Nenda kwa yaliyomo

Kizito kidogo

Kutoka wikishia

Al-Thiql al-aṣghar (Kiarabu: الثقل الأصغر) ni sifa ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w) katika hadithi ya vizito viwili (Athaqalaini). Thiqlu ni neno lenye maana ya mzigo mzito[1] na Thaqlu ni neno lenye maana ya kila kitu chenye hadhi na thamani kubwa.[2] kwa mujibu wa maneno ya Feiruz abaady, (alie fariki mwaka 817q) katika kamusi ya Al-qaamsul-muhiit, neno Thaqlaini katika hadithi ya Thaqalain linatokana na neno Thaqlu.[3]

Mtume (sa.w.w) katika hadithi ya Thaqalaini, (vizito viwili), alikitambulisha kizazi chake kama Thaqlu Asghar (kizito kidogo) na Qur'an aliitambulisha kama Athaqlul-akbar kiasi kwamba waislaamu ikiwa watashikamana na vizito viwili hivyo kamwe hawata potea.[4] Pia Mtume (sa.w.w) katika khutba ya Ghadiir aliiarifisha Qur'an kama Thaqlu Akbar na kizito kikubwa, na akamuarifisha Ali (a.s) na watoharifu miongoni mwa wanawe kuwa ni Thaqlul-asghar (kizito kidogo).[5]

Imamu Ali (a.s) nae pia katika moja ya hotuba zake[6] na pia katika usia wake aliompata Kumayl bin Ziyad alijitambulisha yeye kama Thaqlul- Asghar (kizito kidogo) na kuiarifisha Qur'an kama Thaqlu Akbar.[7]

Kwa mtizamo wa Abdallah Jawaady Aamuliy, mfasiri wa Qur'an tukufu, ni kuwa Ahlul-Bayt (a.s) kwa mtizamo wa ulimwengu wa kidhahiri na katika nafasi mzunguko wa mafunzo na maarifa ya dini ni Thaqlul- As'ghar ni kizito kidogo, ama kwa kuangalia daraja za kimaanawi na katika ulimwengu wa baatini si wenye hadhi ndogo kuliko qur'an.[8] kwa msingi wa riwaya mbali mbali, Imamu Aliy (a.s) ameiarifisha Qu'an kuwa ni kitabu kisicho tamka na kujiarifisha yeye kuwa ni kitabu chenye kutamka cha Mwenyezi Mungu.[9]

Imamu Khomeiniy, katika kitabu na barua yake ya usia wa kisiasa anasema- Ewe Mola wangu kwa hakika wewe mwenyewe umewataja Ahlul-baiti kwa anwani ya ( Thaqlul- Akbar).[10]

Rejea

  1. Ibnu Mandhuur, Lisaanul-arab, cha mwaka 1411, juz. 11, uk. 85.
  2. Fairuz abad, Al-qaamusul-muhiit, cha mwaka 1426 q, uk. 972 (chini ya neno Thaqlu).
  3. Fairuz abad, Al-qaamusul-muhiit, cha mwaka 1426 q, uk. 972 (chini ya neno Thaqlu).
  4. Ayyaashiy, tafsiirul-ayaashiy, cha mwaka 1380 q, juz. 1, uk. 5.
  5. Yaaquubiy, Taarikhu Ya'aqubiy, Daru Swaadir, juz. 2, uk. 112; Ibnu Twawous, Iqbaalul-aamal, cha mwaka 1409 q, juz. 1, uk. 455- 456.
  6. Nahjul-balaghah, kilicho sahihishwa na Subhiy Swaleh, khutba namba 87 uk. 120.
  7. Majlisiy, Buharul-an'waar, cha mwaka 1390 q, juz. 74, uk. 375.
  8. Jawadu Aamuliy, Tasniim, cha mwaka 1385 sh, juz. 1, uk. 76.
  9. Huurul- Aamuliy, Wasaailus-shia, cha mwaka 1409 q, juz. 27, uk. 34.
  10. Khomainiy, Swahifatul-imam, cha mwaka 1389 sh, juz. 21, uk. 393.

Vyanzo

  • Ibnu Twawous, Ali bin Mussa, Iqbaalul-aamaal, Tehran, Darul-kutubil-islaamiyah, chapa ya pili, mwaka 1409q.
  • Ibnu Mandhuur, Muhammd, bin Mukrim, Lisaanul-arab, Bairut, Daru ihyaait-turaathil-arabiy, mwaka 1411q.
  • Jawaad Aamuliy, Abdallah, Tasniim, Qom, Markaze nashri Asraa, mwaka 1385sh.
  • Hurru Aamuliy, Muhammad bin Hasan, Wasaailus-shiah, Qom, Muassasatu Aalul-baiti, mwaka 1409q.
  • Khomeiniy, Rouhullah, Swahifeye Imam, Tehran, Muassasatu tandhiim wa nashri Aathari Imamu khomeiniy, chapa ya tano, mwaka 1389sh.
  • Ayyashiy, Muhammad bin Mas'oud, Tafsiirul-ayyahiy, kilicho hakikiwa na Sayyid Haashim Rasouliy Mahlallaatiy, chapa ya Ilmiyeh, Tehran, mwaka 1380q.
  • Fairuz Aabadiy, Al-qaamusul-muhiit, Daru ihyaait-traathil-arabiy, Bairut, mwaka 1412q.
  • Majlisiy, Muhammad Baaqir, Buharul-an'waar, Tehran, Darul-kutubil-islaamiyah, mwaka 1390q.
  • Nahjul-balaghah, kilicho sahihishwa na Subhiy Swaleh, Qom, Hijrat, chapa ya kwanza, mwaka 1414q.
  • Yaaqubiy, Ahmad, Taarikhu Yaaqubiy, Bairut, Daru Swaadir, Biitaa.