Nenda kwa yaliyomo

Labbaika ya Hussein

Kutoka wikishia
Bendera ya Labaika Ya Hussein katika Maombolezo

Labbaika ya Hussein (Kiarabu: لَبَّيكَ يا حسين) ni kauli-tamko ya kitamaduni katika madhehebu ya Kishia inayofanya kazi kama ni jibu la kiibada kwa ajili ya kuitikia mwito wa Imamu Hussein (a.s) aliyoutoa kwa ajili mapambano ya Karbala. Vyanzo vya kihistoria vinabainisha kwamba; Imamu Hussein (a.s) aliomba msaada mara kadhaa katika mapambano yake dhidi ya wafwasi wa Yazid bin Muawia. Maarufu zaidi ya wito wa kutaka msaada ulitolewa siku ya Ashura kupitia kauli isemayo: «Hal min nasirin yansuruni?» (Je, yupo msaidizi atakayenisaidia?) Ambayo imekuwa ni miongoni mwa mihimili ya utambulisho wa kumbukumbu za Ashura.

Kwa mtazamo wa kijamii na kitamaduni, «Labbaika ya Hussein» ni tamko la uaminifu, mshikamano wa kijamii na utayari wa kutoa msaada kwa Imamu Hussein (a.s). Kauli hii hulifanya tukio la Karbala litazamwe kama mwendelezo wa kihistoria (historical continuum) na imekuwa ni chombo cha kudumisha “dira ya Ashura” katika ulimwengu wa kiroho na kimatendo kwa waumini. Aidha, kauli hii inafasiriwa kama alama ya kupinga utawala na uendeshaji wa kibeberu, mapambano dhidi ya ukandamizaji, na msimamo wa kukataa aina zote zile za udhalili.

Labbaika ya Hussein, ni semi na kauli mbiu ya Kishia inayojitokeza katika ibada za maombolezi ya Muharram kama tamko la utii na mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s). Ushawishi wa kauli hii umechochea kuibuka kwa kazi kadhaa kisanaa, kama vile; mashairi, michoro pamoja na filamu). Kauli hii pia huonekana kutumika katika nyanja za kivita pamoja na mazishi ya mashahidi mbali mbali. Kwa urudufu wa kimuundo na kimaana, kauli imezalisha semi nyengine kadhaa tanzu zinazotumika katika harakatia za kihimaya, maandamano na pa moja naibada za umma, miongoni mwazo ni pamoja na; «Labbaika ya Haidar, «Labbaika ya Mahdi», na «Labbaika ya Khamenei».

Utambulisho

Labbaika ya Hussein kama semi na kauli maarufu ya siku ya Ashura,[1] hueleweka kama mwitikio wa waumini wa kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s).[2] Kimaandishi, simulizi zinaonesha kwamba; kuanzia Makka hadi Iraq, Imamu Hussein (a.s) alitoa kauli kadhaa za miito ya kuomba usaidizi.[3] Miongoni mwa miito hiyo, ni ule mwito aliyoutoa akiwa mjini Makka. Mwito huu ulibeba ujumbe usemao; (Mimi ninaelekea mahali ambapo mbwamwitu wa jangwani wataniraruararua… (Hivyo basi) yeyote yule aliye tayari kutoa damu yake kwa ajili yangu, basi aje Karbala).[4] Pia mwito wake mwengine, ni ule ulioko kwenye barua aliyowatuma wakuu wa mji wa Basra, akiwataka wakuu hao kumpa himaya na kumuunga mkono katika harakati zake za mapambano.[5] Kilele cha mwito huu ni kilipatikana katika hotuba yake ya Ashura,[6] iliyoambatana na kauli mbiu isemayo; «Hal min nasirin yansuruni?» (Je, kuna msaidizi yeyote yule atakayenisaidia?) [7] Kauli hii imekuwa ni moja ya mihimili mikuu na maarufu zaidi inayotumika katika kuadhimisha tukio la Karbala, hasa hasa tukio la siku ya Ashura.[7]

Nafasi na Umuhimu wa Kauli ya Labbaika ya Hussein

Tokea zama za tukio la Ashura hadi leo, Mashia mara kwa mara wamekuwa na kawaida ya hutangaza mshikamano wao na Imamu Hussein (a.s), kupitia kauli isemayo: «Labbaika ya Hussein».[8] Kikawaida, Mashia hutumia kauli hii kama ni tangazo la kutangaza utayari wao wa kushikamana na Imamu Hussein (a.s), kama ni wafuasi wa Imamu Hussein (a.s), ambao wako tayari kujitolea kwa maisha yao, mali zao na hata watoto wao kwa ajili ya kushikamana na njia ya Imamu Hussein (a.s).[9] Imeelezwa kuwa kauli mbiu hii, ni moja ya kauli mbiu za kimataifa,[10] wala haikufungamani tu na kipindi fulani cha kihistoria;[11] bali nembo maalumu inalolitambulisha tukio la Ashura kama mkondo endelevu wa kihistoria unaoendelea katika zama tofauti.[12] Hivyo, pamoja na kudhamini uhai wa tukio la Ashura,[13] pia kauli mbiu hii, imedumisha muktadha na urithi wa fikra ya Ashura.[14]

Imeelezwa kwamba; Miongoni mwa athari za kauli mbiu ya: «Labbaika ya Hussein», ni kuleta matunda ya heshima na hadhi, kujiepusha na udhalili na fedheha,[15] kupambana na dhuluma na kujitoa muhanga katika njia ya haki,[16] kujikomboa kutokana na nguvu za utawala haramu,[17] kuvuruga njama za maadui[18] na kuvunja utawala wa ubeberu.[19] Hiyo ndiyo sababuiliyopelekea, kauli mbiu hii kutazamwa kama ni alama ya kupinga ubeberu na ya kukataa udhalilishaji.[20] Baadhi ya wataalamu pia wameihisisha kauli mbiu hii na ushindi, uimara na uenezaji wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, wakisema kwamba; ushikamanaji na utekelezaji wa kauli mbiu hii ndiyo sabau hasa kufanikiwa katika sekta hizo mbali mbali.[21]

Labbaik katika Matini za Kidini

Tangu enzi za kale, Istilahi ya neo «Labbaik» imekuwa ikitumika kama ni fomula maalumu ya mwitikio wa kukubali mwito wa mwingine.[22] Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), pia nao walionekana kuitumia istilahi hii katika mazingira na miktadha tofauti.[23] Miongoni mwa matukio yaliyoitikiwa kwa mwitikio wa kauli ya Labbaik, ni tukio la vita vya Hunain (Ghazwatu Hunain).[24]Kutokana na ushahidi huu wa kihistoria na kimaandishi, yale madai wa Mawahabi yasemayo kwamba; matumizi ya istilahi hiyo kwa wasiyekuwa Mungu ni shirk hayawezi kuwa na nafasi yeyote ile ndani tafakuri za jamii ya Kiislamu.[25] Zaidi ya hapo, katika mojawapo ya matini za Ziara za Imamu Hussein (a.s) zinazohusishwa na Imamu Ja‘far al-Sadiq, imeelezwa kwamb; miongoni mwa adabu za ziara katika kumzuru Imamu Hussein (a.s), ni kurudia (kukariri) mara saba ibara isemayo «Labbaika da‘i Allah».[26] Pia katika Ziara Rajabiyya ya Imamu Hussein, tunakuta Imamu (a.s) anahutubiwa kwa kauli isemayo «Labbaika ya da‘i Allah».[27] Kadhalika, katika Du‘ā al-‘Ahd, kuna kauli isemayo «Labbaik», ambayo inahusiana na suala la kuitikia mwito wa Imam Mahdi (a.s).[28]

Wataalamu na watafiti wa lugha wanasema kwamba; neno «labbaika» kiasili lina ya «utiifu»[29] na «ijaba» (kuitikia mwito).[30] Wataalamu hawa wanaamini kwamba; neno «labbaik» - ambalo asili yake ni «labban laka»,[31] linamaanisha kubaki katika hali ya utayari wa kutii na kuitikia mwito wa mtu fulani.[32] Neno hili hutumika pia kama ni «talbiya» (Labbayka Allahumma Labbayk, Labbayka la sharika laka Labbayk), ibara ambayo hutamkwa wakati wa kuingia katika ihramu ya Hija ya Tamattu‘u (Hija ya Wajibu) au ‘Umra.[33]

Matumizi ya Kauli Mbiu

Kauli-mbiu «Labbaik ya Husayn» hutumiwa katika ibada za maombolezo na katika kuonyesha mahaba na utiifu kwa Imam Husayn (a.s.), na pia kauli hii katika nyanja za kitamaduni na sanaa pamoja na halfa mbali mbali zinazohusiana na masuala ya kimapinduzi.

Katika amali za maombolezo mbali mbali ya kidini

شعار لبیک یا حسین به خط ثلث، اثر برگزیده فراخوان حروف‌نگاری لبیک یا حسین.[34]

hasa katika maadhimisho ya tukio la Karbala, semi ya «Labbaika ya Hussein» huibuka kama kauli mbiu inayotamkwa ndani ya nchi mbali mbali katika muktadha wa kuadhimisha tukio hilo kimataifa. Miongoni mwa nchi zinazotumia ibara hiyo ni nembo maalumu katika maadhimisho hayo ni pamoja na; Nigeria,[35] Uturuki,[36] Lebanoni,[37] Iran,[38] Iraq, pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Uholanzi.[39] Katika siku ya Ashura, jamii za wa watu wa Iraq - hasa wakaazi wa mji wa Tuwairij[40] na watu wa kabila la Bani Asad,[41] huitamka kauli mbiu hii pale wanapoingia katika haram ya Imamu Hussein (a.s.). Kuna mikusanyiko kadhaa mikubwa nchini Iran, iliyopewa jila «Ijtima‘i Labbaik ya Hussein». Pia pale Mashia wanapotekeleza desturi yao ya kubadilisha bendera zilizoko kwenye maeneo matukufu (Atabāt ‘Āliyāt) kabla ya kuingia msimu wa maombolezo, mara nyingi amali hiyo huambatana na kauli isemayo «Labbaik ya Hussein».[42] Aidha, mnamo mwaka 1397 (kwa kalenda ya Shamsia), kuna bendera kubwa yenye maandishi yasemayo «Labbaik ya Hussein», ambayo ilitanda eneo lote lililoko katika Baina al-Haramain, Karbala, ambayo iliwasilishwa hadharani wakati wa matembezi ya Arbaʿīn yaliyofanyika mwaka huo.[43]

Mfano wa Uthibitisho wa Kiuumla katika Kitabu Kamil al-Ziyarat
Kauli mbiu ya «Labbaika ya Hussein», inamaanisha uwepo thabiti katika uwanja wa mapambano, hata kama utakuwa ni wewe tu ndiye uliepo uwanjani humo, na hata pale jamii inapojiondoa na kukuacha peke yako, au ikakushutumu na kukutelekeza bila nusura. Aidha, «Labbaika ya Hussein», yaani ni ule uwepo wako binanfsi katika uwanja huo, unaoandamana na rasilimali yako, mke pamoja na watoto wako.[44]

Katika Nyanja za Sanaa na Utamaduni

Katika nyanja za utamaduni na sanaa, kauli mbui ya «Labbaika ya Hussein», imeonekana kuakisiwa vya kutosha ndani ya sanaa mbali mbali, zikwemo sanaa za mashairi pamoja na kazi mbalimbali za kitamaduni na kisanii.[45] Kuna kazi kadhaa za kisanii zililzotungwa na kuwasilishwa kwa anwani ya «Labbaika ya Hussein». Miongoni mwa kazi hizo ni video ya muziki iitwayo «Labbaika ya Hussein», iliyoimbwa na Sadegh Ahangaran, iliyotolewa kwa mnasaba wa adhimisho la siku ya Arubaini (Arbaeen).[46] Katika fani ya kaligrafia, pamoja na kuandikwa kwa kazi nyingi zenye ibara ya «Labbaika ya Hussein», bado kumekuwa na miito maalumu ya mashindano ya uandishi wa kaligrafia kuhusiana na sentensi hii.[47]

Matumizi ya Labbaika ya Hussein Katika Matukio Mbali Mbali ya Kisiasa

Ndani ya matukio mbalimbali ya kijamii na kisiasa, nchi mbali mbali zimeonekana kutumia semi wa «Labbaika ya Hussein» kama ni nembo maalu ya mwamko katika jamii zao. Baada ya kutolewa kwa fatwa ya jihadi na Ayatullah Sayyid Ali Sistani dhidi ya Daesh, makundi ya wananchi wa Iraq yaliipokea fatwa hiyo kwa ukelele wa «Labbaika ya Hussein»[48] huku wakiiweka mbele kauli hiyo, katika harakati na operesheni zao mbali mbali za kupambana dhidi ya vikozi vya Daesh.[49] Kauli mbiu hiyo imeendelea kuonekana kutumika katika mbali mbali za umma, hususan katika maziko ya kuwazika mashahidi wa muqawama nchini Iran,[50] Iraq[51] na Lebanon.[52]

Vilevile, kwa urudufu wa kimuundo na kimaana, kuna tanzu kadhaa zilizoibuka zikiwa na muundo kama huo, ambazo zimeonekana kutumika katika makongamano, maandamano na ibada za umma. Miongoni mwa tanzu hizo ni pamoja na; «Labbaika ya Rasula Allah»,[53] «Labbaika ya Haidar»,[54] «Labbaika ya Zainab»,[55] «Labbaika ya Qur’an», «Labbaika ya Mahdi»,[56] «Labbaik ya Abalffadhl»,[57] «Labbaika ya Khomeini», na «Labbaik ya Khamenei».[58]

Rejea

  1. «شرح لبیک یا حسین بخش اول: نوشتاری از استاد هادی سروش»، شفقنا
  2. «شعار «لبیک یا حسین» به معنای اجابت دعوت سیدالشهدا(ع) است»، خبرگزاری مهر
  3. «شعار «لبیک یا حسین» به معنای اجابت دعوت سیدالشهدا(ع) است»، خبرگزاری مهر
  4. حلوانی، نزهة الناظر، ۱۴۰۸ق، ص۸۶؛ ابن‌طاووس، اللهوف، ۱۳۴۸ش، ص۶۰
  5. ابن طاووس، اللهوف، ۱۳۴۸ش، ص۳۸
  6. ابن‌طاووس، اللهوف، ۱۳۴۸ش، ص۱۱۶؛ ابن‌نما حلی، مثیر الاحزان، ۱۴۰۶ق، ص۷۰
  7. محدثی، فرهنگ عاشورا، ۱۳۷۶ش، ص۴۷۱
  8. «لبیک یا حسین موجب ماندگاری گفتمان عاشورایی است»، خبرگزاری رضوی
  9. «شعار «لبیک یا حسین» به معنای اجابت دعوت سیدالشهدا(ع) است»، خبرگزاری مهر
  10. «شعار لبیک یا حسین جهانی شده است»، ایسنا
  11. «لبیک یا حسین موجب ماندگاری گفتمان عاشورایی است»، خبرگزاری رضوی
  12. «فراخوان رقابتی حروف نگاری لبیک یا حسین»، کانون هنری شیعی
  13. «شعار «لبیک یا حسین» به معنای اجابت دعوت سیدالشهدا(ع) است»، خبرگزاری مهر
  14. «لبیک یا حسین موجب ماندگاری گفتمان عاشورایی است»، خبرگزاری رضوی
  15. «شعار لبیک یا حسین مبارزه با استکبار ستیزی است»، خبرگزاری رسا
  16. «شعار لبیک یا حسین مبارزه با استکبار ستیزی است»، خبرگزاری رسا
  17. ««لبیک یا حسین یعنی رهایی از همه قدرت ها: نوشتاری از استاد هادی سروش – بخش هفتم»، شفقنا
  18. «لبیک یا حسین خنثی کننده توطئه دشمنان است»، حوزه نمایندگی ولی فقیه در امور حج و زیارت
  19. «شعار ” لبیک یا حسین” هیمنه استکبار را درهم‌شکسته است»، زرین خبر
  20. «شعار لبیک یا حسین مبارزه با استکبار ستیزی است»، خبرگزاری رسا
  21. «شعار لبیک یا حسین مبارزه با استکبار ستیزی است»، خبرگزاری رسا
  22. برای نمونه نگاه کنید به: طبری، تاریخ الامم و الملوک، ۱۳۸۷ق، ج۸، ص۸۴؛ ابن‌سعد، الطبقات الکبری، ۱۴۱۰ق، ج۳، ص۹۲؛ دینوری، الاخبار الطوال، ۱۳۶۸ش، ص۳۶۵
  23. برای نمونه نگاه کنید به: مقریزی، إمتاع الأسماع، ۱۴۲۰ق، ج۶، ص۳۶۹؛ ج۱۲، ص۳۷۶؛ ج۱۳، ص۳۷۹؛ بیهقی، دلائل النبوة، ۱۴۰۵ق، ج۵، ص۱۷۴؛ بلاذری، فتوح البلدان، ۱۹۸۸م، ص۴۸
  24. واقدی، المغازی، ۱۴۰۹ق، ج۳، ص۹۰۰-۹۰۱؛ طبری، تاریخ الامم و الملوک، ۱۳۸۷ق، ج۳، ص۷۵-۷۶
  25. «شرح لبیک یا حسین بخش اول: نوشتاری از استاد هادی سروش»، شفقنا
  26. ابن‌قولویه، کامل الزیارات، ۱۳۵۶ش، ص۲۳۰
  27. ابن‌طاووس، إقبال الاعمال، ۱۴۰۹ق، ج۲، ص۷۱۳-۷۱۴؛ شهید اول، المزار، ۱۴۱۰ق، ص۱۴۲
  28. ابن مشهدی، المزار الکبیر، ۱۴۱۹ق، ص۶۶۶-۶۶۳؛ کفعمی، المصباح، ۱۴۰۵ق، ص۵۵۲-۵۵۰
  29. فراهیدی، کتاب العین، ۱۴۱۰ق، ج۸، ص۳۴۱
  30. ازهری، تهذیب اللغة، بیروت، ج۱۵، ص۲۴۲
  31. ازهری، تهذیب اللغة، بیروت، ج۱۵، ص۲۴۲
  32. جوهری، الصحاح، بیروت، ج۱، ص۲۱۶؛ صاحب بن عباد، المحیط فی اللغة، ۱۴۱۴ق، ج۱۰، ص۳۱۲
  33. شهید ثانی، مسالک الافهام، ۱۴۱۶ق، ج۲، ص۲۲۶؛ فاضل هندی، کشف اللثام، ۱۴۱۶ق، ج۵، ص۲۰؛ نجفی، جواهر الکلام، ۱۳۶۲ش، ج۱۸، ص۳-۴.
  34. پایگاه ارتباطات رسانه‌ای حزب‌الله
  35. «بی‎‌توجهی جامعه بین‌‎المللی به نقض حقوق‎ بشری شیعیان نیجریه»، خبرگزاری میزان
  36. بدل، «شرایط دینی و مذهبی کشور ترکیه»، ص۲۹۸
  37. «دسته‌های عزای عاشورایی در سراسر لبنان»، الکوثر
  38. «اجتماع عظیم اردبیلی‌ها در روز تاسوعا با شعار لبیک یا حسین»، خبرآنلاین
  39. «شعار لبیک یا حسین(ع) و لبیک یا خامنه‌ای در لاهه هلند»، خبرنامه دانشجویان ایران
  40. «دسته طویریج دسته‌ای به بلندای چهارده قرن»، خبرآنلاین
  41. «فریاد "لبیک یا حسین" زنان قبیله بنی‌اسد در حرم سیدالشهدا طنین‌انداز شد»، خبرگزاری مهر
  42. «لبیک یا حسین موجب ماندگاری گفتمان عاشورایی است»، خبرگزاری رضوی
  43. تعویض پرچم گنبدحرمهای کربلا. خبرگزاری مهر
  44. برای نمونه نگاه کنید به: «لبیک یاحسین -(ازعمق جان بگو لبیک یاحسین)»، امام هشت.
  45. برای نمونه نگاه کنید به: «لبیک یاحسین -(ازعمق جان بگو لبیک یاحسین)»، امام هشت
  46. «لبیک یا حسین جدیدترین اثر حاج صادق آهنگران»، رجانیوز
  47. «فراخوان رقابتی حروف نگاری لبیک یا حسین»، کانون هنری شیعی
  48. «شعار لبیک یا حسین در حرم طنین انداز شد»، حوزه نمایندگی ولی فقیه در امور حج و زیارت
  49. «نام عملیات از "لبیک یا حسین" به "لبیک یا عراق" تغییر کرد»، خبرگزاری جمهور
  50. «تشییع پیکر شهید حاج قاسم سلیمانی در مشهد»، افکار نیوز
  51. «صحن اباعبدالله؛ لبیک یا حسین در هنگام ورود پیکر شهدا»، راسخون
  52. «طنین شعار لبیک یا حسین(ع) در مراسم تشییع شهید «علی یوسف علاء الدین» از رزمندگان حزب‌الله» خبرگزاری دانشجو
  53. «ایران اسلامی در سالروز رحلت پیامبر به سوگ نشست»، پایگاه اطلاع رسانی حج.
  54. «اجتماع دانش‌آموزان شیرازی در حرم مطهر حضرت شاهچراغ + فیلم»، خبرگزاری تسنیم.
  55. «طنین ندای "لبیک یا زینب(س)" در سراسر ایران»، خبرگزاری حوزه.
  56. «سید حسن نصرالله: تکفیری‌ها پشت‌پرده انفجارهای زینبیه هستند/ با شعار «لبیک یا حسین» به خیابان‌ها می‌آییم»، خبرگزاری تسنیم؛ «ندای لبیک یا مهدی همراه با عطر یاس مهدوی در میعادگاه منتظران»، وبگاه ایرنا.
  57. «مردم گچساران لبیک یا ابوافضل(ع) را درشب تاسوعا سردادند»، خبرگزاری ایسنا
  58. «برگزاری راهپیمایی روز ملی مبارزه با استکبار در کرمان»، خبرگزاری ایکنا

Vyanzo

  • Ibn Taawus, Ali bin Musa, Iqbaal al-A‘maal, Tehran, Daar al-Kutub al-Islaamiyyah, chapa ya pili, 1409 H / 1988 M.
  • Ibn Taawus, Ali bin Musa, Al-Luhuuf ‘Alaa Qatlaa al-Tufuuf (Kiarabu pamoja na tarjuma), tarjuma Ahmad Farhi Zanjani, Tehran, Nashr Jahaan, 1348 Sh / 1969 M.
  • Ibn Qulawayh, Ja‘far bin Muhammad, Kaamil al-Ziyaaraat, Najaf, Daar al-Murtadhawiyyah, 1356 Sh / 1977 M.
  • Ibn Mashhadi, Muhammad bin Ja‘far, Al-Mazaar al-Kabiir, Qum, Jaami‘at al-Mudarrisiin, 1419 H / 1998 M.
  • Ibn Nama al-Hilli, Muthiir al-Ahzaan, Qum, Madrasat al-Imaam al-Mahdi, 1406 H / 1985 M.
  • Ibn Sa‘d, Muhammad, Al-Twabaqaat al-Kubraa, tahqiq Muhammad ‘Abd al-Qaadir ‘Atwaa, Beirut, Daar al-Kutub al-‘Ilmiyyah, 1410 H / 1989 M.
  • “Ijtimaa‘ Adhiim Ardabiilihaa dar Rooz Taasuu‘aa baa Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn”, Khabar Online. Tarehe ya kuchapishwa: 20 Mehr 1395 Sh / 11 Oktoba 2016 M.
  • Azhari, Muhammad bin Ahmad, Tahdhiib al-Lughah, Beirut, Daar Ihyaa al-Turaath al-‘Arabi, bila tarehe.
  • “Dastah Tuwairiij Dastah’ii baa Bulandaaye Chaarda Dah Qarn”, Khabar Online.
  • Badal, Hasan, “Sharaait Diinii wa Madhhabii Kishwar Turkiyah”, Pazhoohishnaamah Hikmat wa Falsafah Islaami, namba 10 na 11, kiangazi na mapukutiko 1383 Sh / 2004 M.
  • Baladhuri, Ahmad bin Yahyaa, Futuuh al-Buldaan, Beirut, Daar wa Maktabat al-Hilaal, 1988 M.
  • Bayhaqi, Ahmad bin Husayn, Dalaa’il al-Nubuwwah wa Ma‘rifat Ahwaal Saahib al-Sharii‘ah, tahqiq ‘Abd al-Mu‘ti Qal‘aji, Beirut, Daar al-Kutub al-‘Ilmiyyah, 1405 H / 1985 M.
  • “Parcham Labbayk Yaa Husayn dar Bayn al-Haramayn”, Khabarguzaari Mehr. Tarehe ya marejeo: 11 Aghosti 2023 M.
  • “Tashyii‘ Paykar Shahiid Haaj Qaasim Sulaymaani dar Mashhad”, Afkaar News. Tarehe ya kuchapishwa: 15 Day 1398 Sh / 5 Januari 2020 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • Thaqafi, Muhammad, “Ta’thiir ‘Aashuraa dar Adabiyaat ‘Aashuraa (2)”, uk. 30, Darshaayii az Maktab Islaam, mwaka wa 43, namba 1, Farwardiin 1382 Sh / Aprili 2003 M.
  • “Ta‘wiidh Parcham Gunbad Haramhaay Karbalaa”, Khabarguzaari Mehr. Tarehe ya marejeo: 11 Aadhar 1402 Sh / 2 Disemba 2023 M.
  • Jawhari, Ismaa‘il bin Hammaad, Al-Sihaah, Beirut, Daar al-‘Ilm li al-Malaayiin, bila tarehe.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn dar Haram Twaniin Andaaz Shud”, Hawzah Numaayandagi Wali Faqih dar Umuur Hajj wa Ziyaarat. Tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • Halwaani, Husayn bin Muhammad bin Hasan bin Nasr, Nuzhat al-Naadhir wa Tanbiih al-Khaatir, Qum, Madrasat al-Imaam al-Mahdi (a.t.f.s), 1408 H / 1987 M.
  • “Dastahaay ‘Azaay ‘Aashuraayii dar Saraasar Lubnaan”, Al-Kawthar. Tarehe ya kuchapishwa: 8 Mordaad 1402 Sh / 30 Julai 2023 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • Dinawari, Ahmad bin Daawud, Al-Akhbaar al-Tiwaal, Qum, Manshuraat Radi, 1368 Sh / 1989 M.
  • “Sayyid Hasan Nasrallah: Takfiiriihaa Posht Pardah Infijaarhaay Zaynabiyyah Hastand / baa Shi‘aar “Labbayk Yaa Husayn” bih Khayaabaanhaa Mi Aayiim”, Khabarguzaari Tasniim. Tarehe ya kuchapishwa: 6 Mordaad 1402 Sh / 28 Julai 2023 M; tarehe ya kutembelewa: 12 Aadhar 1402 Sh / 3 Disemba 2023 M.
  • “Sharh Labbayk Yaa Husayn, Bakhsh Awwal: Nuwishtaarii az Ustaadh Haadi Suroosh”, Shafaqna. Tarehe ya kuchapishwa: 8 Mordaad 1401 Sh / 30 Julai 2022 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn Haymanah Istikbaar ra Darham Shikastah Ast”, Zarrin Khabar. Tarehe ya kuchapishwa: 31 Mordaad 1402 Sh / 22 Agosti 2023 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar “Labbayk Yaa Husayn” bih Ma‘naay Ijaabat Da‘wat Sayyid al-Shuhadaa (‘a) Ast”, Khabarguzaari Mehr. Tarehe ya kuchapishwa: 10 Mordaad 1401 Sh / 1 Agosti 2022 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn (‘a) wa Labbayk Yaa Khaamene’ii dar Laahah Huland”, Khabarnaamah Danishjuyaan Iran. Tarehe ya kuchapishwa: 22 Aadhar 1391 Sh / 12 Disemba 2012 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn Jahaanii Shudah Ast”, ISNA. Tarehe ya kuchapishwa: 28 Mordaad 1400 Sh / 19 Agosti 2021 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn dar Saraasar Kishwar Twaniin Andaaz Mi Shawad / Shukuuh ‘Azaadaarii dar Ustaan Ardabiil Bii Nadhiir Ast”, Khabarguzaari Tasniim. Tarehe ya kuchapishwa: 8 Shahrivar 1399 Sh / 29 Agosti 2020 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn Mubaaraazah baa Istikbaar Sitiizii Ast”, Khabarguzaari Rasa. Tarehe ya kuchapishwa: 12 Aabaan 1394 Sh / 3 Novemba 2015 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • Shahiid Awwal, Muhammad bin Makki, Al-Mazaar fii Kayfiyyat Ziyaaraat al-Nabii wa al-A’immah (‘alayhim al-salaam), Qum, Madrasah Imaam Mahdi (‘a), 1410 H / 1989 M.
  • Shahiid Thaani, Masaalik al-Afhaam ilaa Tanqiih Sharaa’i‘ al-Islaam, Qum, Ma‘aarif Islaami, 1416 H / 1995 M.
  • “Bii Tawajjuhii Jaami‘ah Bayn al-Milalii bih Naqdh Huquuq Basharii Shi‘iyaan Nayjariyah”, Khabarguzaari Miizaan. Tarehe ya kuchapishwa: 7 Mordaad 1402 Sh / 29 Julai 2023 M; tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • Shaykh Hurr ‘Aamili, Muhammad bin Hasan, Ithbaat al-Hudaat bi al-Nusuus wa al-Mu‘jizaat, Beirut, A‘lami, 1425 H / 2004 M.
  • Saahib bin ‘Abbaad, Ismaa‘il bin ‘Abbaad, Al-Muhiit fii al-Lughah, Beirut, ‘Aalam al-Kutub, 1414 H / 1994 M.
  • “Sahn Abaa ‘Abdillah; Labbayk Yaa Husayn dar Hangaam Wuruud Paykar Shuhadaa”, Raasikhun.
  • Tabari, Muhammad bin Jariir bin Yaziid, Taariikh al-Umam wa al-Muluuk, tahqiq Muhammad Abu al-Fadl Ibrahim, Beirut, Daar al-Turaath, chapa ya pili, 1387 H / 1967 M.
  • “Twaniin Shi‘aar Labbayk Yaa Husayn (‘a) dar Maraasim Tashyii‘ Shahiid ‘Ali Yusuf ‘Alaa al-Diin az Razmandagaan Hizbullah”, Khabarguzaari Danishju. Tarehe ya kutembelewa: 5 Aadhar 1402 Sh / 26 Novemba 2023 M.
  • “Twaniin Nidaa “Labbayk Yaa Zaynab (s)” dar Saraasar Iran”, Khabarguzaari Hawzah. Tarehe ya kuchapishwa: 15 Aabaan 1393 Sh / 6 Novemba 2014 M; tarehe ya kutembelewa: 12 Aadhar 1402 Sh / 3 Disemba 2023 M.
  • Faadhil Hindi, Muhammad bin Hasan, Kashf al-Lithaam, Qum, Nashr Islaami, 1416 H / 1995 M.
  • Faraahidi, Khaliil bin Ahmad, Kitaab al-‘Ayn, Qum, Nashr Hijrat, chapa ya pili, 1410 H / 1989 M.
  • “Faraakhwaan Riqaabatii Huruuf Nigaarii Labbayk Yaa Husayn”, Kanoon Hunarii Shi‘ii. Tarehe ya kuchapishwa: 30 Mordaad 1399 Sh / 20 Agosti 2020 M.
  • Tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Faryād ‘Labbaik Yā Husayn’ zanān qabīlah Banī-Asad dar haram Sayyid ash-Shuhadā tanīn-andāz shud”, Khabarguzārī-ye Mehr, 8 Desemba 2012, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Kurdī, Hamīdrizā; “Shī‘iyān Nijeriyah (Fursat-hā, Tahdīd-hā, Bāvar-hā)”, Nashriyah Payām, toleo la 116, Majira ya Baridi 2015.
  • Kaf‘amī, Ibrāhīm bin ‘Alī ‘Āmilī, Al-Misbāh fī al-Ad‘iyah wa as-Salawāt wa az-Ziyārāt, Qum, Dār ar-Ridhā, 1405 H.
  • Kulaynī, Muhammad bin Ya‘qūb bin Is’hāq, Al-Kāfī, Qum, Dār al-Hadīth, 1429 H.
  • “Labbaik Yā Husayn jadīdtarīn athar Hāj Sādiq Āhangarān”, Rajā News, tarehe ya kuchapishwa: 10 Desemba 2015, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Labbaik Yā Husayn khunthī kunandah tawti’ah dushmanān ast”, Hawzah Namāyandagī Walī Faqīh dar Umūr Hajj wa Ziyārat, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Labbaik Yā Husayn mujib māndigārī guftamān ‘Āshūrā’ī ast”, Khabarguzārī Razawī, tarehe ya kuchapishwa: 24 Septemba 2017, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Labbaik Yā Husayn ya‘nī rahāyī az hameh qudrat-hā: Nuwishtārī az Ustād Hādī Surūsh – sehemu ya saba”, Shafaqnā, tarehe ya kuchapishwa: 12 Agosti 2022, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Labbaik Yā Husayn! Labbaik Yā Mahdī!”, Bahā’ī Pazhūhī, tarehe ya kuchapishwa: 2 Septemba 2022, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Labbaik Yā Husayn – (Az ‘umq jān bigū Labbaik Yā Husayn)”, Imām Hasht, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Muhaddithī, Jawād, Farhang ‘Āshūrā, Qum, Nashr Ma‘rūf, 1997.
  • Murakkabī, Sayyid Husayn, Labbaik Yā Husayn: Guftārhā-ye ‘Āshūrā’ī Sayyid Hasan Nasrullah, Tehran, Nashr Khaymah, 2014.
  • Maqrīzī, Ahmad bin ‘Alī, Imtā‘ al-Asmā‘ bimā lin-Nabī min al-Ahwāl wa al-Amwāl wa al-Hafadah wa al-Matā‘, tahqīq Muhammad ‘Abd al-Hamīd an-Numaysī, Beirut, Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah, 1420 H.
  • “Nām ‘Amaliyāt az ‘Labbaik Yā Husayn’ bih ‘Labbaik Yā ‘Irāq’ taghyīr kard”, Khabarguzārī Jumhūr, 28 Mei 2015, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Najafī, Muhammad Hasan, Jawāhir al-Kalām, kwa juhudi za Qūchānī na wengineo, Beirut, Dār Ihyā’ at-Turāth al-‘Arabī, chapa ya saba, 1983.
  • “Nidā-ye Labbaik Yā Husayn dar Īrān”, Khabarguzārī Sedā wa Sīmā, tarehe ya kuchapishwa: 29 Agosti 2020, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Nawbakhtī, Hasan bin Mūsā, Firaq ash-Shī‘ah, ta‘līq Sayyid Muhammad Sādiq Bahr al-‘Ulūm, Najaf, Maktabah al-Haydariyyah, 1388 H.
  • “Nidā-ye Labbaik Yā Mahdī hamrāh bā ‘itr Yās Mahdawī dar Mī‘ādgāh Muntazirān”, IRNA, tarehe ya kuchapishwa: 8 Machi 2023, tarehe ya kutazamwa: 12 Desemba 2023.
  • Wāqidī, Muhammad bin ‘Umar, Kitāb al-Maghāzī, tahqīq: Marsden Jones, Beirut, Mu’assasah al-A‘lamī lil-Matbū‘āt, 1409 H.
  • “Shi‘ār Labbaik Yā Husayn (a) wa Labbaik Yā Khāmene’ī dar Lāhah Holand”, Khabarnāmah Dānishjūyān Īrān, tarehe ya kuchapishwa: 13 Desemba 2012, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Shi‘ār Labbaik Yā Husayn jahānī shudah ast”, ISNA, tarehe ya kuchapishwa: 19 Agosti 2021, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Shi‘ār Labbaik Yā Husayn dar sarāsar keshwar tanīn-andāz mīshawad / Shukūh ‘Azādārī dar Ustān Ardabīl bī-nazīr ast”, Khabarguzārī Tasnīm, tarehe ya kuchapishwa: 29 Agosti 2020, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Shi‘ār Labbaik Yā Husayn mubārizah bā istikbār-sitīzī ast”, Khabarguzārī Rasā, tarehe ya kuchapishwa: 3 Novemba 2015, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Shahīd Awwal, Muhammad bin Makkī, Al-Mazār fī Kayfiyyat Ziyārāt an-Nabī wa al-A’immah ‘alayhim as-salām, Qum, Madrasah Imām Mahdī, 1410 H.
  • Shahīd Thānī, Masālik al-Afhām ilā Tanqīh Sharā’i‘ al-Islām, Qum, Ma‘ārif Islāmī, 1416 H.
  • “Bī-tawajjuhī Jāmi‘ah Bayn al-Milalī bih Naqd Huqūq Basharī Shī‘iyān Nijeriyah”, Khabarguzārī Mīzān, tarehe ya kuchapishwa: 29 Julai 2023, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • Shaykh Hurr ‘Āmilī, Muhammad bin Hasan, Ithbāt al-Hudāt bin-Nusūs wa al-Mu‘jizāt, Beirut, A‘lamī, 1425 H.
  • Sāhib bin ‘Abbād, Ismā‘īl bin ‘Abbād, Al-Muhīt fī al-Lughah, Beirut, ‘Ālam al-Kutub, 1414 H.
  • “Sahn Abā ‘Abdillah; Labbaik Yā Husayn dar hangām wurūd paykar shuhadā”, Rāskhūn.
  • Tabarī, Muhammad bin Jarīr bin Yazīd, Tārīkh al-Umam wa al-Mulūk, tahqīq Muhammad Abu al-Fadl Ibrāhīm, Beirut, Dār at-Turāth, chapa ya pili, 1387 H.
  • “Tanīn shi‘ār Labbaik Yā Husayn (a) dar marāsim tashyī‘ shahīd ‘Alī Yūsuf ‘Alā’ ad-Dīn az razmandagān Hizbullāh”, Khabarguzārī Dānishjū, tarehe ya kutazamwa: 5 Desemba 2023.
  • “Tanīn nidā-ye ‘Labbaik Yā Zaynab (s)’ dar sarāsar Īrān”, Khabarguzārī Hawzah, tarehe ya kuchapishwa: 6 Novemba 2014, tarehe ya kutazamwa: 12 Desemba 2023.
  • Fādhil Hindī, Muhammad bin Hasan, Kashf al-Lithām, Qum, Nashr Islāmī, 1416 H.
  • Farāhīdī, Khalīl bin Ahmad, Kitāb al-‘Ayn, Qum, Nashr Hijrat, chapa ya pili, 1410 H.
  • “Farākhwān Riqābatī Hurūf Nigārī Labbaik Yā Husayn”, Kānūn Honarī Shī‘ī, tarehe ya kuchapishwa: 21 Agosti 2020.