushindi wa Waislamu katika vita vya Badr, kubadilishwa kibla cha Waislamu kutoka Masjid al-Aqswa na kuwa Kaaba na kufunga ndoa Imamu Ali (a.s) na Bibi Fatima Zahra (a.s) ni miongoni mwa matukio ya mwaka huu (pili Hijiria).
Matukio
- Kubadilishwa kibla cha Waislamu kutoka Masjid al-Aqswa na kuwa Kaaba tarehe 15 Rajab [2] au 15 Shaaban. [3]
- Mwanzo wa kuwa wajibu Saumu (28 Shaaban). [4]
- Kufunga ndoa Imamu Ali (a.s) na Bibi Fatima Zahra (a.s). (1 Dhul-Hijja). [5]
- Kupatiwa Imamu Ali (a.s) lakabu ya Abu Turab na Mtume wa M.Mungu (s.a.w.w). [6]
- Kusilimu Khuzaymah bin Thabit, mmoja wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) na masahaba wa Imamu Ali (a.s). [7]
Matukio ya Kivita
- Vita vya Abwa, vita vya kwanza vya Mtume (s.a.w.w) ambavyo vilifikia tamati bila mapigano kwa kutiwa saini mkataba wa amani na kabila la Dhamra. [8]
- Sariyya ya Abdallah bin Jahsh (Sariyya al-Nakhla): Shambulio la Waislamu bila ya idhini ya Mtume (s.a.w.w) dhidi ya msafara wa kibiashara wa Washirikina wa Makka. [9]
- Ushindi wa Waislamu dhidi ya Washirikina wa Makka katika vita vya Badr. (17 Ramadhan) [11]
- Sariyya Banu Qaynuqa: Vita vya kwanza vya Mtume (s.a.w.w) na Mayahudi wa Madina. [15 Shawwal). [12]
- Sariyya ya 'Ubayda bin Harith bin Abd al-Muttalib kwa ajili ya kukabiliana na washirikina ambao ilikuwa kuna uwezekano wakashambulia viunga vya mji wa Madina. [13] Tabari amelitambua tukio hilo kuwa lilitokea mwaka wa kwanza Hijiria. [14]
- Vita vya Sawiq kwa ajili ya kuwafuatilia na kuwasaka washirikina ambao baada ya Vita vya Badr walishambulia viunga vya Madina kwa ajili ya kulipiza kisasi. (4 Dhul-Hijja). [15]
Mazazi na Vifo
- Kuzaliwa Amr bin Hurayth Makhzumi, mmoja wa maafisa wa utawala wa Bani Umayya Kufa. [16]
- Kuaga dunia Ruqayya binti ya Mtume (s.a.w.w). (17 Ramadhan). [17]
- Kuaga dunia Othman bin Madh'un, sahaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w). [18]
- Kufariki dunia Abu Lahab (24 Ramadhan) mmoja wa maadui wakubwa wa Uislamu. [19]
- Kuaga dunia Talib bin Abi Talib kaka wa Imamu Ali (a.s). [20]