Haihata mina al‑dhilla

Haihata Mina al‑Dhilla (Kiarabu: هَیهَاتَ مِنَّا الذِّلَّة) (hasha! kamwe hatutasalimu kwa udhalili): Tamko au ibara hii ni sehemu ya khutba ya Imamu Hussein (a.s) aliyoitoa siku ya Ashura, akilihutubia majeshi la Ibnu Sa‘ad.[1]
Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Imam Hussein (a.s) alitamka kauli hii akimjibu Ibnu Ziyad aliyempa hiari kati ya kusalimu amri au kuchukua maamuzi ya kupigana.[2] Katika hutuba yake hii, Imamu Hussein (a.s), alimjibu Ibnu Ziad kwa kuwambia kuwa; Kwa kuwa hakuna hata mmoja kati ya Mwenye Ezi Mungu na Mtume, na wala hakuna akili timamu inayokubali udhalili, basi kifo cha kufa kiheshima ni bora mno kwake, kuliko maisha ya fedheha.[3]

Mas‘udi ambaye ni mmoja wapo wa wanahistoria wa karne ya nne Hijiria, ananukuu ibara hii kama ifuatavyo:
- «ألا وَإنَّ الدَّعيَّ ابنَ الدَّعيِّ قَد رَكَّزَ بَينَ اثنَتينِ بَينَ السِلَّهِ وَالذِلَّةِ وَهَيهاتَ مِنّا الذِلَّةُ» “(Eleweni ya kwamba; Mpachikwa nasabu isiyokuwa yake (mwana wa zinaa), na mwana wa mpachikwa nasabu isiyokuwa yake) amenihiarisha kati ya mambo mawili: ima upanga (vita) au (kukubali) udhalili; nasi kamwe hatukubali (kutumbukia katika) udhalili.” }}.[5]
Hata hivyo, baadhi ya vyanzo vimenukuu «القتلة» kwa maana ya vita, badala ya neno «السلة» lenye maana ya kuchomoa upanga kwa ajili ya vita,[6] pia vyanzo vyengine vimenukuu neno «الدَّنِیئَةُ» lenye maana ya uduni, badala ya neno «الذِّلَّة» lenye maana ya udhalili.[7]
Katika zama za hivi sasa, ibara ya “Haihata mina al‑dhilla” imegeuka kuwa ni moja ya kauli mbiu muhimu ya kiupinzani katika muktadha wa kisasa. Waumini wa jumuia mbali mbali za Kishia, huinua sauti zao wakiitamka kauli hiyo katika maombolezo pamoja na maandamano yao mbali mbali, ili kutangaza kutosalimu kwao amri mbele ya ubeberu pamoja na kukataa aina mbali mbali za udhalilishaji.[8]
Rejea
- ↑ Rejea: Mas'udi, Ithbat al-Wasiyyah, 1384 AH, uk. 166.
- ↑ Mas'udi, Ithbat al-Wasiyyah, 1384 AH, uk. 166.
- ↑ Mas'udi, Ithbat al-Wasiyyah, 1384 AH, uk. 166.
- ↑ "Matembezi ya Amani siku ya Ashura kwa ajili ya Kuadhimisha Kifo cha Imam Hussein, (a.s), katika mji mkuu...", Taasisi ya Shahidi Zayd Ali Muslih.
- ↑ Mas'udi, Ithbat al-Wasiyyah, 1384 AH, uk. 166.
- ↑ Khawarizmi, Maqtal al-Hussein, 1381 AH, juz. 2, uk. 10.
- ↑ Ibn Shuu'bah Harrani, Tuhaf al-'Uquul, 1404 AH, uk. 241.
- ↑ Tazama: Matembezi ya Amani siku ya Ashura kwa ajili ya Kuadhimisha Kifo cha Imam Hussein, (a.s), katika mji mkuu...", Taasisi ya Shahidi Zayd Ali Muslih.
Vyanzo
- Ibn Shu’bah Harrani, Hassan ibn Ali, Tuhaf al-‘Uquul An al-Rasul, Utafiti: Ali Akbar Ghaffari, Qom, Daftar Intisharat Islami, Chapa ya Pili, 1404 AH.
- Al-Khawarizmi, Muwafaq bin Ahmad, Maqtal al-Hussein (a.s), Utafiti: Muhammad Samawi, Qom Anwar al-Huda, 1381 AH/1423 AH.
- Mas’udi, Ali ibn Hussein, Ithbat al-Wasiyyah l-Imam Ali bin Abi Talib, Qom, Itisharat Ansarian, Chapa ya Tatu, 1384 AH.
- "Matembezi ya Amani siku ya Ashura katika ukumbusho wa kuuawa shahidi Imam Hussein (a.s) katika mji mkuu #Sana'a, Sharii al-Matar...", Taasisi ya Shahidi Zaid Ali Muslih, Tarehe ya kuingizwa makala, Julai 16, 2024 AD, Tarehe ya kuhaririwa makala: Julai 2, 2025 AD.
- «Matembezi ya Amani siku ya Ashura katika ukumbusho wa kuuawa shahidi Imam Hussein (a.s) katika mji mkuu #Sana'a, Sharii al-Matar...», Tarehe ya kuingizwa makala, Julai 16, 2024 AD, Tarehe ya kuhaririwa makala: Julai 2, 2025 AD.