Nenda kwa yaliyomo

Dua ya thalathini na mbili ya Sahifa Sajjadiya

Kutoka wikishia

Dua ya thalathini na mbili ya Sahifa Sajjadiya: Ni moja ya miongoni mwa dua zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Dua zilizomo ndani ya kitabu hichi, ni dua maalumu zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s.). Dua ya thalathin I na moja ni dua maalumu iliyokuwa ikisomwa na Imamu Sajjad (a.s) baada ya kumaliza ibada yake ya Sala za Usiku. Katika dua hii yake, Imamu anungama na kukiri dhambi zake, huku akiomba msamaha kutoka kwa Mola wake. Zaidi ya hayo, aidha dua hii inafafanua dhana kadhaa muhimu kwa ajili ya wacha-Mungu, zikiwemo baadhi ya sifa za Uungu wa Mwenye Ezi Mungu, hulka za Ibilisi, mbinu zake za kupenyeza fikra zake ndani mawazo ya mwanadamu, na sifa bainifu kuhusiana na adhabu ya moto wa Jehanamu. Baaya ya Imamu kutoa uchambuzi wa dhana hizi, anafafanua na nasisitiza baadhi ya fikra zinazoweza kuwakomboa wanadamu kutokana na adhabu zinazosababishwa na amali zao mbali mbali. Miongoni mwa fikra hizo ni pamoja na; kuomba msamaha na kutafuta rehema za Mwenye Ezi Mungu, kuikimbilia hifadhi Yake, pamoja na shufaa Yake, ikiwa ndiyo misingi wa ukombozi kutoka kwa ushawishi wa Ibilisi na adhabu zitokanazo na amali zao.

Kuna vitabu kadhaa vilivyochambua na kufasiri dua hii ya thalathini na mbili, sambamba na dua nyengine zilizomo katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilivyofasiri na kuchambua dua hii kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; "Diare Asheqan", kazi ya Hossein Ansarian na "Shuhud wa Shenakht", kazi ya Hasan Mamduhi Kermanshahi. Ama vitabu vilivyofasiri dua hii kwa Lugha ya Kiarabu ni kile kitabu maarufu kiitwacho "Riad as-Salikin", kazi ya Sayyid Ali Khan Madani. Mafundisho Yaliyomo Ndani ya Dua ya Thalathini na Mbili Da ya thalathini na mbili yaliyomo ndani ya Sahifa Sajjadiyya, ni dua maalumu ya kinathari ailiyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), aliyokuwa akiisoma baada ya kukamilisha ibada zake za usiku. Humo, hukiri na kukubali makosa yake huku akimwasilisha ombi lake la maghufira kwa Mola wake Mtukufu. Umuhimu wa dua hii unatokana na maudhui yake yaliyojaa sifa za Mwenye Ezi Mungu na njia za unyenyekevu zenye kuamsha mwitikio wa rehema ya Kiungu. [1] Misingi ya kielimu ya dua hii imebainishwa katika dhana ifuatavyo:

• Dhana ya udumifu wa milele wa ufalme na mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu. • Uwezo wa Mungu si wenye mipaka na wala hauhitaji msaada wa viumbe kama jeshi au wasaidizi. • Utkufu wa Mungu ni sifa ya daima isiyobadilika daima. • Mungu ni asili isiyo na mwanzo wala mwisho na wala haina ukomo wa eneo wala nyakati. • Upungufu wa lugha na akili ya binadamu katika kutoa maelezo kamili juu ya uhakika wa Dhati ya Mwenye Ezi Mungu. • Uwezo na utawala wa mamlaka ya Mungu usio weza kufikiwa na kiumbe yeyote. • Utawala mkuu wa Mwenye EziMungu usio na mpinzani juu ya viumbe vyote. • Kutowepo uwezo wa kumjua Mungu na msambaratiko wa fikra za waja katika jitihada za kumjua Mola wao. • Uasili wa Mungu ni wa tangu na tangu (azali) na wa milele na milele (abadi). • Ithibati ya upungufu wa mwanadamu katika utendaji wake. • Ithibati ya kuwepo kwa matarajio makuu ndani ya nafsi ya mwanadamu. • Mwanadamu kutoweze timiza wajibu wake wa kiibada na utiifu pasi na kuwepo msaada wa Kiungu. • Msamaha wa Kiungu kama matumaini na lengo kuu la mwanadamu. • Kutafuta hifadhi mbele ya Mungu dhidi ya mikakati, hila, na njama za Kishetani. • Kuomba rehema na msamaha wa Mwenye Ezi Mungu kutokana na uhaba wa matendo ya utiifu na wingi wa maasi. • Kutafuta hifadhi mbele ya Mwenye Ezi Mungu kama mbinu ya kujinasua na kuepukana na mitego ya matendo maovu. • Ujuzi wa Mwenye Ezi Mungu usio na kikomo, unaoangaza matendo yote ya binadamu (ujuzi wake unaozingira mfumo mzima wa ulimwengu). • Kuwasilisha mbele ya Mungu malalamiko, dhidi ya Ibilisi na kutafuta ulinzi wa Mungu dhidi ya uovu wa Shetani. • Madhara na hatima ya kumfuata Shetani ni: kuangamia, kutenda maasi, na kuchochea ghadhabu za Mungu. • Nadharia ya mwanguko wa taratibu wa mwanadamu. • Mungu kama kimbilio, mtoa shufaa, na mkombozi pekee wa mwanadamu. • Ombi la msamaha wa Mwenye Ezi Mungu. • Ungamo la dhambi mbele ya Mwenye Ezi Mungu. • Stara ya Mwenye Ezi Mungu ya kuyafinika makosa ya mja wake. • Imani ya kati na kati baina ya khofu (woga wa adhabu) na raja (tumaini la mafanikia) mbele ya Mwenye Ezi Mungu. • Mungu ndiye anayestahili zaidi kuaminiwa na kutegemewa. • Rehema na msamaha wa Mungu ndio chanzo cha matumaini ya waja. • Ombi la Kumuomba Mwnye Ezi Mungu stara ya kuhifadhi siri za waja wake Siku ya Kiyama. • Kuweka tumaini kwa Mwenyezi Mungu katika kupata msamaha na maghufira Yake. • Hatua za uumbaji wa mwanadamu (maelezo ya hali ya mwanadamu akiwa tumboni mwa mama yake). • Mipango ya Mungu katika hatua za ukuaji wa mwanadamu. • Kukosa imani katika uruzuku wa Mungu ni sababu ya kupuuza ibada na uwajibikaji. • Shetani ndio chanzo cha dhana mbaya dhidi ya Mwenye Ezi Mungu na ndiyo sababu ya kukumbwa na udhaifu wa yakini. • Kunyenyekea na kumporomokea Mwenye Ezi Mungu kwa ajili kupata kinga dhidi ya hila na udanganyifu wa Shetani. • Fadhila za daima za Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake. • Ombi la kuomba njia ya kupata riziki kiwepesi. • Ombi la kuomba taufiki ya kuridhika na majaaliwa ya Mwenye Ezi Mungu pamoja na kufurahia fungu na riziki ya mja kama lilivyo. • Kuomba umri na mwili, vyote kwa pamoja viwe katika utumishi wa kutumikia yale yalioko kwenye njia ya utiifu na ibada ya Allah. • Kujikinga mbele ya Mwenye Ezi Mungu dhidi ya moto na adhabu ya Jahanamu. • Sifa za moto wa Jahanamu. • Aina za adhabu ya Jahanamu. • Kutumainia fadhila na rehema za Mwenye Ezi Mungu kwa ajili ya kuokolewa na moto wa mateso mbali mbali. • Kuomba msamaha wa kusamehewa makosa na kutodhalilishwa na Mwenye Ezi Mungu, kwani Yeye ndiye mbora wa kuhifadhi. • Swala na salamu kwa Mtukufu Muhammad pamoja na Aali zake. [2]

Tafsiri na Maelezo ya Dua ya Thalatini na Mbili Maelezo ya tafsiri ya dua ya thelathini na mbili, yanapatikana katika vitabu mbali mbali vilivyofasiri dua za Sahifa Sajjadiyah. Miongoni mwa vitabu vilivyofasiri na chambua dua ya tahalathini na mbili kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; Diar Asheqan, kitabu kilichoandikwa na Hossein Ansarian, [3] Shuhud wa Shenakht kazi ya Mohammad-Hasan Mamduhi Kirmanshahi [4] na Sharhe wa Tarjumeye Sahifa Sajjadiyyeh, kazi iliyofanywa na Sayyid Ahmad Fahri. [5] Aidha, kuna waandishi kadhaa waliotumia baadhi ya muda wao muhiumu kwa ajili ya kufasiri na kuchambua Dua ya thelathini na mbili pamoja na dua nyengine zilizomo katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vya Kiarabu vilivyofanya kazi hiyo ni pamoja na; Riadhu al-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Muhammad Jawad Mughniyyah, [7] Riadhu al-Arifina, kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi [8] na Afaqi al-Ruh, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [9] Maneno na msamiati wa dua hii, pia nao imefanyiwa kazi kwa kuchambuliwa kwa mfumo kilugha kupitia vitabu mbali mbali. Baadhi ya vitabu vya kilugha vilivyojumuisha msamiati wa dua hii pamoja na msamiati wa dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kama vile; Ta'aliqat Ala al-Sahifa al-Sajjadiyyah, kilichoandikwa na Faidhu Kashani [10] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Izzu al-Din Jazairi. [11]

Matini ya Kiarabu na Maelezo ya Kiswahili ya Dua ya Thalathini na Mbili وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیه‌السلام بَعْدَ الْفَرَاغِ مِنْ صَلَاةِ اللَّیلِ لِنَفْسِهِ فِی الِاعْتِرَافِ بِالذَّنْبِ Na ifuatayo ilikuwa dua yake (amani iwe juu yake). Aliyokuwa akiiomba baada ya kumaliza sala zake za usiku. Dua ambayo alikuwa akijiombea yeye mwenyewe, huku akikiri na kukubali makosa yake (Mbele ya Mola wa wake). اللَّهُمَّ یا ذَا الْمُلْک الْمُتَأَبِّدِ بِالْخُلُودِ Ewe Mwenye Ezi Mungu, Mwenye ufalme wa milele unaodumu daima dawama. وَ السُّلْطَانِ الْمُمْتَنِعِ بِغَیرِ جُنُودٍ وَ لَا أَعْوَانٍ. Na (Ewe Mwenye Ezi Mungu mwenye) mamlaka thabiti yasiyotegemea majeshi wala wasaidizi. وَ الْعِزِّ الْبَاقِی عَلَی مَرِّ الدُّهُورِ وَ خَوَالِی الْأَعْوَامِ وَ مَوَاضِی الْأَزمَانِ وَ الْأَیامِ Na ule utukufu udumuo (ubakiao) daima, usioathiriwa na mfululizo wa dahari, miaka, nyakati wala masiku. عَزَّ سُلْطَانُک عِزّاً لَا حَدَّ لَهُ بِأَوَّلِیةٍ، وَ لَا مُنْتَهَی لَهُ بِآخِرِیةٍ (Ewe Mwenye Ezi Mungu) Yametukuka amlaka yako kwa uadhama usio na kikomo katika uazali yake (utangu wake), na wala haina upeo katika uabadi wake (uendelevu wake). وَ اسْتَعْلَی مُلْکک عَلُوّاً سَقَطَتِ الْأَشْیاءُ دُونَ بُلُوغِ أَمَدِهِ Na umepaa ufalme wako, kwa mpao wenye uadhama na upeo wa juu mno (usio na mipaka), kiasi ya kwamba vitu vyote huporomoka pasi kuufikia upeo wake. وَ لَا یبْلُغُ أَدْنَی مَا اسْتَأْثَرْتَ بِهِ مِنْ ذَلِک أَقْصَی نَعْتِ النَّاعِتِینَ. Na hata kilele cha wasifu wa waelezaji wote (wanaojaribu kukusifu), hakiwezi kufikia hata kile kiwango cha chini kabisa cha yale uliyojihusisha nayo. ضَلَّتْ فِیک الصِّفَاتُ، وَ تَفَسَّخَتْ دُونَک النُّعُوتُ، وَ حَارَتْ فِی کبْرِیائِک لَطَائِفُ الْأَوْهَامِ Sifa zote hufilisika pale Wewe unapohusika, wasifu wote hufifia kabla ya kukufikia, na hata zile fikra maridadi kabisa (ziwazwazo na viumbe) hupigwa na butwaa mbele ya ukuu (utukufu) wako. کذَلِک أَنْتَ اللَّهُ الْأَوَّلُ فِی أَوَّلِیتِک، وَ عَلَی ذَلِک أَنْتَ دَائِمٌ لَا تَزُولُ Hivyo ndivyo Wewe, ndiye mwenye mwanzo wa utanga katika asili Yako ya utangu. Na kwa muktadha huo, Wewe ndiye wa milele, usiyekoma kuwepo. وَ أَنَا الْعَبْدُ الضَّعِیفُ عَمَلًا، الْجَسِیمُ أَمَلًا، خَرَجَتْ مِنْ یدِی أَسْبَابُ الْوُصُلَاتِ إِلَّا مَا وَصَلَهُ رَحْمَتُک، وَ تَقَطَّعَتْ عَنِّی عِصَمُ الْآمَالِ إِلَّا مَا أَنَا مُعْتَصِمٌ بِهِ مِنْ عَفْوِک ami ni mja wako, dhaifu katika utendaji wa amali (njema), ila matumaini (yangu) makubwa mno. Njia zote za mafungamano (uokovu) zimeniponyoka kutoka mikononi mawangu, isipokuwa ile iliyounganishwa na rehema Zako. Na kamba (zote) za matumaini zimenikatikia, isipokuwa ule msamaha wako ninaoushikilia. قَلَّ عِنْدِی مَا أَعْتَدُّ بِهِ مِنْ طَاعَتِک، و کثُرَ عَلَی مَا أَبُوءُ بِهِ مِنْ مَعْصِیتِک وَ لَنْ یضِیقَ عَلَیک عَفْوٌ عَنْ عَبْدِک وَ إِنْ أَسَاءَ، فَاعْفُ عَنِّی. Utiifu ninaouhesabu kuwa na uzito mbele Yako ni mchache, na umepindukia ukuba ule mzigo wa maasi ninaoukiri (mbele Yako). Na kamwe msamaha Wako kwa mtumishi Wako haiwezi kudhikika, hata kama atafanya makosa. Kwa hivyo, nakuomba unisamehe. اللَّهُمَّ وَ قَدْ أَشْرَفَ عَلَی خَفَایا الْأَعْمَالِ عِلْمُک، وَ انْکشَفَ کلُّ مَسْتُورٍ دُونَ خُبْرِک، وَ لَا تَنْطَوِی عَنْک دَقَائِقُ الْأُمُورِ، وَ لَا تَعْزُبُ عَنْک غَیبَاتُ السَّرَائِرِ Ewe Mwenye Ezi Mungu, na kwa yakini elimu Yako imezunguka siri za amali zote (zitendwazo na waja wako), na wala hakuna chochote kile kilichositiriwa ispokuwa kimekuwa ni dhahiri mbele ya khabari Zako. Na wala hayapote (hayajifichi) Kwako yale yaliyomo ndani ya nyoyo (za waja wako). وَ قَدِ اسْتَحْوَذَ عَلَی عَدُوُّک الَّذِی اسْتَنْظَرَک لِغَوَایتِی فَأَنْظَرْتَهُ، وَ اسْتَمْهَلَک إِلَی یوْمِ الدِّینِ لِإِضْلَالِی فَأَمْهَلْتَهُ.

Na kwa yakini, adui Yako amepata nguvu juu yangu; adui ambaye aliomba fursa ya kuahirishwa kwa lengo la kunipotosha, nawe ukamridhia (nakumpuruzia kamba). Aidha, aliwasilisha ombi la kupewa muda hadi Siku ya Malipo, kwa madhumuni ya kuniongoza upotevuni, nawe ukampa muda. فَأَوْقَعَنِی وَ قَدْ هَرَبْتُ إِلَیک مِنْ صَغَائِرِ ذُنُوبٍ مُوبِقَةٍ، وَ کبَائِرِ أَعْمَالٍ مُرْدِیةٍ حَتَّی إِذَا قَارَفْتُ مَعْصِیتَک، وَ اسْتَوْجَبْتُ بِسُوءِ سَعْیی سَخْطَتَک، فَتَلَ عَنِّی عِذَارَ غَدْرِهِ، وَ تَلَقَّانِی بِکلِمَةِ کفْرِهِ، وَ تَوَلَّی الْبَرَاءَةَ مِنِّی، وَ أَدْبَرَ مُوَلِّیاً عَنِّی، فَأَصْحَرَنِی لِغَضَبِک فَرِیداً، وَ أَخْرَجَنِی إِلَی فِنَاءِ نَقِمَتِک طَرِیداً. Hivyo, akanitumbukiza [katika maasi], na hali ya kuwa hapo mwanzo nilikuwa nikikukimbilia Wewe (nikitafuta ulinzi) kwa ajili ya kuepukana na yale madhambi madogo madogo yenye kuangamiza, pamoja na madhambi makubwa yenye kuhilikisha. Hatimae nikatumbukia kwenye maasi Yako, na nikawa na mwenye kustahiki adhabu Yako kutokana na ovu wangu, hapo ndipo aliponivulia kinyago cha usaliti wake, akanipokea kwa neno la ukafiri wake, akageuza uso wake na kajitenga na nami, na akanipa kisogo akitoroka. Hivyo basi akaniacha pweke mbele ya ghadhabu Zako, na akanitimua na kuniongoza kwenye uwanja wa kisasi Chako. لَا شَفِیعٌ یشْفَعُ لِی إِلَیک، وَ لَا خَفِیرٌ یؤْمِنُنِی عَلَیک، وَ لَا حِصْنٌ یحْجُبُنِی عَنْک، وَ لَا مَلَاذٌ أَلْجَأُ إِلَیهِ مِنْک. Sina mwombezi wa kuniombea kwako, wala mlinzi wa kunilinda (wa kinipa dhamana) dhidi yako, wala ngome ya kunificha usinione, wala kimbilio la kukukimbia ndani yake. فَهَذَا مَقَامُ الْعَائِذِ بِک، وَ مَحَلُّ الْمُعْتَرِفِ لَک، فَلَا یضِیقَنَّ عَنِّی فَضْلُک، وَ لَا یقْصُرَنَّ دُونِی عَفْوُک، وَ لَا أَکنْ أَخْیبَ عِبَادِک التَّائِبِینَ، وَ لَا أَقْنَطَ وُفُودِک الْآمِلِینَ، وَ اغْفِرْ لِی، إِنَّک خَیرُ الْغَافِرِینَ.

Basi huu ndio msimamo wa anayetafuta hifadhi kwako na (hapa ndipo) mahali pa anayeungama mbele zako. Basi, (jaalia) fadhila zako zisiwe finyu kwangu, na msamaha wako usinikome kabla yangu. Na (Nijaalie) nisiwe mimi ndiye yule niliyekatishwa tamaa zaidi miongoni mwa waja wako watubiao, wala (nisiwe) ndiye aliyevunjika moyo zaidi kati ya wale waliomo kwenye msafara wa wanokujia kwa matumaini. Na unisamehe, kwani Wewe ndiye Mbora wa wasamehevu.

اللَّهُمَّ إِنَّک أَمَرْتَنِی فَتَرَکتُ، وَ نَهَیتَنِی فَرَکبْتُ، وَ سَوَّلَ لِی الْخَطَاءَ خَاطِرُ السُّوءِ فَفَرَّطْتُ.

Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Wewe uliniamuru, nami nikaachana na amri zako, na ulinikataza nami nikapuuza (nikaachana na makatazo yako). Na msukumo wa uovu ulinirembeshea (ulinipambia) dhambi, na matokeo yake nikazembea (na kuingia hatiani).

وَ لَا أَسْتَشْهِدُ عَلَی صِیامِی نَهَاراً، وَ لَا أَسْتَجِیرُ بِتَهَجُّدِی لَیلًا، وَ لَا تُثْنِی عَلَی بِإِحْیائِهَا سُنَّةٌ حَاشَا فُرُوضِک الَّتِی مَنْ ضَیعَهَا هَلَک.

Wala, siwasilishi funga yangu ya mchana kama ithibati ya uchaji-Mungu wangu, wala sijilindi (sitegemea) visimamo vyangu vya usiku (na kudhani kuwa ndivyo vitakavyoniokoa). Kadhalika, na katu siwezi kusifika kutokana na utekelezaji wangu wa amali za Sunna, (kwani mimi sina amali) zaidi ya zile amali zawajibu, ambazo huangamia kila mwenye kuachana nazo. وَ لَسْتُ أَتَوَسَّلُ إِلَیک بِفَضْلِ نَافِلَةٍ مَعَ کثِیرِ مَا أَغْفَلْتُ مِنْ وَظَائِفِ فُرُوضِک، وَ تَعَدَّیتُ عَنْ مَقَامَاتِ حُدُودِک إِلَی حُرُمَاتٍ انْتَهَکتُهَا، وَ کبَائِرِ ذُنُوبٍ اجْتَرَحْتُهَا، کانَتْ عَافِیتُک لِی مِنْ فَضَائِحِهَا سِتْراً.

Wala sijikurubishi Kwako kupitia nyenzo ya sala za nafila (Sunna), hali nikiwa na wingi wa mambo niliyoghafilika nazo miongoni mwa wajibu wa fardhi Zako. Nimepituka mipaka Yako na kuingia kwenye maeneo ya makatazo Yako (nikavunja heshima Yako), na hatimae kuchuma madhambi makubwa (kabairi), ila usamehevu Wako kwangu imekuwa ndiyo sitara inayonisitiri mbele ya fedheha zake. وَ هَذَا مَقَامُ مَنِ اسْتَحْیا لِنَفْسِهِ مِنْک، وَ سَخِطَ عَلَیهَا، وَ رَضِی عَنْک، فَتَلَقَّاک بِنَفْسٍ خَاشِعَةٍ، وَ رَقَبَةٍ خَاضِعَةٍ، وَ ظَهْرٍ مُثْقَلٍ مِنَ الْخَطَایا وَاقِفاً بَینَ الرَّغْبَةِ إِلَیک وَ الرَّهْبَةِ مِنْک. Huu ndio hali ya yule mwenye kutahayari (kujionea haya) mbele Yako, anayeikasirikia nafsi yake [kwa makosa yake], akiwa na ridhaa kamili juu Yako. Hivyo basi, amekuja Kwako akiwa na roho nyenyekevu, utiifu kamili, na mgongo uliolemewa na mzigo wa dhambi (zake). Amesimama katikati ya hali mbili, hali ya na matumaini Nawe [kupata rehema Yako] na wakati huo huo akikuogopa [kwa adhabu Yako]. وَ أَنْتَ أَوْلَی مَنْ رَجَاهُ، وَ أَحَقُّ مَنْ خَشِیهُ وَ اتَّقَاهُ، فَأَعْطِنِی یا رَبِّ مَا رَجَوْتُ، وَ آمِنِّی مَا حَذِرْتُ، وَ عُدْ عَلَی بِعَائِدَةِ رَحْمَتِک، إِنَّک أَکرَمُ الْمَسْئُولِینَ. Nawe ndiye unayestahili zaidi kutumainiwa, na mwenye haki zaidi ya kuogopwa na kuheshimiwa. Hivyo basi, Ee Bwana (wangu), nipe ninachokitumainia, na unilinde kutokana na ninachokihofia. Na daima nijaalie baraka na rehema zako, kwani hakika Wewe ndiye mkarimu mkuu kuliko waombwao wengine wote. اللَّهُمَّ وَ إِذْ سَتَرْتَنِی بِعَفْوِک، وَ تَغَمَّدْتَنِی بِفَضْلِک فِی‌دار الْفَنَاءِ بِحَضْرَةِ الْأَکفَاءِ، فَأَجِرْنِی مِنْ فَضِیحَاتِ‌دار الْبَقَاءِ عِنْدَ مَوَاقِفِ الْأَشْهَادِ مِنَ الْمَلَائِکةِ الْمُقَرَّبِینَ، وَ الرُّسُلِ الْمُکرَّمِینَ، وَ الشُّهَدَاءِ وَ الصَّالِحِینَ، مِنْ جَارٍ کنْتُ أُکاتِمُهُ سَیئَاتِی، وَ مِنْ ذِی رَحِمٍ کنْتُ أَحْتَشِمُ مِنْهُ فِی سَرِیرَاتِی. Ewe Mwenyezi Mungu, kwa kuwa umenistiri kwa msamaha wako na kunifunika kwa fadhila zako katika maisha haya ya mpito, nikiwa mbele ya wenzangu, basi niepushe na fedheha za maisha ya milele mbele ya mashahidi miongoni mwa Malaika walio karibu Nawe, Mitume watukufu, pamoja na mashahidi na watu wema. Na niepushe na aibu mbele ya jirani niliyekuwa nikimficha makosa yangu, na mbele ya jamaa niliyekuwa nikimwonea haya kumfichulia yale (mabaya) yaliomo moyono mwangu. لَمْ أَثِقْ بِهِمْ رَبِّ فِی السِّتْرِ عَلَی، وَ وَثِقْتُ بِک رَبِّ فِی الْمَغْفِرَةِ لِی، وَ أَنْتَ أَوْلَی مَنْ وُثِقَ بِهِ، وَ أَعْطَی مَنْ رُغِبَ إِلَیهِ، وَ أَرْأَفُ مَنِ اسْتُرْحِمَ، فَارْحَمْنِی. (Mola wangu), katu sikuwategemea wao kunisitiri (kutokana na aibu zangu), lakini nimekutegemea Wewe katika msamaha Wako juu yanu. Na Wewe ndiye unayestahili zaidi kutegemewa (kuliko wote), mkarimu kuliko wote wanaombwa, na mwenye huruma kuliko wote wanaotakiwa rehema. Hivyo basi, nirehemu (mja Wako). اللَّهُمَّ وَ أَنْتَ حَدَرْتَنِی مَاءً مَهِیناً مِنْ صُلْبٍ مُتَضَایقِ الْعِظَامِ، حَرِجِ الْمَسَالِک إِلَی رَحِمٍ ضَیقَةٍ سَتَرْتَهَا بِالْحُجُبِ، تُصَرِّفُنِی حَالًا عَنْ حَالٍ حَتَّی انْتَهَیتَ بی‌إِلَی تَمَامِ الصُّورَةِ، وَ أَثْبَتَّ فِی الْجَوَارِحَ کمَا نَعَتَّ فِی کتَابِک: نُطْفَةً ثُمَّ عَلَقَةً ثُمَّ مُضْغَةً ثُمَّ عَظْماً ثُمَّ کسَوْتَ الْعِظَامَ لَحْماً، ثُمَّ أَنْشَأْتَنِی «خَلْقاً آخَر»َ کمَا شِئْتَ. Ewe Mwenyezi Mungu, na Wewe ndiye uliyenileta duniani humu, (ambapo umiumba) kutokana na maji hafifu (yasiyo na thamani) yaliyotoka kwenye uti wa mgongo, wenye mifupa iliyoshikana (iliyofinyana). Ukaniongoza (ukanielekeza) kwenye tumbo la uzazi lililo finyu, ambalo umelisitiri kwa tabaka za kinga maalumu. Humo ulinibadilisha kutoka hatua moja hadi nyingine, hadi ukalikamilisha umbo langu na kuvithibitisha viungo vyangu. Haya ni kulingana na vile ulivyoeleza katika Kitabu Chako, ukisema ya kwamba: (hatua ya kwanza kabisa) ni tone la mbegu, kisha pande la damu, kisha pande la nyama, kisha mifupa, kisha ukaivika mifupa hiyo (nguo ya) nyama. Halafu ukaniumba nikiwa "kiumbe kipya kabisa" kama ulivyotaka. حَتَّی إِذَا احْتَجْتُ إِلَی رِزْقِک، وَ لَمْ أَسْتَغْنِ عَنْ غِیاثِ فَضْلِک، جَعَلْتَ لِی قُوتاً مِنْ فَضْلِ طَعَامٍ وَ شَرَابٍ أَجْرَیتَهُ لِأَمَتِک الَّتِی أَسْکنْتَنِی جَوْفَهَا، وَ أَوْدَعْتَنِی قَرَارَ رَحِمِهَا. Na hadi ulipofika wakati wa kuihitaji riziki Yako, huku nikishindwa kujitegemea pasipo na msaada wa fadhila Zako, (hapo) ulinijaalia lishe (yangu) iwe inatokana na ziada (mabaki) ya chakula na kinywaji ulichompitishia mjakazi Wako (mama yangu), uliyenikalisha tumboni mwake na kunihifadhi ndani ya mfuko wake wa uzazi.

وَ لَوْ تَکلُنِی یا رَبِّ فِی تِلْک الْحَالاتِ إِلَی حَوْلِی، أَوْ تَضْطَرُّنِی إِلَی قُوَّتِی لَکانَ الْحَوْلُ عَنِّی مُعْتَزِلًا، وَ لَکانَتِ الْقُوَّةُ مِنِّی بَعِیدَةً. Na endapo, Ewe Mola wangu Mlezi, ungenitegemeza kwenye mamlaka yangu mwenyewe, huku nikiwa katika mazingira hayo, au kunishurutisha nitegemee nguvu zangu, basi katu nisingekuwa na mamlaka kama hayo, na nguvu hizo zingelikuwa zimbali nami (nisingekuwa na uwezo kuthibitisha nguvu hizo). فَغَذَوْتَنِی بِفَضْلِک غِذَاءَ الْبَرِّ اللَّطِیفِ، تَفْعَلُ ذَلِک بی‌تَطَوُّلًا عَلَی إِلَی غَایتِی هَذِهِ، لَا أَعْدَمُ بِرَّک، وَ لَا یبْطِئُ بی‌حُسْنُ صَنِیعِک، وَ لَا تَتَأَکدُ مَعَ ذَلِک ثِقَتِی فَأَتَفَرَّغَ لِمَا هُوَ أَحْظَی لِی عِنْدَک. Basi ulinilisha kwa fadhila Zako lishe iliyojaa wema na upole. Umekuwa ukinifanyia yote hayo kwa ukarimu Wako mkuu kwangu, hadi kufikia hapa nilipo leo. Kamwe sijawahi kukosa wema Wako, na katu uzuri wa muamala Wako haujawahi kuchelwa kunifikia (wala sijawahi kupungukiwa na hisani Yako). Na yote hayo ulioniotendea, bado imani yangu haijaimarika, na kuziweka wakfu juhudi zangu kwa ajili yale yenye hadhi ya juu zaidi mbele Yako. قَدْ مَلَک الشَّیطَانُ عِنَانِی فِی سُوءِ الظَّنِّ وَ ضَعْفِ الْیقِینِ، فَأَنَا أَشْکو سُوءَ مُجَاوَرَتِهِ لِی، وَ طَاعَةَ نَفْسِی لَهُ، وَ أَسْتَعْصِمُک مِنْ مَلَکتِهِ، وَ أَتَضَرَّعُ إِلَیک فِی صَرْفِ کیدِهِ عَنِّی. Hakika Shetani ameumiliki usukani wa mwelekeo wangu, wenye kuelekea kwenye fikra mbovu na imani haba. Hivyo, ninakulalamikia Wew juu ya ujirani wake muovu kwangu na utiifu wa nafsi yangu kwake. Ninakuomba unikinge dhidi ya udhibiti wake, na ninakuomba kwa unyenyekevu uondoshee vitimbi vyake. وَ أَسْأَلُک فِی أَنْ تُسَهِّلَ إِلَی رِزْقِی سَبِیلًا، فَلَک الْحَمْدُ عَلَی ابْتِدَائِک بِالنِّعَمِ الْجِسَامِ، وَ إِلْهَامِک الشُّکرَ عَلَی الْإِحْسَانِ وَ الْإِنْعَامِ، فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ سَهِّلْ عَلَی رِزْقِی، وَ أَنْ تُقَنِّعَنِی بِتَقْدِیرِک لِی، وَ أَنْ تُرْضِینِی بِحِصَّتِی فِیمَا قَسَمْتَ لِی، وَ أَنْ تَجْعَلَ مَا ذَهَبَ مِنْ جِسْمِی وَ عُمُرِی فِی سَبِیلِ طَاعَتِک، إِنَّک خَیرُ الرَّازِقِینَ. Na ninakuomba (Ewe Mola wangu), unifanyie wepesi njia ya riziki yangu. Basi sifa zote njema Zako, juu ya kuanza Kwako kutuneemesha kwa neema Zako kuu, na kwa kututupa ilhamu (hisia) ya shukrani juu ya hisani Zako na ukarimu Wako. Basi, Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake, na unifanyie wepesi riziki zangu, na unijaalie niikinai qadari Yako juu yangu, na uniridhishe kwa fungu langu ulilonigawia. Na ujaalie kile kilichotumika katika mwili wangu na umri wangu kiwe katika hisabu ya njia ya utiifu Kwako. Hakika Wewe ndiye Mbora wa kururuku. اللَّهُمَّ إِنِّی أَعُوذُ بِک مِنْ نَارٍ تَغَلَّظْتَ بِهَا عَلَی مَنْ عَصَاک، وَ تَوَعَّدْتَ بِهَا مَنْ صَدَفَ عَنْ رِضَاک، وَ مِنْ نَارٍ نُورُهَا ظُلْمَةٌ، وَ هَینُهَا أَلِیمٌ، وَ بَعِیدُهَا قَرِیبٌ، وَ مِنْ نَارٍ یأْکلُ بَعْضَهَا بَعْضٌ، وَ یصُولُ بَعْضُهَا عَلَی بَعْضٍ. Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi najilinda Kwako kutokana na moto wa Jahannam ambao umeunoa kwa ajili ya wale waliokuasi, na ukauahidi kama onyo kwa wale wanaopuuza radhi Zako; na (ninajilinda Kwako) dhidi ya Moto ambao nuru yake ni giza, na adhabu yake nyepesi kabisa ni chungu iumizayo kupita budi, (moto ambao) yaliyo mbali nao ni ya karibu kwake; na (ninajilinda Kwako) kutokana na Moto ambao, unakulana wenyewe kwa wenyewe, na sehemu zake zavamiana wenyewe kwa wenyewe. وَ مِنْ نَارٍ تَذَرُ الْعِظَامَ رَمِیماً، وَ تَسقِی أَهْلَهَا حَمِیماً، وَ مِنْ نَارٍ لَا تُبْقِی عَلَی مَنْ تَضَرَّعَ إِلَیهَا، وَ لَا تَرْحَمُ مَنِ اسْتَعْطَفَهَا، وَ لَا تَقْدِرُ عَلَی التَّخْفِیفِ عَمَّنْ خَشَعَ لَهَا وَ اسْتَسْلَمَ إِلَیهَا تَلْقَی سُکانَهَا بِأَحَرِّ مَا لَدَیهَا مِنْ أَلِیمِ النَّکالِ وَ شَدِیدِ الْوَبَالِ (Ewe Mola, nakuomba unikinge) na ule Moto unaoiacha mifupa ikiwa ni majivu yaliyosagika, na kuwanywesha watu wake kinywaji kitibukacho moto. Na (unikinge na) Moto ambao haumbakishi yeyote anayeulilia mbele yake, wala haumrehemu yeyote yule anayeuomba rehema, na wala hauwezi kumpunguzia adhabu yule anayejidunisha (anayejidogosha) na kujisalimisha mbele yake. Huwapokea waja (waovu) kwa ukali wake wote, wenye mateso yenye maumivu makali na maangamizi makubwa kupita budi.

وَ أَعُوذُ بِک مِنْ عَقَارِبِهَا الْفَاغِرَةِ أَفْوَاهُهَا، وَ حَیاتِهَا الصَّالِقَةِ بِأَنْیابِهَا، وَ شَرَابِهَا الَّذِی یقَطِّعُ أَمْعَاءَ وَ أَفْئِدَةَ سُکانِهَا، وَ ینْزِعُ قُلُوبَهُمْ، وَ أَسْتَهْدِیک لِمَا بَاعَدَ مِنْهَا، وَ أَخَّرَ عَنْهَا. Na ninajikinga Kwako dhidi ya nge wake wenye midomo iliyowachwa wazi, na nyoka wake wanaouma vibaya kwa meno yao makali. Pia ninajikinga (Kawako) dhidi ya kinywaji chake ambacho hukatakata matumbo (machango) na nyoyo za wakazi wake, na kung'oa mioyo yao (kutoka vifuani mwao). Na ninakuomba unielekeze kwenye yale yatakayoniweka mbali na moto huo na kuniepusha nao.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَجِرْنِی مِنْهَا بِفَضْلِ رَحْمَتِک، وَ أَقِلْنِی عَثَرَاتِی بِحُسْنِ إِقَالَتِک، وَ لَا تَخْذُلْنِی یا خَیرَ الْمُجِیرِینَ

Ewe Mwenyezi Mungu, mbariki Muhammad na Aali zake, na unilinde kutokana na ubaya wake (ubaya wa moto huo) kwa fadhila ya rehema Zako. Na unighufirie dhambi zangu kwa wema wa msamaha Wako, na wala usinitelekeze (usinidunishe), Ewe Mlinzi aliye bora kuliko wote.

اللَّهُمَّ إِنَّک تَقِی الْکرِیهَةَ، وَ تُعْطِی الْحَسَنَةَ، وَ تَفْعَلُ مَا تُرِیدُ، وَ أَنْتَ عَلَی کلِّ شَیءٍ قَدِیرٌ Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe ndiye Mkingaji wa shari, na Mtoaji wa kheri, Nawe ni Mtendaji wa yale uyatakayo. Na hakika Wewe ni Muweza juu ya kila jambo. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، إِذَا ذُکرَ الْأَبْرَارُ، وَ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، مَا اخْتَلَفَ اللَّیلُ وَ النَّهَارُ، صَلَاةً لَا ینْقَطِعُ مَدَدُهَا، وَ لَا یحْصَی عَدَدُهَا، صَلَاةً تَشْحَنُ الْهَوَاءَ، وَ تَمْلَأُ الْأَرْضَ وَ السَّمَاءَ. Ewe Mwenyezi Mungu, msalie Muhammad na Aali zake, kila wanapotajwa (wakumbukwapo) watu wema. Na mswalie Muhammad na Aali zake, kadiri ya mapishana ya usiku na mchana. (Msalie) Sala isiyo na ukomo katika mfululizo (mtirirko) wake, wala isiyohisabika idadi yake. (Msalie) Sala iliyosheheni ndani ya hewa, na kuijaza ardhi pamoja na mbingu.

صَلَّی اللَّهُ عَلَیهِ حَتَّی یرْضَی، وَ صَلَّی اللَّهُ عَلَیهِ وَ آلِهِ بَعْدَ الرِّضَا، صَلَاةً لَا حَدَّ لَهَا وَ لَا مُنْتَهَی، یا أَرْحَمَ الرَّاحِمِینَ. Mwenyezi Mungu amrehemu (Muhammad na Aali zaske) hadi aridhike, na aendeleze rehema Zake juu yake na Aali zake, hata baada ya radhi hiyo. (Amrehemu) rehema zisizo na ukomo wala hitimisho (ndani yake), Ewe Mrehemevu wa juu kabisa miongoni mwa warehemevu.