Malaika

Kutoka wikishia

Malaika au Malak (Kiarabu: الملائكة) ni viumbe wa Mwenyezi Mungu wasioonekana ambao hutumwa kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu duniani na akhera. Kuamini kwamba, malaika wapo, ni katika itikadi za Waislamu. Pamoja na hayo, wanazuoni wa Kiislamu wana mitazamo tofauti kuhusiana na utambulisho wa malaika.

Wasomi wa elimu ya theolojiia wao wanaamini kwamba, malaika ni viumbe wenye mwili ambao hujitokeza kwa sura na maumbile tofauti tofauti. Hata hivyo wasomi wa elimu ya falsafa wao wanasema kuwa, malaika ni viumbe wasio na umbile au mwili.

Kwa mujibu wa wanachuoni wa Kishia, malaika ni maasumu (hawatendi dhambi), kwa hiyo hawatendi dhambi au kuasi amri za Mungu. Kadhalika malaika hawazembei katika kutekeleza majukumu yao.

Majukumu yao ni:Kuabudu, kumtakasa na kumsabihi Mwenyezi Mungu, kuandika kitabu cha matendo, kufikisha wahyi kwa Mitume, kuwalinda watu, kuwasaidia waumini, kufikisha riziki za kimaada na kiroho (kimaanawi), kutoa roho (uhai), kuongoa nyoyo, na kutekeleza adhabu ya Mwenyezi Mungu. Malaika wana makundi na vyeo tofauti; Jibril, Mikail, Israfil na Israil ni malaika ambao wana nafasi ya juu kuliko malaika wengine. Malaika hawa wanatambulika kama Malaika wakuu.

Ubora wa Malaika juu ya wanadamu, umaasumu wa malaika na kuwa na umbo au kutokuwa kwao na mwili ni baadhi ya mada ambazo zimejadiliwa na kubainishwa katika vitabu vya tafsiri na vya kitheolojia na kuelezwa mitazamo tofauti kuhusiana na jambo hili.

Utambulisho wa malaika

Malaika ni viumbe wasioonekana ambao ni viunganishi baina ya Mwenyezi Mungu na ulimwengu wa kibinadamu, na Mwenyezi Mungu amewateua na kuwapa majukumu maalumu. [1] malaika (ملائکه) ni wingi wa malak. [2]

Kuhusiana na utambulisho wa malaika, kuna tofauti za kimitazamo; wasomi na wanazuoni wa elimu ya theolojia wanaamini kwamba, malaika wana miili myembamba na yenye nuru na wanaweza kuja kwa sura tofauti tofauti. [3] Allama Majlisi ameinasibisha nadharia na mtazamo huu na Waislamu wote isipokuwa baadhi ya wanafalsafa wachache na akaongeza kuwa, Manabii na mawasii wao walikuwa wakiwaona malaika. [4] Hata hivyo kundi fulani ya wanafalsafa linaamini kwamba, malaika ni zaidi ya mwili na kuwa na umbo na wanaamini kuwa, wana wasifu ambao hauwezi kutosheleza katika mwili. [5] Kwa mujibu wa Allamah Tabatabai ni kwamba, kinachotajwa katika hadith kuhusu kuonekana malaika katika maumbo ya kimaumbile ni ushabihishaji (yaani kitu kinamtokea mtu katika umbo maalumu). [6] Aidha kwa mtazamo wake ni kwamba, hii kwamba, imeondokea kuwa mashuuhuri ya kwamba, malaika na majini wana na hujitoikeza katika maumbo tofauti tofauti, ni jambo ambalo halina hoja na mashiko madhubuti. [7] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ni kwamba, malaika wameumbwa kutokana na nuru. [8]

Umuhimu na nafasi yao

Kuamini kuwepo kwa malaika ni miongoni mwa imani na itikadi za Waislamu [9] na imani juu yao ni kama imani kuhusiana na Swala na Swaumu na inachukuliwa kuwa moja ya mambo lazima ya imani kwa Utume. [10]

Neno malak limetumika mara 88 katika Qur'an [11]. Katika Khutba ya Ashbah, Imam Ali (a.s) anaashiria kuumbwa malaika, migawanyiko yao, sifa zao maalumu pamoja na majukumu yao. [12] Katika kitabu cha Bihar al-Anwar kumenukuliwa hadithi zaidi ya 100 zinazozungumzia utambulisho wa malaika, majukumu yao, umaasumu wa malaika na sifa za mailaka Muqarrab (walio na daraja ya juu). [13] Dua ya tatu katika kitabu cha Sahifat al-Sajjadiyah kutoka kwa Imam Sajjad (a.s) ni maalumu kwa malaika walio na daraja ya juu zaidi; katika dua hii kunaelezwa kuwa, Sala, dua na amani ya Mwenyezi Mungu ni sababu ya usafi na utakasifu wao. [14]

Kwa mujibu wa hadithi, malaika ndio viumbe vingi zaidi vya Mwenyezi Mungu, na katika hadithi nyingi, wingi wao umetajwa na kubainishwa. [15] Imeelezwa katika hadithi kwamba, malaika waliumbwa baada ya kuumbwa kwa nuru ya Mtume (s.a.w.w) na Maimamu. (as) [16]

Kundi la washirikina lilikuwa likiwaabudu malaika na kuwahesabu kuwa ni viumbe vya Mungu, lakini pamoja na hayo walikuwa wakiamini kwamba wana uhuru katika matendo. [17] Baadhi ya washirikina pia waliwahesabu kuwa ni mabinti wa Mungu. [18]

Malaika katika dini zingine

Malaika wametajwa pia katika dini zingine; katika dini ya uzartoshti, inaelezwa kuwa, malaika wameumbwa na Ahura Mazda, na kila Amesha Spenta (lakabu ya malaika wa ngazi ya juu wa dini ya Zartoshti) ni dhihiriisho la moja ya sifa zake. Katika dini ya Uyahudi malaika wana daraja ya waja wa Mwenyezi Mungu ambao wanatekeleza maagizo yake ardhini na kuwafikishia wanadamu Wahyi. Kwa mujibu wa kitabu kitakatifu cha Wakristo ni kwamba, malaika aliumbwa kabla ya mwanadamu ni ni walinzi wa mwanadamu. ni jambo lililoenea baina ya makanisa ya Wakkristo kusalimia na kuabudu baadhi ya malaika kama Mikail. [19]

Majukumu

Katika kitabu cha Qur'ani tukufu kumetajwa majukumu ya malaika: Kuwa wao ni kiunganishi katika kushuka Wahyi (kufuikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa Mitume), [20] kuwa na tadibiri katika mambo ya dunia, kufikisha neema za Kiungu kwa viumbe, [21] kufanya istighfari [22] kuwafanyia uombezi waumini, [23] na kuwasaidia, [24] kuulaani makafiri, [25] kusajili na kuandika amali na matendo ya waja [26] na kutoa roho. [27] Kuna kundi la malaika ambalo daima limo katika hali ya kumsabihi na kumdhukuru Mwenyezii Mungu na halijihusishi na kazi nyingine. [28] Kuna malaika pia katika ulimwengu wa barzakhi (kaburini), [29] na akhera; kundi kati yao lipo peponi [30] na kundi jingine ni walinzi wa jahanamu na wakazi wake. [31]

Daraja na mgawanyo

Allama Tabatabai anasema, malaika wana daraja na vyeo mbalimbali. Baadhi ya malaika wana daraja ya juu huku wengine wakiwa na daraja ya chini. [32] Kwa mujibu wa Aya za Qur'an Tukufu, kundi miongoni mwa malaika ni mawakala wa malaika wa wahyi (Jibril) [33] na kundi jingine ni mawakala wa malaika wa mauti (Izraili) [34].

Mulla Sadra amewagawanya malaika katika aina kadhaa, ikiwa ni pamoja na malaika wakuu (walio karibu zaidi na Mungu), roho zinazozunguka (al-arwah al-muhayyamah), malaika wanaohusika na miili ya ulimwengu wa mbinguni. [36]

Sifa maalumu

Baadhi ya sifa za malaika ni:

Umaasumu

Allama Majlisi anasema, Mashia wanaamini kwamba, malaiko wako mbali na kila aina ya dhambi iwe ndogo au kubwa na kimsingi ni maasumu (hawatendi dhambi). Kadhalika walio wengi katika Ahlu-Sunna wana mtazamo na itikadi hii. [37] Pamoja na hayo baadhi ya Masuni hawakubaliani na suala na umaasumu wa malaika bali wanaaamini kuwa kuna baadhi tu ya malaika ambao hawatendi dhambi nao ni kama malaika wa Wahyi na malaika wenye daraja ya juu (malaika muqarrab). [38] Baadhi ya aya zinasema:

Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake. [39]

Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa. [40]

Bibliografia

Kumendikwa vitabu mbalimbali kuhusiana na malaika kwa lugha za Kiarabu, Kifarsi na Kiingereza.

Baadhi ya vitabu hivyo ni:

 • Seir dar Asrar Fereshtegan, waandishi: Muhammadzaman Rostami na Taher Aal-Buwaih.
 • Al-Makhluqaat al-Khafiyah Fil Qur'an: Al-Malaika, al-Jinn, al-Iblis, mwandishi: Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai.


Vyanzo

 • Allāma al-Ḥillī, Ḥasan b. Yūsuf, al-. Kashf al-murād. Qom, Muʾassisa-yi Nashr-i Islāmī, 1413AH.
 • Al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Qom: Daftar-i Nashr-i al-Hādī, 1376 Sh.
 • Ashqar, ʿUmar Sulaymān. ʿĀlam al-malāʾika al-abrār. Jordan: Dār al-nafāʾis, 1421 AH.
 • Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1416 AH.
 • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
 • Ḥasanzāda Āmulī, Ḥasan. Mumidd al-himam dar sharḥ-i fuṣūṣ al-ḥikam. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād, 1378 Sh.
 • Ḥusaynī Hamadānī, Muḥammad. Anwār-i dirakhshān dar tafsīr-i Qurʾān. Tehran: Luṭfī, 1404 AH.
 • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Ādāb al-Ṣalāt. Tehran: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeinī, 1378 Sh.
 • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Sharḥ-i chihil ḥadīth. Qom: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeinī, 1380 Sh.
 • Ījī, Mīr Sayyīd Sharīf. Sharḥ al-mawāqif. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1325 AH.
 • Jawādī Āmulī, ʿAbd Allāh. Taḥrīr tamhīd al-qawāʿīd Ibn Turka. Tehran: Intishārāt-i al-Zahrāʾ, 1372 Sh.
 • Lāhījī, Mullā ʿAbd al-Razzāq. Guhar-i murād. Tehran: Nashr-i Sāya, 1388 Sh.
 • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
 • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Al-Amthal fī tafsīr kitāb Allāh al-munzal. Qom: Madrisat Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib, 1421 AH.
 • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
 • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Payām-i Imām Amīr al-Muʾminīn (a) tafsīr-i Nahj al-balāgha. Qom: Madrasat al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib (a), 1387 Sh.
 • Muḥyi al-Dīn al-ʿArabī, Muḥammad b. ʿAlī. Tafsīr Ibn ʿArabī. Edited by Samīr Muṣtafā Rabāb. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth, 1422 AH.
 • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Ṭayyib Mūsawī Jazāʾrī. Qom: Dār al-Kitāb, 1404 AH.
 • Rustamī and Āl-i Būya, Muḥammad Zamān and Ṭāhira. Siyrī dar asrār-i firishtigān Qom: Pazhūhishgāh-i ʿUlūm wa Farhang Islāmī, 1393 Sh.
 • Sabziwārī, Muḥammad. Irshād al-adhhān ilā tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1419 AH.
 • Ṣadr al-Dīn Shīrāzī, Muḥammad b. Ibrāhīm. Mafātīḥ al-ghayb. Tehran: 1363 Sh.
 • Ṣadr al-Dīn Shīrāzī, Muḥammad b. Ibrāhīm. Tafsīr al-Qurʾān al-karīm. Edited by Muḥammad Khājawī. Qom: Bīdār, 1366 Sh.
 • Sayyid Raḍī, Muḥammad Ḥusayn. Nahj al-balāgha. Edited by Ṣubḥī Ṣaliḥ. Qom: Hijrat, 1414 AH.
 • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1417 AH.
 • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Muḥammad Jawād Balāghī. 3rd edition. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
 • Ṭurayḥī, Fakhr al-Dīn b. Muḥammad al-. Majmaʿ al-baḥrayn. Edited by Sayyid Aḥmad Ḥusaynī. Tehran: al-Maktaba al-Murtaḍawīyya, 1416 AH.
 • Zarkashī, Mūhammad b.ʿAbd Allāh. Al-Baḥr al-muḥīṭ fī uṣūl al-fiqh. Dār al-kutubī: 1414 AH.