Magharibi ya kisheria
Magharibi ya kisheria (Kiarabu: الغروب) ni mwanzo wa kuswali Sala ya Magharibi ambapo katika baadhi ya milango ya fiq’h hili hujadiliwa na kuzungumziwa. Magharibi ya kisheria ina matumizi katika masuala kama kumalizika wakati wa Sala ya Alasiri, kuanza wakati wa Sala ya Magharibi, mwisho wa funga ya Saumu (wakati wa kufuturu) na vilevile na kusimama kwa hiari katika jangwa la Arafa. Kwa msingi huo, hili hujadiliwa katika milango mbalimbali ya fiq’h kama Sala, Saumu na Hija.[1]
Kuhusiana na wakati wa Magharibi ya kisheria, kuna hitilafu za kimitazamo baina ya mafakihi. Baadhi ya mafakihi (wanazuoni wa fiq’h) wanaitambua Magharibi ya kisheria kwamba, ni kuzama kwa jua,[2] lakini Sahib al-Jawahir anasema, mafakihi wengi wanaitambua Magharibi ya kisheria kwamba, ni kutoweka wekundu wa mbingu wa mashariki.[3] Katika mtazamo huu, kuzama kwa jua na Magharibi ya kisheria ni vitu viwili tofauti. Kuzama kwa jua ni mwisho wa wakati wa Sala ya Alasiri, lakini kutoweka wekundu wa mashariki ya mbingu ni wakati wa kufurutu na kuwa wajibu Sala ya Magharibi.[4]
Rejea
Vyanzo
- Bahjat Fumani, Muhammad Taqi, Istiftaat, Qom: Daftar Ayatullah Bahjat
- Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-kalam, Mhakiki: Ibrahim Sultani, Beirut: Dar Ihya al-Turath al-'Arabi, 1362 HS
- Tabatabai Yazdi, Sayyid Muhammad Kadhim, al-'Urwah al-Wuthqa, Usahihishaji: Sayyid Abdul Karim Musawi Ardabili, Qom: Muasasat al-Nashr Lijamiat al-Mufid Rahmatullah, 1431 HS
- Muasasat Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhange Fiqh Farsi, Qom: Muasasat Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami. 1385 S.