Usiku wa Mwezi 21 Ramadhani

Kutoka wikishia

Usiku wa Ishirini na Moja wa Ramadhani (Kiarabu: الليلة الحادية والعشرون من رمضان) ni usiku wa kifo cha Imamu Ali (a.s) na ni kati ya matukio muhimu katika kalenda ya Shia.

Kulingana na ripoti za kihistoria ni kwamba; Imamu Ali (a.s) alipigwa upanga na Ibnu Muljim Muradi usiku wa kumi na tisa wa Ramadhani, na kutokana na kipigo hicho alifariki dunia usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani.[1] Hii ndiyo sababu iliopelekea Mashia kuomboleza ndani ya usiku huu.[2]

Katika maeneo fulani ya Iran, mnamo usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani, hufanyika tamasha la maombolezi liitwalo Tamasha la Qanbar na Imam Ali (a.s)[3]

Kulingana na Hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya Shia ni kwamba; Usiku wa mwezi ishirini na moja pamoja na usiku wa kumi na tisa na ishirini na tatu wa Ramadhani, ni miongoni mwa nyusiku zinaoweza kuwa ni Usiku wa Kadri (Lailatulqadri).[4] Kwa hiyo, Mashia huadhimisha usiku huu kwa kukesha na kufanya ibada maalumu za Usiku wa Kadri hali wakiwa majumbani mwao, misikitini, kwenye Husseiniyya na maeneo mengine ya kidini.[5] Sheikh Abbas Qomi katika kitabu chake cha Mafatih al-Jinan ameandika akisema kuwa; Fadhila za usiku wa ishirini na moja ni kubwa zaidi kuliko usiku wa kumi na tisa wa Ramadhani. Baadhi ya ibada zilizopendekezwa katika usiku huu ni pamoja na:

  1. Kukesha
  2. Kukoga josho kwa ajili ya Usiku wa Kadri
  3. Kusoma Sala ya Usiku wa Kadri
  4. Kusali Sala ya rakaa mia moja
  5. Kuweka Qur’ani juu ya kichwa
  6. Kutawasali kwa Ma’sum kumi na nne.[6]

Baadhi ya Mashia hutoa nadhiri, futari na chakula cha daku katika usiku wa ishirini na moja wa Ramadhani.[7] Katika mkoa wa Lorestan nchini Iran, huwa kua aina maalum ya nadhiri inayo tayarishwa katika usiku huu, inayojulikana kwa jina la Halwa ya Ishirini na Moja.[8]

Mada Zinazo Husiana

Rejea

  1. Mufid, Al-Irshad, 1413 AH, juz. 1, uk. 9.
  2. Majidi Khamene, «Shab-haye Qadr Dar Iran», uk. 19.
  3. Majidi Khamene, «Shab-haye Qadr Dar Iran», uk. 20.
  4. Majlisi, Mir-at al-Uqul, 1404 AH, juz. 16, uk. 381.
  5. Majidi Khamene, «Shab-haye Qadr Dar Iran», uk. 20.
  6. Qomi, Mufatihu al-Janan, Amal Shab Qadr Dar Iran, Amal Makhusus Shab Bisto Yek.
  7. Majidi Khamene, «Shab-haye Qadr Dar Iran», uk. 20.
  8. «Aiyanhaye Ramadhan Dar Istanhaye- 36 Rusum Shab Shahadat Imam Ali; Buye Haluwi 21 Ramadhan Khanehaye Ra Muatar Mikonad», Khabargozari Mehr.

Vyanzo