Sisi ni taifa la Imamu Hussein
Sisi ni taifa la Imamu Hussein: Kauli mbiu maarufu isemayo “Sisi ni taifa la Imamu Hussein”, iliyooenekana kuenea nchini Iran mwezi wa Muharram wa mwaka 1442 Hijria, [1] ni sehemu ya maneno yaliyokopiwa kotoka katika pamoja ya mihadhara ya Qasim Suleimani. [2] Bwana Qasim Suleimani, alikuwa ni mmoja wa makamanda muhimu wa IRGC aliyekuwa akisimamia Kikosi cha Quds. [3] Suleimani alikuwa na nafasi muhimu katika vita vya Iran-Iraq, na baadaye akawa alama na nembo ya mapambano ya kieneo nchini Iran na hata ulimwenguni. [4] Mnamo Januari 2020, Seleimani aliuawa kupitia shambulio la ndege zisizo na rubani la Marekani akiwa nchini Iraq, tukio lililozua msisimko mkubwa wa kisiasa ulimwenguni. Kampeni hii ya kijamii ilizinduliwa na Shirika la Hifadhi na Uenezi wa Urithi wa Shahidi Haj Qasim Suleimani. [5] Katika harakati za wito huu, raia waliombwa kushiriki maombolezo ya Muharram kwa kutumia kauli hii mbiu isemayo “Sisi ni Taifa la Imamu Hussein”. Pia mwito huu ulionekana kupamba moto katika zama za kipindi cha COVID-19, ambapo watu walitakiwa kutoa msaada kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaoishi katika hali ngumu, hasa wale waliodhurika na gonjwa hayo sugu. [6] Kama sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kitaifa nchini Iran, kauli mbiu ya “Sisi ni Taifa la Imam Hussein” ilionekana kwenye mchoro mkubwa wa ukutani kwenye eneo la raoundabout) duara liitwalo Wali Asri, moja ya barabara zilizopo jijini Tehran. [7] Ili kuienzi kauli mbiu hii adhimu, wananchi wa miji mbali mbali nchini humo, huonekana kuichachua na kuikoleza rangi kauli hii kwa kutumia shughuli mbali mbali, kama vile: • Kujenga au kusimamisha vituo maalumu kwa ajili ya kugawa sadaka (vituo vya baraka — services tents) [8] • Kuandika au kuchapa kauli hiyo kwenye magari • Kusambaza na kugawa bendera zenye ujumbe huo [9] Gazeti la Keihan lilitoa makala maalumu ya kiuchambuzi kuhusiana na namna ya wananchi walivyoungana katika kuadhimisha huzuni ya Karbala kupitia kauli hiyo adhimu. [10]