Nenda kwa yaliyomo

Jihadi Dhabbi

Kutoka wikishia

Jihadi Dhabbi (Jihadi ya Kuahami Uislamu): ni nadharia mashuhuri katika fiqhi ya Kiislamu, inayozungumzia wajibu wa kupambana dhidi ya uonevu wa uadui fulani, ili kulinda na kuuhifadhi Uislamu pamoja na uwepo maadili yake. [1] Kinyume na jihadi ya utashi wa kisiasa au upanuzi wa maeneo, nadharia hii inahusu tu hali ya hatari inayohatarisha uwepo wa mfumo wa Kiislamu. Hivyo basi kwa mujibu wa mtazamo huu, iwapo maadui fulani wataonyesha dalili za kutaka kuangamiza Uislamu au misingi yake ya kidini, katika hali kama hii, itakuwa faradhi (wajibu) kwa kila Mwislamu kusimama na kuitetea dini yake (wajib aini). [2] Jihadi Dhabbi ni moja ya dhana zilizobuniwa na kuanzishwa na mmoja wa wanazuoni wakuu fani ya fiqhi katika chuo kikuu cha Kiislamu kilichoko Qom nchini Iran, ajulikanaye kwa jina la Ayatullahi Muhammad Jawad Fadhil Lankarani. Fadhil Lankarani aliibua dhana hii kutokana na maandishi ya wanazuoni wa sheria za fiqhi walitangulia kabla yake. [3] Ayatullahi Lankarani ameiainisha jihadi hii kama ni aina ya tatu ya jihadi, ambayo ni tofauti na 'jihadi ya kuanzishwa na Wailamu (Jihad Ibtidai), na jihadi ya kujihami (Jihad Difai). [4] Jihadi hii ni tofauti na aina mbili hizo, kwani Jihadi ya Kuahami Uislamu, haina masharti maalum, na si lazima mtu awe na uhakika wa kufanikiwa (kushinda). Wala jihadi hii, haishartishwi mtu kuwa na hofu ya kupoteza maisha, mali, au heshima yake. Hivyo basi Muislamu yeyote yule atakayeuawa katika harakati hizi, huhesabiwa kuwa ni shahidi na hupewa hadhi zote za mtu aliyekufa kishahidi. [5] Kwa mujibu wa maelezo ya Ayatullahi Muhammad Jawad Fadhil Lankarani, Jihadi Dhabbi haijatungwa kiholela, bali imesimama juu ya misingi mikuu mitano ya kisheria ambayo ni sehemu muhimu ya ujenzi wa hoja katika fiqhi ya Kishia, misingi mitano hiyoi ni: • Qur'an kama chanzo cha maamrisho ya msingi. {Maelezo 1: Vifungu vya Qur'ani vinavyotajwa kama ushahidi ni pamoja na: Suratu ya Al-Hajj, Aya ya 39 na 40; Suratu At-Tawba, Aya ya 123; Suratu Al-Baqara, Aya ya 193; na Suratu An-Nisaa, Aya ya 75 na 76.} • Hadithi na Riwaya za Maimamu wa upande wa Ahlul-Bait (a.s). [6] {Maelezo 2: Basi, Imam Ridha (a.s.) akamwambia: '...lakini anapigana kwa ajili ya Baidhatu al-Islam (chimbuko na hadhi ya Uislamu); kwani hakika katika kuondoka kwa Baydhat al-Islam (asili ya Uislamu) ni sawa na kufutika kwa utajo wa Muhammad (s.a.w.w).} • Ijma (mawafikiano) ya mafaqihi wa madhehebu. [7] • Dalili za kiakili (istidlal-aqli) zinazounga mkono hoja za wajib. [8] • Na kanuni ya (hisbiyya) isemayo kuwa; Sheria ya Kiislamu haiwezi kuridhia kuwepo kwa hali ya kutojali majukumu ya kijamii. [9] Kulingana na itikadi ya Ayatullahi Fadhil Lankarani, ni kwamba; sababu halisi ya msimamo wa Imamu Hussein (a.s) lililopelekea vita vya Karbala, ilikuwa ni kuutetea Uislamu wenyewe, na haikuwa ni jihadi ya anzilishi ya kuanzisha vta dhidi ya adui zake, wala si jihadi ya kujihami. Hii kwa kuwa Imamu (a.s) aliondoka Makka kwa hiari yake mwenyewe. [10] Kwa mtazamo wake, harakati za Imamu Hussein hazikuwa ni za msingi wa 'kuamrisha mema na kukataza maovu', kwani hukukua na sharti hata moja lililotimia kati ya masharti ya kukataza kuamrisha mema na kukataza maovu. Na ni jambo lililo wazi kabisa kwamba; wajibu wa kufanya hivyo hutegemea kukamilika kwa masharti fulani, kama vile; kuwa na uhakika wa mafanikio na kutokuwepo kwa madhara ya kimwili au kifedha yanayoweza kutokea kutokana na utekelezaji wa jambo hilo. Hivyo basi, lengo la msimamo wa Imamu Hussein (a.s), lilikuwa ni kuilinda dini kama dini, kwa kuwa hakuna jema muhimu zaidi kuliko kuihifadhi dini, na hakuna ovu kubwa zaidi kuliko kuiangamiza dini. [11] Mwanazuoni huyu akizidi kusisitiza mtazamo wake juu ya nadharia yake, ameyataja mapambano ya Wapalestina na Hizbullahi ya Lebanon dhidi ya Israeli, pamoja na vita dhidi ya داعش (ISIS), kama mifano hai ya Jihadi Dhabbi. [12]