Aya ya Indhar

Kutoka wikishia
Aya ya Indhar (Onyo)

Aya ya Indhari (Kiarabu: آية الإنذار) (Shuaraa: 214) inamuamrisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwamba, awaonye watu walio karibu naye (jamaa zake) na awatangazie na kuwalingania Uislamu kwa sura ya wazi kabisa. Kufuatia kushuka Aya hii, Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwaaliika watu 40 katika jamaa zake wa karibu na baada ya kuwalingania kwa dhahiri na kwa uwazi Uislamu alimtangaza na kumtambulisha Ali bin Abi Talib (a.s) kuwa mrithi wake na kiongozii wa umma baada yake. Wanateolojia wa Kishia wakitegemea hadithi zinazozungumzia kushuka kwa Aya hii wanazitumia kama hoja na nyaraka za kuthibitisha kuwa Imamu Ali (a.s) ni kiongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w).

Wafasiri wa Kishia wanaamini kuwa, kujiepusha na tuhuma za ubaguzi kwa jamaa katika kuona na kutahadharisha juu ya kutoghafilika na wengine katika dini, na pia kujua jamaa na ndugu kuhusu rekodi safi ya Mtume ni miongoni mwa sababu za kuanza kuwalingania wao.

Uthibitiisho wa kwanza wa Uimamu wa Imamu Ali (a.s)

Aya ya 214 katika Surat al-Shuaraa ndio Aya mashuhuri zaidi inayojulikana kwa jina la Aya ya Indhari (onyo). Inaelezwa kuwa, Aya ya 7 Surat al-Shuura na Aya za 1 na 2 za Surat Muddaththir zinajulikana pia kwa jina hili. [1] Katika Aya hii anamuamrisha Mtume Muhammad (s.a.w.w), awaonye watu walio karibu naye (jamaa zake) na awatangazie na kuwalingania Uislamu kwa sura ya wazi kabisa na kama ilivyokuja katika Tafsir Nemooneh ni kuwa awatishe kuhusiana na matokeo mabaya ya shirki na kupingana na Mwenyezi Mungu. [2]

Aya hii inatambuliwa kuwa Aya ya kwanza iliyoshuka kwa Mtume ikimtaka atangaze wazi dini ya Uislamu. [3] Baadhi wakitegemea hadithi zilizonukuliwa kuhusu kushuka Aya ya Indhar kuhusiana na uongozi wa Imamu Ali (a.s) baada ya Mtume (s.a.w.w) wanasema kuwa, Aya hii ni hoja na waraka imara na ushahidi usio na shaka kuhusiana na Uimamu wa Imamu Ali bin Abi Talib (a.s). [4] Wanahistoria wanasema kuwa, Aya ya Indhar ilishuka mwaka wa 3 baada ya kubaathiwa na kupewa Utume Mtume Muhammad (s.a.w.w). [5]

وَ أَنْذِرْ عَشیرَتَکَ الْأَقْرَبین



Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. [26]

Kutangazwa uongozi wa Imamu (a.s) baada ya Mtume (s.a.w.w)

Makala kuu: Hadith Yaum al-Dar

Kwa mujibu wa tafsiri za Qur'an za Waislamu wa Kishia na Kisunni ni kwamba, baada ya kushuka Aya ya Indhar, Mtume (s.a.w.w) aliwaalika watu 40 miongoni mwa jamaa zake wa karibu na akawataka na kuwalingania wamuabudu Mungu mmoja na kumtii Mtrume wake. Inanukuliwa kwamba, baada ya wageni kumaliza kula chakula alisimama na kusema: Enyi wana wa Abdulmuttalib, kwa hakika Mwenyezi Mungu amenituma kwa watu wote kwa ujumla na kwenu nyinyi niwaite katika Uislamu. Mwenyezi Mungu ameniamrisha kuwa ni waonye ndugu (jamaa) zangu wa karibu, hivyo ninawaita katika mambo mawili ambayo ni mepesi sana katika ulimi, lakini ni mazito sana katika mizani (siku ya Kiyama). Mambo hayo ni Shahada ya Laa Ilaaha Illallah na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Yeyote atakayezingatia (atakayeitikia) wito huu na kunisaidia atakuwa ndugu yangu, msaidizi (Waziri) wangu, Wasii wangu, Mrithi wangu na Khalifa baada yangu". Inaelezwa kuwa, Mtume alisema mara tatu, nani atanisaidia katika kazi hii ili awe wangu, Wasii wangu, Mrithi wangu na Khalifa baada yangu"? hakuna aliyejibu, watu wote walikuwa kimya. Kila mara Mtume alivyosema hivyo, Ali (a.s) alikuwa akisema kila mara baada ya kimya cha wengine kwamba: "Mimi Ewe Mtume wa Allah". Mtume alikuwa akimwambia kaa chini. Baada ya mara ya tatu: Mtume aliweka mkono wake katika bega la Ali na kutangaza: "Huyu (Ali) Ni Ndugu Yangu, Wasii Wangu, Waziri (Msaidizi) Wangu, Mrithi Wangu Na Khalifa Baada Yangu Kwenu, Hivyo Msikilizeni Na Mtiini". [6] Sababu hii ya kushuka Aya hii imetambuliwa katika kitabu cha Majmaa al-Bayan kuwa ni mashuhuri baina ya Mashia na Masuni. [7]

Wanateolojia wa Kishia, wanasema kuwa, mapokezi ya hadithi ya tukio hili ni mutawatir [8] na wameitumia kuthibitisha uongozi na ukhalifa wa Imamu Ali (as) mara tu baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w). [9]

Kwa nini da'awa ianzie kwa jamaa na watu wa karibu

Wafasiri wa Qur'an tukufu katika kubainisha sababu ya Mtume (s.a.w.w) kuanza da'awa na ulinginiaji wake wa Uislamu kwa jamaa na watu wake wa karibu wametoa hoja mbalimbali. Miongoni mwazo ni:

  1. Kujiepusha na tuhuma za ubaguzi kwa jamaa katika kuonya na kutahadharisha juu ya kutoghafilika na wengine katika suala la dini. [10]
  2. Kuwa rahisi kwa Mtume kuwakusanya jamaa na ndugu wa karibu na kuwaonya ikilinganishwa na kuwakusanya watu wa makabila mengine. [11]
  3. Mtume kupata himaya na uungaji mkono wa ndugu na jamaa zake wa karibu kama wataaamini na kukubali mwito wake. [12]
  4. Mpango wa mapinduzi mapana unapaswa kuanza na dura dogo. [13]
  5. Jamaa na ndugu wa Mtume s.a.w.w) wana ufahamu bora zaidi na udugu na ujamaa unapelekea wasikilize maneno yake kuliko watu wengine na kuwa mbali na chuki, husuda na uadui kwa Mtume ikilinganishwa na watu wengine. [14]

Vyanzo

  • Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1416 AH.
  • Furāt al-Kūfī, Abu l-Qāsim Furāt b. Ibrāhīm. Tafsīr furāt al-kūfī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. ʿAbd Allāh al-. Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Edited by Muṣṭafā al-Saqā. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1419 AH.
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatollāh Marʿashī al-Najafī, 1404 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1406 AH.