Aya ya Infa'q

Kutoka wikishia

Aya ya Infaq (Kiarabu: آية الإنفاق) (al-Baqara: 274) au kutoa imeshuka kuhusiana na suala la kutoa na namna ya kutekeleza jambo hili katika mazingira tofauti. Wafasiri wanasema kuwa, sababu ya kushuka Aya hii ni hatua ya Imam Ali (a.s) ya kutoa ambaye alitoa dirhamu 4 usiku na mchana kwa siri na dhahiri. Baadhi wanaamini kwamba, Aya hii inajumuisha watu wote ambao wanalifanya kazi hii yaani wanatoa mali na kusaidia wengine katika hali ya dhahiri na siri. Kusamehewa dhambi, kuwekwa mbali na adhabu, utulivu wa dhamira na kinafsi na kuondolewa ghamu na huzuni ni mambo yaliyotajwa kuwa ni matunda ya kutoa na kusaidia katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Andiko la Aya na tarjumi

Aya ya 274 iliyoko katika Surat al-Baqarah inafahamika kama Aya ya Infaq (kutoa). [1] Baadhi wameitambua Aya hii kwamba ni mkusanyiko wa Aya 14 za kabla yake kuhusiana na Infaq. [2] Katika Aya hii kumezungumziwa namna ya kutoa, ujira wa hilo [3] na taathira yake katika utulivu wa mwanadamu [4] na fadhila za hilo katika mazingira tofauti na katika wakati wote. [5]


الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ

Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.



Aya ya infaq (kutoa) inawataja watu ambao daima hutoa mali zao katika mazingira yoyote yale; [6] utayari na uzingatiaji wao wa kutoa katika hali zote, [7] pamoja na athari za kidunia na za baadaye akhera [8]).

Sababu ya kushuka

Wafasiri wa Kishia wakitumia hadithi na riwaya mbalimbali wameitambua Aya hii kwamba, ilishuka kwa Imam Ali (a.s) ambaye alitoa dirhamu 4, moja usiku, nyingine moja mchana, moja nyingine kwa dhahiri na nyingine moja kwa siri. [9]

Wafasiri wa Kisunni wana mitazamo miwili kuhusiana na sababu ya kushuka Aya ya Infaq; baadhi yao wametambua kwamba, Aya hii ilishuka kwa sababu moja tu nayo ni kuhusiana na Imam Ali (a.s). [10] Kundi la pili sambamba na kuashiria sababu ya kushuka Aya hii kwa Imam Ali (as) wameweka kando yake pia kuhusu uwezekano mwingine kama vile kutoa Abdul-Rahman bin Awf [11] na Abu Bakr; [12] wameashiria kwamba, Abdul-Rahamn bin Awf alitoa mchana na Imam Ali (a.s) alikuwa akitoa mali usiku [13[ au kila kila mtu ambaye anaatoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu [14[ bila ya isirafu na ufujaji [15] na hata watu ambao wanawapa chakula farasi wa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. [16]

Baadhi ya wengine baada ya kutaja mambo mbalimbali kama uwezekano kuhusiana na kushuka Aya hii, wamekomea hapo na kueleza kutojua kwako kuhusiana na sababu maalumu ya kushuka Aya hiyo. [17]

Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba, hata kama Aya hii imeshuka kuhusiana na mtu maalumu; lakini hukumu yake haihusiana na jambo fulani tu maalumu, bali inajumuisha watu wote ambao wanatoa mali namna hii; [18] pamoja na kuwa, kutoa kwa Imam Ali (a.s) kutokana na kutangulia kwake katika hilo kuna fadhila nyingi. [19]

Tafsiri

Katika Aya ya Infaq (kutoa mali) kumeashiriwa njia mbalimbali; kwa sura hii kwamba, kama kutakuwa hakuna haja ya kudhihirisha hilo basi mtu atoe katika hali ya siri na kificho [20] ili kutotia dosari hadhi na heshima ya mpokeaji, [21] na kama katika sehemu nyingine kutokana na mazingira yalivyo, kutoa kwa dhahiri kuna maslahi kama vile kushajiisha na kuwapa moyo wa kutoa watu wengine na kuadhimisha shaari na alama, basi inawezekana na inajuzu kutoa kwa kudhihirisha; licha ya kuwa ni vyema mtu kutoa usiku badala ya mchana na kutoa kwa siri bali ya kutoa kwa dhahiri. [22] Infaq na kutoa maana yake ni kusaidia kimali [23] na kutatulia wengine mapungufu na shida za kimali. [24]

Katika Aya hii kumebainishwa pia ujira wa infaq (kutoa) kama vile kusamehewa madhambi na kuwekwa mbali na adhabu. Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba, Mwenyezi Mungu kwa kitendo chake hiki anaanda mazingira ya utulivu wa kinafsi na kuwaondolea ghamu na huzuni watu wanaotekeleza amali hii, [25] kwani yumkini baadhi kutokana na wasiwasi wa mustakabali au woga wa kupoteza mali na utajiri wakajizuia kutoa; hivyo anawatambua watu ambao wanatoa kuwa ni wale ambao hawana woga na mustakabali na hawatakuwa na ghamu na huzuni ya kupoteza sehemu ya mali na utajiri wao; [26] licha ya kuwa Tabarsi katika tafsiri yake ya Maj'ma al-Bayan, [27 na wafasiri wengine wanaamini kuwa, makusudio ya Aya kuhusu kutokuwa na woga na wahka, hili linahusiana na Siku ya Kiyama.

Kutengwa mbali na ghamu [29], kuwa na moyo wa kutoa, utulivu na usalama ni miongoni mwa mambo yaliyotambuliwa kuwa ni jumbe na risala za Aya hii. [30].

Vyanzo

  • Abu Hayyan, Muhammad bin Yusuf. al-Bahr al-Muhith fi al-Tafsir, Beirut: Dar al-Fikr. 1420 H.
  • Alusi, Sayyid Mahmud, Ruh al-Ma'ani fi Tafsir al-Qur'an al-‘Azhim, Riset: Ali Abdul Bari Athiyah, Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiyah. 1415 H.
  • Amid, Hussein. Farhangg-e Farsi Amid, Teheran: Amir Kabir, 1360 HS.
  • Ayashi, Muhammad bin Masud Kitab al-Tafsir ,Riset: Hashim Rasuli, Teheran: Maktabah al-Ilmiah al-Islamiyah, 1380 HS
  • Baghawi, Hussein bin Masud, Tafsir al-Baghawi (Ma'alim al-Tanzil), Riset: Abdurrazzaq Mahdi, Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, 1420 H.
  • Baidhawi, Abdullah bin Umar, Anwar al-Tanzil wa Asrar al-Ta'wil, Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, 1418 H.
  • Dainuri, Al-Wadhih fi Tafsir al-Qur'an al-Karim, Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiyah, 1424 H.
  • Fakhrurrazi, Muhammad bin Umar, al-Tafsir al-Kabir (Mafatih al-Ghaib), Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, Cet. Ketiga. 1420 H.
  • Haskani, Shawahid al-Tanzil li Qawaid al-Tafsil, Riset: Muhammad Baqir Mahmudi, Teheran: Wezarate Farhang va Ershade Eslami. 1411 H.
  • Ibnu Jauzi, Abdurrahman bin Ali, Zad al-Masir fi Ilmi al-Tafsir, Beirut: Dar al-Kitab al-Arabi, 1422 H.
  • Ibnu Kathir, Ismail bin Umar, Tafsir al-Quran al-Azhim, Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, 1419 H.
  • Ibnu Sulaiman, Maqatil, Tafsir Maqatil bin Sulaiman, Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, 1423 H.
  • Ja'fari, Yakub. Tafsir Kautsar, Qom: Yayasan Penerbitan Hijrat, 1376 S.
  • Jurjani, Abdul Qadir bin Abdurrahman, Darju al-Durar fi Tafsir al-Qur'an al-'Azhim Oman: Dar al-Fikr, 1430 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Tafsir Nemuneh. Teheran: Dar al-Kitub al-Islamiyah. Cet. Kesepuluh. 1371 S.
  • Maturidi, Muhammad bin Muhammad. Ta'wilat Ahli al-Sunnah. Dar al-Kutub al-Ilmiyah, Beirut: Mansyurat Muhammad Ali Baidhun, 1426 H.
  • Mawardi, Ali bin Muhammad. al-Nakt wa al-Uyun Tafsir al-Mawardi. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah. Tanpa tahun.
  • Mughniyah, Muhammad Jawad. Tafsir al-Kasyif. Qom: Dar al-Kitab al-Islami. 1424 H.
  • Qiraati, Muhsen. Tafsir Nur. Teheran: Markaz Farhanggi Darshai az Qur’an. 1388 S.
  • Qurtubi, Muhammad bin Ahmad. al-Jami' li Ahkami al-Qur'an. Teheran: Nashir Khosro. 1364 S.
  • Rezai Isfahani, Muhammad Ali. Tafsir Qur'an Mehr. Qom: Pajuheshaye Tafsir va Oloume Qur'an. 1387 S.
  • Samarqandi, Nashr bin Muhammad. Tafsir al-Samarqandi al-Musamma Bahr al-Ulum. Beirut: Dar al-Fikr. 1416 H.
  • Sekelompok peneliti. Farhang Name Ulume Qurani. Qom: Pajuheshgah Oloum va Farhange Eslami. 1394 HS.
  • Shan'ani, Abdurrazzaq bin Humam. Tafsir al-Qur'an al-Aziz al-Musamma Tafsir Abdurrazzaq. Beirut: Dar al-Ma’rifah. 1411 H.
  • Suyuthi, Abdurrahman bin Abi Bakr. al-Dur al-Manstur fi Tafsir bi al-Ma'tsur. Qom: Perpustakaan Umum Ayatullah Mar’asyi Najafi ra. 1404 H.
  • Shahatah, Abdullah bin Masud.,Tafsir al-Qur'an al-Karim, Kairo: Dar Gharib. 1421 H
  • Shaibani, Muhammad bin Hasan, Nahju al-Bayan 'an Kasyfi Ma'ani al-Qur'an, Riset: Husein Darghahi. Qom: penerbit al-Hadi. 1413 H.
  • Tabatabai, Muhammad Hussein., al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an ,Beirut: Muassasah al-A'lami. Cet. Kedua. 1390 H.
  • Tabrani, Sulaiman bin Ahmad al-Tafsir al-Kabir : Tafsir al-Quran al-Azhim, Arbad Arden, Dar al-Kutub al-Tsaqafi. 2008.
  • Tabrasi, Fadhl bin Hasan. Majma' al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an. Teheran: Nashir Khosro, Cet. Ketiga, 1372 S.
  • Thusi, Al-Tibyan fi Tafsir al-Qur'an. Beirut: Dar Ihya al-Turatth al-Arabi, Tanpa Tahun.
  • Wahidi, Ali bin Ahmad. al-Wajiz fi Tafsir al-Kitab al-Aziz. Beirut: Dar al-Qalam. 1415 H.
  • Zamahkshari, Mahmud bin Umar, al-Kasyaf 'an Haqaiq Ghawamidh al-Tanzil wa Uyun al-Aqawil fi Wujuh al-Ta'wil, Beirut: Dar al-Kitab al-Arabi. Cet. Ketiga.1407 H.