Tukio la pongezi

Kutoka wikishia

Tukio la pongezi (Kiarabu: قضية التهنئة) ni tukio linalohusiana na Masahaba wa Mtume Muhammad (S.A.W.W), khususan khalifa wa kwanza na Khalifa wa pili, kumpongeza Imam Ali (A.S) baada ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) kumtangaza Ali (A.S) katika tukio la Ghadir, kuwa yeye ndiye imamu au khalifa atakayeshika nafasi ya ukhalifa baada yake. Tukio hili linachukuliwa kuwa ni uthibitisho wa usahihi wa haki ya Ali (A.S) katika kushika nafasi ya Mtume (S.A.W.W).

Ibara ya Pongezi

Tukio la pongezi linahusu pongezi za Masahaba wa Mtume Muhammad (S.A.W.W) baada ya tangazo la uongozi wa Imam Ali (A.S) uliotangazwa na Mtume (S.A.W.W) kwenye bonde la Ghadiir. Tukio hili lilitokea mwezi 18 Dhul-Hijjah katika mwaka wa 10 Hijiria. Katika tukio hili, Omar bin Al-Khattab alimpongeza Ali bin Abi Talib kwa kusema: (بَخٍّ بَخٍّ لَک یا عَلِی أَصْبَحْتَ مَوْلَای وَ مَوْلَی کلِّ مُؤْمِنٍ وَ مُؤْمِنَةٍ), Tafsiri yake ni kwamba; "Hongera, hongera juu yako ewe Ali, umekuwa ni wangu (kiongozi wangu) na bwana (kiongozi) wa kila Muumini wa kike na wa kiume." [2] Katika baadhi ya nukuu za tukio hili, badala ya jina Ali, limetumika jina la "Ibn Abi Talib" [3] pia katika nikuu nyengine limetumika jina la "Amir al-Mu'minin" [4]. Katika baadhi ya maandiko, badala ya neno Muumin (مُؤْمِنٍ) na Muuminah (مُؤْمِنَةٍ), kumetumika neno Muslimin (مسلم). [ 5] Ahmad Ibn Hambal pia alinukuu usemi wa Omar katika pongezi zake za kumpongeza Ali (A.S) kama ifuatavyo: (هَنِیئًا یا ابْنَ أَبِی طَالِبٍ، أَصْبَحْتَ وَأَمْسَیتَ مَوْلَی کلِّ مُؤْمِنٍ وَمُؤْمِنَة), Tafsiri yake ni kwamba: “Hongera, ewe Ibn Abi Talib, umeamkia katika siku hii na katika jioni hii ukiwa ni mabwana (kiongozi) wa waumini wote wa kike na wa kume”. [6]

Ni nani walimpongeza Ali bin Abi Talib?

Miongoni mwa Masahaba waliompongeza Ali (A.S) katika tukio la Ghadir Khum ni Abu Bakr, Umar bin Khattab, Talha na Zubair. [7] Baadhi ya waandishi wamesema kwamba Abu Bakr na Umar, kwanza walikuwa na shaka kuhusiana na ukhalifa wa Ali baada ya Mtume (S.A.W.W) kwama jee hiyo ni amri ya Mtume (S.A.W.W) itokayo kwa Mola wake au la. Baada ya wao kuhakikishiwa kwamba hiyo ni amri ya Mwenye Ezi Mungu na Mtume Wake (S.A.W.W), hapo ndipo walipokwenda kumpongeza Ali (A.S). [8] Wao walifanya hivyo baada ya kutambua ya kwamba, kupinga suala hilo ni kupingana na amri ya Mwenye Ezi Mung kunakopelekea mtu kuingia katika ukafiri. [9] Katika baadhi ya maandiko kuhusiana na tukio hili, imeelezwa ya kwamba; Omar alifirahi kupita budi, furaha yake hiyo ikampelekea kutamka ibara hiyo ya pongeza kuhusiana na Imamu Ali (A.S), [10] ibara ambayo inaonesha kuwa pongezi za Omar zikuwa ni pongezi moto zaidi ukulinganisha na pongezi za Masahaba wengine. [11][Maelezo 1] Pia kuna ripoti zisemazo kwamba; Omar alikuwa ni mtu wa kwanza kumpoongeza Imam Ali (A.S), [12] au mmoja miongoni mwa watu wa mwanzo [13] walimpongeza Ali (A.S). Ingawaje katika vyanzo vingi, ibara hii ya pongezi yamehusishwa na Omar bin Khattab, [14] ila katika baadhi ya vyanzo vyengine imeelezwa kwamba; Abu Bakr na Umar ndiwo waliompongeza Ali (A.S) kupitia ibara hiyo. [15]

Pia baadhi ya vitabu vimenukuu ya kwamba; Tukio hili la pongezi linahusiana na Sayyid Aal Adiy [16] au Sayyid Bani Adiy. [17] Kuna baadhi pia zilizonkuu tukio hili bila ya kutaja jina mpongezaji wake.[19].

Kwa mujibu wa moja ya riwaya ni kwamba; Baada ya kutangazwa kwa Uimamu wa Ali (A.S), Khalifa wa pili alimfahamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W) kwamba, amemuona kijana aliyekuwa akitangaza ya kwamba, jambo hili halipuzwi isipokuwa na wanafiki tu. Baada ya yeye kumpa habari hiyo, Mtume (S.A.W.W) akamwambia kwamba kijana huyo uliyemuona alikuwa ni Jibril. [20]

Ithibati Juu ya Uimamu wa Ali bin Abi Talib (A.S)

Suala la pongezi za khalifa wa pili kwa Imam Ali (A.S) katika tukio la Ghadir, linazingatiwa kuwa ni uthibitisho wa nia ya Mtume (S.A.W.W) ya kumtambulisha Ali (A.S) kuwa mrithi wa nafasi yake. [21] Pia tukio hilo ni ithibati juu ya hadhi, nafasi na ubora wa elimu ya Imamu Ali (A.S) kulingana na Masahaba wengine. [22] [23] Katika baadhi ya maandiko, imeelezwa kwamba; Baada ya kupita fulani, Imam Ali (A.S) alipokutana na Khalifa wa kwanza katika majadiliano ya suala la ukhalifa, aliashiria tukio la Ghadir na pongezi alizopongezwa kuhusiana na tukio hilo, kama ni ithibati katika kuthibitisha uhalali wa haki yake ya kushika nafasi ya ukhalifa baada ya Mtume (S.A.W.W). [24] Kwa mujibu wa maelezo ya Faiz Kashani; Baada ya Khalifa wa pili kutamka ibara hii katika tukio la Ghadir, kila alipokutana na Ali (A.S) alikuwa akimdalimia huku akimpa heshima kwa kumwita jina la Amirul-Muuminin. [25]

Wakati wa Tukio la Pongezi

Vyanzo vingi vimethibitisha ya kwamba; Tukio la pongezi za Masahaba katika kumpongeza Ali (A.S) juu ya nafasi yake ya ukhalifa, lilitokea katika tukio la Ghadir, baada ya Mtume Muhammad (S.A.W.W) kuumtangaza Imam Ali (A.S) kuwa ndiye mshika nafasi ya ukhalifa baada yake. [26] Kwa mujibu wa daadhi ya Riwaya ni kwamba; Baada ya Ali (A.S) kutangazwa kuwa ndiye khali baada ya Mtume (S.A.W.W). Mtume (S.A.W.W) aliamrishwa lisimamishwe hema maalumu kwa ajili ya Imamu Ali (A.S), kila mmoja baada ya mwengine miongoni mwa masahaba waingie hemani humo kwa ajili ya kumpongeza. [27]

Katika baadhi ya vyanzo, tukio hili limehusishwa na siku ya Mubahala na tukio la Mtume (S.A.W.W) la kuunga udugu baina ya Waislamu, ambapo baada ya Mtume (S.A.W.W) kuutangaza ukahalifa wa Imam Ali (A.S), Omar bin Khattab alimpompongeza Ali (A.S). [28]

Vyanzo

  • Al-Tafsīr al-mansūb ilā al-Imām al-Ḥasan b. ʿAlī al-ʿAskarī. Edited by Madrisa al-Imām al-Mahdī (a). Qom: 1409 AH.
  • Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn. Al-Ghadīr fī al-kitāb wa al-sunna wa al-ʾadab. Qom: Markaz al-Ghadīr li-l-Dirāsāt al-Islāmiyya, 1416 AH.
  • Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Madīnat maʿājiz al-aʾimat al-ithnay ʿashar. Qom: Muʾassisa al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1313 AH.
  • Daylamī, Ḥasan b. Abī l-Ḥasan al-. Irshād al-qulūb. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1412 AH.
  • Daylamī, Ḥasan b. Muḥammad. Ghurar al-akhbār wa durar al-āthār fī manāqib abī al-aʾimma al-aṭhār. Edited by Ismāʿīl Ḍaygham. Qom: Dalīl-i Mā, 1427 AH.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Muḥsin. Nawādir al-akhbār fīmā yataʿllaq b-i usūl al- dīn. Tehran: Muʾassisa-yi Muṭāliʿat wa Taḥqīqāt-i Farhangī, 1371 sh.
  • Furāt al-Kūfī, Abu l-Qāsim Furāt b. Ibrāhīm. Tafsīr furāt al-kūfī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. ʿAbd Allāh al-. Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
  • Hilālī, Sulaym b. Qays. Kitāb Sulaym b. Qays al-Hilālī. Edited by Muḥammad Anṣārī Zanjānī. Qom: Al-Ḥadī, 1405 AH.
  • Ḥillī, ʿAlī b. Yūsuf b. al-Muṭahhar al-. Al-Udad al-qawīyya li dafʿ-i al-mukhāwif al-yawmīyya. Qom: Kitābkhāna-yi Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1408 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Ibn Baṭrīq, Yaḥya b. Ḥasan. ʿUmdat ʿuyūn ṣiḥāḥ al-akhbār fī manāqib Imām al-abrār. Qom: Jāmiʿa-yi Mudarrisīn, 1407 AH.
  • Ibn Ḥanbal, Aḥmad b. Muḥammad. Musnad al-Imām Aḥmad b. Ḥanbal. Edited by Abd Allāh b. ʿAbd al-Muḥsin al-Turkī and others. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1416 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH.
  • Ibn Shādhān al-Qummī, Shādhān b. Jabraʾīl. Al-Rawḍa fī faḍāʾīl al-Imām Amīr al-Muʾminīn ʿAlī b. Abī Ṭālib (a). Edited by ʿAlī Shikarchī. Qom: Maktabat al-Amīn, 1423 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Ṭaraf min al-ʾAnbaʾ wa al-manāqib. Edited by Qays ʿAṭṭār. Mashhad: Tāsūʿā, 1420 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Edited by Sayyid Hashim Rasūlī Maḥallātī. Tabriz: Banī Hāshimī, 1381 AH.
  • Karājakī, Muḥammad b. ʿAlī. Kanz al-Fawāʾid. Edited by ʿAbd Allāh Niʿma. Qom: Dār al-Dhakhāʾir, 1410 AH.
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Edited by Musṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
  • Khuṣaybī, Ḥusayn b. Ḥamdān al-. al-Hidāya al-kubrā. Beirut: al-Balāgh, 1419 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Masārr al-Shīʿa fī tawārīkh al-sharīʿa. Edited by Mahdī Najaf. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamī li-Alfīyat al-Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Tehran: Kitābchī, 1376 Sh.
  • Shāmī, Yūsuf b. Ḥātam al-. Al-Durr al-naẓīm fī manāqib al-aʾimma al-hāmīm. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1420 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. Third edition. Tehran: Islāmiya, 1390 sh.