Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Arubaini na Mbili ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya Arubaini na Mbili ya Sahifa Sajjadiyya: ni miongoni mwa dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), aliyekuwa akiisoma dua hiyo kila anapohitimisha Qur'ani Tukufu. Ndani yake dua hii, Imamu Sajjad (a.s) ametubainishia sifa za kipekee inayosifika nazo Qur'ani Karim, huku akitufunza athari zinazopatikana kwa anayezifanyia kazi Aya zake. Aidha, Imamu Sajjad (a.s) kupitia dua hii, anatukumbushia baadhi ya sifa muhimu za bwana Mtume (s.a.w.w), pamoja na changamoto alizokumbana nazo wakati wa kueneza ujumbe wa Uislamu utokao kwa Mola wake. Baada ya ufafanuzi huo, Imamu Sajjad (a.s) anamuomba Mwenye Ezi Mungu ampatie daraja za juu kabisa Siku ya Kiyama. Aidha, dua hii imekeja ikiwatambulisha Maasumina (watoharifu watokanao na nyumba ya Mtume) (a.s), na kuwatambua kama niwo watunzaji (maboharia) na wafasiri halisi wa Qur'ani Tukufu. Bwana wa wachamungu, Immu Zainul Abidin (a.s) anaelekeza ombi lake kwa Mwenye Ezi Mungu, akitaraji na kumuomba Mola wake kupitia wasila wa Qur'ani Tukufu, awasamehe waumini makosa yao na awaghufirie dhambi zao. Aidha, anamuomba Mola wake ampatie hifadhi na amani dhidi ya dhiki za mauti, na hali kadhalika dhidi ya majonzi na khofu ya Siku ya Kiyama, na hatimaye anamwomba Mwenye Ezi Mungu, aifanye Qur'ani kuwa mpatanishi na mwombezi (shafii) wake siku ya ufufuo wa walimwengu (Yawm al-Hashr). Dua ya Arubaini na Mbili imefasiriwa na kufafanuliwa kupitia wanazuoni mbali mbali waliofasiri na kuchambua dau za Sahifa Sajjadiyya kwa lugha mbali mbali. Kwa upande wa lugha ya Kiajemi, tafsiri chambuzi ya dua hii sambamba na dua nyenginge za Sahifa Sajjadiya, inapatikana katika vitabu kiitwacho 'Diare Ashiqan' cha Hussein Ansarian pamoja na 'Shuhud wa Shinakht' kilichoandikwa na bwana Hassan Mamduhi Kermanshahi. Ama kwa upande wa lugha ya Kiarabu, katika kitabu 'Riyadh as-Salikin' ni moja ya vitabu maarufu vilivyofanya kazi hiyo kwa lugha ya Kiarabi, kazi ambayo ilikamilika kupitia kalamu ya bwana Sayyid Ali Khan Madani.

Mafundisho Yaliyomo Ndani ya Dua ya Arubaini na Mbili Dua ya Arubaini na Mbili, ambayo ni mojawapo ya dua zilizomo katika kitabu cha Sahifa Sajjadiya, ni ile dua maalumu isomwayo baada ya msomaji wa Qur’ani kuhitimisha kisomo cha Qur'ani yake kikamilifu (yaani baada kuhitimisha Qur’ani nzima). Ndani ya dua hii, Imamu Sajjad (a.s), anatufafanulia kwa kina kabisa sifa bainifu za Qur'ani Tukufu. Vilevile, anatoa uchambua maridadi juu ya athari za Qur'ani Tukufu, kulingana na viwango na mbalimbali hadhi (daraja) mbali mbali za wanadamu (kulingana na hali zao za kiroho). Imamu Sajjad (a.s), Ametufafanulia vya kutosha jinsi Qur’ani inavyoweza kuathia hatima na maisha ya duniani pamoja na Akhera, huku akitilia mkazo lengo la Qur’ani katika kumkurubisha mwanadamu na Mola wake. [1] Mafunzo ya dua ya arubaini na mbili yamekua katika vipengele vifuatavyo: • Qur'ani imeteremshwa katika mfumo wa ufunuo wenye nuru. • Nafasi na dhima ya Qur'ani katika kumwepusha mwanadamu na migawanyiko ya kiitikadi na kumuondolea shaka mbali mbali welewe wake. • Qur'ani ni kigezo pambanuzi (muhaymin) na msimamizi (shahidi) juu ya maandiko matakatifu yaliyotangulia na ndiyo kauli yenye uzito zaidi. • Qur'ani ni kigezo cha kupambanua haki na batili (Furqan) na ni mizani ya uadilifu wa Kiungu. • Qur'ani ni maandiko yenye ubainifu usio na shaka ndani yake, na ni kitabu kilichohifadhiwa dhidi ya upotoshaji. • Qur'ani ni wahyi wa Mwenye Ezi Mungu alioshusiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). • Uongofu umtengao mja kutokana na upotovu, unapatikana kupitia nuru ya Qur'ani. • Sharti za ufanisi wa unufaikaji kamili na Qur'ani, unapatikana kwa kuzingatia hoja zake za kimantiki (burhan), tafakuri ya kina (tadabbur), na usikivu wenye utulivu kwa lengo la kupata mwongozo. • Dua ya kuomba mananikio katika kutekelezaji wa wajibu wa Qur'ani. • Kukiri uhalali wa Aya zenye tafsiri tatanishi (mutashabihat) na kukukubaliana na Aya msingi zilizo wazi (muhkamat) na zielewekanazo bila matatizo. • Ufasaha wa Qur'ani katika muundo wa kilugha mfumo wa maneno pamoja na maana. • Uelewa wa kina wa Qur'ani umefungamana moja kwa moja na tafsiri chmbuzi za Maasumina (a.s). • Ahlul Bayt (a.s) ni wahifadhi na hazina ya elimu ya Qur'ani. • Uwezo wa kiakili wa watu wa kawaida hutofautiana katika kuifasiri Qur'ani. • Kushikamana na kamba thabiti (Urwatul Wuthqa) ya Qur'ani (haki ielezwayo na Qur’ani). • Kutumia Aya msingi (muhkamat) za Qura’ni katika kufasiri zile Aya zenye tafsiri tatanishi (mutashabihat). • Mfungamano usiovunjika kati ya Qur'ani na Ahlul Bait (a.s). • Kuomba kupata shufaa ya Qur'ani. • Kupata msamaha wa dhambi kupitia Qur'ani. • Athari za kuishi kwa mujibu wa mafunzo ya Qur'ani, ni pamoja na; kuishi kwa utulivu katika giza la usiku na kupata utulivu wa kiroho kupitia urafiki wa Qur’ani, kupata kinga dhidi ya maovu, ulinzi dhidi ya vishawishi vya kishetani, udhibiti wa kauli, kuondokana na hali ya kutojitambua (mghafala), ustawi wa kiuchumi, na ukombozi wa kuondoka na itikadi za kikafiri. • Qur'ani ni ngao ya amani na usalama kwa ajili ya Akhera. • Qur'ani ndio njia ya kufikia kilele cha utukufu, na ni hakikisho la wokovu wa Akhera. • Qur'ani ni chombo cha kujitakasa na maovu ya kitabia. • Qur'ani hupunguza masaibu ya sakaratul mauti (wakati wa hekaheka za kutolewa roho). • Ombi la kuombi la kupata amani kutokana na makazi marefu ya kaburini. • Ombi la kumuomba Mungu alifanye kaburi la mja wake kuwa ni sehemu ya makazi bora ya mja, baada ya mja huyo kuyahama makazi duniani na kuingia kaburini. • Ombi la kumuomba Mungu aupanue mwanandani wa kaburi la mja Wake kupitia rehema zake zisizo na kikomo. • Ombi la kuepushwa na aibu mbele ya umma Siku ya Hukumu. • Dua ya kuondolewa mashaka ya maisha yanayofuata baada ya kifo. • Qur'ani ndiyo kinga dhidi ya majonzi na vitisho vya Siku ya Kiyama. • Siku ya Kiyama, nyuso za waonevu zitatawaliwa giza ndani yake. • Dua ya kumuomba Mungu nuru uso wenye nuru, pale waja watakapokuwa katika kisimomo cha Siku ya Majuto (Yaum al-Hasrah), yaani siku ya Kiama. • Kuomba kuepushwa na dhiki za maisha. • Uchamungu (utumishi wa kumtumikia Mungu ipaswavyo), ndio msingi wa ukamilifu wa mwanadamu. • Kukaribiana na nuru ya Qur'ani kunahitaji utekelezaji, sio usomaji pekee. • Dua ya kumtakie amani bwana Mtume (s.a.w.w) kwa kutimiza wajibu wake wa kuufikisha ufunuo wa Mwenye Ezi Mungu kikamilifu. • Hadhi ya bwana Mtume (s.a.w.w), kama Mtume mkuu na mwenye hadhi ya juu zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu. • Isma (utakasifu wa kutotenda dhambi, kutokosea katika otoaji wa maamuzi) wa Mtume (s.a.w.w) katika nyanja zote za unabii wake. • Uvumilivu na subra ya bwana Mtume (s.a.w.w), katika kukabiliana na yale magumu mbali mbali katika kazi ya tabligh. • Dua ya kumpandisha daraja bwana Mtume (s.a.w.w) huko Akhera. • Dua ya kuomba maisha yaendanayo na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), kufariki katika njia ya Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), pamoja na kufufuliwa katika kundi lake (s.a.w.w). • Dua ya kumuomba Mwenye Ezi Mungu ampe Mtume (s.a.w.w.) kheri za kudumu zisizo na kikomo. • Dua ya kumuombea Mtume (s.a.w.w.), malipo ya juu zaidi, kupindukia malipo ya wale Malaika waliokaribu Mwenye Ezi Mungu, na kupindukia malipo Mitume wote. [2]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Arubaini na Mbili Kuna tafsiri kadhaa chambuzi zilizoandikwa kwa lugha mbali mbali, kwa nia ya kutoa tafsiri chambuzi ya dua ya arobaini na mbili, pamoja na dua nyengine zilizomo katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi, kwa ajili ya kuwarahisishia wazungumzaji wa lugha hiyo, ni pamoja na; "Diare ‘Asheghan" kitabu kilichoandikwa na Hossein Ansarian, [3] "Shuhud va Shenakht" kazi iliyofanywa na Mohammad Hasan Mamduhi Kermanshahi, [4] pamoja na “Sherh wa Tarjume Sahife Sajjadiyya” kazi iliofanywa na Sayyed Ahmad Fahri. [5] Zaidi ya hayo, pia kuna makala kadhaa zilizoandikwa na waandishi mbali mbali kurejelea dua hii ya arubaini. Makala hizo ziliandikwa kwa lengo la kuchunguza majina na sifa mbali mbali za Qurani Tukufu. [6] Aidha, kuna juhudi kubwa zilizofanywa katika kazi ya kuifasiri Du'a ya arubaini na mbili ya Sahifa Sajjadiyya kwa lugha ya Kiarabu, pamoja na dua nyengine zilizomo ndani ya kitabu hicho. Miongoni mwa vitabu maarufu vilivyoandikwa kuhusiana na kazi hiyo, ni kile kitabu kiitwacho "Riyadh al-Salikin" kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani. [7] Hata hivyo, hiyo haikuwa ni kazi pekee iliyoandikwa kwa ajili ya watumizi wa lugha ya Kiarabu, bali kuna wanazuoni wengine kadhaa waliochukuwa jukumu la kutumia baadhi ya muda wao muhimu katika kuihudumia shughuli hiyo. Miongoni mwao ni pamoja na; bwana Muhammad Jawad Mughniyya, aliyeandika kitabu kiitwacho "Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyya", [8] mwanazuoni Muhammad bin Muhammad Darabi, mmilikiwa kazi iitwayo "Riyadh al-Arifin" [9], pamoja na mwanazuoni aitwaye Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah, mwandishi wa kitabu kiitwacho "Afak al-Ruh" [10]. Pia wale walikaa kitako kwa ajili ya kufafanua msamiati wa du'a hii sambamba na wa dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya. Waandisi hawa waliukusanya msamiati uliomo ndani ya Sahifa Sajjadiyya kiwa kuuweka katika tungo ya kilugha (kamusi), ili kuwarahisishia watumizi wa kitabu hicho pamoja na wahakiki mbali mbali. Miongoni mwa tungo hizo ni pamoja na; "Ta'liqat 'ala al-Sahifa al-Sajjadiyya" kazi ya mwanazuini aitwaye Fayd Kashani [11] na "Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyya" kitabu kilichoandikwa na bwana Izzu al-Din Jaza'iri. [12]

Matini ya Kiarabu ya Dua ya Arubaini na Mbili Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ عِنْدَ خَتْمِ الْقُرْآنِ Na (ifuatayo) ni moja ya dua zake (amani iwe juu yake), alizokuwa akiomba pale alipotiza kusoma Qur'ani nzima (alipohitimisha Qur’ani). اللَّهُمَّ إِنَّكَ أَعَنْتَنِي عَلَى خَتْمِ كِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَهُ نُوراً، وَ جَعَلْتَهُ مُهَيْمِناً عَلَى كُلِّ كِتَابٍ أَنْزَلْتَهُ، وَ فَضَّلْتَهُ عَلَى كُلِّ حَدِيثٍ قَصَصْتَهُ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe umenisaidia kukihitimisha Kitabu chako, kile ulichokiteremsha kikiwa ni nuru (kwa waja Wako), na ukakifanya kuwa ni msimamizi, mwamuzi na mlinzi juu ya kitabu kitabu ulichokiteremsha (kabla yake), na ukakipa ubora kuliko kila simulizi ulilolisimulia (kwenye maandiko yako mbali mbali).

وَ فُرْقَاناً فَرَقْتَ بِهِ بَيْنَ حَلَالِكَ وَ حَرَامِكَ، وَ قُرْآناً أَعْرَبْتَ بِهِ عَنْ شَرَائِعِ أَحْكَامِكَ وَ كِتَاباً فَصَّلْتَهُ لِعِبَادِكَ تَفْصِيلًا، وَ وَحْياً أَنْزَلْتَهُ عَلَى نَبِيِّكَ مُحَمَّدٍ- صَلَوَاتُكَ عَلَيْهِ وَ آلِهِ- تَنْزِيلًا.

Na (umeiteremsha Qur'ani hii ikiwa ni) Furqani (Pambanuo), ambayo kwayo ulipambanua baina ya halali Yako na haramu Yako; na kwayo ulibainisha wazi sheria za hukumu Zako; nacho ni kitabu ulichokifafanua kwa waja Wako kwa ufafanuzi kamili; na (kitabu hichi ni) Wahyi ambao uliuteremsha kwa Nabii Wako Muhammad – Swala na Salamu Zako ziwe juu yake pamoja na Aali zake – kwa mteremsho maalumu kabisa.

وَ جَعَلْتَهُ نُوراً نَهْتَدِي مِنْ ظُلَمِ الضَّلَالَةِ وَ الْجَهَالَةِ بِاتِّبَاعِهِ، وَ شِفَاءً لِمَنْ أَنْصَتَ بِفَهَمِ التَّصْدِيقِ إِلَى اسْتِمَاعِهِ، وَ مِيزَانَ قِسْطٍ لَا يَحِيفُ عَنِ الْحَقِّ لِسَانُهُ، وَ نُورَ هُدًى لَا يَطْفَأُ عَنِ الشَّاهِدِينَ بُرْهَانُهُ، وَ عَلَمَ نَجَاةٍ لَا يَضِلُّ مَنْ أَمَّ قَصْدَ سُنَّتِهِ، وَ لا تَنَالُ أَيْدِي الْهَلَكَاتِ مَنْ تَعَلَّقَ بِعُرْوَةِ عِصْمَتِهِ.

Na ukakaijaalia (Qur’ani hiyo) kuwa ni nuru, ambayo kwayo tunaongoka kutokana na viza vya upotofu na ujinga kwa kuifuata nuru hiyo. Na tena (ukaijaalia kuwa) ni ponyo kwa yeyote yule anayeisikiliza kwa makini, kwa nia sadikifu lenye lengo la kufikia ufahamu (wa Qur’ani hiyo). Na (imefanya Qur’ani hii kuwa ni) kipimo cha (kupimia) uadilifu, ambayo katu lugha yake haupotoki na kuikengeuka haki. Na (umeifanya kuwa ni) nuru ya uongofu, ambayo katu hoja (nuru) yake hawaizimikii wale wanaoishuhudia (wanaosimama mbele yake). Pia (imeifanya kuwa ni) bendera ya wokovu, ambayo katu hawezi kupotea (haimpotezi) yule mwenye dhamira ya kufuata mwenendo wake, na wala mikono ya maangamizi haimfikii yeyote yule anayeshikamana na mashiko ya hifadhi yake.

اللَّهُمَّ فَإِذْ أَفَدْتَنَا الْمَعُونَةَ عَلَى تِلَاوَتِهِ، وَ سَهَّلْتَ جَوَاسِيَ أَلْسِنَتِنَا بِحُسْنِ عِبَارَتِهِ، فَاجْعَلْنَا مِمَّنْ يَرْعَاهُ حَقَّ رِعَايَتِهِ، وَ يَدِينُ لَكَ بِاعْتِقَادِ التَّسْلِيمِ لِمُحْكَمِ آيَاتِهِ، وَ يَفْزَعُ إِلَى الْإِقْرَارِ بِمُتَشَابِهِهِ، وَ مُوضَحَاتِ بَيِّنَاتِهِ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, kwa kuwa umetuneemesha kwa tawfiki ya kukisoma Kitabu Chako Kitukufu, na ukazilainisha ndimi zetu kwa ufasaha wa ibara zake yake (ufasha wa maneno yake), basi (tunakuomba) utujaalie tuwe ni miongoni mwa wenye kuchunga haki haki zake kikamilifu, na (tuwe ni miongoni mwa wale) wenye kukutii wewe kwa kupitia imani yao ya kusalimu amri mbele ya zile Aya zake zilizowazi na zisizokuwa na mpingamizi (Muhkamat), na (utujaalie tuwe ni miongoni mwa wale) wenye kufanya haraka katika kukiri na kuziamini kwa dhati kabisa, zile aya zake zenye maana ya tatanishi (Mutashabihat), pamoja na kukiri na kuamini (zile Aya) fafanuzi za bayana zake. اللَّهُمَّ إِنَّكَ أَنْزَلْتَهُ عَلَى نَبِيِّكَ مُحَمَّدٍ- صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ- مُجْمَلًا، وَ أَلْهَمْتَهُ عِلْمَ عَجَائِبِهِ مُكَمَّلًا، وَ وَرَّثْتَنَا عِلْمَهُ مُفَسَّراً، وَ فَضَّلْتَنَا عَلَى مَنْ جَهِلَ عِلْمَهُ، وَ قَوَّيْتَنَا عَلَيْهِ لِتَرْفَعَنَا فَوْقَ مَنْ لَمْ يُطِقْ حَمْلَهُ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe uliiteremsha (Qur'ani hii) kwa Nabii wako Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake pamoja na Aali zake) ikiwa katika mkunjo mmoja, (kwa mkunjo wa ujumla). Kisha, ukampa ilhamu (elimu ya ufahamu wa kiufunuo) na kumuelimisha maajabu yake kwa ukamilifu. Nasi ukatrithisha elimu yake, huku ikiwa na tafsiri chambuzi (yenye ufafanuzi kamili), na ukatupandisha daraja, hivyo tukawa juu kuliko wale wasioijua elimu hiyo. Pia, ukatupa nguvu ya kuimudu, ili kutuinua daraja juu ya wale ambao hawakuweza kuubeba uzito wake. اللَّهُمَّ فَكَمَا جَعَلْتَ قُلُوبَنَا لَهُ حَمَلَةً، وَ عَرَّفْتَنَا بِرَحْمَتِكَ شَرَفَهُ وَ فَضْلَهُ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ الْخَطِيبِ بِهِ، وَ عَلَى آلِهِ الْخُزَّانِ لَهُ، وَ اجْعَلْنَا مِمَّنْ يَعْتَرِفُ بِأَنَّهُ مِنْ عِنْدِكَ حَتَّى لَا يُعَارِضَنَا الشَّكُّ فِي تَصْدِيقِهِ، وَ لَا يَخْتَلِجَنَا الزَّيْغُ عَنْ قَصْدِ طَرِيقِهِ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, basi kama vile ulivyozifanya nyoyo zetu kuwa ni chombo chake (kama ulivyozifanya nyoyo zetu kuwa ni wa wachukuzi wa Kitabu chako). Na kwa rehema Zako ukatuarifisha (ukatuelimisha) utukufu wake pamoja na fadhila zake, basi mswalie Muhammad, aliye mhubiri wake, pamoja na Aali zake, walio watunzaji wake. Na utujaalie tuwe miongoni mwa wale wanaokiri kwamba; kitabu hichi ni kitabubu kitokacho Kwako, ili isitokee shaka (fulani) iatakayokua ni pingamizi katika imani ya kukiamini (kitabu Chako), na wala tusije kanganya na upotofu katika lengo la njia yake. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْنَا مِمَّنْ يَعْتَصِمُ بِحَبْلِهِ، وَ يَأْوِي مِنَ الْمُتَشَابِهَاتِ إِلَى حِرْزِ مَعْقِلِهِ، وَ يَسْكُنُ فِي ظِلِّ جَنَاحِهِ، وَ يَهْتَدِي بِضَوْءِ صَبَاحِهِ، وَ يَقْتَدِي بِتَبَلُّجِ أَسْفَارِهِ، وَ يَسْتَصْبِحُ بِمِصْبَاحِهِ، وَ لَا يَلْتَمِسُ الْهُدَى فِي غَيْرِهِ. Ewe Mwenyezi Mungu, mswalie Muhammad na Aali zake. Na utujaalie tuwe miongoni mwa wale wanaojishikiza kwa nguvu kwenye kamba yake (yaani, wanaoshikama na mafunzo ya Qur’ani), na wanaokimbia kutoka kwenye (mitetemo ya) Aya tata (Al-Mutashabihaat), na kutafuta hifadhi ndani ya ngome ya Aya changanifu (Muhkamaat). Na (tujaalie tuwe miongoni mwa wale) wanaopata utulivu chini ya kivuli wa bawa lake. Na (utujaalie tuwe ni miongoni mwa wale) wanaoongozwa na nuru ya pambazuko lake, na wanaofuata mng'ao wa mchomozo wa hoja zake (mwongozo wa Aya zake), na wanaopata mwangaza utokanao na taa yake, na wala hawatafuti uongofu kutoka kwenye chanzo chengine chochote kile kisichokuwa Qur’ani.

اللَّهُمَّ وَ كَمَا نَصَبْتَ بِهِ مُحَمَّداً عَلَماً لِلدَّلَالَةِ عَلَيْكَ، وَ أَنْهَجْتَ بِآلِهِ سُبُلَ الرِّضَا إِلَيْكَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلِ الْقُرْآنَ وَسِيلَةً لَنَا إِلَى أَشْرَفِ مَنَازِلِ الْكَرَامَةِ، وَ سُلَّماً نَعْرُجُ فِيهِ إِلَى مَحَلِّ السَّلَامَةِ، وَ سَبَباً نُجْزَى بِهِ النَّجَاةَ فِي عَرْصَةِ الْقِيَامَةِ، وَ ذَرِيعَةً نَقْدَمُ بِهَا عَلَى نَعِيمِ دَارِ الْمُقَامَةِ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, na kama ulivyomteua Muhammad kuwa ni nembo (bendera) ya uongofu iongozoyo (waja Wako) Kwako, na ukaonesha bayana (wazi) njia ya kupata radhi Zako kupitia Kizazi chake, basi mbariki Muhammad na Aali zake, Kisha uijaalie Qur'ani iwe ni wasila wetu (ni chombo chetu) cha kuelekea kwenye daraja (Zako) adhimu (utukufu), na iwe ni ngazi (yetu) itakayotupaisha hadi kwenye makao makuu yenye amani na utulivu. Kadhalika, (ifanye Qur’ani hii) iwe ndiyo sababu ya kulipwa malipo ya wokovu kwenye uwanja wa Siku ya Kiyama, na kiwe ni kisingizio (kiunganishi) tutachokitumia kwa ajili kunufaika na neema za Dar-ul-Muqama (Makao ya Kudumu).

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ احْطُطْ بِالْقُرْآنِ عَنَّا ثِقْلَ الْأَوْزَارِ، وَ هَبْ لَنَا حُسْنَ شَمَائِلِ الْأَبْرَارِ، وَ اقْفُ بِنَا آثَارَ الَّذِينَ قَامُوا لَكَ بِهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَ أَطْرَافَ النَّهَارِ حَتَّى تُطَهِّرَنَا مِنْ كُلِّ دَنَسٍ بِتَطْهِيرِهِ، وَ تَقْفُوَ بِنَا آثَارَ الَّذِينَ اسْتَضَاءُوا بِنُورِهِ، وَ لَمْ يُلْهِهِمُ الْأَمَلُ عَنِ الْعَمَلِ فَيَقْطَعَهُمْ بِخُدَعِ غُرُورِهِ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mswalie Muhammad na Aali zake. Na uyaporomoshe madhambi yetu (utuondolee uzito wa madhambi) kwa baraka (jaha) ya Qur'ani. Na uturuzuku (Utukirimu) kwa kutupa muonekano (sura) wa watu wema. Na utupe taufiki ya kufuata nyayo za wale waliosimama nyakati za usiku pamoja sehemu za nyakati za mchana kwa ajili Yako, (wakikuabudu) kupitia Qur'ani hiyo. (Tufanyie hisani hiyo), ili ututakase na kila uchafu kwa utakaso wake (kwa utakaso wa Qur’ani). Na utujaalie kufuata nyayo za wale waliotafuta uongofu kupitia na nuru yake, ambao hawakuaacha kutenda mema kwa kupumbazwa na matumaini ya kuishi maisha marefu (ya kidunia), na lau wangelipumbaa, basi hadaa za matumaini yao zingeliwamegua na kuwatenganisha na amali njema na hatima yake wangelifeli katika maisha yao ya Akhera.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلِ الْقُرْآنَ لَنَا فِي ظُلَمِ اللَّيَالِي مُونِساً، وَ مِنْ نَزَغَاتِ الشَّيْطَانِ وَ خَطَرَاتِ الْوَسَاوِسِ حَارِساً، وَ لِأَقْدَامِنَا عَنْ نَقْلِهَا إِلَى الْمَعَاصِي حَابِساً، وَ لِأَلْسِنَتِنَا عَنِ الْخَوْضِ فِي الْبَاطِلِ مِنْ غَيْرِ مَا آفَةٍ مُخْرِساً، وَ لِجَوَارِحِنَا عَنِ اقْتِرَافِ الْآثَامِ زَاجِراً، وَ لِمَا طَوَتِ الْغَفْلَةُ عَنَّا مِنْ تَصَفُّحِ الِاعْتِبَارِ نَاشِراً، حَتَّى تُوصِلَ إِلَى قُلُوبِنَا فَهْمَ عَجَائِبِهِ، وَ زَوَاجِرَ أَمْثَالِهِ الَّتِي ضَعُفَتِ الْجِبَالُ الرَّوَاسِي عَلَى صَلَابَتِهَا عَنِ احْتِمَالِهِ. Ewe Mwenye Ezi Mungu, mswalie (mrehemu) Muhammad na Aali zake, na ifanye Qur'ani iwe ni mfariji wetu katika giza za usiku, na ufanye iwe ni mlinzi wetu dhidi ya uchochezi na hatari za wasiwasi Shetani, na ni hatamu (pingu) ya miguu yetu, ili isipige hatua kwa ajili ya kuyaelekea maasi, na kufuli ya ndimi zetu (ifanye iwe ni kinyamazishi cha ndimi zetu), ili (ndimi hizo) zisizame kwenye mazungumzo ya upuuzi, na (ifanye iwe ni mkemeaji wa viungo vtu), ili (viungo hivyo) isitende maasi, na uifanye iwe ni mfichuzi wa yale mazingatio muhimu yaliyofunikwa na pazia la mghafala wetu. (Tufanyie hisani hizi) hadi zifikishe nyoyo zetu kwenye welewa wa maajabu yake yasiyona kifani, na (hadi uzifikishe kwenye welewa wa kuelewa) nguvu za makemeo ya mifano yake; makemeo ambayo kwayo imedhoofika hata ile milima thabiti, licha ya uimara wake, na ikashindwa kuhimili uzito wa makemeo hayo.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَدِمْ بِالْقُرْآنِ صَلَاحَ ظَاهِرِنَا، وَ احْجُبْ بِهِ خَطَرَاتِ الْوَسَاوِسِ عَنْ صِحَّةِ ضَمَائِرِنَا، وَ اغْسِلْ بِهِ دَرَنَ قُلُوبِنَا وَ عَلَائِقَ أَوْزَارِنَا، وَ اجْمَعْ بِهِ مُنْتَشَرَ أُمُورِنَا، وَ أَرْوِ بِهِ فِي مَوْقِفِ الْعَرْضِ عَلَيْكَ ظَمَأَ هَوَاجِرِنَا، وَ اكْسُنَا بِهِ حُلَلَ الْأَمَانِ يَوْمَ الْفَزَعِ الْأَكْبَرِ فِي نُشُورِنَا.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake, Na udumishe utengemao wa dhahiri yetu (muonekano wetu). Na (tunakuomba) uzikinge dhamira zetu zisipitiwe na mawazo ya wasiwasi kwa jaha na baraka za Qur’ani. Na (tunakuomba) kupitia hadhi na jaha ya Qur’ani, uzitakase nyoyo zetu kutu za dhambi pamoja na mafungamano ya mizigo ya dhambi zetu. Na (tunakuomba) kwa jaha ya Qur’ani hiyo, uyakusanye (utukusanyie) pamoja yale mambo yetu yaliyotawanyika. Na (tunakuomba) kwayo, uzizime zile kiu zetu zitokanazo na joto kali, siku (pale) tutakaposimama mbele Yako kwa ajili ya hukumu. Na (tunakuomba) kwayo, utuvishe vazi la amani siku ya mfazaiko mkuu, wakati wa ufufuo wetu.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْبُرْ بِالْقُرْآنِ خَلَّتَنَا مِنْ عَدَمِ الْإِمْلَاقِ، وَ سُقْ إِلَيْنَا بِهِ رَغَدَ الْعَيْشِ وَ خِصْبَ سَعَةِ الْأَرْزَاقِ، وَ جَنِّبْنَا بِهِ الضَّرَائِبَ الْمَذْمُومَةَ وَ مَدَانِيَ الْأَخْلَاقِ، وَ اعْصِمْنَا بِهِ مِنْ هُوَّةِ الْكُفْرِ وَ دَوَاعِي النِّفَاقِ حَتَّى يَكُونَ لَنَا فِي الْقِيَامَةِ إِلَى رِضْوَانِكَ وَ جِنَانِكَ قَائِداً، وَ لَنَا فِي الدُّنْيَا عَنْ سُخْطِكَ وَ تَعَدِّي حُدُودِكَ ذَائِداً، وَ لِمَا عِنْدَكَ بِتَحْلِيلِ حَلَالِهِ وَ تَحْرِيمِ حَرَامِهِ شَاهِداً.

Ee Mwenye Ezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake. Na tunakuomba utuzibie pengo letu linalotokana na hali ya uhitaji wetu kwa baraka na jaha ya Qur'ani. Na (tunakuomba) kwa baraka ya jaha yeke, utujaalie maisha yenye ustawi na fadhila za wingi wa riziki. Na (kwa baraka ya jaha hiyo tunakuomba) utuweke mbali na sifa chukivu pamoja na maadili duni. Na kwayo tunakuomba utuhifadhi na mporomoko wa kuporomoka ndani ya shimo la ukanushaji (ukafiri) pamoja na vichocheo vya unafiki. (Tupe hisani hizi), ili (Qur’ani Yako) iwe ni nuru kwetu Siku ya Kiyama, na ni muongozo thabiti wa kuielekea ridhaa Yako na bustani Zako za milele. Na katika maisha ya dunia, (ijaaliye Qur’ani hiyo) iwe ni kinga madhubuti dhidi ya ghadhabu Zako, na iwe ni kinga dhidi ukiukaji wa sheria Zako. Na (uijaalie) iwe ni shahidi wako kwa yale yaliyoko Kwako, ambayo tuliyahalalisha kama yalivyohalalisha na Qur’ani, huku mengine tukiyaharamisha kama yalivyoharamishwa na Qur’ani. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ هَوِّنْ بِالْقُرْآنِ عِنْدَ الْمَوْتِ عَلَى أَنْفُسِنَا كَرْبَ السِّيَاقِ، وَ جَهْدَ الْأَنِينِ، وَ تَرَادُفَ الْحَشَارِجِ إِذَا بَلَغَتِ النُّفُوسُ‏ التَّراقِيَ، «وَ قِيلَ مَنْ راقٍ‏» وَ تَجَلَّى مَلَكُ الْمَوْتِ لِقَبْضِهَا مِنْ حُجُبِ الْغُيُوبِ، وَ رَمَاهَا عَنْ قَوْسِ الْمَنَايَا بِأَسْهُمِ وَحْشَةِ الْفِرَاقِ، وَ دَافَ لَهَا مِنْ ذُعَافِ الْمَوْتِ كَأْساً مَسْمُومَةَ الْمَذَاقِ، وَ دَنَا مِنَّا إِلَى الْآخِرَةِ رَحِيلٌ وَ انْطِلَاقٌ، وَ صَارَتِ الْأَعْمَالُ قَلَائِدَ فِي الْأَعْنَاقِ، وَ كَانَتِ الْقُبُورُ هِيَ الْمَأْوَى إِلَى مِيقَاتِ يَوْمِ التَّلَاقِ

Ewe Mwenye Ezi, mbariki Muhammad na Aali zake. Na uzisahilishie nafsi zetu ugumu (uchungu) wa mauti wakati wa kutoka roho, kwa baraka na hadi ya Qur'ani. Na (kwa jaha ya Qur’ani tunakuomba), utuwepesishie taabu ya kuugua (maradhi ya kifo), na mashaka yatokanayo na mkoromo koo ya mtokwaji roho, pale (nafsi) roho ikapo kwenye mifupa ya mwishoni mwa kifua cha mwanadamu (pale ambapo roho hufikia kwenye mitulinga), na ikasemwa: "Nani basi awezaye kumtibu mtokaji roho huyu?" Wakati ambao Malaika wa Mauti (Malakul-Maut) atapojibainisha kutoka kwenye sitara za ulimwengu wa ghaibu, ili aichukue (roho ya mja huyo). Na akampopoa kwa mishale ya khofu ya utengano (wa kutengana na dunia) itokayo kwenye upinde wa mauti. Kisha akakitayarishia kikombe cha sumu kali ya mauti (dhihafu) chenye ladha ya kuangamiza (kuua). Na pale safari na mwelekeo wa kuelekea Akhera inapowadia kutoka kwetu; huku amali zikigeuka kuwa mikufu (ining’iniayo) shingoni (mwa watendaji wake), na makaburi yakawa ndiyo hifadhi hadi miadi ya Siku ya Mkutano (Yawm at-Talāq). اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ بَارِكْ لَنَا فِي حُلُولِ دَارِ الْبِلَى، وَ طُولِ الْمُقَامَةِ بَيْنَ أَطْبَاقِ الثَّرَى، وَ اجْعَلِ الْقُبُورَ بَعْدَ فِرَاقِ الدُّنْيَا خَيْرَ مَنَازِلِنَا، وَ افْسَحْ لَنَا بِرَحْمَتِكَ فِي ضِيقِ مَلَاحِدِنَا، وَ لَا تَفْضَحْنَا فِي حَاضِرِي الْقِيَامَةِ بِمُوبِقَاتِ آثَامِنَا.

Ewe Mwenyezi Mungu, mshushie rehema Zako Muhammad na Aali zake. Na utubariki wakati wa kwenye makazi kaburini mwetu (kwenye nyumba ya uchakavu/kongeshaji), na uturehemu (utubariki tukiwa) katika makazi ya muda mrefu tukiwemo baina ya tabaka za ardhini. Na jaalia makaburi yetu tutakayobaki ndani yake baada ya kuachana na dunia, yawe ni makazi ya kheri. Na utupanulie ule mwanandani wa kaburi ulio mwembamba, kwa fadhila za Rehema Zako. Pia, usitufedheheshe mbele ya hadhara ya Siku ya Kiyama kwa maovu maangamizi yatokanayo na dhambi zetu. وَ ارْحَمْ بِالْقُرْآنِ فِي مَوْقِفِ الْعَرْضِ عَلَيْكَ ذُلَّ مَقَامِنَا، وَ ثَبِّتْ بِهِ عِنْدَ اضْطِرَابِ جِسْرِ جَهَنَّمَ يَوْمَ الْمَجَازِ عَلَيْهَا زَلَلَ أَقْدَامِنَا، وَ نَوِّرْ بِهِ قَبْلَ الْبَعْثِ سُدَفَ قُبُورِنَا، وَ نَجِّنَا بِهِ مِنْ كُلِّ كَرْبٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَ شَدَائِدِ أَهْوَالِ يَوْمِ الطَّامَّةِ

Na uturehemu kwa baraka za Qur'ani tukufu (hali tukiwa) katika kile kisimamo chetu dhalili, cha kuanikwa kwa amali (zetu) tukihesabiwa mbele Yako. Na iimarishe miguu yetu kwa baraka na jaha ya Qur’ani, ili isiteleze wakati wa mtetemo wa daraja la Jahannam, Siku ya kulivuka daraja hizo. Na yamurike makaburi yetu kwa nuru ya Qur’ani, kabla ya kuingia Siku ya Kiama, (ili tuneemeke na nuru ya Qur’ani kabla ya Siku ya Kiama). Na kwa Qur'ani, utuokoe na kila dhiki ya Siku ya Kiyama na mashaka ya vitisho vya Siku ya Msiba Mkuu. وَ بَيِّضْ وُجُوهَنَا يَوْمَ تَسْوَدُّ وُجُوهُ الظَّلَمَةِ فِي يَوْمِ الْحَسْرَةِ وَ النَّدَامَةِ، وَ اجْعَلْ لَنَا فِي صُدُورِ الْمُؤْمِنِينَ وُدّاً، وَ لَا تَجْعَلِ الْحَيَاةَ عَلَيْنَا نَكَداً. Na zing'arishe (zinawirishe) nyuso zetu Siku ambayo nyuso za madhalimu zitatandwa na giza (zitakuwa nyeusi), (nalo ni tukio litakalotokea) katika Siku ya Majuto na Masikitiko. Na utujaalie mapenzi yate yanawiri ndani nyoyo za waumini (Padikiza mapenzi yetu ndani ya nyoyo za Waumini), na wala usiyafanye maisha yetu kuwa na dhiki.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ عَبْدِكَ وَ رَسُولِكَ كَمَا بَلَّغَ رِسَالَتَكَ، وَ صَدَعَ بِأَمْرِكَ، وَ نَصَحَ لِعِبَادِكَ.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mbariki Muhammad, ambaye ni mja na mjumbe wako, kwa ile jitihada yake ya kutekeleza jukumu la kuwasilisha utume wako ipaswavyo, akaipambanua amri yako kwa uwazi (kama ilivyotakiwa), na akatoa miongozo ya kheri kwa viumbe vyako. اللَّهُمَّ اجْعَلْ نَبِيَّنَا- صَلَوَاتُكَ عَلَيْهِ وَ عَلَى آلِهِ- يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَقْرَبَ الْنَّبِيِّينَ مِنْكَ مَجْلِساً، وَ أَمْكَنَهُمْ مِنْكَ شَفَاعَةً، وَ أَجَلَّهُمْ عِنْدَكَ قَدْراً، وَ أَوْجَهَهُمْ عِنْدَكَ جَاهاً.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mjaalie Nabii wetu (Swala na Salamu Zako zimwendee yeye na Aali zake), awe na daraja ya ukaribu zadi kwako Siku ya Kiama kuliko madabii wengine wote. Mfanya awe ndiye mwenye uwezo wa shufaa yenye nguvu zaidi mbele Yako, mwenye hadhi tukufu zaidi mbele Yako, na mwenye jaha adhimu zaidi mbele ya hadhira Yako. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ شَرِّفْ بُنْيَانَهُ، وَ عَظِّمْ بُرْهَانَهُ، وَ ثَقِّلْ مِيزَانَهُ، وَ تَقَبَّلْ شَفَاعَتَهُ، وَ قَرِّبْ وَسِيلَتَهُ، وَ بَيِّضْ وَجْهَهُ، وَ أَتِمَّ نُورَهُ، وَ ارْفَعْ دَرَجَتَهُ

Ewe Mwenye Ezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake. Itukuze hadhi ya (bunyan) ya utume wake (itukuze hadhi yake), utukuze uthibitisho wake (dalili zake), na uitie uzito mizani ya amali zake Siku ya Malipo. Na uyakubali maombezi yake (shufaa yake), na mrahisishie njia yake ya kupata ukuruba Nawe. Unawirishe uso wake, na umkamilishei nuru yake, na uinue daraja yake. وَ أَحْيِنَا عَلَى سُنَّتِهِ، وَ تَوَفَّنَا عَلَى مِلَّتِهِ وَ خُذْ بِنَا مِنْهَاجَهُ، وَ اسْلُكْ بِنَا سَبِيلَهُ، وَ اجْعَلْنَا مِنْ أَهْلِ طَاعَتِهِ، وَ احْشُرْنَا فِي زُمْرَتِهِ، وَ أَوْرِدْنَا حَوْضَهُ، وَ اسْقِنَا بِكَأْسِهِ

Na utujaalie uhai wenye kushikamana na Sunna zake, na uzichukue roho zetu tukiwa katika mila (dini) yake. Tuongoze kwenye mwenendo wake, na utupitishe katika njia yake (tupitishe kwenye mapito yako). Tufanye tuwe miongoni mwa watu kwake, na utufufue tukiwa katika kundi lake. Tufikishe kwenye hodhi lake, na utunyweshe kwa kikombe chake. وَ صَلِّ اللَّهُمَّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، صَلَاةً تُبَلِّغُهُ بِهَا أَفْضَلَ مَا يَأْمُلُ مِنْ خَيْرِكَ وَ فَضْلِكَ وَ كَرَامَتِكَ، إِنَّكَ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ، وَ فَضْلٍ كَرِيمٍ.

Na Ewe ewe Mwenye Ezi Mungu, mbariki Muhammad na Aali zake; baraka ambazo kwazo utamwezesha kufikia kilele cha matumaini yake anayoyatarajia kutoka katika kheri Zako, fadhila Yako na ukarimu Wako. Kwa hakika, Wewe ndiwe Mwenye kumiliki Rehema kunjufu na Fadhila adhimu. اللَّهُمَّ اجْزِهِ بِمَا بَلَّغَ مِنْ رِسَالاتِكَ، وَ أَدَّى مِنْ آيَاتِكَ، وَ نَصَحَ لِعِبَادِكَ، وَ جَاهَدَ فِي سَبِيلِكَ، أَفْضَلَ مَا جَزَيْتَ أَحَداً مِنْ مَلَائِكَتِكَ الْمُقَرَّبِينَ، وَ أَنْبِيَائِكَ الْمُرْسَلِينَ الْمُصْطَفَيْنَ، وَ السَّلَامُ عَلَيْهِ وَ عَلَى آلِهِ الطَّيِّبِينَ الطَّاهِرِينَ وَ رَحْمَةُ اللهِ وَ بَرَكَاتُهُ. Ee Mwenye Ezi Mungu, tunakuomba umlipe (mtume Wako Muhammad) (s.a.w.w), kutokana na zile juhudi za uwasilishaji wake wa maagizo Yako (ujumbe Wako), pia kutokana na zake juhudi zake za utoaji wa nasaha kwa viumbe Wako, na kutokana na juhudi zake za mapambano yake katika njia Yako. (Tunakuomba) ujira mkubwa ulioje, ujira ambao hujawahi kumlipa yeyote yule miongoni mwa Malaika Wako Wateule (Muqarrabin), wala yoyote yule miongoni mwa Manabii Wako Al-Mursalina (uliowatuma kwa viumbe wako) waliochaguliwa (kwa ajili ya kazi Yako). Na (tunamuombea) mani imshukie yeye (Muhammad) pamoja na Aali zake watoharifu, (imani yenye kufungamana na) na rehema na baraka za Mwenye Ezi Mungu.