Yaumu al-Muqawamati al-Alamiyya

Yaumu al-Muqawamati al-Alamiyya (Kiarabu: اليوم العالمي للمقاومة) (Siku ya Mapambano ya Kiupinzani Dunianiani): Siku ya Kimataifa ya Mapambano ya Kiupinzani dhidi ya dhulma za ukaliaji wa ardhi za wengine kimabavu. Nayo ni siku ya tarehe 13 ya mwezi wa Dey kulingana na kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Kalenda ya Shamsia).[1] Siku hii adhimi imetengwa kwa ajili ya kumuenzi Shahidi Qassim Suleimani, aliyepata daraja ya kifo cha kishahidi mnamo tarehe 13 mwezi wa Dey mwaka 1398 Shamsia.[2]
Kwa mara ya kwanza kabisa, wazo hili adhimu, lilianzishwa kufuatia pendekezo la Kitengo maalumu cha serikali kijulikanacho kwa jina la; Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kitamaduni la Kueneza Athari na tarehe 17 Dey, mnamo mwaka 1398. Mara tu baada ya kupasi na kukubalika, kwa wazo hili liliongezwa katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa jina la: "Siku ya Kimataifa ya Mapambano ya Kiupinzani; Ushahidi wa Amiri Jeshi Shahidi Qassim Suleimani (ambaye ni) Nembo ya Ikhlasi na Amali Njema, (tukio lililojiri) Kupitia Mikono wa Dola la Kidhalimu Duniani".[3]
Kwa mujibu wa uamuzi huu, kila mwaka siku hii ya 13 Dey huadhimishwa na kupewa nafasi maalum, kama ni moja ya siku muhimu za kitaifa nchini Iran. Siku hii ya kimataifa, huadhimishwa kuptia programu tofati, na imegeuka kuwa ni alama na nembo muhimu inayofichua uovu na uadui wa utawala wa Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mataifa mengine ya Kiislamu huru.[4] Si Iran tu inayoadhimisha siku hii uluimwenguni, pia kuna nchi nyengine kadhaa zinazoshirikiana na Iran katika kuadhisha siku hii muhimu.[5]
Makala Zinazo Fungamana
Rejea
- ↑ Yaad, Faryad «Margi Bar Amerika» wa «Intiqam! Intiqam!» Dar Bahne Iraq wa Iran, uk. 77
- ↑ 13 Dey؛ Ruze Jahani Muqawamat Namegozari Shud, Shirika la Habari la IRNA.
- ↑ «Ruze Jahani Muqawamat» Tas-wib Shud, Shirika la Habari la Difau Muqadas.
- ↑ Ruze Shahadat Sardor Suleimani Ruze Jahani Muqawamat Dar Taqwim Keshvar Sabit Shud, Shirika la Habari la Fars.
- ↑ Buzrgedosht Chahromin Salgard Shahadat Sardor Suleimani Dar Kharij Az Keshvar, Shirika la Utamaduni na Mawasiliano la Kiislamu.
Vyanzo
- Shahadat Sardor Suleimani Dar Kharij Az Keshvar, Shirika la Utamaduni na Mawasiliano la Kiislamu, Tarehe ya kuchapishwa kwa habari: 16 Dey 1402.
- Yaad, Faryad «Margi Bar Amerika» wa «Intiqam! Intiqam!» Dar Bahne Iraq wa Iran, uk. 77.
, Kayhan Farhangi, Azar wa Dey 1398 - Nambari 396 na 397.
- «Ruze Jahani Muqawamat» Tas-wib Shud, Shirika la Habari la Difau Muqadas, Tarehe ya kuchapishwa kwa habari: 12 Dey 1400.
- Ruze Shahadat Sardor Suleimani Ruze Jahani Muqawamat Dar Taqwim Keshvar Sabit Shud, Shirika la Habari la Fars, tarehe ya kuchapishwa kwa habari: 8 Bahman 1398 S.
- 13 Dey؛ Ruze Jahani Muqawamat Namegozari Shud, Shirika la Habari la IRNA, Tarehe ya kuchapishwa kwa habari: 17 Dey 1398 S.