Kafara ya swaumu

Kutoka wikishia

Kafara ya funga (Kiarabu: كفارة الصوم) ni adhabu ambayo huwekwa kutokana na kubatilisha na kuharibu funga ya mwezi wa Ramadhan, funga ya nadhiri ya muda maalumu, na pia kadhwaa au malipo ya funga ya mwezi wa Ramadhan ikiwa itaharibiwa na kubatilishwa baada ya adhana ya adhuhuri, funga ambayo ilikuwa ni wajibu kwa mukallaf. Kafara ya kuharibu na kufungua kwa makusudi kila funga ni kama ifuatavyo, kufunga ya miezi miwili ambapo ni lazima kufunga siku 31 mfululizo au kumlisha fukara na asie jiweza.

Kafara ya funga huwa ni wajibu katika sura ambayo mfungaji atafahamu ya kuwa anacho fanya ni miongoni mwa vitu vinavyobatilisha na kuharibu funga. Vivyo hivyo kwa mujibu wa fat'wa za baadhi ya wanazuoni na mafakihi ni kwamba kutenda na kutekeleza moja wapo kati ya vibatilisho vya funga kwa makusudi ni sababu ya kuwajibika kwa kafara. Mkabala wa hawa mafakihi, kuna mafakihi wengine wanaitakidi kwamba kubatilisha funga kwa makusudi haimaanishi kuwa kafara inakuwa ni wajibu na lazima.

Kwa mujibu wa mtazamo na itikadi ya wanazuoni wa Kishia ni kwamba, ikiwa mukallaf ataiharibu na kuibatilisha funga kwa kufanya tendo la haramu kama vile kunywa kilevi au kuzini na akaibatilisha funga kwa matendo haya, ni lazima kutoa kafara ya kukusanya (kwa maana ya kufunga miezi miwili mfululizo na kuwalisha mafakiri) pamoja na hali hii baadhi ya mafakihi wanasema kuwa kulipa kafara ya kukusanya katika sura hii ni ihtiyat ya mustahabu na wengine wamesema kuwa ni ihtiyat ya wajibu.

Utambuzi wa Maana ya Maneno

Kafara ni adhabu ya kimali au pesa au kimwili adhabu ambayo hutekelezwa pale yanapofanyika baadhi ya madhambi, na ni adhabu apewayo mukallaf kwa tendo hilo.[1] na mara nyingi kafara hupelekea kupunguzwa au kutoweka na kuanguka kwa malipo ya adhabu ya Akhera au kosa na dhambi ile.[2]

Wanazuoni wa fiqh wanaamini na kuitakidi kwamba kafara inaambatana na kufungamana na ubatilishaji na kuharibu baadhi ya aina za funga kama vile:

Aina za Kafara ya Funga

Kauli mashuhuri kati ya wanazuoni na mafakihi wa kishia ni kuwa kafara ya funga ni moja wapo kati ya sehemu hizi tatu zifuatazo:

 • Funga ya miezi miwili mfululizo funga ambayo ni lazima kufunga siku 31 mfululizo.[4]
 • Kumlisha fakiri.
 • Kumuachia mtumwa huru.[5] (lakini kumuachia mtumwa huru hivi leo ni hukumu isiyokuwa na maudhui yaani maudhui yake hayapatikani tena hivyo basi hukumu hiyo inatoka na kuondolewa.[6]

Athari ya Kufahamu na Kutofahamu Katika Hukumu ya Kafara ya Funga

Kwa mujibu wa mtizamo wa wanazuoni na mafakihi, ikiwa mukallaf atabatilisha na kuharibu funga yake kwa makusudi na bila sababu ya kisheria, pamoja na kuwa ni wajibu kwake kulipa funga hiyo pia ni wajibu kutoa kafara.[7] Pamoja na haya ni kuwa katika kuwajibiki kwa kafara ni sharti kwamba mtu awe ni mwenye kufahamu ya kwamba jambo alitekelezalo ni miongoni mwa mambo yanayobatilisha funga.[8]

Kutokana na haya, hukumu ya kafara haimjumuishi wala kumuhusu jahil al-Qaaswir (mjinga asiye wa kujitakia)[9] na jahil al-Muqaswir(mjinga wa kujitakia.[10] Japo kuwa baadhi wanaitakidi kuwa Jahil al-Muqaswir hukumu yake ni sawa na mtu mwenye kufahamu na kutambua vitu vinavyo batilisha, hivyo basi pamoja na kutakiwa kulipa funga, pia analazimika kutoa kafara.[11]

Vibatilishi vya Funga Ambavyo Vinawajibisha Kafara

Swahibul-jawaahir anaitakidi kwamba kwa mujibu wa riwaya mbalimbali ni kuwa kufanya kwa makusudi moja wapo kati ya vibatilishi vya funga pamoja na kadhwaa ya funga ni sababu ya kutoa kafara.[12] Sayyid Abul-qaasim Khui anaamini na kuitakidi kwamba kila kitu ambacho kina batilisha na kuharibu funga kwa kukifanya kama vile kumzulia uongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake au kujitapisha makusudi, kufanya mambo hayo kwa makusudi hupelekea kafara kuwa wajibu.[13]

Mkabala wake, wanazuoni wengine wanaitakidi kwamba kubatilisha funga kwa makusudi haina ulazima wa kuwa kafara ni wajibu.[14] kwa mujibu wa fat'wa ya Imamu Khomeini ni kwamba ikiwa mukalaaf atapatwa na janaba usiku, kisha akaamka mara tatu na hakufanya ghusli na josho la janaba kisha akalala hadi adhana ya asubuhi na asiamke, atakacho takiwa kufanya ni kulipa funga hiyo na hana wajibu wa kutoa kafara, na mukallaf ambae atajitapisha kwa makusudi akiwa amefunga pia hukumu yake ni kama hii.[15]

Tofauti ya Kafara Funga Ikibatilishwa kwa Jambo la Haramu au Halali

Mafakihi kadhaa wanaitakidi kwamba ikiwa mtu ataharibu na kubatilisha funga yake kwa kufanya jambo la halali kama vile kula na kunywa, hapana budi pamoja na kutakiwa kulipa funga hiyo, ni wajibu kutekeleza moja kati ya aina za kafara zilizo tajwa.[16] Ama ikiwa ataiharibu funga kwa kufanya tendo la haramu kama vile kuzini au kunywa kileo. Hapana budi kutekeleza kafara zote tatu na hiyo ndio iitwayo Kafaaratul-jam'i[17] lakini baadhi ya maraajiu wanaamini na kuitakidi kuwa kafara ya kukusanya ni ihtiyat mustahabu[18] na baadhi wanasema kuwa ni ihtiyat ya wajibu.[19]

Tofauti Kati ya Kafara ya Funga na Fidia

Wakati mwingine katika mazungumzo ya watu ya kawaida hutumika neno kafara kwa maana ya fidia, kama mfano kibaba kimoja ambacho ni sawa na (gram 750 ya ngano na mfano wa ngano) huitwa kwa jina la Kafara ya funga,[20] wakati ambapo fidia ni badala ya funga, na hutolewa badala ya funga kwa sababu ya kutoweza na kushindwa kufunga kutokana na ugonjwa na mfano wa hayo, na kuchelewesha kadhwaa au malipo ya funga ya mwezi wa ramadhan (kafara ya kuchelewesha).[21]

Rejea

 1. Tazama: kitabu cha Mishkini, Mustwalahaatul- fiqhiyah, 1419 H, uk. 465.
 2. Mishkiniy, Mustwalahaatu fiqhiyah, 1419 H, uk. 465.
 3. Khui, Minhaajus-swalihiin, 1410 H, juz. 1, uk. 269.
 4. Imamu Khomeini, Tawdhiihul-masaail, 1426 H, uk. 347.
 5. Swadouq, Majmuuatul-fataawa ibni Baabawaihi, Qom, uk. 73.
 6. Makaarim, Risaalatu- tawdhiihil-masaail, 1429 H, uk. 253.
 7. Imamu Khomeini, Istifta'aat, 1422 H, juz. 1, uk. 330.
 8. Rouhaani, Minhajus-swalihiin, juz. 1, uk. 355.
 9. Khui, Minhaajus-swalihiin, juz. 1, uk. 270.
 10. Khui, Minhaajus-swalihiin, juz. 1, uk. 270. Sistaani, Minhaajus-swalihiin, 1417 H, juz. 1, uk. 327.
 11. Rouhaani, Minhajus-swalihiin, juz. 1, uk. 355.
 12. Khui, Minhaajus-swalihiin, juz. 1, uk. 270; Sistaani, Minhaajus-swalihiin, 1417 H, juz. 1, uk. 327.
 13. Najafi, Jawaahirul-kalaam, 1404 H, juz. 16, uk. 226.
 14. Tazama kitabu cha: Twabatwabai Yazdi, Al-ur'watul-wuthqaa, 1428 H, juz. 2, uk. 38.
 15. Imamu Khomeini, Tawdhiihul-masaail, 1426 H, uk. 346.
 16. Bahjat, Jaamiul-masaail, 1426 H, juz. 2, uk. 29.
 17. Bahjat, Jaamiul-masaail, 1426 H, juz. 2, uk. 29.
 18. Sistani, Tawdhiihul-masaail, 1393 S, uk. 298-299.
 19. Imamu Khomeini, Tawdhiihul-masaail, 1426 H, uk. 344.
 20. Tazama kitabu cha: Khomenei, Aj'wibatul-istifta'aat, 1420 H, juz. 1, uk. 138, no. 802.
 21. Swadru, Maa wara'al-fiqhi, 1420 H, juz. 9, uk. 120.

Vyanzo

 • Imamu Khomeini, Sayyied Rouhu llah, Istifta'aat, Qom, daftar Intishaaraat islaamiy, chapa ya tano, mwaka 1422 H.
 • Imamu Khomeini, Sayyied Rouhu llah, Tawdhiihul-masaail, kilicho hakikiwa na kusahihishwa na: Muslim qalipoor, giilaaniy, Qom, Muassaseye nadhmi wa nashri Aathar Imamu Khomeini, chapa ya kwanza, mwaka 1426 H.
 • Bahjat, Muhammad taqi, Jaamiul-masaail, Qom, Dafrat Aayatullahi Bahjat, chapa ya pili, mwaka 1426 H.
 • Khui, Sayyied Abul-qaasim, Minhaajus-swalihiin, Qom, Nashru madiinatil-ilmi, chapa ya ishirini na nane, mwaka 1410 H.
 • Khui, Sayyied Abul-qaasim, Mawsuuatul-imamil-khuiy, Qom, Muassasatu ihyaait-turaathil-imamil-khuiy, chapa ya kwanza, mwaka 1418 H.
 • Rouhaani, Sayyied Swaadiq, Minhaajus-swalihiin, Biijaa, bitaa.
 • Sistani, Sayyied Ali, Tawdhiihul-masaail, Mash'had, Daftar Ayatullah Sistaniy, mwaka 1393 S.
 • Sistani, Sayyied Ali, Tawdhiihul-masaail, Mash'had, Daftar Ayatullah Sistaniy, Qom, chapa ya tano, mwaka 1417 H.
 • Swadru, Sayyied Muhammd, Maa waraa'al-fiqhi, kilicho sahihshwa na Jaafar Haadiy Dujailiy, Bairut, Darul-adhwaa litwiba'aa wan-nashri wat-tawzii'il, mwaka 1420 H.
 • Swadouq, Ali bin Hussein, Majmuatul- fataawa ibnu Baabawaihi, kilicho kusanywa na: Abdur-rahiim Buruujerdi, kilicho hakikiwa na : Ali panaah ishtihardiy, Qom, Biitaa, chapa ya kwanza, Biitaa.