Nenda kwa yaliyomo

Saumu ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani

Kutoka wikishia

Saumu ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani: ni zoezi la kufunga siku moja au zaidi kabla ya kuingia kwa mwezi wa Ramadhani. [1] Ingawa istilahi hii haihisabiwi kuwa ni miongoni mwa istilahi zenye nafasi katika vyanzo vya kifiqhi, ila ni istilahi mashuhuri iliozoeleka kijamii na kiutamaduni. Istilahi hii inahusishwa na saumu zinazofungwa katika siku za mwisho za mwezi wa Shaaban kama maandalizi ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani. [2] Kulingana na moja ya Riwaya kutoka kwa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s), ni kwamba; “Thawabu za kufunga ya siku tatu za mwisho za mwezi wa Shaaban ni sawa na thawabu za kufunga miezi miwili mfululizo”. [3] Vile vile, kwa mujibu wa Hadithi ya Imamu Ali al-Ridha (a.s) ni kwamba; kufunga siku ya mwisho ya Shaaban ni amali inayompelekea mja kupata maghfira ya dhambi kutoka kwa Mola wake. [4] Pia katika vyanzo vya Hadithi vya upande wa madhehebu ya Kisunni, kuna Hadithi zisemazo kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) aliitaja funga ya mwezi wa Shaaban kama moja ya saumu zenye thamani zaidi mingoni mwa funga mbali mbali, na akaeleze kwamba, funga hii ni alama ya kuuheshimu mwezi wa Ramadhani. [5] Kulingana na Hadithi hizo, imethibiti kuwa; hata yeye alikuwa alikuwa na kawaida ya kufunga saumu hiyo ya mwezi wa Shaaban na kuiunganisha moja kwa moja na mwezi wa Ramadhani. [6] Hata hivyo, wanazuoni wa madhehebu ya Kisunni, kwa kutegemea baadhi ya riwaya, hawaruhusu siku moja au mbili za mwisho wa mwezi wa Shaabani, kwani kwa mtazamo wa Kisunni, ni haramu kufunga siku ya Yaumu Al-Shakk, [7] ila si haramu kwa yule aliyeanza kufungu siku za nyuma yake hadi kumaliza mwezi mzima wa Shaabani. Pia si tatizo kwa yule mwenye kawaida ya kufunga siku moja na kuacha siku ya pili kwa muda wa mwaka mzima, hata kama funga yake itaangukia ndani ya mwezi 28 au 29 Shaabani. [9] Sayyid Ibn Tawus anaamini kwamba; umarufuku huu unawahusu wale waliokamilisha saumu ya Shaabani mzima. Kwa umarufu huu umekuja kuwata wale angalau siku moja au mbili ili wapate nafasi ya kupumzika na kuimarika kimwili kabla ya kuingia mwezi wa Ramadhani. [10] Mada Zinazohusiana • Saumu ya Kuunganisha • Saumu ya Kukaa Kimya