Dua ya Arubaini ya Sahifa Sajjadiyya
Dua ya Arubaini ya Sahifa Sajjadiyya: ni miongoni mwa dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), aliyekuwa akiisoma hiyo pale alipokuwa akikumbuka kifo au kusikia habari za msiba. Katika dua hii, Imam (a.s) anamuomba Mwenye Ezi Mungu amuepushe na udanganyifu wa tamaa ya nafsi ya kushikamana na mbali na ya muda mrefu. Badala yake, anamuomba ajiandae kwa ajili ya kifo chema kwa kufanya matendo mema. Dua hii inawasilisha ombi la mja la kuzoena kifo (kukubaliana na maamuzi ya kifo na kuto), na kuwa shauku ya kukutana na Mwenye Ezi Mungu. Kuna wanazuoni kadhaa wa lugha mbali mbali waliowasilisha tafsiri zao chambuzi kuhusiana na Dua ya Arubaini, sambamba na dua nyengine za kitabu kitakatifu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa juhudi hizo, pamoja na kazi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiajemi (Kifgarsi), ambazo ni pamoja na; kitabu cha Diare Asheqan, cha mwanazuoni Hussein Ansarian na Shohud wa Shenakht, cha Sheikh Hassan Mamduhi Kermanshahi. Kadhalika, waandishi wengine wamewasilisha uchambizi wao kwa lugha ya Kiarabu. Miongoni mwa kazi maarufu zilizoandikwa kwa lugha hiyo, inapatikana katika kitabu kiitwacho Riadhu as-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo Yaliyomo Ndani ya Dua ya Arubaini Dua ya arubaini, mojawapo ya dua zilizomo katika kitabu cha Sahifa Sajjadiya, nayo ni ile dua iliyokuwa ikisomwa na Imam Sajjad (a.s.) pindi alipokuwa akilizingatia la mauti, au pale anapofikishiwa taarifa za kifo cha mtu fulani. Madhumuni msingi ya dua hii; yanahusiana na maombi ya Imamu Sajjad (a.s), aliyoyawasilisha kwa Mwenye Ezi Mungu amuepushia na matamanio ya kuishi muda mrefu, ambayo ndiyo sababu inayomtumbukiza mwanadamu katika hali ya ghafla, na kusahau mauti. Aidha, dua hii inasisitiza umuhimu wa kuwa katika hali ya maandalizi ya mauti kupitia utendaji wa amali njema, pamoja na kuwa na uzoefu wa kirafiki na mauti, na kutoyakhofu mauti hayo kwa namna yoyote ile. [1] Mafunzo ya dua ya arubaini yamewasilishwa katika vipengele vifuatavyo: • Kujiepusha na matumaini marefu ya kidunia (tamaa ya kuishi maisha marefu). • Kuondokana na tamaa ya kuishi maisha marefu, na kushika njia ya kutenda yaliyo ya haki na sahihi, kama ni njia msigi ya kuepukana na hilo. • Ombi la kupata ukumbusho wa daima wa kukumbuka kifo. • Kuomba kupana hisia ya kupenda mauti, na kupata amani katika kivuli cha hisia hiyo. • Kuomba hufadhi na ulinzi dhidi ya udanganyifu wa matumaini ya uongo. • Matumaini ya kuishi maisha marefu (matumaini ya kidunia), ndilo pingamizi kuu la ukamilifu wa mja. • Kughafilika na mauti ni ukinzani dhidi ya hakika na lengo kuumbwa kwa ulimwengu. • Shauku ya kukutana na Mwenye Ezi Mungu. • Ombi la kuomba taufiki ya kutenda amali njema kwa ajili ya maandalizi ya akhera. • Ombi la kuomba mauti yatakayomkuta mtu akiwa katika hali ya uelekezi, unyenyekevu, na majuto ya kweli (toba ya kweli). • Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wa thawabu za watendao mema na mrekebishaji wa vitendo vya mafisadi. • Umuhimu wa kuomba ombi la kupata mwisho mwema, ni sawa na umuhimu wa kuomba kuishi maisha adilifu. [2] Tafsiri Chambuzi za Dua ya Arubaini Kuna wanazuoni wengi walioshika kalamu katika kufanya kazi ya kufasiri na kuichambua Dua hii ya Arobaini, sambamba na dua nyengine zakitabu cha Sahifa Sajjadiyya kwa lugha mbali mbali. Miongoni mwa kazi mbali mbali zlizoandikwa kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na: kitabu kiitwacho Diare Ashiqan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [3] Shuhud wa Shenakht, cha Mohammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, [4] na Sharh wa Tarjumeh Sahifa Sajjadiyya, ambacho ni kazi ya Sayyid Ahmad Fahri. [5] Aidha kuna baadhi ya wanazuoni waliotumia muda wao wakifasiri na kuichambua dua ya arubaini ya Sahifa Sajjadiya kwa lugha ya Kiarabu sambamba na dua nyengine mbalimbali zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilizoandikwa kwa luhga ya Kiarabu katika mlolongo wa kazi hizo ni pamoja na; Riadhu al-Salikin, cha Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi iliyofanya na Muhammad Jawad Mughniyayh, [7] Riadhu al-Arifina, kitabu kilichotungwa na Muhammad bin Muhammad Darabi, [8] pamoja na Afaqu al-Ruh, kazi ya Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [9] Ukiachana na kazi hizo maridadi, pia kuna waliochukua bidii ya kukusanya msamiati wa maneno yaliyotumika katika dua hii, sambamba na dua ndyengine za Sahifa Sajjadiyya, kisha kuuchambua na kuuweka katika mfumo wa kitabu. Miongoni mwa vitabu vilivyotoa ufafanuzi wa lugha kuhusiana na dua hizo, ni kama vile; Ta'liqat 'ala al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Faidhu Kashani, [10] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Izzu al-Din Jaza'iri. [11] Matini ya Kiarabu ya Dua ya Arubaini Pamoja na Melezo Yake kwa Kiswahili
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا نُعِيَ إِلَيْهِ مَيِّتٌ، أَوْ ذَكَرَ الْمَوْتَ Na hii (ifuatayo) ilikuwa ni miongoni mwa dua zake (rehema na amani ziwe juu yake) aliokuwa akisoma pindi aliposikia habari za kifo cha mtu, au alipokumbuka mauti. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اكْفِنَا طُولَ الْأَمَلِ، وَ قَصِّرْهُ عَنَّا بِصِدْقِ الْعَمَلِ حَتَّى لَا نُؤَمِّلَ اسْتِتْمَامَ سَاعَةٍ بَعْدَ سَاعَةٍ، وَ لَا اسْتِيفَاءَ يَوْمٍ بَعْدَ يَوْمٍ، وَ لَا اتِّصَالَ نَفَسٍ بِنَفَسٍ، وَ لَا لُحُوقَ قَدَمٍ بِقَدَمٍ Ewe Mwenye Ezi Mungu, mshushie rehema na amani Yako Muhammad na Aali zake. Na utuepushe na shari ya matumaini marefu (matumaini ya kuishi maisha marefu), na uyapogowe (uyasitishe/uyazuiye) matumaini hayo yasiwezu kutufikia, kwa kutuimarisha na kutuwezesha kufanya matendo ya haki, ili (yawe ni ngao itakayotufanya) kamwe tusitarajie kukamilisha saa moja baada ya nyingine, wala kumaliza siku moja baada ya nyingine, wala kuvuta pumzi moja baada ya nyingine, wala kupiga hatua moja baada ya nyingine. وَ سَلِّمْنَا مِنْ غُرُورِهِ، وَ آمِنَّا مِنْ شُرُورِهِ، وَ انْصِبِ الْمَوْتَ بَيْنَ أَيْدِينَا نَصْباً، وَ لَا تَجْعَلْ ذِكْرَنَا لَهُ غِبّاً
Na utuepushe na hadaa zake (hadaa za dunia), na utupe amani dhidi ya shari zake. Yafanye (yachomeke) mauti (yetu) yawe daima mbele ya macho yetu, na usiifanye kumbukumbu ya kukumbuka kwetu (kifo) kuwa ni nadra. وَ اجْعَلْ لَنَا مِنْ صَالِحِ الْأَعْمَالِ عَمَلًا نَسْتَبْطِئُ مَعَهُ الْمَصِيرَ إِلَيْكَ، وَ نَحْرِصُ لَهُ عَلَى وَشْكِ اللَّحَاقِ بِكَ حَتَّى يَكُونَ الْمَوْتُ مَأْنَسَنَا الَّذِي نَأْنَسُ بِهِ، وَ مَأْلَفَنَا الَّذِي نَشْتَاقُ إِلَيْهِ، وَ حَامَّتَنَا الَّتِي نُحِبُّ الدُّنُوَّ مِنْهَا Na miongoni mwa matendo mema, tujaalie tendo jema fulani ambalo litatufanya tuione safari ya kurejea Kwako kuwa ni yenye utulivu na amani. Na utufanye tuwe na shauku kubwa ya kukutana nawe mapema, ili kifo kwetu sisi kiwe na jambo la faraja tunalofarijika nalo, na ni kituo cha upendo tunachokitamani, na kiwe ni kama jamaa wa karibu ambaye tunapenda kuwa naye.
فَإِذَا أَوْرَدْتَهُ عَلَيْنَا وَ أَنْزَلْتَهُ بِنَا فَأَسْعِدْنَا بِهِ زَائِراً، وَ آنِسْنَا بِهِ قَادِماً، وَ لَا تُشْقِنَا بِضِيَافَتِهِ، وَ لَا تُخْزِنَا بِزِيَارَتِهِ، وَ اجْعَلْهُ بَاباً مِنْ أَبْوَابِ مَغْفِرَتِكَ، وَ مِفْتَاحاً مِنْ مَفَاتِيحِ رَحْمَتِكَ
Na pindi utakapokileta (utakapokiingiza kifo chako) kwetu na kukishusha juu yetu, basi tufanye tuwe ni wenye furaha kwa ujio wake kama (tunavyonfurahia) mgeni, na utufariji kwa kuwasili kwake. Wala usitutaabishe kwa ugeni wake, na wala usituaibishe kwa ziara yake. Na ukijaalie kuwa ni mlango miongoni mwa milango ya msamaha Wako, na ufunguo miongoni mwa funguo za rehema Zako. أَمِتْنَا مُهْتَدِينَ غَيْرَ ضَالِّينَ، طَائِعِينَ غَيْرَ مُسْتَكْرِهِينَ، تَائِبِينَ غَيْرَ عَاصِينَ وَ لَا مُصِرِّينَ، يَا ضَامِنَ جَزَاءِ الْمُحْسِنِينَ، وَ مُسْتَصْلِحَ عَمَلِ الْمُفْسِدِينَ Tufishe tukiwa katika hidaaya (uongofu), na wala (usitufishe tukiwa) katika upotofu. (Tufishe tukiwa) katika hali ya utiifu kamili, na wala tusiwe katika ujabari (katika hali ya kutakabari), (tufishe) huku tukiwa ni wenye kutubia, na si wenye kufanya maasi wala kushikilia madhambi. Ewe mdhamini wa jaza njema kwa walio wema, na Mrekebishaji wa amali za mafisadi.