Nenda kwa yaliyomo

Dua ya thelathini na tano ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya thelathini na tano ya Sahifa Sajjadiyya: ni miongoni mwa dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Nayo ni dua maalumu inayohusiana na umuhimu wa mwanadamu kuridhia majaaliwa na hukumu (maamuzi) ya Mwenye Ezi Mungu. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anamshukuru Mwenye Ezi Mungu kwa baraka alizompa pamoja na zile ambazo hakumpa (kutokana na hekima Yake maalumu). Pia Imamu Sajjad (a.s), anawakanya wanadamu wasiwe na wivu (husuda) juu ya kile walichojaaliwa waja wengine kutoka kwa Mola wao. Aidha, Imamu (a.s) anasisitiza akisema kuwa; utukufu na heshima ya kweli hupatikana katika njia ya kumwabudu Mwenye Ezi Mungu, na anaonya waja dhidi ya kuwadharau watu masikini, na kupigwa na butwaa mbele ya wenye nguvu na mamlaka. Dua hii ya thelathini na tano imefafanuliwa kwa kina kabisa kupitia vitabu mbalimbali vilivyofanya kazi ya kuchambua dua zilizomo ndani ya Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa kazi maridadi za tafsiri chambuzi ya dua hii, inapatokana na pamoja na ile inayopatika kwenye kitabu kiitacho Diare Asheqan, kilichoandikwa na Hossein Ansarian, pamoja na Shuhud wa Shenakht, cha Hassan Mamdouhi Kirmanshahi, vyote vikiwa vimeandikwa kwa lugha ya Kiajemi. Pia tafsiri chambuzi ya dua hii inapatikana kwa lugha ya Kiarabu, kupitia kitabu kiitwacho Riadhu al-Salikin, kazi ya Sayyid Ali Khan Madani. Mafunzo ya Dua ya Thalathini na Tano Dua ya 35 kutoka katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, ni dua adhimu kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni inazungumzia jinsi ya mwanadamu anavyopaswa kukubaliana na maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu. Kulingana na maelezo ya mchambuzi wa kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, bwana Muhammad Jawad Mughniyya, ni kwamba; Ule msemo "Ridhaa ya Mungu, ndiyo yetu..." ulikuwa ni moja ya misimamo mikuu ya familia ya bwana Mtume Muhammad (a.s). [1] Aidha, mfasiri mwingine wa kitabu cha Sahifa Sajjadiyya aitwaye Mamduhi Kirmanshahi, anaeleza akiema kuwa; Kuridhika na kile anachokupa Mwenye Ezi Mungu, ni daraja yenye kiwango cha juu zaidi, kupindukia ila daraja ya mtu anayekuwa na subira wakati wa shida. Amesema hivyo kwa sababu ya kwamba, mtu anayeridhika na maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu, kiuhalisia huwa amekukibali kwa moyo mmoja kile alichoamuliwa (alichochaguliwa) na Mola wake. Kwa upande mwingine, mtu anayevumilia misukosuko, anaweza kuwa ni mvumilivu wa misukosuko hiyo, ila bado hajakubaliana na uamuzi huo wa Mola wake kikamilifu ndani ya nafsi yake. [2] Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anaonyesha shukrani zake kwa yale aliyopewa na Mwenye Eiz Mungu, pamoja na kumshukuru Mola wake kwa yale ambayo hajabahatika nayo kutoka kwa Mola wake. [3] Mafunzo ya dua hii yamefafanuliwa katika vipengele vifuatavyo: • Kukiri na kushuhudia kuwa Mwenye Ezi Mungu anagawanya riziki kwa waja wake kwa uadilifu. • Kutambua kuwa fadhila na neema za Mwenye Ezi Mungu zimeenea kila mahali. • Fikra ya kuwa na ridhaa na kuridhika na majaaliwa ya Mungu. • Kuomba kuepushwa na vyanzo na sababu za husuda. • Kusadiki uadilifu wa Mwenye Ezi Mungu katika kuwapa riziki waja wake. • Kuyahisabu majaaliwa uliopewa na Mwenye Ezi Mungu, kuwa ni kheri kwako. • Kuomba uwezo wa kushukuru zaidi juu ya vile ambavyo hukupatiwa kuliko vile ulivyopewa. • Kutowadharau masikini na kutowashangaa matajiri kupita kiasi. • Kuelewa kuwa heshima na utukufu wa kweli vinapatikana tu katika kumtii na kumwabudu Mungu. • Kuomba utajiri usioisha na heshima ya kudumu. • Kumsifu Mwenye Ezi Mungu kwa upweke wake; ya kwamba hakuzaa wala hakuzaliwa, na kwamba hakuna yeyote yule anayefanana naye. [4] Tafsiri Chambuzi za Dua ya Thalathini na Tano Dua ya Thelathini na Tano ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya, imefasiriwa na kufafanuliwa na wasomi kadhaa wa lugha mbali mbali, ikiwemo lugha ya Kiajemi na Kiarabu. Kwa upande wa lugha ya Kiajemi, baadhi ya vitabu maarufu vilivyoifafanua dua hii ni pamoja na: Diyare Asheqan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [5] Shuhud wa Shenakht, cha Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, [6] na Sharh wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyeh, kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri. [7] Kwa upande wa lugha ya Kiarabu, dua hii pia imefafanuliwa kupitia vitabu vifuatavyo: Riadhu as-Salikinm, cha Sayyid Ali Khan Madani, [8] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Muhammad Jawad Mughniyah, [9] Riyadhu al-Arifin, cha Muhammad bin Muhammad Darabi, [10] na Afaq al-Ruh, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [11] Aidha, kuna wanazuoni maalumu waliojitolea kutunga vita vyenye kutoa maana na uchambuzi wa msamiati na istilahi zilizotumika katika dua hii. Miongoni mwa vitabu vya ufafanuzi wa kilugha vilivyofanya kazi hiyo ni pamoja na; Ta'aliqat 'ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, cha Fayd Kashani [12] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Izzu al-Din Jaza'iri. [13]

Matini ya Dua Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الرِّضَا إِذَا نَظَرَ إِلَى أَصْحَابِ الدُّنْيَا

Hii ni moja ya dua zake (rehema na amani zimshukie) kuhusiana na suala la kuridhika (na maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu), aliyokuwa akiiomba pale alipowaona watu waliokumbatia mambo ya dunia.

الْحَمْدُ لِلَّهِ رِضًى بِحُكْمِ اللَّهِ، شَهِدْتُ أَنَّ اللَّهَ قَسَمَ مَعَايِشَ عِبَادِهِ بِالْعَدْلِ، وَ أَخَذَ عَلَى جَمِيعِ خَلْقِهِ بِالْفَضْلِ Shukrani zote zinamstahikia Mwenye Ezi Mungu, kama dhihirisho la kukubaliana na maamuzi Yake ya kimamlaka. Ninathibitisha kwa yakini kwamba; Mungu amegawa rasilimali za maisha ya viumbe vyake kwa misingi ya uadilifu, na amevitawala viumbe vyake vyote kwa ukarimu Wake mkuu. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا تَفْتِنِّي بِمَا أَعْطَيْتَهُمْ، وَ لَا تَفْتِنْهُمْ بِمَا مَنَعْتَنِي فَأَحْسُدَ خَلْقَكَ، وَ أَغْمَطَ حُكْمَكَ. Ewe Mwenyezi Mungu, mshushie baraka zako Muhammad na Aali zake. Na usinijaribu (usinitahini) kwa kile ulichowapa wao, wala usiwajaribu wao kwa kile ulichoninyima mimi, ili niisije nikaanza kuwahusudu viumbe wako na kuidharau hukumu yako.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ طَيِّبْ بِقَضَائِكَ نَفْسِي، وَ وَسِّعْ بِمَوَاقِعِ حُكْمِكَ صَدْرِي، وَ هَبْ لِيَ الثِّقَةَ لِأُقِرَّ مَعَهَا بِأَنَّ قَضَاءَكَ لَمْ يَجْرِ إِلَّا بِالْخِيَرَةِ، وَ اجْعَلْ شُكْرِي لَكَ عَلَى مَا زَوَيْتَ عَنِّي أَوْفَرَ مِنْ شُكْرِي إِيَّاكَ عَلَى مَا خَوَّلْتَنِي Ewe Mwenyezi Mungu, msalie (mrehemu) Muhammad na Aali zake. Na uitakase nafsi yangu ili iridhie (itulie) hukumu (maamuzi) Yako, na ukipanue kifua changu kwa ajili ya kuhimili nyanja mbali mbali za maamuzi Yako, na unipe yakini kamili, ili niitumie yakini hiyo kwatika kukiri ya kwamba; hukumu Yako haipiti isipokuwa kwa njia ya kheri (kwa ajili ya yaliyo bora zaidi). Na ujaalie shukrani zangu Kwako juu ya yale uliyonizuilia (ulioninyima), ziwe nyingi kupindukia zile ninazokushukuru kwa ajili ya yale uliyonipa. وَ اعْصِمْنِي مِنْ أَنْ أَظُنَّ بِذِي عَدَمٍ خَسَاسَةً، أَوْ أَظُنَّ بِصَاحِبِ ثَرْوَةٍ فَضْلًا، فَإِنَّ الشَّرِيفَ مَنْ شَرَّفَتْهُ طَاعَتُكَ، وَ الْعَزِيزَ مَنْ أَعَزَّتْهُ عِبَادَتُكَ Na unihifadhi dhidi ya dhana ya kumchukulia mhitaji (msinakitu) kuwa ni mtu duni, au kumwona mwenye utajiri kuwa ni mtu mweye thamani zaidi. Kwa hakika, hadhi halisi ni ya yule aliyepata hadhi kupitia utiifu kwako, na aliye mbora, ni yule aliyepata ubora wake kupitia ibada kwako. فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ مَتِّعْنَا بِثَرْوَةٍ لَا تَنْفَدُ، وَ أَيِّدْنَا بِعِزٍّ لَا يُفْقَدُ، وَ اسْرَحْنَا فِي مُلْكِ الْأَبَدِ، إِنَّكَ الْوَاحِدُ الْأَحَدُ الصَّمَدُ، الَّذِي لَمْ تَلِدْ وَ لَمْ تُولَدْ وَ لَمْ يَكُنْ لَكَ كُفُواً أَحَدٌ. Basi, mrehemu Muhammad na Aali zake. Na tukirimie rasilimali isiyo na ukomo, tuimarishe kwa adhama isiyopungua (kwa ubora usiopungua), na utupe fursa ya kuishi bila vizuizi katika mamlaka Yako ya milele. Kwa hakika, Wewe ndiye Mmoja (Al-Waahid) wa Kipekee asiye na mfano (Al-Ahad) katika upweke wake, Nawe Ndiye kimbilio la viumbe vyote (As-Samad) (mtegemewa wa viumbe vyote). Hukuzaa wala hukuzaliwa, na hapana yeyote anayeweza kulingana nawe katika dhati yako.