Ulul-amri

Kutoka wikishia
Aya ya ulul-amri: Aya ya 59 surat al-Nisaa

Ulul-amri (Kiarabu: أولو الأمر) ina maana ya wenye mamlaka, hawa ni watu ambao ni wajibu kuwatii kwa msingi wa Aya ya Ulul-Amr. Istilahi hii imekuja na kuelezwa ndani ya aya ya 59 ya surat al-Nisaa. Ama kuhusiana na kuhifadhiwa na Ismah ya Ulul-amri na kwamba ni watu gani au ni akina nani hao Ulul-amri, ni suala ambalo limekuwa na mitazamo na nadhiria tofauti ndani ya vitabu vya kiitikadi na tafsiri, vya kishia na kisunni.

Kwa mujibu wa itikadi ya madhehebu ya Imamiyyah makusudio ya neno Ulul-amri, ni Maimamu wa Kishia, lakini kwa mtazamo wa Ahlu-sunna, Ulul-amri ni khulafaaur-rashidiin (Makhalifa walio ongoka na kuongozwa), ni watawala waadilifu na Ijmai ni miongoni mwa maswaadiq na vielelezo vya Ulul-amri.

Mashia wanaitakidi na kuamini kwamba kutokana na dalili na uthibitisho wa aya ya Ulul-amri wa kutilia mkazo na msisitizo juu ya wajibu wa kuwatii Ulul-amri bila sharti wala qaidi yolote, kwa hakika aya hii inathibitisha suala la kuhifadhika na Ismah ya Ulul-amri na wenye mamlaka hawa, lakini maulamaa wengi wa Ahlu-sunnah wanaamini na kuitakidi kwamba Ismah na kuhifadhiwa kwa Ulul-amri hakuthibiti kupitia aya hii. Yaani aya hii haithibitishi Ismah na kuhifadhiwa kwa Ulul-amri.

Aya ya Ulul-amri

Aya ya Ulul-amri au Aya ya Utiifu na twa'ah (Al-Nisaa 59) imewaamuru waumini kumtii Mwenyezi Mungu, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na Ulul-amri (wenye mamlaka na watawala). Kwa mtazamo wa Mashia na baadhi ya Ahlu-sunnah kama vile Fakhrur-raziy, aya hii inathibitisha Ismah na kuhifadhiwa kwa Ulul-amri kunako kufanya makosa na madhambi. Mashia kwa msingi wa riwaya mbali mbali, wanaitakidi na kuamini kuwa makusudio ya Ulul-amri ni maimamu wa kishia, ama Ahlu-sunnah kuhusiana na suala hili au maudhui haya wametofautiana na wamekuwa na nadharia na mitizamo tofauti kuhusiana na jambo hili kama ifuatavyo:

  1. Khulafaur-rashiidiin,
  2. kila mtawala muadilifu,
  3. Maulamaa wa kidini
  4. kundi la watu wa umati huu ni miongoni mwa vielelezo na maswadiqi ambazo maulamaa wa Ahlu-sunnah wamebainisha na kufafanua kuwa ni miongoni mwa Ulul-amri.


Maandishi na Tafsiri ya Aya

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ الله وَأَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى الله وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً


...Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyeezi Mungu na mtiini Mtume na Wenye mamlaka katika nyinyi, na kama mkigombana katika jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyeezi Mungu na Mtume ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho. Hilo ni bora zaidi na ni lenye mwisho mzuri zaidi.



(Quran: 4: 9)


Neno Ulul-amri (أولو الأمر) lina maana ya wenye mamlaka ya utawala ni neno litokalo kwenye aya 59 ya surat al-Nisaa na limechukuliwa kutoka kwenye aya ya 59 ya surat al-Nisaa kama ilivyo pokelewa kutoka kwenye aya hiyo. Wafasiri wa kishia kama vile Fadhlu binil-hasan Twabarsi na Allamah Twabatwabai[1] na maulamaa wa akida wa madhehebu ya Imamiyah[2] wamefahamu na kuthibitisha Ismah na kuhifadhiwa kwa maimamu na ulul-amri kutokana na aya hii. Vivyo hivyo wameyafahamu hayo kwa kujitegemeza kwenye riwaya mbali mbali zihusianazo na maswaadiq na vielelezo vya Ulul-amri na kwamba ni akina nani hao Ulul-amri na kupitia riwaya hizo huthibitisha na kutoa ushahidi wa kuhifadhiwa kwa maimamu kumi na mbili wa kishia na Ismah yao.[3].

Ismah na Kuhifadhiwa kwa Ulul-amri

Dalili za Mashia juu ya Ismah na kuhifadhiwa kwa Ulul-amri kwa kujitegemeza au kuitegemea aya ya Ulul-amri zimesimamia juu ya msingi huu kwamba aya ya Ulul-amri imeamrisha kuwatii Ulul-amri bila qaidi wala sharti.[4]

Dalili zao juu ya mas'ala haya kwanza ni Itlaqi ya aya (aya kutokuwa na qaidi wala sharti la kutii) kwa maana twa'ah yao haijafungamanishwa na jambo lolote wala qaidi yoyote), kwa maana kwamba aya baada ya kuamrisha kuwatii Ulul-amri, haikuleta istithnai yoyote. Pili ni kwamba ndani aya hii kuna amri ya kuwatii Ulul-amri, ikiwa imeambatana pembezoni mwake na amri ya kumtii Mtume(s.a.w.w) na amri zote zimekuja zikiwa zimeambatana. Kwa Imani na itikadi yao ni kwamba mas'ala haya yanaonyesha na kuthibitisha kwamba kama vile ambavyo ni wajibu na nilazima kumtii Mtume(s.a.w.w) bila qaidi wala sharti, vivyo hivyo ni lazima na wajibu kuwatii Ulul-amri bila qaidi wala sharti.[5] Kwa kuzingatia msingi huu, istidlali na uthibitishaji wao wa mas'ala haya unakuwa kama ifuatavyo: kwa mujibu wa aya hii, ni wajibu kuwatii Ulul-amri bila qaidi wala sharti lolote.

Kwani ikiwa Ulul-amri hawakuwa maasumiin na hawakuwa ni wenye kuhifadhiwa kutokana na utendaji dhambi na ufanyaji makosa itakuwa inamaana kuamrisha tendo la haram, kutakuwa na ukinzani wa amri na maamrisho ya aina mbili ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu kwa upande mmoja ni wajibu kuwatii Ulul-amri hivyo itatulazimu kufanya tendo la haram, na kwa upande mwingine hilo ni kitendo cha haram ambalo haipaswi kwetu sisi kulitenda. Kwa msingi huu Ulul-amri ni lazima wawe Maasumiin na walio hifadhiwa.[6]

Fakhrur-raziy ambae pia ni miongoni mwa maulama na wanazuwoni wa Ahlu-sunnah pia yeye ana mtizamo kama huu,[7] ama maulamaa wengine wa kisunni, wanamtizamo mwingine kuhusiana na mas'ala haya. Kwa mujibu wa itikadi ya maulamaa hao ni kwamba katika aya ya Ulul-amri baada ya kuamrishwa kuwatii Ulul-amri imekuja kwamba ikiwa kutakuwa na tofauti ya kimitizamo au tofauti kuhusiana na mas'ala fulani basi rejeeni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w). Alama na qarina hii (ishara) inaonyesha na kuthibitisha kwamba wajibu wa kuwatii Ulul-amri si kweli kwamba ni twa'ah (utii) isiyokuwa na qaidi wala sharti.

Wakati wowote ambapo wataamrisha tendo la haramu, haitapaswa kuwatii kwenye jamabo hilo. Na kwa msingi huu Imani na itikadi yao ni kwamba aya hii haina uthibitisho wowote kuhusiana na Ismah na kuhifadhiwa kwa Ulul-amri.[8] Mkabala wake ni kwamba itikadi na Imani ya mashia ni kwamba, amri iliyopo kwenye aya imebainishwa kwa namna ambayo haikubali istithnaa, kwa maana kwamba kwa mujibu wa mtizamo wa Urfu kuhusu jambo hili ni kuwa kinacho fahamika kutoka kwenye aya ni kwamba ni wajibu kuwatii Ulul-amri bila qaidi wala sharti na mafhumu ilzami ya maneno haya ni kwamba watu hawa wamehifadhiwa na wana Ismah.[9]

Kielelezo cha Ulul-amri

Kuhusiana na vielelezo na maswadiiq za Ulul-amri (wenye mamlaka ya utawala) kuna tafiti nyingi sana zilizo fanyika kwenye vitabu vya tafsiri za kishia na kisunni,[10] na kuna tofauti na ikhtilafu za kimitizamo na kinadharia baina ya mashia na masunni kuhusu jambo hilo.

Kwa mujibu wa khabari na hadithi ya Jaabir hadithi ambayo imetajwa kwenye vitabu vya riwaya vya kishia kama vile Kifayatul-athar[11] na Kamaalud-dini,[12] kwa mujibu wa riwaya hii Maimamu kumi na mbili ndio vielelezo na maswadiqi za Ulul-amri.

Vile vile mashia kwa ajili ya kuthibitisha madhumuni na jambo hili pia wamejitegemeza na kutumia riwaya mbali mbali kama vile hadithi ya safina (Hadithus-safiinah) na hadithi ya vizito viwili (Hadithut-thaqalaini).[13] Kwa mujibu wa maneno ya Allamah Al-hilli ni kwamba kuna riwaya ambazo ni Mutawaatir kutoka kwa Mashia na Ahlu-sunnah, riwaya ambazo zinathihbitisha mas'ala haya.[14]

Wanazuwoni na maulamaa wa Ahlu-sunnah hawaukubali mtizamo huu na wao kama wao wanao mtizamo mwingine kinyume na huu. Baadhi ya wanazuwoni wa Ahlu-sunnah wanaamini ya kwamba makusudio ya Ulul-amri ni khulafaur-rashidiin, na itikadi ya wengine ni kwamba makusudio ya Ulul-amri ni wanazuwoni wa kidini au maulamaa wa dini na kwa mujibu wa itikadi na mtizamo wa wanazuwoni wengine ni kuwa, makamanda wa vikundi vya kijeshi ndio vielelezo na mswadiqi za Ulul-amri.[15] Zamakhshariy ameandikwa kwamba makusidio ya Ulul-amri ni kila mtawala muadilifu ambae anatawala na kuendeha serikali kwa mujibu wa misingi ya dini kama vile khulafaaur-rashidiin na watawala wengine wenye kutenda kama wao au wenye kutawala kama wao.[16]

Fakhrud-dini raziy kutokana na kwamba mtizamo wake ni kinyume na mtizamo wa wanazuwoni wengine wa kisunni ni kwamba yeye anaitakidi kama wanavyo itakidi mashia na anamtazamo sawa na mashia, yeye anaitakidi kwamba kwa mujibu wa aya hii ni lazima Ulul-amri awe ni maasumu na mtu alie hifadhiwa na utendaji makosa, anasema makusudio ya Ulul-amri ni Ijmai.[17] Na uthibitisho pia ushahidi wake juu ya hilo ni kwamba maasum ima ni Ummah wote ni maasumu na wenye kuhifadhika au baadhi ya watu wa umati huu ndio maasumiina. Na kutokana na ukweli kwamba hivi leo na katika zama hizi hakuna uwezekano wa kuwafahamu watu ambao ni maasumiina na walio hifadhiwa, kwani baadhi ya watu wa umati huu sio maasumini na sio wenye kuhifadhika. Kwa msingi huu hapana budi kusema ya kwamba maasumu ni Ijmai ya waislaam (Itifaki ya waislaam). Makusudio yake kuhusiana na Ijmai ni Ahlul-hilli wal-aqdi, yaani wanazuwoni na maulamaa wa ummah wa kiislaam.[18]

Makala Zinazo Fungamana

Rejea

  1. Twabrasi, Majmaul-bayaan, 1372, j 3, ukurasa 100 na 101, Twabatwabai, Al-miizaan, 1417 q, j4 uk 319.
  2. kama mfano muangalie Allamah Al-hilli, Kashful-murad, 1417Q ukuraa 493.
  3. Twabrasi, Majmaul-bayaan, 1372, j3 ukurasa 100 na 101, Twabatwabai, Al-miizan 1417 Q, j4, ukurasa 319.
  4. kama fano muangalie Allamah Al-hilli, Kashful-murad, 1417Q ukuraa 493, Misbah Yazdi, Rah wa rahnamaa shanaasii, 1376 sha, ukurasa 206.
  5. Angalia kitabu cha Misbah Yazdi, Rah wa rahnamaa shanasiy, 1376sh, ukurasa 206
  6. Allamah Al-hilli, Kashful-muraad, 1417Q, ukurasa 493, Misbaahu Yazdi, Raah wa rahnaamaa shenaasiy, 1376 sh, ukurasa 206.
  7. Angalia kitabu cha Fakhrud-dini Raaziy, Mafaatihul-ghaib, 1420Q, j10, ukurasa 113.
  8. Angalia kitabu cha Taftaazaaniy, Sharhul-maqaaswid, 1409Q, j5, ukurasa 250.
  9. Angalia kitabu cha Misbah Yazdi, Raah wa rahnamaa shenasiy, 1376 sh, ukurasa 207.
  10. kama mfano angalia kitabu cha Twabatwabai, Al-miizaan, 1417 Q, j4, ukurasa 392-401, Fakhrud-dini Raziy, Mafaatihul-ghaib, 1420Q, j10, ukurasa 112-114.
  11. Khazzaz Raziy, Kifaayatul-athar, 1401Q, ukurasa 54-55.
  12. wadouq, Kamaalud-dini, 1395Q, j1, ukurasa 253-254.
  13. kama mfano angalia kitabu cha Twabatwabai, Al-miizan, 1417Q, j4, ukurasa 399.
  14. Angalia kitabu cha Allamah Al-hilli, Kashful-muraad, 1417Q, ukurasa 539.
  15. Fakhrud-dini Raziy, mafaatihul-ghaib, 1420Q, j10, ukurasa 133-114.
  16. Angalia kwenye kitabu cha Zamakhshariy, Tafsiirul-kashaaf, 1407Q, j1, ukurasa 524.
  17. Angalia kitabu cha Fakhrud-dini Raziy, Mafaatihul-ghaib, 1420Q, j10, ukurasa 113.
  18. Angalia kitabu cha Fakhrud-dini Raziy, Mafaatihul-ghaib, 1420Q, j10, ukurasa 113.

Vyanzo

  • Taftazaaniy, saadud-dini Masoud bin Omar, Sharhul-maqaaswid, kilicho hakikiwa na Abdur-rahman bin Umairah, Qom, As-sharifur-radhiy, chapa ya kwanza, 1409Q.
  • Khazzaaz Raziy, Ali bin Muhammad, Kifayatul-athar fin-nassi alal-aimmati Al-ithnay ashar, kilicho sahihshwa na Abdullatif Huseiniy Kuuhkamariy, Qom, Biidar, chapa ya pili, mwaka 1401Q.
  • Zamahshariy, Mahmoud, Al-kas-shaf an haqaaiqi ghawamidhi At-tanziil, Bairut, Darul-kitabil-arabi, chapa ya tatu, mwaka 1407Q.
  • Shekhe Swadouq, Muhammd bin Ali, Kamaalud-dini watamamun-niimah, Tehran,, Darul-kutubil-islaamiyah, mwaka 1395Q.
  • Twabatwabai, Sayyid Muhammad Husein, Al-miizaan fii tafsiiril-qur'an, Qom, Intishaaraat islaami, chapa ya tano, mwaka 1417Q.
  • Twabrasi, Fadhlu bin Hasan, Majmaul-bayaan fi tafsiiril-qur'an, Tehran, Naasir khosro, mwaka 1372 sh.
  • Allamah Al-hilliy, Hasan bin Yusuf, Kashful-muraad fii sharhi tajriidil-iitikad, kilicho hakikiwa na Hasan Hasan zaadah Al-aamuliy, Qom, daftar intishaarat islaami, chapa ya saba, mwaka 1417Q.
  • Fakhrud-din Raaziy, Abu Abdallah Muhammad bin Omar, Mafaatihul-ghaib, Bairut, Daru ihyaait-turaathil-arabiiy, chapa ya tatu, mwaka 1420Q.
  • Misbahu yazdi, Muhammad taqiiy, Raah wa rahnamaashanaasiy, Qom, Intishaaraat muassase Aamuzeshii wapar'wareshii Imamu khomeiniy, chapa ya kwanza, mwaka 1376sh.