Siku ya kimataifa ya Quds

Kutoka wikishia

Siku ya Quds au Siku ya Kimataifa ya Quds ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran tarehe 7 Agosti 1979 alitangaza rasmi Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds na siku ya kufanya maandamano kutangaza himaya na uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Katika ujumbe wake wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa "Siku ya Kimataifa ya Quds", Imam Khomeini aliwataka Waislamu na wapenda haki kote ulimwenguni kujitokeza kila mwaka katika siku hii kwa ajili ya kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kuungana kwa ajili ya kukata mikono ya utawala haramu wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina huku ukitenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi hao madhulumu. Kutangazwa siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds kulipokewa kwa mikono miwili na uungaji mkono kutoka kwa wanafikra na shakhsia mbalimbali. Hii leo mbali na nchini Iran, wananchi wa mataifa mbalimbali ulimwenguni hufanya maandamano na makongamano katika Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za duru za habari, maadhimisho haya yanafanyika katika nchi 80 katika mabara mbalimbali duniani.

Historia ya Siku ya Quds na Umuhimu Wake

Siku ya Quds au siku ya kimataifa ya Quds ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran tarehe 7 Agosti 1979 alitangaza rasmi Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kuwa, siku ya kimataifa ya Quds na siku ya kufanya maandamano kutangaza himaya na uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Katika ujumbe wake wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa "Siku ya Kimataifa ya Quds", Imam Khomeini aliwataka Waislamu na wapenda haki kote ulimwenguni kujitokeza kila mwaka katika siku hii kwa ajili ya kutangaza himaya na uungaji mkono kwa wananchi wa Palestina na kuungana kwa ajili ya kukata mikono ya utawala haramu wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina huku ukitenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi hao madhulumu. [1] Ujumbe huo ulitolewa kama radiamali na jibu la hujuma na mashambulio ya vikosi vya utawala vamizi wa Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na vilevile mashambulio ya mabomu dhidi ya eneo la kusini mwa Lebanon. [2] Baada ya maandamano ya kwanza ya siku ya Kimataifa ya Quds mjini Tehran yaliyofanyika mwaka 1979, balozi wa Palestina nchini Iran alisoma risala ya Yassir Arafat. Vilevile Mahdi Bazargani, Waziri Mkuu wa muda wa wakati huo wa Iran, Abdul-Halim Khaddam, Waziri wa Mashauuri ya Kigeni wa Syria, Sayyid Ali Khamenei na Muhammad Mojtahed Shabestari walihutubia katika maadhimisho hayo. [3] Kabla ya kufanyika kumbukumbu ya Siku ya Quds, shakhsia 25 wakiwemo waandishi na wanafikra walitangaza katika taarifa yao kwamba, watashiriki katika maandamano ya siku ya Quds na kuwa pamoja na wanamapambano wote katika njia ya uhuru na demokrasia. [4]

Siku ya Kimataifa ya Quds ina nafasi maalumu katika hotuba za viongozi wa Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran, Imam Ruhullah Khomeini, Sayyid Ali Khamenei, Marajii Taqlidi wa Kishia na Sayyid Hassan Nasrullah, katibu mkuu wa harakati ya mapambano ya kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Imam Khomeini ameitambua Siku ya Quds kwamba, sio siku ya Palestina tu, bali ni siku ya Uislamu na siku ya utawala wa kiislamu. [5] na kwamba, huo ni utangulizi wa uhamasishaji wa kiislamu kwa ajili ya kuunda chama cha wastadhaafu (wanyonge) dunia nzima. [6] Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran anaamini kwamba, kuadhimisha siku ya kimataifa ya Quds kunawafanya wapalestina wanaoshambuliwa na utawala wa Israel kutojihisi wako peke yao na hivyo kuweza kusimama kidete. [7]

Sheikh Nasser Makarem Shirazi mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia analitambua suala la kushiriki katika maandamano ya siku ya Quds kuwa ni wajibu wa kisheria. Kwa mujibu wa fatuwa yake: kama mume hatompa idhini mkewe ya kushiriki katika maandamano ya siku ya Quds, mwanamke huyo anaweza kutoka bila idhini ya mumewe na kwenda kushiriki katika maandamano ya siku ya Quds. [8] Anaamini kwamba, siku ya Quds inapaswa kubadilishwa na kuwa malalamiko na upinzani mkubwa, wa wote na wa pamoja dhidi ya maghasibu na wavamizi. [9] Sayyid Hassan Nasrullah, katibu mkuu wa harakati ya mapambano ya kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon anaamini kwamba, Israel sio hatari tu kwa Palestina, bali ni tishio pia dhidi ya usalama, amani na mamlaka ya kujitawala ya mataifa yote ya Mashariki ya kati. [10]

Maadhimisho ya Siku ya Quds

Maandamano ya siku ya Quds hufanyika katika mataifa mbalimbali duniani katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo Malaysia, India, Singapore, Indonesia, Marekani, Canada, Norway, Azerbaijan, Uturuki, Sudan, Uingereza, Bahrain, Bosnia Herzegovina, Tunisia, Pakistan, Australia, Ujerumani, Nigeria, Romania, Kuwait, Uhispania, Afrika Kusini, Sweden, Kenya, Venezuela, Lebanon, Tanzania, Iran, Albania, Iraq, Yemen, Ugiriki na kadhalika. [11] Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za duru za habari, maadhimisho haya yanafanyika katika nchi 80 katika mabara mbalimbali duniani, katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. [12] Maandamano ya siku ya kimataifa ya Quds ambayo hufanyika katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani [13] na kuakisiwa na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni [14], katika mataifa ya Magharibi kutokana na kuwa siku ya Ijumaa ni siku ya kazi, kumbukumbu hiyo badala yake hufanyika katika siku za mapumziko za Jumamosi au Jumapili. ]15] Hata hivyo, maandamano hayo katika baadhi ya nchi hufanyika chini ya mbinyo na vikwazo vya serikali husika. [16]