WikiShia ni Ensaiklopidia ya mtandaoni ambayo dhamira yake ni kueleza na kubainisaha dhana, fikra na mafahimu ambazo zina mchango katika kufahamu Ushia na madhehebu zingine. Mafahimu hizi zinajumuisha itikadi, watu, elimu (kama teolojia, fiqhi, usulul fiq’h), vitabu, maeneo, matukio, hafla, amali za Hija, makundi yanayoamini Ahlul-Bayt (a.s), historia ya Ushia na kila mafuhumu na maana nyingine ambayo kwa namna moja au nyingine ina uhusiano na Ahlul-Bayt (a.s) na wafuasi wao. Istilahi na majina ambayo ni lazima kwa ajili ya kutekeleza na kufikisha risala hii yanatolewa ufafanuzi na maelezo.

Nembo ya Ensaiklopidia ya WikiShia

Katika WikiShia, kunaepukwa suala la kuwasilisha uchambuzi, tathmini na maoni ya mtu binafsi pamoja na nadharia mpya ambazo hazijathibitishwa kitaalumu na kielimu. Suala la kuhukumu kuhusiana na hitilafu za kielimu na kihistoria ni jukumu la wasomaji na katika hili WikiShia haiegemei upande wowote. Kwa kuzingatia tofauti za kimadhehebu, waandishi wa WikiShia wamejikita katika kutumia vyanzo vinavyokubalika na madhehebu kuu mbili za Kiislamu (Shia na Sunni).

Mtandao huu wa WikiShia una mfungamano na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s). Ensaiklopidia hii kwa sasa inaendesha shughuli zake ikiwa na jumla ya lugha 22.

Msukumo na malengo ya kuanzishwa

Katika Ensaiklopidia kuna taarifa nyingi kuhusiana na Uislamu na madhehebu ya Kishia; lakini kwa kuzingatia kuwa, waandishi wa Ensaiklopidia hii ima hawana ufahamu sahihi kuhusiana na maarifa ya Kiislamu au yumkini hawana itikadi na imani na Uislamu au madhehebu ya Kishia, na kwa msingi huo kunashuhudiwa makosa katika makala zinazohusiana na Uislamu na madhehebu ya Shia. Kwa kuzingatia matatizo yaliyopo katika mitandao ya intaneti kuhusiana na imani na itikadi ya madhehebu ya Shia na vilevile Mashia duniani na utafutataji kwa ajili ya kupata kwa urahisi taarifa au makala za itikadi asili za Uislamu na madhehebu ya Shia, Idara ya Masuala ya Kiutamaduni ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), ilichukua uamuzi wa kuanzisha Ensaiklopidia ya mtandaoni ya WikiShia kwa shabaha ya kutambulisha na kutetea fikra na maktaba ya Ahlul-Bayt (a.s).

Historia ya WikiShia

 
Uzinduzi rasmi wa Ensaiklopidia ya Wikishia na Hassan Rouhani, aliyekuwa Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Juni 22, 2014.

Tarehe 22 Mei 2013 kulifanyika kikao cha kwanza cha uratibu wa waandishi wa WikiShia na baada ya vikao kadhaa, hatimaye Juni 18 mwaka huo huo, makala ya kwanza WikiShia iliwekwa katika mtandao wa Wikishia.

Tarehe 22 Juni 2014 sambamba na kufanyika Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s) mjini Tehran, mtandao wa WikiShia ulizinduliwa rasmi na aliyekuwa Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hassan Rouhani.

Sifa Maalumu

Baadhi ya sifa maalumu za WikiShia ni:

Wigo mpana wa maudhui

Maudhui na muhtawa wa WikiShia ni:

  • Itikadi, watu, elimu (kama teolojia, fiqhi, usulul fiq’h), vitabu, maeneo, matukio, hafla, amali za Hija, makundi yanayoaamini Ahlu-Bayt (a.s), historia ya Ushia na kila mafuhumu na maana nyingine ambayo kwa namna moja au nyingine ina uhusiano na Ahlul-Bayt (a.s) na wafuasi wao.
  • Mafahimu (dhana) jumla ya Kiislamu yanayoaminiwa na Waislamu wote au yanayohusiana na historia ya Uislamu pia yanatajwa na kubainishwa katika mtandao huu wa WikiShia.
  • Mafahimu na fikra zinazohusiana na madhehebu zingine za Kiislamu zinatambulishwa katika WikiShia ikiwa kwa namna fulani zinahusiana na maktaba (njia) ya Ahlu al-Bayt (a.s) au kama matumizi yake katika makala za WikiShia ni mengi sana.

Uangalizi wa muhtawa

Katika WikiShia kuna uangalizi wa muhtawa (kinachoandikwa na kuwasilishwa). Kwa muktadha huo, Ensaiklopidia ya WikiShia inahesabiwa kuwa chanzo chenye itibari cha kutambulisha madhehebu ya Shia. Kwa sasa WikiShia ni Ensaiklopidia ya maarifa ambayo inafanya kazi zake kwa mipaka maalumu (kutokana na sababu mbalimbali); lakini katika mustakabali ina mpango wa kufanya mambo yake kwa uhuru kamili ili Mashia wote wenye mapenzi, shauku na uwezo waweze kuwa na mchango katika kuikamilisha Ensaiklopidia hii na hivyo kusambaza mafundisho ya Maktaba ya Ahlul-Bayt (a.s). Ili kuingia katika Ensaiklopidia hii ni lazima uidhinshwe na wakurugenzi na viongozi husika. Sehemu hii katika WikiShia inamruhusu mtumiaji kwa kushirikiana aweze kuongeza katika uandishi wa makala na hivyo azidishe thamani ya kielimu ya makala.

Baraza la Mipango

Baraza hili linaundwa na wakurugenzi na wasimamizi wa lugha, wakurugenzi wa kielimu na wataalamu wa WikiShia. Baraza hili lina jukumu la kuandaa sera, mipango na mikakati katika vitengo mbalimbali vya WikiShia.

Sera zisizoegemea upande wowote

  • Sera zisizoegemea upande wowote zinachungwa katika maudhui za mijadala ya kifikra ndani ya madhehebu ya Shia na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s); lakini ni jambo lililo wazi kwamba, WikiShia ni muenezaji na msambazaji wa maktaba na mafundisho ya Ahlu-Bayt (a.s) na kwa muktadha huo makala zinaandikwa kwa minajili ya kubainisha na kutetea mafundisho haya.
  • Makala za WikiShia, sio makala kwa ajili ya masuala ya kielimu na kiutafiti. Kwa maana kwamba, sio kwa ajili ya kuzitumia katika masuala ya mijadala na uga wa kiutafiti. Kwa maneno mengine ni kwamba, mjadala sio wa moja kwa moja na wala hazifanyiki juhudi za kutatua matatizo ya kielimu; bali linalofanywa na WikiShia ni kujaribu kuwasilisha taarifa kwa mujibu wa vyanzo vilivyopo na kwa msingi huo, waandishi hawapaswi kuwasilisha mawazo na mitazamo yao binafsi.
  • Utoaji hukumu kuhusiana na hitilafu za kielimu na kihistoria umeachiwa wasomaji wetu wapendwa.
  • Katika hili mtandao wa WikiShia hauegemnei upande wowote ule. Kwa kuzingatia tofauti za kimadhehebu, waandishi wapendwa wa makala za WikiShia wanajitahidi kadiri wawezavyo kutumia vyanzo vinavyokubalika kutoka kwa madhehebu kuu mbili za Kiislamu (Shia na Sunni).

Sifa zingine muhimu

  • Uwezekano wa kufanya masahihisho daima ya makala.
  • Uwezekano wa kujadidisha na kuongeza taarifa za makala.
  • Kuweko ukurasa wa historia fupi ya makala. Katika ukurasa wa historia fupi, kila mabadiliko yanayofanyika katika makala yanaweza kuonekana. Watembeleaji (wa mtandao wa WikiShia) wanaweza kujua kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na waandishi.
  • Ukurasa wa mabadiliko ya karibuni. Ukurasa huu unaowanyesha watumiaji mabadiliko ya karibuni yaliyofanywa katika kurasa zote za WikiShia.
  • Uwezekano wa kurejesha maudhui na mabadiliko ya zamani.
  • Maunganisho ya makala kila moja; kwa njia hii, msomaji wa makala anaweza kufungua na kusoma ukurasa unaohusiana na dhana hiyo ili kuelewa kila moja ya maneno yaliyotumiwa katika maandishi katika lahadha hiyo hiyo bila ya kuhitajia kutumia njia ya “tafuta”. Sifa hii inamfanya mtembeleaji kuelewa kwa urahisi dhana zote zinazotumiwa katika makala hiyo anaposoma kila makala na kupata taarifa kamili kuhusu maudhui aliyosoma.
  • Kutumia viuanganishi (links) mwishoni mwa makala.
  • Mchoro wa viboksi (Navigation templates). Hivi ni visanduku vinavyokusanya dhana zinazohusiana na makala katika kisanduku mlalo kilicho chini ya makala. Michoro na vielelezo hivi wakati mwingine hutumiwa kama visanduku wima juu ya vifungu. Uhusiano kati ya majina yaliyojumuishwa katika majedwali haya ni ya sura ya upana; hii ina maana kwamba anuani zote za chini zimewekwa chini ya anuani moja jumuishi.
  • Sanduku la taarifa (onfobox). Masanduku ambayo yamewekwa juu ya kifungu yana jukumu la kukusanya taarifa muhimu za kifungu kwa sura ya mukhtasari. Kwa kurejea katika sanduku la taarifa, unaweza kujua taarifa zilizomo katika maandishi ya makala bila kusoma makala.
  • Ukurasa wa majadiliano: Kila ukurasa wa makala katika WikiShia una ukurasa wa majadiliano. Watumiaji katika ukurasa huu wa majadiliano wanaweza kuandika na kuwafikishia mitazamo yao waandishi na wasahihishaji wa makala kuhusiana na makala husika. Ukurasa wa majadiliano, kimsingi ni mahali kwa ajili ya mazungumzo ya wenye mitazamo na maoni na wapenzi wa maudhui ya makala husika, na hilo linasaidia kutajirisha muundo wa makala na maudhui iliyoandikwa ya makala husika.

Nembo

Takribani katikati ya mwaka 2023, mtandao wa WikiShia ulizindua nembo (logo) yake mahsusi. Nembo hii inajumuisha heruri za “و” na “W” ambazo ni ishara ya herufi ya kwanza ya WikiShia katika lugha za Kifarsi na lugha za kilatini. Katika nembo hii kumetumiwa kuba na mihrabu kama nembo za Kiislamu na madhehebu ya Kishia.

Historia ya uzinduzi wa lugha mbalimbali za WikiShia

Namba Lugha Tarehe ya uzinduzi Makala ya kwanza Maelezo
1 Kifarsi June 18, 2013
صریا
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
2 Kiarabu November 25, 2013
تهذيب الأحكام (كتاب)
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
3 Kingereza November 30, 2013
Al-Hannana Mosque
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
4 Kiurdu March 18, 2014
امام علی علیہ السلام
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
5 Kituruki April 10, 2014
Hz. Fatıma Zehra (s.a)
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
6 Kihispania May 22, 2014
Profeta Muhammad (PBD)
Ilizinduliwa tarehe 1 Julai 2014, wakati wa Kongamano la Sibt al-Nabi (a.s).
7 Kiindonesia August 25, 2014
Imam Ali bin Abi Thalib as
8 Kifaransa August 26, 2014
Verset d'al-Mubâhala
9 Deutsch September 20, 2016
Die Vier Stellvertreter
10 Русский February 28, 2018
Хадис Сакалайн
11 中文 July 15, 2022
后世
Ilizinduliwa katika kikao cha 7 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt
12 Kiswahili July 18, 2022
Eid al-ghadir
Ilizinduliwa katika kikao cha 7 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt
13 हिन्दी July 29, 2022
आय ए इकमाल
Ilizinduliwa katika kikao cha 7 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt
14 বাংলা August 22, 2022
প্রথম মুসলিম
Ilizinduliwa katika kikao cha 7 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt
15 Тоҷикӣ August 22, 2022
Аввалин мусулмон
Ilizinduliwa katika kikao cha 7 cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt
16 Pashto January 16, 2023
د شیعو امامان
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
17 Azəricə January 17, 2023
Məvəddət ayəsi
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
18 Burmese January 26, 2023
آیه صلوات
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
19 Kireno February 1, 2023
Imames xiitas
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
20 Kiitalia February 8, 2023
WikiShia
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
21 Kihausa February 9, 2023
Kyautar zobe
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
22 Thai February 12, 2023
อะบาอับดิลลาฮ์ (ฉายานาม)
Ilizinduliwa katika mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Vyanzo