Dua ya thelathini na tatu ya Sahifa Sajjadiyya
Dua ya thelathini na tatu ya Sahifa Sajjadiyya: ni dua iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s.), aliyokuw akiitumia katika muktadha wa kuomba kheri kutoka kwa Mungu wake. Katika dua hii, Imamu sajjad (a.s) anaiarifisha dhana ya welewa (wa kutambua haki) kama ndiyo kigezo kikuu cha kinachomwezesha mja kupata taufiki ya kuridhia na kukubali kadari (majaaliwa) ya kiungu. Zaidi ya hayo, pia dua hii inatoa mwelekeo wa maombi yenye kuomba kuifikia daraja ya kusalimu amri mbele ya maamuzi ya Allah, kupata yakini (uhakika usio na shaka), pamoja na kuepushwa na maasi yanayosababishwa na kuhgafilia na kutengana na Mwenye Ezi Mungu. Uchambuzi wa kitafsiri wa Dua ya Thelathini na Tatu, unapatikana katika vitabu vya tafsiri ya dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na; Diare Asheqan (Ardhi ya Wapenzi), kitabu kilichoandikwa na Hossein Ansarian, na Shuhud wa Shenakht (Ushuhuda na Utambuzi), kazi ya Hassan Mamduhi Kirmanshahi, ambavyo viwili vimeandikwa kwa lugha ya Kiajemi. Vilevile, dua hii imefafanuliwa kwa lugha ya Kiarabu kupitia kitabu kiitwacho Riadhu as-Salikin (Bustani za Washika Njia ya Haki), cha Sayyid Ali Khan Madani. Mafundisho Yaliyomo Ndani ya Dua ya Thalathini na Tatu Dua ya Thelathini na Tatu ni miongoni mwa dua tukufu za Sahifa Sajjadiyya. Hii ni dua ya Imamu Sajjad (a.s) aliyokuwa akiisoma kwa ajili ya kumuomba Mola wake mjaaliwa ya kheri. Mwanachuoni maarufu ajulikanaye kwa jina la Mamduhi Kirmanshahi, ni miongoni mwa wafasri muhuimu walioichambua dua hii adhimu. Suala la Istikhara, ni miongoni mwa masuala yaliokoza rangi katika uchambuzi wa bwna Mamduhi. Akizungumzia mada hiyo, anasema kwamba; Istikhara ni miongoni mwa njia maalumu za kupata uongofu wa Allah (Subhanahu wa Ta'ala), pale ambapo mja anapokuwa katika njia panda, wakati ambao waja hushindwa kupata jawabu muwafaka, hata baada ya kutafuta shauri kutoka kwa watu mbali mbali. Hapo ndipo mja humuelekea Mola wake na Muumba kuomba hidaya na kutafuta muongoza ktokana na utata wa jambo fulani. [1] Mafuzo ya Dua hii yamekuja katika vipengele vifuatavyo: • Kumuomba Mwenye Ezi Mungu kheri na baraka katika kila jambo. • Ombi la kufikia daraja la utiifu kamilifu na yakini thabiti mbele ya hadhara ya Mwenye Ezi Mungu. • Kutafuta kinga dhidi ya maasi na hali ya mghafala wa kiroho. • Kuomba taufiki ya kujaliwa ridhaa juu ya kadari na hukumu za kiungu, pamoja na kipata taufiki ya kujisalimisha kikamilifu mbele ya Aalla. • Ombi la kunufaishwa na yakini za watu wenye yakini na ikhlasi. • Ufahamu wa kile kinachopelekea kupata ridhaa na utulivu mbele ya makadirio ya Mwenye Ezi Mungu. • Kuomba kuridhika na yale yote yaliyopangwa na Mwenye Ezi Mungu. • Ombi la kumuomba Mola aufanye wepesi mtihani wa Qadhaa Yake. • Maombi ya utiifu, unyenyekevu, na ujisalimishaji kamili mbele ya mapenzi na irada (mataka na makadirio) ya kiungu. • Mwenyezi Mungu ndiye chanzo cha kila kheri, na Ndiye mgawaji wa neema kuu. • Maombi ya kupata hatima njema na yenye baraka. [2]
Matini ya Dua Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili وَ کانَ، مِنْ دُعَائِهِ علیهالسلام فِی الِاسْتِخَارَةِ Na miongoni mwa dua zake (amani iwe juu yake) ilikuwa ni ile dua inayohusiana na Istikhara (kumuomba mwenye Ezi Mungu mwongozo katika kufanya maamuzi). اللَّهُمَّ إِنِی أَسْتَخِیرُک بِعِلْمِک، فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اقْضِ لِی بِالْخِیرَةِ Ee Mwenye Ezi Mungu! hakika mimi nakuomba maamuzi, kupitia elimu Yako. Hivyo basi, mmiminie baraka zako Muhammad na Aali zake, na uniamulie suala langu kwa njia yenye kheri. وَ أَلْهِمْنَا مَعْرِفَةَ الِاخْتِیارِ، وَ اجْعَلْ ذَلِک ذَرِیعَةً إِلَی الرِّضَا بِمَا قَضَیتَ لَنَا وَ التَّسْلِیمِ لِمَا حَکمْتَ فَأَزِحْ عَنَّا رَیبَ الِارْتِیابِ، وَ أَیدْنَا بِیقِینِ الْمُخْلِصِینَ. (Ewe Mwenye Ezi Mungu), tupambanulie nuru ya utambuzi (wa kuchagua lenye kheri) katika maamuzi yetu, na uyafanye maamuzi hayo kuwa ndiyo sababu ya kutufikisha kwenye utulivu wa moyo juu ya yale uliyotupangia (uliyotukadiria), na itupelekee kwenye kusalimu amri mbele ya maamuzi yako. Basi, zitenge nyoyo zetu giza la wasiwasi (linalotokomeza matumaini), na utukite imara kwenye imani thabiti, kama ile ya wale waliotakaswa (wenye ikhlasi). وَ لَا تَسُمْنَا عَجْزَ الْمَعْرِفَةِ عَمَّا تَخَیرْتَ فَنَغْمِطَ قَدْرَک، وَ نَکرَهَ مَوْضِعَ رِضَاک، وَ نَجْنَحَ إِلَی الَّتِی هِی أَبْعَدُ مِنْ حُسْنِ الْعَاقِبَةِ، وَ أَقْرَبُ إِلَی ضِدِّ الْعَافِیةِ Na wala usitupandikize ulemavu wa kiutambuzi juu yale uliyoyateua (uliyotuamulia), ili tusije tukapuuza takdiri Yako (amri au kipimo chako cha kimantiki) katika maamuzi yako, na tukabughudhi nafasi (mahala) ya ridhaa yako, na tukaelemea kwenye mwelekeo ulio mbali zaidi na matokeo (hatima) bora, na tukawa karibu zaidi na kinyume cha ustawi (tukaelekewa moporomkoni). حَبِّبْ إِلَینَا مَا نَکرَهُ مِنْ قَضَائِک، وَ سَهِّلْ عَلَینَا مَا نَسْتَصْعِبُ مِنْ حُکمِک Ewe Mola wetu, tupendezeshee yale tunayoyachukia katika Qadhaa yako (maamuzi yako yasiyopingika), na utusahilishie yale tunayoyaona kuwa ni mazito katika Hukumu yako (amri zako). وَ أَلْهِمْنَا الِانْقِیادَ لِمَا أَوْرَدْتَ عَلَینَا مِنْ مَشِیتِک حَتَّی لَا نُحِبَّ تَأْخِیرَ مَا عَجَّلْتَ، وَ لَا تَعْجِیلَ مَا أَخَّرْتَ، وَ لَا نَکرَهَ مَا أَحْبَبْتَ، وَ لَا نَتَخَیرَ مَا کرِهْتَ. Na tujaalie uwezo (muongozo) wa kukubali yale uliyotujaalia kulingana na matakwa yako, ili tusipende kuchelewesha ulichoharakisha, wala kuharakisha ulichokichelewesha, wala tusichukie ulichokipenda, na tusichague kile ulichokichukia.
وَ اخْتِمْ لَنَا بِالَّتِی هِی أَحْمَدُ عَاقِبَةً، وَ أَکرَمُ مَصِیراً، إِنَّک تُفِیدُ الْکرِیمَةَ، وَ تُعْطِی الْجَسِیمَةَ، وَ تَفْعَلُ مَا تُرِیدُ، وَ أَنْتَ عَلَی کلِّ شَیءٍ قَدِیرٌ. Na utukhitimishie kwa hatima yenye kusifiwa zaidi (iliyo njema zaidi), na marejeo yaliyo matukufu zaidi. Hakika Wewe hutoa yaliyo bora zaidi, na unaneemesha yaliyo adhimu, nawe hutenda upendavyo, Nawe ni Mweza juu ya kila kitu (Nawe ni Mweza wa kutenda lolote lile ulitakalo).