Nenda kwa yaliyomo

Silaha za Maangamizi ya Halaiki (WMD)

Kutoka wikishia

Silaha za Maangamizi ya Halaiki (WMD): Mada ya tumizi ya silaha za maangamizi ya halaiki inahusiana na suala la matumizi ya silaha zinaangamiza idadi kubwa ya watu wa kawaida ambao si wanajeshi. Silaha hizi huwa na athari mbaya mno kwa mazingira ya tabia nchi pamoja na viumbe waishiwo ndani yake. Kwa mujimbu wa imani ya mafaqihi wa upande wa madhehebu ya Kishia, ni kwamba: Haijuzu kwa Muislamu yeyeto yule kuanzisha matumizi ya silaha hizo dhidi ya adui yake. Ila kuna ukinzani baina ya wanazuoni katika hali ambayo, adui yao atakuwa ndiye mwanzishi wa matumizi hayo! Katika hali kama hiyo, wapo wanaoruhusu matumizi ya silaha hizo, huku wengine wakishikilia msimamo wa kuharamisha kabisa kabisa bila ya kutofautishi baina ya hali mbili hizo. Mara baada ya kuongezeka kwa silaha hatari zikiwemo silaha za nyuklia na kemikali, wataalamu wa fiqhi ya Kishia walilazimika kuchukua msimamo wa wazi juu ya matumizi ya silaha hizo. Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa juu na marja’a (mufti mwenye hadhi maalumu) wa Kishia aliyeko Iran, alitoa fatwa iliyo wazi kabisa akisema: Hairuhusiwi kwa Muislamu yeyote yule kutengeneza, kutumia au kutunza silaha za nyuklia. Katika mtazamo wa Ayatullahi Khamenei, silaha hizi ni adui dhidi ya uhai wa binadamu wote kwa jumla, na ni haramu kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislamu.

Maana na Umuhimu wa Maudhui ya Silaha za Maangamizi ya Halaiki Silaha za maangamizi ya halaiki zinaelezwa kuwa ni zile ambazo, licha ya kutumiwa kwa malengo ya kijeshi, pia husababisha vifo vya raia wasiohusika na walio nje ya uwanja wa kivita, vile vile hupelekea uhuharibifu wa mazingira kwa njia isiyoweza kurekebishwa. [1] Suala la uwezekano wa silaha za kivita kuwaathiri raia—akina mama, watoto, wazee na hata mateka waliomo mikononi mwa Kiislamu—lilikuwapo tangu enzi za bwana Mtume (s.a.w.w), nalo ni suala lililoripotiwa ndani ya vyanzo mbali mbali vya Riwaya za Kishia. [2] Kwa mujibu wa ripoti ya Profesa Abul Qasim Alidoust, ambaye ni mmoja wa wakufunzi wa fiqhi za kiwango cha juu huko Qom, ni kwamba; masuala ya athari za silaha kwa wasiokuwa wapiganaji, yamekuwa yakijadiliwa na wanazuoni wa Kishia kwa muda wa zaidi ya karne kumi hivi sasa (kiasi cha muda wa miaka elfu). [3] Katika karne ya 14 na 15 ya Shamsi (sawa na karne ya 20-21 Miladi), kumezuka aina mpya kabisa za silaha za maangamizi, kama vile nyuklia na kemikali, jambao ambalo limeleta mabadiliko kadhaa ya kimsingi katika dhana ya vita na kuibua mijadala na fikra mbali mbali ambazo hazikufikirika wala kuhapo awali. [4] Kwa mantiki hii, suala hili katika zama za hivi sasa, linatazamwa kama changamoto mpya kabisa ya kifikra ndani ya sheria za Kiislamu, inayojulikana kitaalamu kama Masaa'il Mustahdathah (masuala mapya ya zama maalumu). [5] Msimamo wa Fiqhi ya Kishia kuhusiana na Silaha za Maangamizi ya Halaiki (WMDs) Wanazuoni wa Kishia wakichambua suala la matumizi ya silaha za maangamizi ya halaiki (kama nyuklia au kemikali), wameligawa suala hili katika nyanja tatu zifuatazo: • Kutumia silaha hizo kabla ya adui ya adui zao kuwapiga kwa kutumia silaha hizo • Kuzalisha au kuzihifadhi silaha hizo haramu. • Kutumia silaha hizo wakati wa dharura. Kwa mujibu wa utafiti, wanazuoni wote wa Kishia, wote wanakubaliana kuwa; ni haramu kwa Muislamu kutumia silaha za maangamizi katika hatua ya kwanza. [6] Abu Al-Qasi Alidust, ambaye ni miongoni mwa watafiti wa upande wa madhehebu ya Shia, akijadili suala hili anasema kwamba: Kwa upane wa madhehebu ya Kishia, kuna fatwa zenye mizizi ya zaidi ya miaka elfu moja iliopita, ambazo zimeweka wazi hukumu ya matumizi ya aina kama hizo za silaha. Kwani Uislamu hauruhusu kabisa matumizi ya silaha za maangamizi ambazo zinateketeza mazingira na uhai wa viumbe mbali mbali waliomo ndani yake. [7] Kwa kuzingatia kuibuka kwa silaha mpya za maangamizi (kama vile nyuklia na kemikali), [8] baadhi ya wanazuoni mashuhuri wa Kishia wametoa fatwa za kuharamisha uzalishaji pamoja na matumizi ya silaha hizi. Ayatollah Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameharamisha moja kwa moja uzalishaji pamoja na matumizi ya silaha za nyuklia. Fatwa yake hii imetoka baada ya kuzingatia tisho kubwa la silaha hizo kwa maisha ya binadamu. [9] Wanazuoni wengine wa fiqhi kama vile; Makarem Shirazi, Nuri Hamadani, Jafar Subhani na Jawadi Amuli, pia nao wameunga mkono moja kwa moja msimamo huu wa kisheria. [10] Makarem Shirazi akijadili hukumu ya suala hili, amesisitiza kuwa; kutengeneza na kutunza silaha hizo ni kinyume na hisia za kimaumbile na utu wa mwanadamu. [11] Katika fiqhi ya Kishia, kuna mitazamo tofauti kuhusiana na uhalali wa matumizi ya silaha za maangamizi ya halaiki, katika hali ambayo ushindi wa Waislamu utategemea matumizi ya silaha hizo. Baadhi ya wanazuoni mashuhuri akiwemo; Muhaqqiq al-Hilli (602–676 Hijiria), Sheikh Tusi (385–460 Hijiria), pamoja na Shahid Thani (911–955/965 Hijiri), wanaamini kwamba; matumizi ya silaha hizo yanaweza kuruhusiwa katika kipiti cha hali kama hiyo ya dharura. [12] Kwa upande mwingine, Agha Dhiyaa al-Iraqi hakubaliani na nadharia hii. Bali yeye anaona kuwa; ni haramu kutumia aina kama hiyo ya silaha, hata kama ushindi wa Waislamu utategemea matumizi ya silaha fulani hatari. Akisisitiza hilo amesema kwamba; Uislamu ulikataza matumizi ya sumu, ambayo kwa zama zake ilihesabika kama ni moja ya silaha hatari kwa mazingira pamoja na jamii ya viumbe hai. [13]