Aya ya Kumswalia Mtume (s.a.w.w)

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na Aya ya 56 ya Surat al-Ahzab

Aya ya kumswalia Mtume (s.a.w.w) (Kiarabu: آية الصلوات) (Ahzab 56) inaashiria kwamba, Mwenyezi Mungu na Malaika wanamswalia Mtume (s.a.w.w) na inawataka waumini pia wamsalie Mtume. Waislamu wengi wa Madhehebu ya Shia wanaposikia Aya hii humswalia Mtume. Aya hii imetiliwa mkazo isomwe katika swala ya magharibi.

Allama Sayyied Muhammad Hussein Tabatabai katika tafsiri ya al-Mizan anasema kuwa, kumswalia Mtume ni kumfuata Mwenyezi Mungu na Malaika. Katika kitabu cha "Payam Qur'an' yaani Ujumbe wa Qur'an, Ayatullah Nassir Makarem Shirazi akitegemea hadithi zilizonukuliwa katika vitabu vya hadithi na vya tafsiri vya ahlu-sunna, anasema kuwa; kuwatumia salamu na kuwaswalia kizazi cha Bwana Mtume (s.a.w.w) ni sehemu ya kumswalia Mtume kulikotajwa katika Aya ya 56 ya Surat al-Ahzab.

Aya ya kumswalia Mtume na tarjuma yake

إِنَّ اللَّهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

"Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlioamini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu". .
(Quran: 33: 56)

Kusoma Aya hii kama dua ya swala ya magharibi baada ya kukamilisha tasbihi ya Zahra (a.s) kumeusiwa katika kitabu cha Misbahul-Mujtahid cha Sheikh Tusi[1] na katika kitabu cha Mafatihul-Jinan cha Sheikh Abbas Qommi limetajwa hilo pia kwa kunukuu kutoka katika kitabu cha Misbahul-Mujtahid.[2] Kwa muktadha huo baada ya swala ya jamaa ni ada miongoni mwa Waislamu wa Kishia kusomwa Aya hii kwa sauti kubwa na mmoja wa waumini na kisha hadhirina waliohudhuria ibada ya Swala humswalia Mtume mara tatu.

Tafsiri

Allama Tabatabai mfasiri wa Qur’an wa Kishia wa karne ya 15 Hijiria anasema katika kitabu chake cha Tafsiri al-Mizan akitegemea baadhi ya hadithi zilizonukuliwa na Waaislamu wa madhehebu ya Shia na Suni kwamba, mtindo wa kumswalia Mtume ni waumini kumtaka Mwenyezi Mungu amtolee salamu na kumswalia Mtume pamoja na aali zake.[3] Aidha anasema kuwa, hatua ya waumini ya kumswalia Mtume[4], ni kufuata hatua ya Mwenyezi Mungu na malaika ya kumswalia Mtume (s.a.w.w) na hilo linatilia mkazo kuweko katazo katika Aya inayofuata ambapo wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamelaaniwa duniani na akhera.[5] Katika hadithi moja Imam Mussa al-Kadhim (a.s) katika kujibu swali kuhusiana na maana ya Mwenyezi Mungu, malaika na waumini kumswalia Mtume amesema: Swala ya Mwenyezi Mungu ni rehma Zake, Swala ya malaika ni kumsifia kwao Mtume na Swala za waumini ni dua zao kwa mbora huyo wa viumbe.[6] Ayatullah Makarem Shirazi, mmoja wa wanazuoni na Marjaa Taqlidi anasema katika kitabu chake cha Payam Qur’ani “Ujumbe wa Qur’ani” kwamba: Kuwaswalia aali yaani familia na watu wa nyumba ya Mtume nayo kwa mujibu wa hadithi za Mashia na Masuni ni sehemu ya kumswalia Mtume, na katika hili kuna hadithi ambazo zimenukuliwa katika vitabu vya hadithi na tafsiri za Waislamu wa Kisuni;[7] na miongoni mwa vitabu hivyo ni Sahihi Bukhari,[8], Sahihi Muslim[9], Tafsir Durr al-Manthur[10] na Tafsir al-Tabari.[11]

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa na Fadhl bin Hassan Tabrasi katika Tafsiri ya Maj’maa al-Bayan kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ni kwamba: Kama mtu atamswalia Bwana Mtume (s.a.w.w), malaika humswalia mara kumi, humfutia madhambi kumi na humuandikia mema kumi.[12]

Ishara ya kuwa wajibu kumswalia Mtume (s.a.w.w)

Ayatullah Makariz Shirazi mmoja wa Marajii Taqlidi na mfasiri wa Qur’ani anasema: Aya ya 56 ya Surat al-Ah’zab ina ishara hii kwamba, ni wajibu kumswalia Mtume (s.a.w.w) mara moja katika kipindi chote cha umri wa mtu.[13] Imenukuliwa pia kutoka kwa Sheikh Ali Nasef mmoja wa Maulamaa wa Kisuni na mwandishi wa kitabu cha al-Taj al-Jamiu al-Usul kwamba: Maulamaa wameafikiana na kufikia kauli moja kwamba, dhahiri ya Aya ni kwamba, ni wajibu kumtolea salamu na kumswalia Mtume(s.a.w.w).[14]

Rejea

  1. Ṭūsī, Miṣbāḥ al-mutahajjid, uk. 85.
  2. Sheikh Abbas Qomi, Kuliyaat mafatih al-janaan, Intisharaat us'we, uk. 17.
  3. Allamah Tabatabai, Al-Mizan, 1393 H, juz. 16, uk. 338.
  4. Surah Ahzab, aya ya 57.
  5. Allamah Tabatabai, Al-Mizan, 1393 H, juz. 16, uk. 338.
  6. heikh Swadouq, Thawabu al-amal wa iqab al-amal, 1406 H, juz. 1, uk. 156.
  7. Makarem Shirazi, Payam Qur'an, 1381 S, juz. 9, uku. 399-403.
  8. Bukhari, Sahih Bukhari, 1419 H, uk.937, Hadith no. 4797.
  9. Muslim Neishabouri, Sahih Muslim, 1412 H, juz. 1, uk. 305, toleo la 17, Hadith no. 65.
  10. Siyuti, Dar al-Manthur, 1420 H, juz. 6, uk. 646-647.
  11. Tabari, Tafsir Jame al-Bayan, 1422 H, juz. 19, uk. 176.
  12. Tabrasi, Majma al-Bayan, 1406 H, juz. 8, uk. 579.
  13. Makarem Shirazi, Payam Imam Amir al-Muminin, 1386 S, juz. 3, uk. 200.
  14. Makarem Shirazi, Payam Imam Amir al-Muminin, 1386 S, juz. 3, uk. 200-201.

Vyanzo

  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Saudi Arabia: Bayt al-Afkār al-Dawlīyya li-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1419 AH.
  • Muslim Nayshābūrī. Ṣaḥīḥ Muslim. Edited by Muḥammad fuʾād ʿAbd al-Bāqī . Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Kutub al-ʿArabīyya, 1412 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Payām-i Imām Amīr al-Muʾminīn (a). Tehran: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1386 Sh.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Payām-i Qurʾān; rawish-i tāza-ī dar tafsīr muḍuʿī-yi Qurʾān. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1381 Sh.
  • Qummī, Abbās. Mafātīḥ al-jinān. Intishārāt-i Uswa; affiliated to Sāzmān-i Ḥaj wa Uqāf wa Umūr-i Khayrīyya, [n.d].
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Beirut: Dār al-Fikr, 1420 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan. Miṣbāḥ al-mutahajjid. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1418 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1406 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jāmiʾ al-bayān ʿan taʾwīl āyāt al-Qurʾān. Edited by ʿAbd Allāh b. ʿAbd al-Muḥsin al-Turkī. Dār al-Hijr, 1422 AH. [n.p].
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1417 AH.