Tohara
Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine. |
- Tohara(الطهارة) ina tofauti na tat'hir(تطهیر / kutoharisha)
Tohara (Kiarabu: الطهارة) ni istilahi ya kifiqh ambayo ina maana ya hali ya kutokuwa na najisi. Kuwa msafi kutokana na najisi na vilevile kutokana na hadathi kubwa na hadathi ndogo. Makusudio ya hadathi ndogo ni kutokwa na vitu kama mkojo, kinyesi na kutokwa na upepo katika njia ya haja kubwa ambao unabatilisha udhu. Hadathi kubwa ni kama vile janaba na kukutana kimwili.
Kuwa na tohara na kutokuwa na najisi katika baadhi ya mambo kama udhu na swala ni jambo la lazima. Maji ambayo mtu anatumia kutilia udhu na vilevile mwili na vazi la mtu anayeswali yanapaswa kuwa na tohara yaani yasiwe na najisi. Najisi inaweza kuondolewa kwa kutumia kitu kama maji ambapo vinavyoondoa najisi kama maji vinajulikana kiistilahi kwa jina la Mutahhirat (vitu vinavyotoharisha).
Kuwa na tohara ya hadathi katika asili sio jambo la wajibu; lakini huwa wajibu pale mtu anapotaka kutekeleza faradhi za dini kama swala, tawafu ya wajibu na vilevile kugusa Aya za Qur'an Tukufu. Tohara ya hadathi ndogo inapatikana kupitia kutia udhu na tohara ya hadathi kubwa inapatikana kupitia ghusl (kuoga). Kama hakuna uwezekano wa kutia udhu na kuoga (kwa kutumia maji kutokana na sababu mbalimbali kama kukosekana maji, au maji kuwa na madhara), basi badala yake mtu anaweza kutayamamu (kwa kutumia udongo na vinginevyo vinavyotumiwa kutayamamu).
Maana ya Kifikihi ya Tohara
Katika fikihii makusudio ya tohara aghalabu ni hali ya kuwa na usafi na kutokuwa na najisi na vilevile kuwa msafi kutokana na hadathi kubwa na hadathi ndogo..[1] Makusudio ya hadathi ndogo ni kutokwa na vitu kama mkojo, kinyesi na kutokwa na upepo katika njia ya haja kubwa ambao unabatilisha udhu..[2] Makusudio ya hadathi kubwa ni kama vile janaba, kukutana kimwili na hedhi ambavyo ili mtu arejee katika hali ya kabla yaani ya kuwa na tohara anapaswa kuoga josho(kufanya ghusl)..[3]
Katika vitabu vya fikihi kuna mlango maalumu wa tohara ambapo ndani yake, kunajadiliwa aina za najisi, mutwahirat, udhu, ghusl (josho) na kutayamamu..[4]
Tohara Kunako Najisi
- Kadhalika angalia: Dhati ya Najisi na Mutahhirat
Katika hukumu na sheria za Kiislamu, kila kitu ni kisafi na tohara isipokuwa vitu kumi ambavyo ni najisi kama vile: Mkojo, kinyesi cha mwanadamu na mnyama ambaye nyama yake ni haramu, manii, damu ya mwanadamu na mnyama ambaye akichinjwa damu yake inaruka, nguruwe, mbwa, pombe na kadhalika..[5] Kitu chochote ambacho kitagusana navyo kitanajisika na kiistilahi kinajulikana kama mutanajjis (kichafu na kinachonajisi)..[6] Najisi inaweza kuondolewa kwa kutumia kitu kama maji ambavyo vinavyoondoa najisi na vinajulikana kiistilahi kwa jina la mutwahirat (vitu vinavyotoharisha)..[7]
Hukumu ya Tohara Kunako Najisi
Kwa mujibu wa Fat’wa za mafakihi ni kwamba, ni wajibu maeneo yafuatayo kuwa na tohara:
- Viungo vya mwili wakati wa kutia udhu.
- Maji ya udhu na ya kuogea (ghusl).
- Viungo vya kufanyia tayamamu endapo hilo litawezekana.
- Udongo na vitu ambavyo vinatumiwa kufanyia tayamamu.
- Mahali pa kusujudia.
- Vazi na mwili wa mtu anayeswali na anayefanya tawafu..[8]
Tohara ya Hadathi
Hadathi ni kitu ambacho kinasababisha kutenguka na kuondoka tohara..[9]Wanafikihi wamegawanya hadathi katika vigawanyo viwili, hadathi kubwa na hadathi ndogo..[10] Na mifano ya hadathi ndogo ni kama vile: Kutoka mkojo, kinyesi, upepo (kujamba), kulala usingizi, vitu ambavyo vinaondoa akili (kama vile, uwendawazimu, kulewa na kuzimia) na damu chache ya istihadha..[11]
Vigawanyo vya hadathi kubwa kubwa pia ni: Janaba, kukutana kimwili, damu ya nifasi, istihadha ya wastani na istihadha nyingi na kugusa maiti..[12]
Tohara ya hadathi ndogo inapatikana kupitia kutia udhu na tohara ya hadathi kubwa inapatikana kupitia ghusl (kuoga)..[13] Katika hali ya dharura (kama vile kukosekana maji au maji kuwa na madhara na mtu, badala ya kutia udhu na kufanya ghusli anaweza kutayamamu..[14]
Hukumu ya Tohara ya Hadathi
Tohara ya hadathi yenyewe kama yenyewe sio wajibu; lakini ni wajibu pale mtu anapotaka kufanya amali zifuatazo:
- Swala za wajibu, isipokuwa swala ya maiti.
- Tawafu (kuzunguka Kaaba) ya wajibu.
- Kugusa maandishi ya Qur'an.
- Kugusa majina matukufu ya Mwenyezi Mungu, Mtume na kwa mujibu wa fat'wa mashuhuri kugusa pia majina ya Ahlul-Bayt (a.s).
- Swaumu kwa mujibu wa fat'wa mashuhuri.
- Kusoma Azaim al-Sujud.
- Kubakia msikitini.
- Kuingia katika msikiti wa Makka Masjd al-Haram na Masjid al-Nabi hata bila ya kubakia humo.
.[15]
Katika mambo manne ya awali kutoharika kunako hadathi kubwa na ndogo ni wajibu kwa yote mawili; lakini katika mambo manne yaliyobakia, kutoharika na hadathi kubwa tu ndio wajibu..[16]
Tohara ya hadathi, yaani kutia udhu, kufanya ghusl na kutayamamu kunapaswa kufanywa kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu..[17]
Kuwa na tohara ni mustahabu katika masuala mengi ambapo baadhi ya hayo ni: Kuomba haja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kubeba Qur'an, swala ya maiti, kuzuru Makaburi, kusoma Qur'an na kuingia msikitini..[18]
Rejea
- ↑ Meshkini, Mustalahat al-Fiqh, 1392 S, uk. 379.
- ↑ Faiz al-Kashani, Rasail, 1429 AH, juz. 2, uk. 22.
- ↑ Faiz al-Kashani, Rasail, 1429 AH, juz. 2, uk. 22.
- ↑ Tazama: Khomeini, Tahrir al-Wasilah, 1392 S, juz. 1, uk. 11, 21, 38, 106, 119, 132; Najafi, Jawahar al-Kalam, 1404 AH, juz. 1, uk. 3, 8, 29, 55.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shara'iu al-Islam, 1408 AH, juz. 1, uk. 43-45; Najafi, Jawahir al-Kalam, 1404 AH, juz. 5, uk 273, 290, 294, 354, 366, juz. 6, uk. 2, 38, 41.
- ↑ Suruur, al-Muujam al-Shamil lil-mustwalahatil al-ilmiyya wa ad-diniyya, 1429 AH, juz. 1, uk. 229.
- ↑ Khomeini, Tahrir al-Wasila, 1392 S, juz. 1, uk. 132.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 5, uk. 239.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 3, uk. 246-248.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 3, uk. 246-248.
- ↑ Faiz al-Kashani, Rasail, 1429 AH, Juz. 2, Risale. 4, uk. 22.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shara'iu al-Islam, 1408 AH, juz. 1, uk. 9; Faiz al-Kashani, Rasail, 1429 AH, uk. 22.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shara'iu al-Islam, 1408 AH, juz. 1, uk. 9, 17.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shara'iu al-Islam, 1408 AH, juz. 1, uk. 38-39.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 5, uk. 237-238.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 5, uk. 237-238.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shar'iu al-Islam, 1408 AH, juz. 1, uk.12, 19, 40.
- ↑ Muasase dairatu al-maarif fiqh islami,1387 S, juz. 5, uk. 238.
Vyanzo
- Khomeini, Sayyied Ruhullah, Tahrir Al-Wasila, Tehran, Muasase tandhwim wa nashru athar Imam Khomeini, 1392 S.
- Suruur, Ebrahim Hussein, Al-Mujam al-Shamil lil-mustwalaat al-ilmiyya wa ad-diniyya, Beirut, Daru al-Hadi, 1429 AH.
- Faiz Kashani, MUhammad MUhsen, Rasail faidh al-Kashani, Tahqiq Behzad Jafari, Tehran,Madrase ali Shahid Motahari, 1429 AH.
- Muasase dairatul-maarif fiqh islami, Farhang fiqh mutwabiq ba madhhab ahlu-Bayt, Qom, Muasase dairatul-maarif fiqh islami bar madhhab ahlu-Bayt 1387 S.
- Muhaqiq Hilli, Jafar bin Hasan, Shara'iu al-Islam fi masail al-halal wal-haram, Tahqiq wa tas'hihu Abdul Hussein Muhammad Ali Baqal, Qom, Ismailiyan, chapa davomi, 1408 AH.
- Meshkini Ardabili, Ali, Mustawalahat al-Fiqh, Qom, Daru al-hadith, 1392 S.
- Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam fi Sharh Shaa'iu al-Islam, Tas'hih Abbas Quchani wa Ali Akhundi, Beirut, Daru ihiyai turath al-arabi, chapa haftom, 1404 AH.