Dua ya thelathini na tisa (39) ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya
Dua ya thelathini na tisa (39) ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya: ni dua iliyopokewa kutoka kwa Imam Sajjad (a.s). Muktadha ha wa dua hii ni kuomba msamaha wa Mwenye Ezi Mungu na rehema Zake. Miongoni mwa dhana kuu zilizowasilishwa na Imamu Sajjad (a.s) katika maombi haya, ni ombi la kuondolewa kwa chanzo cha dhambi kilichoko ndani ya nafsi ya mwanadamu, pamoja na kumuomba Mwenye Ezi Mungu awasamehe wale waliotenda dhuluma. Aidha, dua hii inawasilisha ombi la kipekee la kumsihi Mungu amridhishe na amlipa fidia yule aliyekiukiwa (aliyedhulumiwa) haki zake, na ambaye hana uwezo wa kuidai tena haki hiyo. Pia dua hii imeitumia ile dhana ya uumbaji wa mwanadamu, kama kielelezo kinachoashiri na kuthibitisha uwezo mkuu (adhimu) wa Mwenye Ezi Mungu. Tafsiri chambuzi (sherehe) za dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, zinapatikana katika lugha mbalimbali ulimwenguni, ikiwemo lugha ya Kifarsi (Kiajemi) pamoja na Lugha ya Kiarabu. Miongoni mwa vitabu chmbuzi vilivyoandikwa kwa lugha ya Kifarsi ni pamoja na; Diare Asheqan, kazi ya Hussein Ansarian na Shuhud wa Shenakht, kazi ya Hasan Mamduhi Kermanshahi. Ama kwa upande wa lugha ya Kiarabu, dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiya, zinapatikana katika kitabu kiitwacho Riadhu as-Salikin, kazi maridadi iliyofanywa na Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo ya Dua ya Thalathini na Tisa Imamu Sajjad (a.s), katika Dua ya Thelathini na Tisa ya Sahifa Sajjadiya, anatafuta njia ya kujipendekeza mbele ya Mwenye Ezi Mungu ili aweze kupata rehema za Moal wake (Subhanahu wa Ta'ala). Katika dua hii tukufu, Imamu anachukuwa hatua ya kuwasamehe waliomkosea, kama ni wasila (njia) na nyenzo ya kupatia rehema za Mola wake. Anamuomba Allah aamiliane naye kwa Fadhila Zake na si naye kwa Uadilifu Wake, na anamuomba Mwenye Ezi Mungu amjaalie maghfira na amsamehe makosa yake. [1] Miongoni mwa mafunzo ya dua hii yamekuja katika vipengele vifuatavyo: • Ombi la kujiepusha na uchu wa uasi. • Ombi la kung'olewa kwa chimbuko la uovu. • Ombi la kujitenga na vitendo vya udhia na madhara dhidi ya Waumini na Waislamu. • Dua ya kuwatakia msamaha wale waliomdhulumu mwanadamu. • Kuomba afua na Rehema za Mwenyezi Mungu kwa fadhila (kupitia njia) ya kuwasamehe waja wengine. • Kujikurubisha kwa Mungu kupitia dhana (nyenzo) ya msamaha kwa wengine. • Nafasi ya kusameheana katika kupanda daraja kiroho kwa mwanadamu. • Uzito wa kubeba malipo ya amali mbovu. • Kuomba la kumuomba Mwenye Ezi Mungu asimhukumu mja Wake kwa Uadilifu Wake, bali kwa Fadhila Zake adhimu. • Maangamizi ya mwanadamu katika hali ya kunyimwa rehema za Mwenye Ezi Mungu. • Ombi la kuomba kuokolewa na hukumu inayotegemea uadilifu wa Mwenye Ezi Mungu kupitia mwavuli wa hisani Yake. • Kuaamini kwamba; tendo la Mwenye Ezi Mungu kusamehe mja Wake si jambo gumu kwa Yeye. • Kuumbwa kwa mwanadamu ni alama ya Uwezo wa Allah. • Uzito wa mzigo wa dhambi juu ya shingo ya mwanadamu. • Dhuluma ya mwanadamu juu ya nafsi yake kupitia matendo ya dhambi zake. • Maombi ya kumtaka Mwenye Ezi Mungu amfanye mja wake kuwa mfano wa wale walibahatika kupata bahati njema. • Kukiri kustahiki adhabu ya Mwenye Ezi Mungu. • Umuhimu wa kuzingatia uwiano (kukaa na hali ya kati nakti) baina ya khaofu (hofu) na rajaa (matumaini), na kujiepusha na hali ya kukata tamaa juu ya kupata rehema za Mwenye Ezi Mungu, pamoja na kujiepusha na ghururi (majivuno). • Uhalisia wa wanadamu kuwastahikiwa na adhabu ya Mwnebye Ezi Mungu kwa kutokana na utendaji wao dhambi. • Kuhisia kujikatia tamaa kutokana na makosa mengi, na mema yalio machache. • Matumaini ya watenda dhambi katika kutarajia msamaha na rehema za Mungu. • Katazo la kukatazwa kwa wacha-Mungu (Swiddiqina) na tendo la kughururika (kujiona/kuhadalika), pamoja na katazo la kukatazwa kwa waasi na tendo la kukata tamaa ya kupata rehema ya Allah. • Dhana ya kumwepusha Mwenye Ezi Mungu na majina yale yale yanayotumika kurejelea viumbe Wake, ili kusisitiza utofauti Wake kikamilifu. [2] Tafsiri Chambuzi za Dua ya Thalathini na Tisa Kuna kazi kadhaa zilizowasilishwa kwa lugha mbali mbali kama ni tafsiri chambuzi za za Dua ya Thelathini na Tisa sambamba na dua nyengine za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; kitabu kiitwacho "Diare Asheqan", kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [3] "Shuhud wa Shenakht", kazi ya Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, [4] pamoja na "Sharh wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyeh" kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri. [5] Halikadhalika Dua hii ya thelathini na tisa imefasiriwa na kuchambuliwa kwa lugha ya Kiarabu sambamba na dua nyengine zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vya Kiarabu kuhusiana na kazi hiyo ni pamoja na; kitabu kijulikanacho kwa jina la Riadhu as-Salikina, kazi ya Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dhilali as-Sahifat as-Sajjadiyya, kazi ya Muhammad Jawad Mughniyyah, [7] Riadhu al-Arifina, kazii ya Muhammad bin Muhammad Darabi, [8] na Afaq ar-Ruh, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. Aidha kuna baadhi ya wanazuoni walitenga muda wao wenye thamani, kwa ajili ya kufasiri kilugha maneno na msamiati wa dua hii sambamba na dua nyengine zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongi mwa wanazuoni hao ni pamoja na; bwana Faidhu Kashani, mmilikiwa kazi iitwayo Ta'aliqat 'ala as-Sahifat as-Sajjadiyya, [9] pamoja na kazi ya bwana Izzu ad-Din al-Jaza'iri, yeneye jina la Sharh as-Sahifat as-Sajjadiyya, kazi ambazo zimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. [10] Matini ya Dua kwa Kiarabu Pamoja na Maelezo Yake Kwa Kiswahili
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي طَلَبِ الْعَفْوِ وَ الرَّحْمَةِ Na Miongoni mwa Dua Zake (Imam Sajjad), Amani Iwe Juu Yake, ilikuwa ni ile ya Kuomba Msamaha na Rehema (kutoka kwa Mola wake). Dua hii imekuja ikisema: اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اكْسِرْ شَهْوَتِي عَنْ كُلِّ مَحْرَمٍ، وَ ازْوِ حِرْصِي عَنْ كُلِّ مَأْثَمٍ، وَ امْنَعْنِي عَنْ أَذَى كُلِّ مُؤْمِنٍ وَ مُؤْمِنَةٍ، وَ مُسْلِمٍ وَ مُسْلِمَةٍ. Ewe Mwenyezi Mungu, mrehmu Muhammad na Aali zake. Na uivunje shahawa (matamaniyo ya nafsi) yangu, ili ijitenge na kila jambo lililo la haramu. Na ugeuze shauku (uchu wa kupita kiasi) yangu, ili iwe mbali na kila tendo la dhambi. Na uniepushe na kusababisha madhara (adha) kwa kila mu'min awe ni muumini wa kike au wa kiume, na wala (nisimsababishie madhara) muslim yeyote yule, si mwanamume wala si mwanamke. اللَّهُمَّ وَ أَيُّمَا عَبْدٍ نَالَ مِنِّي مَا حَظَرْتَ عَلَيْهِ، وَ انْتَهَكَ مِنِّي مَا حَجَزْتَ عَلَيْهِ، فَمَضَى بِظُلَامَتِي مَيِّتاً، أَوْ حَصَلَتْ لِي قِبَلَهُ حَيّاً فَاغْفِرْ لَهُ مَا أَلَمَّ بِهِ مِنِّي، وَ اعْفُ لَهُ عَمَّا أَدْبَرَ بِهِ عَنِّي، وَ لَا تَقِفْهُ عَلَى مَا عَنْهُمْ فِيَّ، وَ لَا تَكْشِفْهُ عَمَّا اكْتَسَبَ بِي، وَ اجْعَلْ مَا سَمَحْتُ بِهِ مِنَ الْعَفْوِ ارْتَكَبَ، وَ تَبَرَّعْتُ بِهِ مِنَ الصَّدَقَةِ عَلَيْهِمْ أَزْكَي صَدَقَاتِ الْمُتَصَدِّقِينَ، وَ أَعْلَي صِلَاتِ الْمُتَقَرِّبِينَ Ewe Mwenye Ezi Mungu! Kama kuna mja wako yeyote yule ambaye amenidhulumu au amechukua kutoka kwangu kile ulichomharamishia, au amekiuka mipaka ya heshima yangu uliyoiweka; kisha akafariki dunia akiwa na deni la dhuluma hiyo kwangu, au bado yuko hai na bado sijapata haki yangu kutoka kwake; (basi nakuomboa Ewe Mola wangu) umghufirie kwa yale maovu aliyonitendea, na umusamehe kwa yale aliyonikosea (aliyoyapa kisogo miongoni mwa haki zangu). Na (nakuomboa Ewe Mola wangu) usije ukamsimamisha Siku ya Kiyama kwa ajili ya makosa yake kwangu, wala usimfedheheshe kwa ajili ya dhambi alizozichuma kupitia mimi. Na ujaalie msamaha wangu huu kwake ninaoutoa kwa hiari yangu, na hii sadaka ninayojitolea kwa ajili yao (kwa ajili ya watu kama hao), iwe ni sadaka iliyo safi na bora zaidi kuliko sadaka zote zile za wenye kutoa sadaka, na iwe ndiyo njia ya juu kabisa ya kujikurubisha Kwako, kuliko njia nyengine zote zile za wanaotafuta ukaribu wa kukaribiana Nawe.
وَ عَوِّضْنِي مِنْ عَفْوِي عَنْهُمْ عَفْوَكَ، وَ مِنْ دُعَائِي لَهُمْ رَحْمَتَكَ حَتَّى يَسْعَدَ كُلُّ وَاحِدٍ مِنَّا بِفَضْلِكَ، وَ يَنْجُوَ كُلٌّ مِنَّا بِمَنِّكَ. Na (nakuomboa Ewe Mola wangu) unifidie kwa kitendo changu hichi cha kuwasamehe wengine kwa fidia ya (kunipa) msamaha Wako, na (ninakuomba) unilipe kwa kitendo changu cha kuwaombea wao dua hii, kwa malipo ya kunipa rehema Zako. Nimefanya hivyo ili dkila mmoja wetu aweze kufurahia mafanikio yatokanayo na fadhila Zako, na ili sote tuokoke kupitia ukarimu Wako.
اللَّهُمَّ وَ أَيُّمَا عَبْدٍ مِنْ عَبِيدِكَ أَدْرَكَهُ مِنِّي دَرَكٌ، أَوْ مَسَّهُ مِنْ نَاحِيَتِي أَذًى، أَوْ لَحِقَهُ بِي أَوْ بِسَبَبِي ظُلْمٌ فَفُتُّهُ بِحَقِّهِ، أَوْ سَبَقْتُهُ بِمَظْلِمَتِهِ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَرْضِهِ عَنِّي مِنْ وُجْدِكَ، وَ أَوْفِهِ حَقَّهُ مِنْ عِنْدِكَ
Ewe Mwenye Ezi Mungu, na endapo kutakuwa na mja yeyote yule miongoni mwa waja wako ambaye amewahi kufikiwa na madhara fulani yatokayo kwangu, au amepatwa na maudhi fulani kutoka upande wangu, au amekumbana na dhuluma ya moja kwa moja kutoka kwangu, au (amekumbwa na dhulma hiyo) kwa sababu yangu mimi, kisha mimi nikawa nimeshindwa kumpa haki yake, au (kukawa kuna mja fulani ambaye) nimemtangulia kwa tendo la dhuluma; basi nakuomba umteremshie rehema Mtume (Wako) Muhammad pamoja na Aali zake, kisha umridhishe mtu (mja) huyo kwa niaba yangu kupitia hazina Yako na ukarimu Wako, na umlipe haki yake kikamilifu kutoka Kwako. ثُمَّ قِنِي مَا يُوجِبُ لَهُ حُكْمُكَ، وَ خَلِّصْنِي مِمَّا يَحْكُمُ بِهِ عَدْلُكَ، فَإِنَّ قُوَّتِي لَا تَسْتَقِلُّ بِنَقِمَتِكَ، وَ إِنَّ طَاقَتِي لَا تَنْهَضُ بِسُخْطِكَ، فَإِنَّكَ إِنْ تُكَافِنِي بِالْحَقِّ تُهْلِكْنِي، وَ إِلَّا تَغَمَّدْنِي بِرَحْمَتِكَ تُوبِقْنِي. Kisha, (nakuomba) unikinge (uniepushe) na kile knacholazimiana na hukumu Yako. Na uniokoe kutokana na yale yanayolazimiana na hukumu za uadilifu Wako, kwani hakika nguvu zangu haziwezi (uwezo wangu) kustahimili adhabu Yako. Na bila shaka uwezo wangu hauwezi kukabiliana na hasira Zako (hauwezi kusimama mbele ya ghadhabu Zako). Kwni ni wazi kwamba, iwapo Wewe utanihukumu kulingana na haki ilivyo (kulingana na uadilifu), basi utanihilikisha, na iwapo hutanifunika kwa rehema Zako, utaniangamiza. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَوْهِبُكَ يَا إِلَهِي مَا لَا يُنْقِصُكَ بَذْلُهُ، وَ أَسْتَحْمِلُكَ، مَا لَا يَبْهَظُكَ حَمْلُهُ. Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi nakuomba zawadi (tunuko), Ewe Mungu wangu, (ninakuomba) kile ambacho utoaji wake haukupunguzii Wewe kitu chochote, na nakuomba unibebee, kile ambacho ubebaji wake haukulemei. أَسْتَوْهِبُكَ يَا إِلَهِي نَفْسِيَ الَّتِي لَمْ تَخْلُقْهَا لَِتمْتَنِعَ بِهَا مِنْ سُوءٍ، أَوْ لِتَطَرَّقَ بِهَا إِلَى نَفْعٍ، وَ لَكِنْ أَنْشَأْتَهَا إِثْبَاتاً لِقُدْرَتِكَ عَلَى مِثْلِهَا، وَ احْتِجَاجاً بِهَا عَلَي شَكْلِهَا. Ewe Mola wangu, ninakukabidhi Wewe nafsi yangu. Nafsi ambayo hukuiumba ili iwe ni kinga yako dhidi ya shari fulani, au iwe ni njia (nyenzo) yako ya kujipatia kheri. Bali, Wewe uliiumba ili kudhihirisha Qudra Yako tukufu juu ya viumbe Wako mfano wake (wanaofafana na nafsi hiyo), na iwe ni hujja (ithibati) na ushahidi dhidi ya viumbe vyote vinavyofanana naye kimaumbile. وَ أَسْتَحْمِلُكَ مِنْ ذُنُوبِي مَا قَدْ بَهَظَنِي حَمْلُهُ، وَ أَسْتَعِينُ بِكَ عَلَى مَا قَدْ فَدَحَنِي ثِقْلُهُ. Na ninakuomba unibebee (unitue/uniondolee) mzigo wa dhambi zangu ambazo zimenielemea, na ninaomba msaada wako dhidi ya yale ambayo uzito wake umenisonga (na kunivunja).
فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ هَبْ لِنَفْسِي عَلَى ظُلْمِهَا نَفْسِي، وَ وَكِّلْ رَحْمَتَكَ بِاحْتَِمالِ إِصْرِي، فَكَمْ قَدْ لَحِقَتْ رَحْمَتُكَ بِالْمُسِيئِينَ، وَ كَمْ قَدْ شَمِلَ عَفْوُكَ الظَّالِمِينَ. Ewe Mola, mswalie (Bwana wetu) Muhammad na Aali zake. Na uipe nguvu nafsi yangu (dhaifu) dhidi ya udhalimu wake (wa kupingana na amri Zako). Na zikabidhi rehema Zako jukumu la kunichukulia mzigo wangu wa dhambi (endelevu). Kwani ni mara ngapi rehema Zako zimekuwa zikiwashukia waovu, na ni mara ngapi kivuli cha msamaha wako kimekuwa kikiwafunika madhalimu. فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْنِي أُسْوَةَ مَنْ قَدْ أَنْهَضْتَهُ بِتَجَاوُزِكَ عَنْ مَصَارِعِ الْخَاطِئِينَ، وَ خَلَّصْتَهُ بِتَوْفِيقِكَ مِنْ وَرَطَاتِ الُْمجْرِمِينَ، فَأَصْبَحَ طَلِيقَ عَفْوِكَ مِنْ إِسَارِ سُخْطِكَ، وَ عَتِيقَ صُنْعِكَ مِنْ وَثَاقِ عَدْلِكَ. Basi, mswalie Muhammad na Jamaa zake. Na unijaalie niwe mfano mwema wa wale uliowainua kwa kughufiria maanguko ya wakosefu, na ukawaokoa kwa taufiki yako kutoka katika mitego ya wahalifu. Hivyo, wakawa wameachiliwa huru kwa msamaha wako kutoka kwenye pingu za ghadhabu yako, na wakakombolewa kwa fadhila zako kutoka kwenye minyororo ya uadilifu wako. إِنَّكَ إِنْ تَفْعَلْ ذَلِكَ يَا إِلَهِي تَفْعَلْهُ بِمَنْ لَا يَجْحَدُ اسْتِحْقَاقَ عُقُوبَتِكَ، وَ لَا يُبَرِّئُ نَفْسَهُ مِنِ اسْتِيجَابِ نَقِمَتِكَ Ewe Mungu wangu, hakika ukifanya hivyo [yaani kunisamehe], utakuwa umemfanyia (hisani hiyo yule) mtu ambaye hakatai kuwa anastahili adhabu Yako, na wala hajioni kuwa hana hatia ya kustahili hasira Zako. تَفْعَلْ ذَلِكَ يَا إِلَهِي بِمَنْ خَوْفُهُ مِنْكَ أَكْثَرُ مِنْ طَمَعِهِ فِيكَ، وَ بِمَنْ يَأْسُهُ مِنَ النَّجَاةِ أَوْكَدُ مِنْ رَجَائِهِ لِلْخَلَاصِ، لَا أَنْ يَكُونَ يَأْسُهُ قُنُوطاً، أَوْ أَنْ يَكُونَ طَمَعُهُ اغْتِرَاراً، بَلْ لِقِلَّةِ حَسَنَاتِهِ بَيْنَ سَيِّئَاتِهِ، وَ ضَعْفِ حُجَجِهِ فِي جَمِيعِ تَبِعَاتِهِ (Ewe Mungu wangu), fadhila hii (hisani hii ya msamaha), unamfanyie yule mja ambaye hofu yake juu ya adhabu yako, ni kubwa zaidi kuliko matumaini yake ya kupata thawabu zako. Mfanyie hivi yule ambaye hisia yake ya kukosa wokovu ni imara zaidi kuliko matarajio yake ya kuokoka. Hii si kwa sababu amekata tamaa kabisa na rehema zako au anajidanganya na uvumilivu wako, la hasha. Bali ni kwa sababu anatambua uchache wa matendo yake mema yakilinganishwa na wingi wa maovu yake, na anatambua udhaifu wa hoja zake za kujitetea mbele ya makosa yake yote. فَأَمَّا أَنْتَ يَا إِلَهِي فَأَهْلٌ أَنْ لَا يَغْتَرَّ بِكَ الصِّدِّيقُونَ، وَ لَا يَيْأَسَ مِنْكَ الُْمجْرِمُونَ، لِأَنَّكَ الرَّبُّ الْعَظِيمُ الَّذِي لَا يَمْنَعُ أَحَداً فَضْلَهُ، وَ لَا يَسْتَقْصِي مِنْ أَحَدٍ حَقَّهُ. Lakini linapokuja Suala lako, Ee Mungu wangu, basi yakustahikia kamba; (hata) wale waliopo kwenye jopo la watu waadilifu (Siddiqina), hawatakiwi kughururike (Nawe) kutokana na dhana ya ukaribu wao Kwako. Pia wahalifu nao hawana haki ya tamaa ya kupata hisani Yako. Hii ni kwa kuwa Wewe ndiye Mlezi Mtukufu, ambaye hazuii fadhila Zake kwa yeyote yule, wala hatekelezi madai ya haki Yake kikamilifu dhidi ya yeyote yule (yaani hamkamui mtu na kumdai haki Yake kama alivyoamrisha, huku akitaraji usafi wa amali zisizo na dosari). تَعَالَى ذِكْرُكَ عَنِ الْمَذْكُورِينَ، وَ تَقَدَّسَتْ أَسْمَاؤُكَ عَنِ الْمَنْسُوبِينَ، وَ فَشَتْ نِعْمَتُكَ فِي جَمِيعِ الَْمخْلُوقِينَ، فَلَكَ الْحَمْدُ عَلَى ذَلِكَ يَا رَبَّ الْعَالَمِينَ. Utukuka utajo Wako kwa utukufu uliopindukia utajo mwnegi wotewote ule wa watajwao, na umetukuka mno utakatifu wa majina Yako (utukufu wa majina unayonasibishwa nayo), na kukiuka kila sifa wanaosifiwa nazo wale wenye kusifiwa. Na neema Zako zimeenea na kuwatawala viumbe wote. Hivyo basi, sifa zote kamilifu ni Zako Wewe kutokana na hisani (juu ya viumbe Vyako), Ewe Mola Mlezi wa walimwengu wote (Rabb al-Alamin).