Kizito kikubwa

Kutoka wikishia

Kizito kikubwa (Kiarabu: الثقل الأكبر) ni sifa ambayo aliitumia Mtume (s.a.w.w) kuielezea na kuitambulisha Qur'an Tukufu katika hadithi ya Vitizo viwili (Hadith al-Thaqalain). Neno Thiqlu linamaana ya mzigo mzito[1] na neno Thaqlu linamaana ya kila kitu yenye thamani na chenye hadhi kubwa.[2] kwa mujibu wa maneno ya Fairuz abaad mwanazuwoni wa kilugha katika karne ya tisa qamariyah, neno Thaqalaini katika hadithi thaqalaini limetokana na Thaqlu.[3]

Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu za hadithi ya Thaqlaini, Mtume (s.a.w.w) katika hadithi hii, ameiita qur'ani kuwa ni Thaqlul- Akbar (kitu kikubwa chenye thamani, na kizazi chake akakiita kuwa ni Thaqlul- asghar (kizoto kidogo) na alivitambulisha vitu hivyo na kusema kuwa ikiwa umati wake utashikamana na vitu viwili hivyo, kamwe hauta potea.[4]Mtume (s.a.w.w) pia katika hotuba ya ghadiir aliiarifisha Qur'an kama Thaqlul- Akbar na Ali (a.s) na kizazi chake kitwaharifu akakiarifisha kuwa ni thaqlul- asghar.[5]

Imamu Ali (a.s) nae pia katika maeneo mbali mbali alijitambulisha kama Thaqlul- Asghar na Qur'an kama Thaqlul- Akbar, na miongoni mwa sehemu hizo ni katika moja wapo ya khutba zake[6] na pia katika usia wake aliompata Kumaili bin Ziyad.[7]

Ama kuhusiana na kwamba kwa nini qur'an imesifiwa kwa neno Thaqlul- Akbar imesemwa kwamba kutokana na ukweli kwamba kizazi cha Mtume (s.a.w.w) ni chenye kuifuata Qur'an, ndio maana Qur'an ikaarifishwa kuwa ni kubwa na yenye hadhi kubwa zaidi kuliko Itrah na kizazi chake.[8] Baadhi pia wamesema:Kutokana na ukweli kwamba Qur'an ni muujiza wa Mtume (sa.w.w) na huzingatiwa kuwa ndio msingi wa dini, hivyo basi Qur'an ni kubwa zaidi na yenye hadhi kubwa zaidi kuliko kizazi na Itrah (Ahlul-Bayt) .[9]

Rejea

  1. Ibnu Mandhuur, Lisaanul-arab, cha mwaka 1414, juz. 11, uk. 85 (chini ya neno Thaqlu).
  2. Fairuzi abad, Al-qaamusul-muhiit, cha mwaka 1426q, uk. 972, (chini ya neno Thaqlu)
  3. Fairuzi abad, Al-qaamusul-muhiit, cha mwaka 1426q, uk. 972, (chini ya neno Thaqlu).
  4. Ayyaashiy, tafsiirul-ayaashiy, cha mwaka 1380q, juz. 1, uk. 5.
  5. Yaaquubiy, Taarikhu Ya'aqubiy, juz. 2, uk. 112, Ibnu Twawous, Iqbaalul-aamal, cha mwaka 1409q, juz. 1, uk. 456.
  6. Nahjul-balaghah, khutba namba 87.
  7. Majlisiy, Buharul-an'waar, cha mwaka 1390q, juz. 74, uk. 375.
  8. Bahraaniy, Sharhu nahju-balagha, cha mwaka 1404q, juz. 2, uk. 187.
  9. Khui, Minhaajul-baraa'ah, cha mwaka 1400q, juz. 5, uk. 234.

Vyanzo

  • Ibnu Twawous, Ali bin Mussa, Iqbaalul-aamaal, Tehran, Darul-kutubil-islaamiyah, cha mwaka 1409q.
  • Ibnu Mandhuur, Muhammd, bin Mukrim, Lisaanul-arab, kilicho sahihishwa na Ahmad Faaris, Bairut, Darul-fikri lit-twiba'ah wan-nashri wat-twazi'I, na Darus-swaadir, cha mwaka 1414q.
  • Bahraaniy, Ibnu Maitham, sharhu nahjul-balaghah, Qom, Matba'atu haidariy. Cha mwaka 1404.
  • Khui, Miirzaa Habiibul-laahi, Minhaajul-baraa'ah fii sharhi nahjul-balaghah, kilicho sahihishwa na Sayyid Ibraahim miyanjiiy, Tehran, Maktabatul-islaamiyah, mwaka 1400q.
  • Ayyasiy, Muhammad bin Masoud, Tafsiirul-ayyashiy, kilicho hakikiwa na Sayyid Ibrahiim Haashim Rasouliy Mahallatiy, cha chapa ya Aalamiyah, Tehran, mwaka 1380q.
  • Fairuza abaadiy, Muhammad bin Yaaqub, Al-qaamusul-muhiit, Bairut, Muassasatur-risaalah, cha mwaka 1426 / 2005 A.D
  • Majlisiy, Muhammd Baaqir, Buharul-an'waar Al-jaamiatu lidurarl-i Akhbaaril-aimmatil-at'haar, Tehran, Darul-kutubil-islaamiyah, cha mwaka 1390q.
  • Yaaqubiy, Ahmad, Taarikhu Yaaqubiy, Bairut, Daru Swaadir, (Biitaa).