Harakati za Imamu Hussein (a.s)

Kutoka wikishia

Harakati za Imam Hussein (a.s) (Kiarabu: قيام الإمام الحسين(ع)) zilikuwa ni harakati za Imamu Hussein (a.s) dhidi ya utawala wa Yazid bin Muawiya ili kuonesha upinzani wake dhidi ya utawala huo. Harakati hizi ndizo zilisababisha kuuawa kwake shahidi pamoja na wafuasi wake mnamo tarehe 10 Muharram mwaka wa 61 Hijiria, na kuishia kutekwa wa familia yake ndani ya tukio hilo. Harakati hizi zilianza kwa kukataa Imam Hussein (a.s) kutoa kiapo cha utiifu cha kumtambua Yazid mbele ya gavana wa Madina ambaye ni mwakilishi wa Yazid. Jambo hili lilifungua ukurasa mpya wa tarehe ambapo Imamu Hussein (a.s) aliondoka Madina mnamo Rajab mwaka wa 60 Hijiria yeye na familia yake, na hatima ya safari hii ilimalizika kwa kurudi kwa mateka mjini Madina.

Harakati za Imam Hussein (a.s) zilipelekea kuzuka kwa harakati kadhaa dhidi ya utawala wa Bani Umayyah, na ikawa ndio sababu ya kuanguka kwake. Waislamu wa madhehebu ya Shia kila mwaka huadhimisha tukio hili kwa maadhimisho yenye sura mbalimbali. Uenezaji wa mila za maombolezo, kufunguliwa kwa ukurasa maalumu wa fasihi inayo husiana na tukio la Ashura, ujenzi wa majengo na maeneo ya kidini, uzalishaji wa kazi za sanaa na kuimarisha roho ya kupingana na dhuluma, ni baadhi ya athari za tukio hili ndani ya jamii na tamaduni za Shia.

Lengo kuu la Imam Hussein (a.s) katika kwa harakati zake hizi, kama inavyokuja katika wosia wake kwa Muhammad bin Hanafiyyah; lilikuwa ni kuirudisha jamii ya Kiislamu kwenye njia sahihi na kupambana na upotoshaji. Hata hivyo, kuunda serikali, kuuawa, kuhifadhi maisha na kukataa kutoa kiapo cha utiifu kwa Yazid pia zimehesabiwa kuwa ni miongoni mwa malengo yake. Baada ya kuandikwa kwa kitabu kiitwacho Shahidel Javid na kujadiliwa sula la Imamu Hussein kuunda serikali kama ndio lengo kuu la harakati zake, ambapo waandishi kadhaa walianza kuandika na kujaribu kuelezea dhana ya za Imamu Hussein (a.s). Baada ya waandishi wa Shia kujadili na kukusoa dhana zilizomo katika kitabu “Shahide Javid”, mjadala wa lengo la Harakati za Imam Hussein (a.s) uliingia katika uwanja mpa juu tafiti za tukio la Ashura, ambapo nadharia tofauti zilijitokeza katika uwanja huu. Kujitolea muhanga na kufa kishahidi na kuunda serikali adilifu ndio natija bora na muhimu zaidi zilizo fikiwa kupitia tafiti hizo.

Tukio la Ashura

Tukio la Karbala linahusiana na vita kati ya Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake dhidi ya jeshi la watu wa Kufa tukio ambalo lilitokea mwezi wa Muharram mwaka wa 61 Hijiria. Tukio hili, ambalo lilijiri baada ya Imam Hussein (a.s) kukataa kutoa kiapo cha utiifu cha kumtambua Yazid bin Muawiya kama ni Khalifa wa Waislamu, lilisababisha kuuawa kwa Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake, na hatimae kutekwa wa familia yake. Imam Hussein (a.s) alitoka Madina mnamo mwezi wa Rajab mwaka wa 60 Hijiria, pamoja na familia yake akiwa pamoja na idadi ya watu kutoka katika koo ya Bani Hashim. [2] Alifanya hivyo ili aepuke kutoa kiapo cha utii kwa gavana wa Madina cha kumtambua Yazid bin Muawia kama ni Khalifa halali.

Alikaa Makkah kwa takriban miezi minne, wakati ambao alipokea barua nyingi za mwaliko kutoka kwa watu wa Kufa, [3] jambo ambalo lilimfanya aamue kwenda mjini Kufa mnamo mwezi 8 Dhul-Hijjah. [4] Kabla ya kufika mjini Kufa, aligundua kwamba watu wa Kufa tayari wamesha msaliti. [5] Akiwa njiani kuelekea mji huo, alikutana na jeshi la Hurr bin Yazid al-Riyahi, na kulazimika aelekee Karbala, ambapo alikutana na jeshi lililoletwa na Ubaydullah bin Ziyad. [6] Majeshi mawili yalipigana tarehe 10 Muharram. Baada ya Imam Hussein na wafuasi wake kuuawa, waathirika wake (walio salimika na kifo) walichukuliwa mateka. [7]

Mazingira ya Chanzo cha Harakati

Baadhi ya watafiti wameona kwamba mazingira na sababu kuu iliyo pelekea harakati za Imam Hussein (a.s) ni kupotea kwa jamii ya Kiislamu na kutoweka kwa imani na maadili ndani ya jamii ya Waislamu. [8] Kwa sababu katika kipindi cha Bani Umayyah, maadili ya kijahilia na ya kikabila yalishamiri na kupata nguvu, [9] na pia tofauti za kikabila, hasa tofauti kati ya Bani Hashim na Bani Umayyah, zilishamiri tena upya. [10]

Pia, kuteuliwa kwa Yazid na Muawiya kama Khalifa na msisitizo wa Yazid kwa Imam Hussein (a.s) wa kumlazimisha kutoa kiapo cha utiifu, ni miongoni mwa sababu na mazingira yaliyo pelekea kuibuka kwa harakati hizi. Imam Hussein (a.s) hakumchukulia Yazid kuwa mtu mwenye kufaa katika nafasi ya ukhalifa, na hakuona uteuzi wake kuwa ni uteuzi halali. Kwa sababu ilikuwa ni kinyume na mkataba wa Imam Hassan (a.s) na Muawiya, kwani mkataba huo ulisema kwamba Muawiya hakuwa na haki ya kutawalisha mwengine yeyote yule atakaye shika nafasi ya Ukhalifa baada ya kifo chake. [11]

Malengo na Mipango ya Harakati

Kulingana na Muhammad Esfandiari mwanahistoria (aliyezaliwa mwaka 1959 Shamsia) katika kitabu "Ashuraa Shenasi", ni kwamba lengo kuu la Imam Hussein (a.s) katika Harakati za Ashura, ilikuwa ni kutetea haki, kuamrish mema na kukataza mabaya, kuhuisha Sunna na kuondoa bid'ah. [12] Pia Ayatullahi Khamenei amesema: Lengo la Imam Hussein (a.s), lilikuwa ni kurudisha jamii ya Kiislamu kwenye njia sahihi na kupambana na upotovu mkubwa. [13] Kwa maoni yake ni kwamba kumepita mchanganyo kati ya malengo na natija (matokeo). Kwani kuna tofauti kati ya lengo na matokeo, kwa sababu matokeo ya lengo hili ilikuwa ni kuunda serikali au kuuawa, hali ya kwamba kuna baadhi wanao amini kwamba mawili haya ni malengo ya Imam Hussein (a.s). [14] Ayatullah Jawadi Amuli mmoja wa wanazuoni wakuu wa Shia wenye mamlaka ya kufutu ya kifiqhi, anaamini kwamba; kuelewa tukio la Karbala na kuzifahamu harakati adhimu za Imam (a.s) kunahitaji bidii na jitiha kubwa, na haiwezekani kwa kila mtu kuwa na uweza kufikia kiwango hicho cha welewa. Kwani baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), walichofanya maadui kwanza kabisa, ilikuwa ni kuteka Qur'an pamoja na dini ili kuifasiri na kuiwasilisha mble ya jamii kulingana na matamanio matakwa yao. Hivyo basi ikawa ni vigumu kwa damu ya wanadamu wa kawaida kuweza kuikomboa Qur'an na dini kutoka katika mikononi mwa utumwa wa maadui hao, Hussein bin Ali (a.s) kwa damu yake aliweza kuubadilisha ujahilia kuwa na kuwa ni akili ya mafunzo ya kiungu na kuokoa dini ya asili kutokana na uharibifu na utumwa. [15]

Kulingana na maelezo ya Esfandiari, mjadala kuhusu lengo la Imam Hussein (a.s) ulianza rasmi baada ya kuchapishwa kwa kitabu Shahide Javid. [17] Yeye anaamini kwamba; kumepita mchanganyo wa dhana mbili (malengo na mipango) kwenye utafiti wa harakari za Imamu Hussein (a.s), kwani kuna tofauti kati ya lengo na mipango ya Imam Hussein (a.s). Akifafanua masuala mawili hayo, amesema kwamba; mipango ya Imam Hussein (a.s) ni kufikia lengo lake kuu. Kwa hiyo mipango ya huhisabiwa ni malengo yake yenye daraja la pili, ambayo alikuwa akiyatumia kufia lengo lake kuu. Bwana Esfandiari amekusanya maoni saba katika uchambuzi wake juu ya jambo hili. [18]

Kukataa Kutoa Kiapo kwa Lengo la Kuhifadhi Maisha Make

Kulingana na mtazamo huu, harakati za Imam Hussein (a.s) kutoka Madinah hadi Makka na kisha kuelekea Kufa, hazikuwa na nia ya kusimama dhidi ya Yazid, bali zilikuwa na nia ya kujihami na kuonesha kutoridhika kwake na utawala wa Yazid. Kwa kuwa alikuwa akikataa kutoa kiapo cha utiif kwa Yazid, siku zote maisha yake yalikuwa hatarini, kwa hivyo aliondoka Madina na kisha akauhama mji wa Makka ili kujilinda na mauti. [19] Ali-Panah Isfahani [20] na Muhammad Sihhatiy Sardari [21] ni watetezi wa mtazamo huu. Kukubali mtazamo huu kumeonekana kuwa ni kuua ushujaa na kuidhoofisha hadhi na cheo cha Imam Hussein (a.s). [22]

Kuunda Serikali

Kulingana na mtazamo huu, Imam Hussein (a.s) alianzisha dhidi ya Yazid bin Muawia, kwa ajili au kwa nia ya kuunda serikali. Ni’imatullahi Salihi Najafuabadiy (aliyeishi kati yam waka 1923 na 2006 Shamsia) ameeleza katika kitabu chake kiitwacho Shahide Javid akisema kwamba; lengo kuu la Imam Hussein (a.s) katika msimamo wake dhidi ya Yazaid ni kuunda serikali. [23] Yeye anaamini kwamba; hata Sayyid Murtadha ambaye ni mwanatheolijia wa Kihsia pia naye anashikilia mtazamo huou hayo. Said Murtadha, akitoa maoni yake juu ya suala hili, ameelelea akisema kwamba; Imamu Hussein (a.s) alikubaliana na wito wa watu wa Kufa baada ya kuona uwezo wao na udhaifu wa serikali ya Kufa. [24] Kwa Imani ya Sayyid Murtadha ni kwamba; sababu za kushindwa kwa Imam Hussein (a.s) zilitokana na matukio ya baadaye ambayo hayakutarajiwa. Pale Imamu Hussein (a.s) alipobaini kwamba; watu wa Kufa walikuwa wamevunja ahadi zao, aliamua kurudi na kuachana na dhamira ya mapigano, kama vile alivyo fanaya Imamu Hassan (a.s). Hata hivyo wazo hili halitimia, kwa sababu maadui zake walilazimisha mapigano hayo kutokea. [25] Imeelezwa ya kwamba; dhana na fikra hii haiendani na dhana ya elimu ya ghaibu ya Imamu Hussein (a.s). Kwa sababu hii itapelekea iaminike ya kwamba; Imamu Hussein (a.s), hakuwa na elimu juu ya matukio maafa na kuto faulu kwake katika mapambano hayo. Katika kujibu ukosoaji huu, imesemwa ya kwamba; Imamu Hussein (a.s), alikuwa akijua fika kuhusiana na matukio na natija ya mapambano yake, ili yeye alikuwa akifuata amri ya Mungu, imtakayo yeye kuamiliana na ulimwengu katika hali ya kawaida, na si kupitia njia za kimiujiza. [26]

Kufa Shahidi

Baadhi wanaamini ya kwamba; Lengo la Imamu Hussein (a.s) katika msimamo wake dhidi ya Yazid, ni kufa shahidi, ila kifo hichi cha kishahidi kimefasiriwa kwa namna mbali mbali:

 • Kufa shahidi kisiasa: Kulingana na nadharia hii, Imamu Hussein Hussein (a.s) ameamua kufa kishihidi ili kifo kiwe ni nyenzo ya kufuta uhalali wa serikali ya Yazid, na hatimaye kuitokomeza sarikali hiyo kupitia nguvu za silaha ya damu yake, na kuuokoa Uislamu kutoka mikononi mwa Bani Umayyah. [27] Kulingana na nadharia hii, kifo cha Imamu kiliibua wimbi la wanajamii kuinuka na kusimama dhidi ya serikali. [28] Kulingana na maelezo ya Muhammad Isfandayari, hii ndio nadharia mashuhuri zaidi yenye kutetewa na yenye wafuasi wengi zaidi miongoni mwa wanazuoni na wahakiki mbali mbali. [29] Miongoni mwa wanazuoni wanaoshikamana na nadharia hii ni; Ali Shariati, Mirza Khalili Kumrei, Murtadha Mutahhari, Sayyid Ridha Sadri, Jalalu al-Ddini Farisi, Sayyid Muhsin Amini, Hashim Ma’arufu al-Hussani, Ayatullahi Gulpeigani na Muhammad Jawadu Mughniyah. [30]
 • Kifo cha kishahidi chenye nia ya ugombozi: Baadhi wanaamini kwamba Imam Hussein (a.s) alikufa shahidi ili awe ni njia ya kugomboka kwa watenda dhambi, na ili wapate shufaa kupitia kwake na waweze kufikia kwenye daraja za juu za kiroho mbele ya Mola wao. [31] Kama vile katika Ukristo kuhusu kuuawa kwa nabi Isa (a.s), pia baadhi Waislamu wana maoni kama hayo kuhusiana na Imamu Hussein (a.s). [32] Sharif Tabātabāʾī, Mullah Mehdi Nārāqī, na Mullah ʿAbd al-Raḥīm Isfahānī ni miongoni mwa wanaoamini nadharia hii. [33] Pia, kwa maoni ya baadhi wanazuoni, Imam Hussein aliuawa ili watu wamlilie na kupita njia hiyo waweze kuongoka na kuelekea kwenye njia ya haki. [34]
 • Kifo cha kishahidi (cha kiirfani) cheye nia ya kufikia daraja za kiroho: Kulingana na mtazamo huu, Imam Hussein (a.s) alisimama dhidi ya utawala wa Yazidi ili kufikia neema na daraja ya kirokho ya (daraja ya shahidi). [35] Na kuwafikisha wengine (wafuasi wake) kwenye neema na daraja hii. [36] Katika tafsiri hii, hakuna neno la mapambano ndani yake, bali nadharia inachambua na kutafiti msimamo wa kisiasa katika harakati za Imamu Hussein (a.s) dhidi ya Yazid, bila ya kuangaza harakati hizo kwa jicho la kimapambano. [37] Sayyid bin Tāwūs, Fāḍhil Darbandī, Ṣafī Ali Shāh, ʿOmaan Samānī, na Nayyir Tabrizi, ndiwo waliotoa tafsiri hii ya kiroho ya kuhusiana harakazi za Imam Hussein (a.s.) na msimamo wake dhidi ya Yazidi. [38]
 • Kifo cha kishahidi cha wajibu wa kisheria: Baadhi wanautambulisha msimamo wa Imam Hussein (a.s) dhidi ya Yazid, kama ni msimamo uliojaa siri. Wao wanaamini kwamba Imamu Hussein (a.s), aliagizwa na Mwenyezi Mungu kujitoa muhanaga na kufa shahidi, lakini lengo hasa la kitendo hicho hakiko wazi kwa wanadamu, na siri yake anaijua Mwenye Ezi Mungu peke yake. [39]

Katika kukosoa nadharia hii imesemwa ya kwamba: Nadharia hii haiendani na vielelezo vya kihistoria kuhusiana na harakati za Imamu Hussein (a.s). Kwani kulingana na vielelezo hivyo ni kwamba yeye alikuwa ajitetea na hakuwa tayari kupoteza roho yake. [40]

Utawala na Kifo cha Kishahidi

Baadhi wanaamini kuwa; msamamo wa Imamu Hussein (a.s) wa kusimama dhidi ya utawala wa Yazid, ulikuwa na malengo mawili sambamba, nayo ni kushika hatamu za utawala pamoja na kufa kishahidi. Kwa mujibu wa maoni haya; Imamu Hussein (a.s) alisimama kwa lengo la kuunda serikali. Lakini alipokata tamaa kutokana na kukosekana kwa waungaji mkono na washirika katika kulifikia lengo hli, lengo lake hili lilibadilika na kuelekea kwenye lengo namba mbili, ambalo ni kufa kishahidi. [41]

Wengine pia wanaamini kwamba, lengo lake la kisiasa lilikuwa limepangwa kwenye hatua nne; Hatua ya kwanza ni kutoka Madina hadi Makka, ambayo ina sifa ya kupinga utawala wa Yazid. Hatua ya pili ni muondoko wake kutoka Makka kwenda Kufa hadi kukutana na jeshi la Hurr, ambalo lilikuwa na lina nia ya kuteka mji wa Kufa na Iraq. Hatua ya tatu ni kukutana na jeshi la Hurr hadi kupambana na jeshi la watu Kufa, ambalo lilidhamiria kumkimbia Ibn Ziyad, na hatua ya nne ni wakati wa kukutana na jeshi la Kufa kwenye ardhi ya Karbala, ambapo alichagua kufa kishahidi. [42]

Athari na Natija ya Kifo cha Imamu Hussein (a.s)

Msimamo wa Imamu Hussein (a.s) ulipelekea kupatikana natija kadhaa, miongoni mwazo ni:

Kuhuika kwa Uislamu na Sunna za Bwana Mtume

Baadhi ya waandishi wameona kuwa athari na natija muhimu zaidi katika harakati na msimamo wa Imamu Hussein (a.s) yalio patikana baada ya kifo chake, ni kuhuika upya kwa Uislamu. [43] Kwa mujibu wa maoni ya Imamu Khomeini, ni kwamba; Kama tukio la Karbala halingefanyika, basi Yazid bin Muawiya angeli uakisi Uislamu na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w) katika picha mbaya. [44]

Kuundwa kwa Harakati za Kupinga Utawala wa Bani Umayyah

Baada ya kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s), harakati za kupinga utawala wa Bani Umayyah zilianza. Kulingana na maelezo ya kitabu Taarikhu Tabari, ni kwamba; Hatua za mwanzo dhidi ya utawala wa Bani Umayyah zilianzishwa mwaka wa 61 Hijiria, ambapo baada ya kuuawa Imamu Hussein (a.s), watu walisimama dhidi ya serikali na waliendelea kufanya hivyo hatua kwa hatua kwa nia ya kulipiza kisasi kutokana na mauaji hayo. [45] Maandamano ya kwanza yalikuwa ni makabiliano kati ya Abdullah bin Afif al-Azdi na Ibn Ziyad. Yeye (Abdullah bin Afif) alikuwa msikiti wa Kufa ambapo alimsikia Ibn Ziyad akitoa hotuba ambayo ndani yake alimsifu Imamu Hussein (a.s) kwa sifa ya mwongo, na akamwita yeye na baba yake kuwa ni waongo. [46] Pia, kulingana na ripoti ilioko katika kitabu kiitwacho Taarikhu Sistan, watu wa Sistan waliasi dhidi ya mtawala wa Sistan, ambaye alikuwa ndugu wa Ubaydullah bin Ziyad, tokio hilo lilitokea baada ya wao kusikia habari za kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s). [47] Watu wa Madina pia waliasi dhidi ya utawala wa Yazid bin Muawiya mwaka wa 63 Hijiria, wakiongozwa na Abdullah bin Handhala bin Abi A’mmar. [48] Ali bin Hussein al-Masudi, mwanahistoria wa karne ya nne, anaamini kuwa mauaji ya Imamu Hussein (a.s) yalikuwa ni moja ya sababu za uasi wa watu wa Madina dhidi ya utawala wa Yazid. [49]

Qiamu al-Tawwaabina (Uasi wa Waliotubia)

Makala Asili: Harakati ya Tawwaabina

Qiamu al-Tawwaabina (Uasi wa Waliotubia): Ulianza baada ya tukio la Ashura kwa lengo la kulipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s) akiwa pamoja na mashujaa wa Karbala, uasi ambao ulifanyika mnamo mwaka wa 65 Hijiria, chini ya uongozi wa Suleyman bin Zurad al-Khuza'i. [50] Wakati jeshi la Tawwaabina lilipofika Karbala, walishuka kutoka kwenye farasi wao na kwa huzuni kubwa wakaliendea kaburi la Imamu (a.s) kwa kilio na kuunda mkutano wenye shauku kubwa. [51] Suleyman alisimama miongoni mwao akasema: Ewe Mungu, wewe ni shahidi kwamba sisi tuko kwenye dini na njia ya Hussein (a.s) na ni maadui wa wauaji wake. [52]

Uasi wa Mukhtar

Makala Asili: Harakati ya Mukhtar

Mukhtar al-Thaqafi alianzisha uasi mwaka wa 66 Hijiria kwa lengo la kulipiza kisasi kutokana na mauwaji Imamu Hussein (a.s) na mashujaa wa Karbala. Uasi huu uliungwa mkono na Waislamu wa Kufa. [53] Mukhtar alitumia kauli mbiu mbili katika uasi wake: Ya Lithaarati al-Hussein (یا لثارات الحسين) (Enyi wenye kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Hussein) na Ya Mansuru Amit (یا منصور اَمِت) (Ewe Manusuriwa uwa). [54] Katika uasi huu, watu wengi waliohusika na tukio la Karbala waliuawa, wakiwemo Ubaydullah bin Ziyad, Omar bin Saad, Shimr bin Dhu al-Jawshan na Kholi. [55]

Uasi wa Zaid bin Ali

Makala Asili: Harakati ya Zaid bin Ali

Uasi wa Zaid bin Ali ulianza mwaka wa 122 Hijiria dhidi ya utawala wa Bani Umayyah. Zaid kupitia msaada wa wafuasi 15,000 kutoka Kufa, alitangaza mapinduzi dhidi ya Khalifa Hisham bin Abdulmalik mwaka huo. Sheikh Mufid, mmoja wa wanazuoni wa Shia, anaamini kwamba; Lengo kuu la ghasia za Zaid bin Ali dhidi ya utawala wa Bani Umayyah, lilikuwa ni kulipiza kisasi kutokana na kifo cha Imamu Hussein (a.s). [56]

Athari na Mapambano ya Karbala katika Kuanguka kwa Bani Umayyah

Uasi wa Karbala ulikuwa na athari muhimu katika kuanguka kwa Bani Umayyah. Hii ni kwa sababu watu waliamini kuwa Bani Umayyah walikuwa na hatia katika tukio la Karbala. Imamu Hussein (a.s) pia katika mapambano hayo dhidi ya utawala wa Yazid alitumia maneno kadhaa yalio weze kuweka wazi uhalisia wa mapambano hayo. Miongoni mwa maneno yake (a.s) kama vile: "’Ala al-Islamu Salamu". Yenye maana ya kwamba; (kama Yazid atashika utawala! Basi Uslamu nao utatoweka). Pia Imamu Hussein alieleza kwamba; Yazid alikuwa ni mfugaji mbwa na mnywa pombe, ibara ambayo ilionesha udhaifu wa utawala wake pamoja wa Bani Umayyah kwa jumla. [57]

Pia harakati za kimapinduzi za Abbasiyyina dhidi ya Bani Umayyah, zilisifiwa na wanaharakati wake kuwa ni harakati zenye nia ya kulipiza kisasi kutokana na mauaji ya Imamu Hussein (a.s). [58]

Athari za Mapinduzi ya Karbala kwenye Jamii ya Shia

Harakati za Imamu Hussein (a.s) zilikuwa na athari kubwa kwa jamii ya Shia. [59] Athari hizi ni pamoja na:

Kuenea kwa mila za maombolezo

Makala Asili: Maombolezo ya Muharamu

Maombolezo na kumlilia Imamu Hussein (a.s.) pamoja na mashujaa wa Karbala ni mojawapo ya mambo yanayounda utambulisho wa jamii ya Shia duniani. [60] Kulingana na ripoti za kihistoria, maombolezo yalianza muda mfupi baada ya tukio la Karbala na kwa msisitizo shinikizo kutoka kwa Maimamu wa Shia. Hata hivyo, kugeuka kwake kutoka katika picha ya vitendo vya kibinafsi hadi kuchukua picha ya maadhimisho ya kijamii na kiumma ni matokeo yaliofuatia baada ya utawala wa Aali-Bueih kushika serikali. [61] Kulingana na maelezo ya Ibnu Kathir, Mnamo mwaka wa 359 Hijiria katika siku ya kuadhimisha tukio la Ashura, Mashia walifunga maduka yao na kuelekea kwenye maadhimisho ya maombolezo. [62] Maombolezo ya kuomboleza maafa ya Imamu Hussein (a.s) ni ya kawaida hasa katika siku kumi za mwanzo za mwezi wa Muharram. Katika maadhimisho haya Mashia katika nchi mbalimbali, huadhimisha tukio hili pamoja na kugawa chakula kwa nia ya kupatapa fadhila kutoka kwa Mola wao. [63]

Uundaji wa Kazi za fasihi za Ashura

Makala Asili: Fasihi za Ashura

Tukio la Ashura lilisababisha sehemu ya fasihi ya Kiarabu kujitolea katika utunzi wa mashairi kuhusiana na tukio la Ashura pamoja na maombolezo kuhusiana na maafa ya tukio hilo. Mshairi wa kwanza wa Kiarabu aliyetunga mashairi kuhusiana na tukio la Ashura alikuwa Uqba bin Amru Sahmiy. [64] Abduljalil Razi akieelezea mashairi ya washairi wa upande wa madhehebu ya Hanafi na Shafi'i kuhusiana na Imamu Hussein (a.s), amesema kwamba mashairi hayo ni mengi yasiyoweza kuhesabika. [65] Kulingana na Encyclopedia ya mashairi ya Ashura (دانشنامه شعر عاشورایی), ni kwamba; Suala la uandishi wa mashairi ya Kiajemi katika maombolezo maafa ya Imamu Hussein (a.s) na tukio la Karbala lilianza katika karne ya nne Hijiria, ambapo shairi la kwanza la kuomboleza liliandikwa na Kisai Marwazi (aliyezaliwa mwaka 390 Hijiria). [66] Katika kipindi cha utawala wa Safawi nchini Iran, sehemu muhimu ya mashairi ya Kiajemi ilijitolea kusifu na kuchambua tukio la Ashura. [67] Mwandishi wa kitabu Encyclopedia ya mashairi ya Ashura (دانشنامه شعر عاشورایی), amekusanya majina ya washairi 345 pamoja na baadhi ya beti za mashairi yao kuhusiana na Imamu Hussein (a.s). [68]

Kuenea kwa Uandishi wa Masimulizi ya Maombolezo ya Mauaji

Makala Asili: Maqtal

Uandishi wa Masimulizi ya Mauaji: Ni aina ya historia inayo inahusiana na jinsi watu mashuhuri walivyo uawa au kufa kishahidi. Vitabu vya Masimulizi ya Mauaji ambavyo vinaelezea Hadithi za mauaji ya Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake ni sehemu ya urithi wa fasihi na kihistoria ya Shia, urithi ambao uliandikwa baada ya tukio la Ashura. Uandishi wa Masimulizi ya Mauaji umekuwa ukifanywa miongoni mwa Shia ili kuelezea namana ya mauaji ya Maimamu (a.s) pamoja na watu mashuhuri kutoka katika madhehebu ya Shia. lakini sababu ya kuenea kwa uandishi wa Masimulizi ya Uuaji kuhusu tukio la Karbala, matumizi ya neno hili yamekuwa ni maarufu zaidi vitabu vinavyo elezea matukio yanayohusiana na mauaji ya Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake.

Kukuza Roho ya Ushujaa katika Kukabiliana na Dhulma

Harakati za Imam Hussein (a.s) zimechukua jukumu muhimu katika kuunda roho ya kupinga dhuluma na kuimarisha mapambano ya Waislamu dhidi ya utawala wa dhuluma katika vipindi tofauti. Baadhi ya waandishi wanaamini kwamba; harakati za mageuzi na mapinduzi ya watu, kama vile Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, yamehamasishwa na harakati za Imamu Hussein (a.s). [69]

Imam Khomeini aliamini kwamba kauli mbiu ya Kila siku ni Ashura (کل یوم عاشورا) inaonyesha umuhimu wa kupambana na dhuluma kila siku na kila wakati. [70]

Ujenzi Uanzilishi wa Majengo Maalum

Waislamu wa upande wa madhehebu ya Shia hujenga majengo maalum kama vile husseiniyyah, takiyyeh (ni jina jengine la Husseiniyyah) na imambara (ni kama zawia kwa Maqadiyyih). Majengo haya hutumika kwa ajili ya maombolezo ya Imam Hussein (a.s). Pia katika baadhi ya maeneo ya India, kuna majengo yanayowakilisha makaburi ya mashujaa wa Karbala na kaburi la Imam Hussein (a.s) pamoja na jemedari mashuhuri wa Karbala ajulikanaye kwa jina la Abbas (a.s). Mashia huhudhuria katika majengo hayo na dua maalumu zinazo husiana na sala na salamu kwa mashujaa hao wa Karbala. [71]

Kazi za Fasihi na Sanaa

Harakati za Imam Hussein (a.s) zimeleta mabadiliko makubwa katika kazi za fasihi na sanaa za kidini kwa upande wa Shia, kuna kazi kadha za sanaa na fasihi zilizoundwa kuhusiana na tukio la Ashura, ikiwa ni pamoja na uchoraji ya mandhari, uchoraji wa picha za watu, uandishi wa herufi, filamu, n.k. [72]

Maoni ya Waislamu wa Madhehebu ya Sunni

Waandishi wa upande wa madhehebu ya Sunni hawana mtazamo na nadharia moja kuhusiana na harakati za Imam Hussein (a.s). Baadhi yao, kama vile Abubakar Ibnu Arabi, wamefasiri harakati hizo kuwa ni; miongoni mwa harakati zisizo halali dhidi ya utawala halali. [73] Ibn Taymiyyah aliamini kwamba; ingawa Imam Hussein (a.s) aliuawa kikatili, ila harakati zake hazikukuwa na manufaa, si manufaa ya kidunia wala Akhera. Yeye alidai kuwa harakati za Ashura zilisababisha fitina nyingi katika Ummah wa Kiislamu, na ilikuwa ni kinyume na mwenendo wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w). [74] Kulingana na maelezo ya Hamid Enayati, katika karne za hivi majuzi, na hasa baada ya zama za Sayyid Jamaluddin Asadabadi, mtazamo wa waandishi wa upande wa madhehebu ya Sunni umebadilika kuhusiana na tukio la Ashura, na wengi wao wamekua wakikubaliana na uhalali wa harakati za Imamu Hussein (a.s). [75] Kulingana na maelezo ya Abduljalil Razi katika kitabu chake Naqdhu, ni kwamba; Baadhi ya wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Sunni, kama vile Muhammad bin Idris Shafi'i, wametunga mashairi ya kuomboleza maafa ya Imam Hussein (a.s) na mashujaa wa Karbala. [76] Miongoni mwa mashairi ya maombolezo yanayo husishwa na imamu Shafi'i ni ushairi unaoanza kwa beti isemayo:

ابکی الحسین و ارثی حجاحا * من اهل بیت رسول الله مصباحا[77]

Bibliografia (Seti ya orodha ya vitabu kuhusiana na maudhui hii)

Kuna kazi tofauti zilizoandikwa kuhusiana msimamo wa Imam Hussein dhidi ya utawala wa Yazid. Baadhi ya kazi zilizoandikwa kwa mtazamo wa uchambuzi juu ya sababu na malengo ya msimamo huo ni kama ifuatavyo:

 • Kitabu «Ashura Shenasi», (kitabu kinacho chunguza malengo ya Imam Hussein (a.s). Kitabu kinajumuisha ndani yake sura tatu: «Utambuzi wa Lengo la harakati za Imamu Hussein (a.s)», «Kufa na Chaguo Sahihi la Imamu» na «Maoni ya Wanazuoni wa Zamani». Katika sehemu ya pili ya kitabu, mwandishi ameorodhesha nadharia saba tofauti kuhusiana na malengo ya Imam Hussein. [78] Mwandishi anaamini kwamba; Imam Hussein (a.s) alisimama lengo la kuunda serikali, kwa hivyo sehemu ya tatu ya kitabu hichi, imejitolea katika kufafanua maoni ya wanachuoni wa Shia kuhusiana na malengo hasa ya Imam Hussein (a.s), ambayo yanakubaliana na maoni ya mwandishi.
 • Baada ya Miaka Hamsini, Utafiti Mpya Kuhusiana na harakati za Hussein (a.s) kilicho andikwa na Sayyid Ja'far Shahidi (aliyeishi baina yam waka 1297 na 1386 Hijiria). Kitabu hichi kimeandikwa kwa mtazamo wa kiuchambuzi, bwana Shahidi ndani ya kitabu chake hichi, anachunguza muktadha wa kijamii, kisiasa, kikabila na kidini katika upatikanaji wa harakati za Imam Hussein (a.s). Kitabu hiki kilichapishwa mwaka wa 1358 Shamsia.
 • Taamuli Dar Nahdha Ashuraa,: Kilicho andikwa na Rasul Ja'fariyan. Kitabu hichi kimeoorodhesha ndani yake, baadhi ya vyanzo vinavyohusiana na tukio la Karbala. Pia kitabu hichi kimeshughulikia mambo kadhaa ndani yake, ikiwemo; muktadha wa msimamo na harakati za Imamu Hussein (a.s), ufafanuzi wa tukio hilo, hekima ya kuuawa kwa Imam Hussein, athari za msimamo huo, vipimo vyake vya kiitikadi na mjengeko wake, upotoshwaji wa tukio la Karbala, na historia ya maombolezo juu ya maafa ya Imam Hussein kwa upande wa madhehebu ya Sunni. [79]
 • Harakati za Ashura katika Maneno na Ujumbe wa Imam Khomeini. Sehemu ya kwanza ya kitabu hichi inajumuisha hotuba tatu kuhusiana na Muharram na Ashura. Sehemu ya pili inajumuisha sababu na mazingira au muqtadha ulio sababisha msimamo wa Ashura, falsafa ya maombolezo pamoja na usomaji wa mashairi ya huzuni. Na mwishoni mwa kitabu hichi mna jopo la hotuba za Imamu Khomeini kuhusiana na Muharram na harakati za Karbala. [80]

Vyanzo

 • Abī Mikhnaf, Lūṭ b. Yaḥyā. Maqtal al-Ḥusayn (a). Edited by Ḥusayn al-Ghifārī. Qom: Maṭbaʿat al-ʿIlmiyya, [n.d].
 • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. [n.p]. [n.d].
 • Abū ʿAlī Miskawayh, Aḥmad b. Muḥammad. Tajārub al-umam. [n.p]. [n.d].
 • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī, Iḥsān ʿAbbās and Muḥammad Ḥamīd Allāh. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, [n.d].
 • Dīnawarī, Aḥmad b. Dāwūd al-. al-Akhbār al-ṭiwāl. Edited by ʿAbd al-Munʿim ʿĀmir. 1st edition. Cairo: Dār Iḥyāʾ al-Kutub al-ʿArabī, 1960.
 • Farmāniyān, Mahdī and Musawīnizhād Sayyid ʿAlī. Zaydīyya; Tārīkh wa ʿaqāʾid. [n.p]. [n.d].
 • Hārūnī, Yaḥya b. Ḥusayn. Al-Ifāda fī tārīkh al-aʾimma al-Zaydīyya. [n.p]. [n.d].
 • Hilālī, Sulaym b. Qays. Kitāb Sulaym b. Qays. Beirut: Dār al-Funūn, [n.d].
 • Ḥusaynī, Sayyid Jawād. Ifshāyi mafāsid-i Muʿawiya wa Yazīd da sukhanān-i Imām Ḥusayn. Pāsdār-i Islām, No: 279-280, 1384 Sh.
 • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, [n.d].
 • Ibn Aʿtham al-Kūfī, Aḥmad b. Aʿtham. Kitāb al-Futūḥ. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1411 AH-1991.
 • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH.
 • Ibn Ṭaqṭaqī, Muḥammad b. ʿAlī b. Ṭabāṭabā. Al-Fakhrī fī ādāb al-sulṭānīya wa al-duwal al-islāmīya. [n.p]. [n.d].
 • Isfandiyārī, Muḥammad. Āshūrā-pazhūhī; pazhūhishī darbāra-yi hadaf-i Imām Ḥusayn. [n.p]. [n.d].
 • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkkāsha. [n.p]. [n.d].
 • ʿInāyat, Ḥamīd. Andīshā-yi siyāsī dar Islām-i muʿāṣir. Translated to Farsi by Bahāʾ al-Dīn Khurramshāhī. Tehran: Intishārāt-i Khwārizmī, 1365 Sh.
 • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Minhāj al-sunna al-nabawīyya fī naqd kalām al-shīʿa al-qadarīyya. [n.p]. [n.d].
 • Group of authors. Zamīnaha-yi Qiyām-i Imām Ḥusayn. Qom: Zamzam-i Hidāyat, 1383 Sh.
 • Jaʿfarī, Ḥusayn Muḥammad. Tashayyuʿ dar masīr-i tārīkh. Translated by Muḥammad Taqī Āyatullāhī. Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1382 Sh.
 • Jaʿfarīyān, Rasūl. Taʾmulī dar nahḍat-i āshūrā. Qom: Nashr-i Muwarrikh, 1386 Sh.
 • Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Maqtal al-Ḥusayn. Edited by Muḥammad al-Samāwī. Qom: Anwār al-Hudā, 1423 AH.
 • Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Maqtal al-Ḥusayn. Edited by Muḥammad al-Samāwī. 1st volume. Qom: Maktabat al-Mufīd, [n.d].
 • Khazaʿlī, Insiyya. Qiyām-i Imām Ḥusayn az dīdgāh-i ʿulamā-yi Ahl-i Sunnat. volume 11. Tehran: Majmaʿ Jahānī-yi Ahl al-Bayt, 1381 Sh.
 • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab wa maʿadin al-jawhar. Edited by Asʿad Dāghir. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
 • Muṭahharī, Murtaḍā. Ḥamāsa Ḥusaynī. 59th edition. Tehran: Intishārāt-i Ṣadrā, 1387 Sh.
 • Muḥammadzāda, Marḍiyya. Dānishnāma-yi sheʿr-i āshūrāʾī. 2nd edition. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād-i Islāmī, 1386 Sh.
 • Mamaqānī, ʿAbd Allāh b. Ḥasan. Tanqīḥ al-maqāl fī ʿilm al-rijāl. [n.p]. [n.d].
 • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī. Imtāʿ al-asmāʾ bimā li-Nabī min al-aḥwāl wa al-amwāl wa al-ḥafda wa al-matāʾ. [n.p]. [n.d].
 • Muʾassisa-yi Shīʿashināsī. Sunnat-i ʿazādārī wa manqabat-khānī. [n.p]. [n.d].
 • Nāṣirī Dawudī, ʿAbd al-Majīd. Nahḍat-i Imām Ḥusayn az manzar-i Ahl-i Sunnat. [n.p]. [n.d].
 • Qazwīnī, ʿAbd al-Jalīl. Al-Naqḍ. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1391 Sh.
 • Raḥmānī, Jabbār. Āʿīn wa usṭūra dar Iran Shīa. Tehran: Intishārāt-i Khayma, 1394 Sh.
 • Sayyid Murtaḍā, ʿAlī b. Ḥusayn. Tanzīh al-anbīyā'. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, [n.d].
 • Shahīdī, Sayyid Jaʿfar. Pas az panjāh sāl; pazhūhishī tāza pīrāmūn-i qiyām-i Imām Ḥusayn. Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1386 Sh.
 • Ṣiḥḥatī Sardrūdī, Muḥammad. Āshūrā-pazhūhī bā rūykardī bi taḥrīf-shināsī-yi tārīkh-i Imām Ḥusayn. 1st edition. Qom: Intishārāt-i Khādim al-Riḍā, 1384 Sh.
 • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Dar al-Turāth al-ʿArabī, 1387 AH.
 • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. 2nd edition. Beirut: Dār al-Turāth, 1967.